home >>
stonecroft>>roho
mtakatifu yuko wapi?>>somo la kwanza 1
Stonecroft
- Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la kwanza (#1)
ROHO MTAKATIFU YUKO WAPI?
SOMO LA KWANZA (1)
KUTAMBUA UWEPO WA ROHO MTAKATIFU
Lucille Sollenberger. B.S., M. A.
Stonecroft Ministries
www.stonecroft.org
P.O.Box 9609, Kancas City, MO 64134-0609
Download Full Swahili
Guidebook
Download Swahili
Guidebook Introduction
Download Swahili Lesson
#1 Guidebook
Download Swahili
Guidebook Front and Back page of folder
Download
Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #1
Mistari ya Biblia
LENGO LA SOMO
• Jifunze Roho Mtakatifu ni nani hasa.
• Kubali kazi za Roho Mtakatifu katika kufanya mahitaji
yetu na wokovu wetu uweze kufanikiwa.
• Kujifunza kuwa Roho Mtakatifu anakuja ndani yetu pale
ambapo tunampokea Roho Mtakatifu.
• Kujua kuwa waamini wote wana Roho Mtakatifu iwe wanajitambua
au hawajitambui kuwa wana Roho Mtakatifu.
Somo hili ,linaelezea vizuri sana kuhusu wokovvu
na jinsi ya kuwa mkristo. Itakuwa vizuri zaidi endapo tutakuwa
na swali la kusema kuwa je unaamini?
Katika kuanza somo anza kwa kuwakaribisha watu kwa
muda muafaka na waruhusu wao wenyewe katika kujitambulisha wao
wenyewe.
MAOMBI
Baba uliyejuu mbinguni, tumekuja kujifunza neon lako.Tusaidie
kuelewa tunapoendelea kujifunza. Ongeza upeo wetu ili tuweze kuona
uwepo wako katika ukuu wako mwenyewe, na kuona upendo wako kwetu
na huruma zako, tu naomba katika jina la Yesu Kristo…..
AMEN
“Hakuna sehemu ya maisha ya
mkristo ambayo hayajatawaliwa na kuwezeshwa na Roho Mtakatifu”
—John MacArthur.
Mwalimu wa Biblia John MacArthur ansema kuwa kila
sehemu ya maisha ya mkristo inawezeshwa na ROHO MTAKATIFU.
Kwa kuwa huu ni ukweli, ni vizuri kusoma sana kuhusu
Roho Mtakatifu, ambaye anafanya kazi kama vile anavyo fanya Mungu
baba, na Yesu Kristo ambaye ni mwana. Pia tunatakiwa kutambua
kuhusu ushiriki war oho Mtakatifu katika maisha ya mtu binafsi.
ROHO MTAKATIFU NI NANI?
Unaweza ukawa unajiuliza sana, Roho Mtakatifu ni
nani?
Roho Mtakatifu yeye ni anaishi, na ni sawa na Mungu
baba na Yesu mwana.
Yeye ni Mungu na ana kila sifa ya uungu.
Angalia katika swa;li la kwanza, na tutaangali Biblia
inasema nini kuhusu Roho Mtakatifu.
Waweke washiriki pamoja na waweze kusoma na
kujibu swali la kwanza. Wape muda ili waweze kuandika majibu yao
katika vitabu vyao vya kujifunzia.
1. Kabla Yesu hajasurubiwa, aliwaambia wanafunzi
wake kwamba kabla hajaondoka, mtu mwingine atatumwa kwa jina
lake, soma katika Yohana 14:26……..
(Use your Bible or Africa Bible Verse
Handbook) a) Ni majina yapi mawili ambayo Yesu alimpa mtu huyo aliyekuwa
anamsema……..
(Msaidizi na Roho Mtakatifu)
b) Nani alimtuma Roho Mtakatifu?........(Mungu Baba)
c) Mstari huu u nasema nini, kuwa atafanya nini?.........(Atafundisha
wanafunzi na kuwakumbusha kile ambacho Yesu alisema). |
Roho Mtakatifu ni mtu. Tunapofikiri kuhusu mtu, tunaangalia taswira
yake ilivyo. Lakini kuna ugumu sana katika kujua taswira ya Roho
Mtakatifu kwa sababu Roho Mtakatifu yeye hana mwili.
