Embedded Microsoft Office presentation, powered by Office.
Hiari: Pakua 'Tone la Matumaini - Mradi wa Shule'' Swahili PowerPoint | |
'Living Water Bible Club' will be located in our 'Drop of Hope School Project' located outside of schools, churches and our Africa Goshen Agro Glamping Resorts.
Masomo haya yameandaliwa katika, kufundisha juu ya kichwa furani
cha somo lakini hata hivyo masomo yanayo husu vitabu vya biblia
yanapatikana katika hatua ya juu.
Masomo ya biblia ya Stonecroft ni rahisi kujisomea katika makundi
madogo na hata makundi makubwa, na masomo haya yanaanzia (4-14 masomo).na
utatu masomo 6 kwa hiyo kitabu kimoja kna masomo 18.
Masomo mengi yanakuwa na kitabu cha mwongozo wa masomo, kitabu
hiki hutumika pamoja na biblia na kila anae shiriki masomo haya
Majadiliano ni njia mojawapo katika ukuaji wa kiroho.
USHAURI WA KUJISOMEA:
Katika maeneo mengi ya Stonecroft washiriki hutumia kitabu cha mwongozo
na biblia ya Kiswahili, ambayo hupatikana madukani, lakini kama
nilivyosema kitabu cha mkononi cha biblia kinapatikana kwa wale
wasio na biblia.
Vikundi hivi vya kujisomea hukutana mara moja kwa wiki, kwa dakika
60-90 .kama dakika ni chache kundi wanaweza kuamua kugawa masomo
haya nusu, kwa kugawana maswali na kusoma andiko.ili kutanua kazi
ya uanafunzi tunashauri kuwa vikundi lazima vitafute njia za kuongeza
washiliki ili ufanisi wake uonekane katika jamii.
MAELEZO YA MASOMO:
Kuna aina tatu za masomo ya biblia ya Stonecroft:
•Masomo ya Utangulizi wa utatu.
• Masomo ya wakristo wanao kuwa.
• Na masomo yahusuyo vichwa vya somo.
Stonecroft waanze na somo la Utangulizi, ambalo linasema “Yesu
ni nani” Mungu yukoje?’ na Je Roho mtakatifu yuko wapi.haya
ni masomo muhimu sana kwa wakristo wapya na hata wale wa zamani
maana ni muhimu hata kwa wale wanao taka majibu ya maswali yao.
Haya masomo yote yamekwisha tafsiliwa Kiswahili na kazi bado inaendela
ya kutafsiri huko Congo na Malawi pia.
KANUNI NA SHERIA ZA MASOMO YA KIBIBLIA YA STONECROFT
Huduma ya Stonecroft imejiwekea kanuni kwa jili ya masomo yake ya
kibiblia, ni muhimu kwa mtu yeyote anae hudumu katika huduma hii
ya Stonecroft afuate hizosheria na kanuni
Injili ya Yesu ambayo imeandikwa katika kila somo la Stonecroft
ni muhimu kuwa ihunbiriwe kwa uhakika na umakini mkubwa.
Huduma ya Stonecroft hawana msimamo mwingine wa imani, au msimamo
wa kisiasa nje ya maelezo yao ya imani.
Wote ambao wanajihusisha na Stonecroft watafanya haya yafuatayo:
• Kukubariana na msingi wa imani ya huduma ya Stonecroft.
• Kutenda kazi kwa ushiriano na kanisa lako.
• Kila neno litakalo nenwa katika mjadala au mazungumzo wakati
wa masomo huo sio msiomamo wetu kama huduma ya Stonecroft.
Katika kujisomea haya masomo ya biblia ya Stonecroft, ni muhimu
wahusika wote wakatumia vitabu ambavyo vimethibitishwa na Sonecroft,
katika somo la utangulizi inashauliwa kuwa wahusika wote watumie
aina moja ya biblia ya Kiswahili.
Watu wote ambao watakuwa wanaisimamia au kuongoza haya masomo ya
kibiblia ya Stonecroft ni lazima watume maombi,waongozaji na wakufunzi
hufundishwa na kiongozi wa eneo husika, video ya masomo hayo imekwisha
andaliwa na Stonecroft Barbados ili kuwezesha kuwafunza wale watu
ambao wako Tanzania, Malawi, Uganda na nchi nyingine za Kiafrica,hii
video ya dakika 15 itarecodiwa kwa Kiswahili na lugha nyingine za
kiafrika, hii yote ni katika kuhakikisha kuwa tunawafunza wale ambao
watakuwa viongozi, ukiambatanisha na Mwongozo hii itawapa uwezo
mkubwa katika huduma.
MKAKATI WA MWONGOZO WA KUFUNZA:
|