home >>vijana wa stonecroft>> huongoza lengo
Huongoza Lengo
KUWAFIKIA: Masomo haya yanatuwezesha kupata njia
ya kushirikiana kujua wokovu wa Yesu Kristo na watu wengine.kwa wale
ambao wana makundi wanaombwa kualika marafiki zao, famila, wafanya
kazi wenzao na pia majirani zao.
Uanafunzi: Wakristo wapya na wale waliokomaa wanaweza
kusoma saaana kuhusu MUNGU na kuweza kukua naye katika uhusiano
uliomzuri. Msomo haya yanatufundisha pia jinsi gani unaweza kutupia
kanuni za kiBiblia katika mazingira ya kila siku.
UPEKEE:
Nini kinachofanya masomo ya stonecroft kuwa wa kipekee sana kuliko
masomo mengine ya kiBiblia katika soko la mafundisho ya Biblia?
• Habari njema ya agano jipya: masomo haya yameundwa katika
mtindo wa kutumia agano jipya kwa sababu kurasa zimewekwa katika
vifungu vile unavyotakiwa kuvitafuta ndani ya Biblia ili kuweka
urahisi kwa wasomaji wa masomo haya. Kurasa hizi zilizowekwa katika
vifungu hivyo vimetoka katika Biblia ya toleo la 4 good news new
testament. na tafsiri hizi zinakubaliwa sana na watu mbalimbali
katika madhehebu tofauti tofauti.
• Masomo haya yameandikwa katika kwa mfumo ambao ni rahisi
wa kwamba hata Yule ambaye ni mara yake ya kwanza kutumia Biblia
basi anaweza kuyatumia vizuri tu. Na haya masomo yanaweza kutafsiriwa
kwa urahisi tu sana katika ulimwengu mzima kwa kutumia lugha yeyote
ile.
• Kiongozi ni mwezeshaji tu na sio mwalimu wa Biblia.
VIFAA:
Masomo ya stonecroft ya kiBiblia ni rahisi sana kusoma.
Maelezo kwa kiongozi yamefungiwa katika mistari iliyowekewa nukta
nukta. Kwa hiyo hayatakiwi kusomwa kwa sauti.
Maelezo mengine yameandikwa yakiwa ndani ya viboksi yapo katika
kitabu kile cha kujisomea au cha kusoma. Sehemu hii inatakiwa kusomwa
kwa sauti na wale wahisika wenyewe yaani wanafunzi wa mmasomo haya.
Ukionna nukta zimeongozana namna hii (…..) inaonyeshs ya
kwamba kiongozi inatakiwa aruhusu kundi ili kuweza kushiriki kwa
kujibu maswali, kusma mistari ya Biblia, au kujadili maada husika.
KABLA YA MASOMO :
Vitu vichache vya muhimu:
• Uhakikiwe kuwa wewe ni kiongozi wa stonecroft kwa kukamilisha
mchakato wa maombi katika Stonecroft.
• Soma malengo, na maelekezo ya masomo haya husika.
• Pata vifaa mbalimbali utakavyo taka kwa ajili ya masomo
yako kutoka katika huduma hii ya Stonecroft _ (800) 525-8627.
• Vifaa vinavyohitajika katika mafunzo haya ni :
- Vitabu vya kujifunzia
- Mwongozo
- Kadi za taarifa
• Tafuta sehemu nzuri kwa ajili ya kujifunzia. Kuwa na muda
wa kujifunza ukiwa upo nyumbani, ofisini, kwenye migahawa na katika
sehemu mbalimbali.
KUJIANDAA KWA AJILI YA KUJIFUNZA:
• Maliza somo kwa kukamilisha kuandika majibu yako kkatika
kitabu chako cha kujifunzia ,kabla ya kusomo mwongozo. Hii itakusaidiakatika
kujua na kuelewa mafkirio yaw engine na jinsi ambavyo majibu yako
uliyoyajibu yapo.
• Fanya mazoezi ya kusoma kwa sauti kama inawezekana. Pigia
mstari maneno na vifungu ambavyo vitakusaidia katika kuelezea mbele
ya kundi lako. Kumbuka muda ambao unatakiwa kwa ajili ya kusoma
ujumbe wako, hii itakusaidia katika kujua muda gan uliobaki wa majadiliano
katika kipindi hicho.
• Thibitisha mahali, muda na ulinzi wa watoto kama kutakuwa
na uwezekano wa kufanya hivyo.
• Waombee wote wale ambao watakuwa wakihudhuria katika masomo
kujifunza.
|