Somo 6
Kufurahia uwepo wa Mungu
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Warumi 7:14 – 25
14 Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho;
mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo:
kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya
lile ambalo nachukia kulifanya. 16 Kwa hiyo kama ninafanya lile
nisilopenda kufanya, hii ina maana kwamba nakubali kuwa sheria
ni njema. 17 Basi, kwa kweli si mimi hasa nitendaye lile nisilolipenda
bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana ninafahamu
kwamba hakuna wema wo wote ndani yangu mimi, yaani katika mwili
wangu wa asili. Ingawa nina nia ya kutenda lililo jema, lakini
ninashindwa kulitenda. 19 Sitendi lile jema nipendalo bali lile
ovu nisilopenda, ndilo nitendalo. 20 Basi kama ninafanya lile
nisilopenda kufanya, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile
dhambi ikaayo ndani yangu.
21 Kwa hiyo imekuwa kama ni sheria: kila ninapotaka kufanya jambo
jema, jambo ovu hujitokeza. 22 Kwa maana ndani yangu ninaifurahia
sheria ya Mungu. 23 Lakini ninaona kuna sheria nyin gine mwilini
mwangu inayopingana na ile sheria ninayoikubali akilini mwangu.
Sheria hii inanifanya kuwa mateka wa sheria ya dhambi ambayo inafanya
kazi mwilini mwangu.
24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa
na huu mwili wa kifo?
25 Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu
Kristo! Kwa hiyo basi, mimi kwa moyo wangu, ninaitumikia sheria
ya Mungu, lakini kwa mwili wangu wa asili ninaitumikia sheria
ya dhambi.
Warumi 8:1-17
1Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya
Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo
Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu
amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu
wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana
wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa
ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa
ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho
na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.
5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili
yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale
waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya
Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni
kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani.
7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa
Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa
kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza
Mungu .
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili,
bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani
yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.
10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa
kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha
kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu
kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu
kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia
ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu
zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13
Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza
matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu
ni wana wa Mungu.15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa
wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho
huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho
mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana
wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi
wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja
naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.
Wakolosai 3:1-17
1 Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo
yenu kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo, upande wa kulia wa
Mungu.2 Yafikirini mambo ya juu na siyo mambo ya hapa duniani.
3 Kwa maana ninyi mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo
kwa Mungu.4 Wakati Kristo ambaye ni uzima wetu ataonekana, ndipo
na ninyi mtakapoonekana pamoja naye katika utu kufu.
5 Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana
na asili yenu ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya,
nia mbaya na choyo ambayo ni ibada ya sanamu.
6 Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu ya Mungu inakuja.
7 Ninyi mlikuwa mkitenda mambo haya katika maisha yenu ya zamani.
8 Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira,
ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani
mwenu.
9 Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu
wa zamani pamoja na matendo yake 10 na kuvaa utu upya ambao unaendelea
kufanywa upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake.11 Katika
hali hii hakuna tena tofauti kati ya Mgiriki na Myahudi, aliyetahiriwa
na asiyetahiriwa, mtu aliyesoma na asiyesoma, mtumwa na mtu huru.
Bali Kristo ni yote na yumo ndani ya wote. 12 Basi, kwa kuwa ninyi
ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu, vaeni moyo wa huruma,
wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu. 13 Vumilianeni na kusameheana
kama mtu ana malalamiko kuhusu mwenzake. Sameheni kama Bwana alivyokwisha
kuwasamehe. 14 Juu ya haya yote, vaeni upendo ambao unaunganisha
mambo haya kuwa kitu kimoja kilicho kikamilifu. 15 Ruhusuni amani
ya Kristo itawale mioyoni mwenu kwa kuwa ninyi kama viungo vya
mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena muwe na shukrani. 16 Neno la
Kristo lidumu ndani yenu kwa wingi, mki fundisha na na kuonyana
katika hekima yote; na huku mkiimba zab uri, nyimbo na tenzi za
rohoni na mkiwa na shukrani kwa Mungu mioyoni mwenu. 17 Na lo
lote mtakalofanya, ikiwa kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika
jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kupitia kwake.
Warumi 12:1-8
1 Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu,
jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu,
ambayo ndio ibada yenu ya kiroho. 2 Msiige tabia na mien endo
ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya,
ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema,
yanayopendeza machoni pake na makamilifu.