Wengi wetu hatuna tatiizo la kufikiria kuwa kuwa Yesu kama mtu.
Tunajua kuwa Yesu alikuwa na mwili alipokuwa hapa duniani, hata
hivyo hatuna ,maelezo ya kina kuhusu mw onekano wake. Pia vilevile
ni vigumu kuiona taswira ya Mungu na Roho Mtakatifu kama wattu kwa
sababu hawana miili kama ya wanadamu wengine.
Angali katika Yohana 4:24…….
Tuna weza kujifunza vitu viwili kutoka katika mstari huu:
• Mungu na Roho Mtakatifu wote ni Roho.
• Hatuwezi kumwabudu Mungu bila msaada wa Roho Mtakatifu.
Munu na Roho Mtakatifu wana haiba binafsi, lakini hawana sura au
mwili ambayo unaweza kuiweka katika akili zetu.
Watu wengi wanafanya makosa kwa kumpa kikomo Roho Mtakatifu kwa
kulazimisha, kwa nguvu N.K. kusema kuwa na nguvu, ushawishi N.K
ni kuchukuahaiba yake na uwezo wake kufanya kazi ambazo mwanadamu
anaweza kufanya. Roho Mtakatifu ni mtu roho.
Angalia katika swali la pili (2) na uone nini kitu kingine ambacho
Biblia inasema kuhusu Roho Mtakatifu kama mwanadamu.
2. Roho Mtakatifu ni mtu. Mistari ya Biblia ifuatayo
inathibitisha hilo.
Andika mstari sahihi baada ya kila sentensi.
Yohana 15:26………
Matendo ya mitume 13:2…….
Warumi 8:14……..
Warumi 8:26……..
a. Roho Mtakatifu huwa anaongea. (Matendo 13:2)
b. Anatuombea sisi. (Warumi 8:26)
c. Anafunua ukweli kuhusu Yesu Kristo. (Yohana 15:26)
d. Anawaongoza wana wa Mungu. (Warumi 8:14) |
3.Yesu aliwaambi awanafunzi wake kwamba atawatumia
msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu baada ya yeye kuondoka. Roho
Mtakatifu alipokuja je alikuwa na dhumuni gani?
2 Wakorinthians 1:21-22………(
Roho Mtakatifu anaingia ndani ya maisha ya kila muamini, kama
garantii ya kwamba Mungu a nawamiliki, na ana Baraka nyingi
juu yao amabzo amezihifadhi kwa wale wote wanaompokea yeye.)
|
Swali linalofuata linahusu nini ambacho Roho Mtakatifu anafanya
kwa kila mtu.
4. Yesu alisema nini kuhusu Roho
Mtakatifu (msaidizi) anachokifanya kwaq watu wa ulimwengu
huu?.
Yohana 16:7-11…….( Roho
Mtakatifu anaonesha na kufunua ukweli wa Mungu na kuwajulisha
watu kuwa wanakosea wasipo muamini Mungu.)
|
Roho Mtakatifu anauhakikishia ulimwengu kuwa unakosea kuhusu wanaoamini
kuhusu dhambi na hukumu. Isaya 5:20 inasema kuwa “ole wao
wasemao uovu ni wema,na kwamba wema ni uovu,watiao giza badala ya
nuru,na nuru badala ya giza,watiao uchungu badala ya utamu na utamu
badala ya uchungu”
Roho Mtakatifu haendani kabisa na dhambi ambazo zinakuwepo nadani
ya maisha yetu. Anatuambia kuwa sisi tumekosea, pale tunaposema
kuwa Mungu ataziachilia mbali dhambi zetu. Inatakiwa tufikilie kuwa
a namaanisha wale watu waovu ndio watakao hukumiwa, na sio sisi
na anatuambia kuwa hukumu ipo inakuja.