3 Kwa sababu ya neema niliyopewa nawaambia kila
mmoja wenu: Msijifikirie kuwa watu wa juu kuliko mlivyo. Badala
yake, muwe na kiasi katika mawazo yenu, kila mmoja wenu ajipime
kutokana na kiasi cha imani aliyopewa na Mungu. 4 Kama vile ambavyo
kila mmoja wenu ana mwili mmoja wenye viungo vingi, na kila kiungo
kina kazi yake, 5 hali kadhalika, ndani ya Kristo sisi tulio wengi
tunakuwa mwili mmoja na kila mmoja wetu ni sehemu ya we ngine
wote. 6 Tumepewa vipawa tofauti kulingana na neema tuliy opokea
kutoka kwa Mungu.
Warumi 12:9-21
9 Upendo wenu uwe wa kweli. Chukieni uovu, mshikilie yaliyo mema.10
Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine
kuliko mnavyojiheshimu wenyewe. 11 Juhudi yenu isipungue, moto
wenu wa kiroho uendelee kuwaka mkimtumikia Mungu. 12 Muwe na furaha
katika tumaini lenu, na katika dhiki muwe na subira. Ombeni wakati
wote.13 Wasaidieni watu wa Mungu walio na shida. Muwe wakarimu
kwa matendo.
14 Waombeeni baraka za Mungu wanaowatesa. Wabarikini wala msiwalaani.15
Furahini pamoja na wenye furaha; huzunikeni pamoja na wenye huzuni.16
Muishi kwa amani ninyi kwa ninyi. Msitake makuu bali muwe tayari
kushirikiana na wanyonge. Kamwe msiwe watu wenye majivuno.
17 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda
yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kaeni kwa
amani na watu wote.19 Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe
nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:“Kisasi ni
juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana.20 Badala yake, adui yakoakiwa
na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya
hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake.21 Usishindwe na ubaya,
bali uushinde ubaya kwa wema.
Warumi 15:1-13
1 Sisi tulio imara katika imani, hatuna budi kuchukuliana na udhaifu
wa wale ambao si imara. Tusitafute kujipendeza wenyewe. 2 Kila
mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake ili kumjenga katika
imani. 3 Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe bali alikuwa
kama ilivyoandikwa: “Matusi yote waliyoku tukana wewe yalinipata
mimi.” 4 Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa
kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika
Maandiko tuwe na tumaini.
5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie
ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 6
ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa
Bwana wetu Yesu Kristo.
7 Mpokeane ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowapokea,
ili Mungu apate kutukuzwa. 8 Maana nawaambia kwamba, Kristo alikuwa
mtumishi kwa Waisraeli ili kuonyesha kuwa Mungu ni mwaminifu,na
kuthibitisha ahadi alizowapa baba zetu. 9 Na pia ili watu wa mataifa
mengine wamtukuze Mungu kwa huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko:
“Kwa sababu hii nitakutukuza kati ya watu wa mataifa, nitaimba
nyimbo za kulisifu jina lako.” 10 Na tena yanasema, “Ninyi
watu wa mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.”
11 Na tena: “Msifuni Bwana enyi watu wote
wa mataifa, watu wote wamsifu.” 12 Na tena Isaya anasema:“Shina
la Yese lita chipuka, atatoka huko atakayetawala mataifa yote;
na watu wa ma taifa watamtumaini.”
13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani
katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa
na tumaini tele.
3. Yohana 15:1 – 8
‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2
Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata;
na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda
zaidi. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili
yowapa. 4 Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi
lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo
hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote. 5 Mimi
ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake,
huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi
kufanya lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi
na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea.
7 Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu,
ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. 8 Mnapozaa matunda kwa
wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi
ni wanafunzi wangu.
Kumzuia Roho Mtakatifu
5. Matendo 7:51
51 “Ninyi watu wenye shingo ngumu! Wenye mioyo ya kipagani!
Mmekuwa viziwi kwa neno la Mungu wala hamchoki kumpinga Roho Mta
katifu! Kama walivyofanya baba zetu nanyi leo mnafanya vivyo hivyo.
I Watessalonike 5:19-20
19 Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 20 msidharau unabii.
Isaya 63:10
Lakini waliasi na kumhuzunisha Roho Mtakatifu
Na akageuka kuwa adui yao, na akapigana nao.
Angalizo-Eneo hili linatueleza Mungu alivyokuwa akihusika na Israeli
ambapo hawakutambua namna Mungu livyo wajali na kuwalea.
Matendo Ya Mitume 5:3
3 Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo
wako kiasi cha kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu
ya fedha ulizopata?
6. Wafilipi 4:6-7
6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni
Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7 Na
amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu
na nia zenu kwa Kristo Yesu.
Warumi 2:15
15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa
katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri
zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine
huwashtaki na mara nyingine huwatetea.
1 Samweli 10:17
Na iwe hivyo, hizo ishara zitakapo kujilia, na ufanye hivyo kwa
kuhitaji,kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.
2 Timotheo 3:16
16 Andiko zima lina pumzi ya Mungu nalo lafaa kwa mafundisho,
kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika
haki
7. 1 Yohana 3:1
Tazameni jinsi Baba alivyotupenda mno, hata tukaitwa watoto wa
Mungu! Na hivyo ndivyo tulivyo. Watu wa ulimwengu hawatutambui
kwa sababu hawakumjua Mungu.
Yohana 15:15
15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli
za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia
kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha.
Wafilipi 3:20-21
20 Lakini uraia wetu uko mbinguni. Nasi tunangoja kwa hamu Mwokozi
kutoka huko, yaani Bwana wetu Yesu Kristo, 21 ambaye, kwa uwezo
unaomwezesha kutawala kila kitu, atabadilisha miili yetu midhaifu
ili iwe na utukufu kama alionao yeye.
Waefeso 3:12
12 ambaye tukiwa ndani yake, tuna ujasiri na uhakika wa kumkaribia
Mungu kwa njia ya imani katika Kristo.
1 Wakorintho 6:19-20
19 Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa
ndani yenu, ambaye mme pewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe;
20 mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika
miili yenu.
8. b. Waefeso 6:10-18
10Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu.
11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana
na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu,
bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu
wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13
Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara
siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme
simama. 14 Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama
mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; 15 na kuvaa Injili
ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara.16 Zaidi
ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia
mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. 17 Vaeni wokovu
kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni
neno la Mungu. 18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala
zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea
watu wote wa Mungu.
9. Yakobo 4:7-8
7 Kwa hiyo, jinyenyekezeni kwa Mungu . Mpingeni shetani, naye
atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Takaseni mikono
yenu, ninyi wenye dhambi; na takaseni mioyo yenu, ninyi wenye
nia mbili.
1 Petro 5: 8-10
8 Kaeni macho. Kesheni, maana adui yenu Ibilisi, huzunguka- zunguka
akinguruma kama simba, akitafuta mtu atakayemmeza. 9 Mpingeni,
mkiwa thabiti katika imani, mkifahamu kwamba ndugu zenu pote duniani
wanapatwa na mateso hayo hayo. 10 Na mkisha kuteseka kitambo kidogo,
Mungu wa neema yote ambaye amewaita katika utukufu wake wa milele
katika Kristo, yeye mwenyewe atawa kamilisheni na kuwathibitisha
na kuwatia nguvu.
Waefeso 6:13
13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara
siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme
simama.
Waefeso 4:22-27
22 Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili
ambayo huharibiwa na tamaa potovu.23 Nia zenu zifanywe upya 24
na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu.
25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu
yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja.
26Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa
nzima 27 na kumpa she tani nafasi.
10. 2 Wakorintho 10:3-5
3 Ingawa tunaishi duniani lakini hatupigani kama watu wa ulimwengu.
4 Silaha zetu si za kidunia, bali silaha zetu zina nguvu ya kimungu
iwezayo kubomoa ngome.5 Tunaharibu hoja na mabishano yaliyo kinyume
cha kumjua Mungu. Tunateka mawazo yote na kuyafanya yamtii Kristo,
2 Wakorintho 6:7
7 katika maneno ya kweli na katika uwezo wa Mungu; kwa silaha
za haki mkono wa kulia na mkono wa kushoto;
Waefeso 6:17
17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga
wa Roho ambao ni neno la Mungu.
Zaburi 50:15
Niite wakati wa taabu, Ntakuokoa, na utanisifu.
1 Yohana 4:4
4 Lakini ninyi watoto wapendwa, ni wa Mungu, nanyi mmekwisha kuwashinda;
kwa maana yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yule aliyeko duniani.
11. 2 Petro 3:18
18 lakini kukua katika neema na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi
Yesu Kristo
Wagalatia 5:16
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute
kutimiza tamaa za mwili.