Angalia ini Biblia inasema kuhusu hukumu katika ukurasa wa Waaamuzi
1:14-16……. Mungu ataleta hukumu kwa wote walio
kinyume na yeye, na wale wote wanao wanaotenda maovu. Kwa maneno
me ngine Mungu atawaadhibu wote wale ambao hawamuheshimu yeye.
Soma Warumi 6:23……..Mungu anasema
kama tukitenda dhambi, tunatakiwa kufa kwa ajili ya kulipa juu ya
dhambi hiyo. Bilia inatuambia kuwa hatuwezi kuingia mbinguni kama
sisi hatupo katika familia ya Mungu. Kazi muhimu ya Roho Mtakatifu
kwetu nikuwa sehemu yake ni kuzliwa kwetu upya. Anatukumbusha kuwa
sisi ni watenda dhambi na ambao tulitakiwa kufa. Kwa hiyo tunataka
mkombozi atakaye tuokoa katika dhambi ili tusifie katika dhambi
hiyo.
KUPOKEA ROHO YA MUNGU
Tunapoamini ukweli kwamba kifo cha kristo pale msalabani kilikuwa
ni kulipa deni ya dhambi zetu, tunamuomba Mungu msamaha ili atusamehe
dhambi zetu na aweze kulinda maisha yetu. Katika wakati huo tunakuwa
tumezaliwa katika familia ya Mungu na kupokea Roho Mtakatifu katika
maisha yetu. Anachuklua nafasi ya kukaa katika maisha yetu kwa ajili
yeye kutulinda kila siku.
5. a. Jinsi gani ambavyo tunazaliwa katika familia
ya Mungu? Yohana 3:5-7…………..
(Kwa Roho ya Mungu, pia anaitwa Roho Mtakatifu.) b.
Tito 3:4-7……….(Roho
Mtakatifu anatupa kuzaliwa upya na maisha kuyafanya kuwa mapya.)
|
Kuzaliwa upya ni kazi ya Roho wa Mungu. Inatokea mara kwa mara,
na sio katika hatua hatua. Pale tunapogundua kuwa na mazingira magumu
ya kuachwa na Mungu au kutengana na Mungu na kumuomba yeye ili atuokoe
sisi Roho Mtakatifu wa munu anaingia nani yetu ammbapo anatupa maisha
marefu na ambayo hayataisha leo wala kesho yaani ni ya milele.
Unapomwamini Yesu kama mwokozi wako, unapokea nini au unapata nini?
Soma Yohana 3:16….. (Uzima wa milele
na Mungu.)
6. Na ni aliyealikwa kuja kupokea zawadi ya ya
maisha ya milele? Ufunuo 22:17…….. (Roho
Mtakatifu anamkaribisha kila mtu kuja.) |
Ingawa Roho Mtakatifu anawalika kila mtu, sio wote wanaobadilika
na kuwa Wakristo. Kupokea wokovu ambao Yesu Kristo alitupa kupitia
kifo chake, mapenzi ya mtu muhusika mwenyewe yanahusika. Hakuna
mtu mwingine yeyote atakaye fanya uchaguzi huu, hapa kinachoangaliwa
sana ni matakwa ya mtu binafsi.
Tunapojishusha kwa Mungu, anachukua maisha yetu ya dhambi na anatupa
maisha ya utakaso yaaani ya utakatifu wa kristo. Kwa hili ili litokee,
ni vizuri matakwa haya yaweze kuhusishwa.
Sisi tumeokoka au tunaokolewa pale tunapompokea Yesu Kristo. Hata
kama sisi ni Wakristo, hatuoni vizuri Mwanzoni mwa maisha ya Ukristo.
Maono yetu yamegubikwa na tabia ya dhambi, na kufikiria dhambi kila
muda.
Maono hayo mabaya yanaondoka pale tunapoendelea kujifunza kuwa
Biblia inatuambia nini. Tunatakiwa kuchagua kile tunachokisoma na
kuweza kuhusisha kujitambua kwetu sisi kama sisi. Baada ya hapo
tutajifunza jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo ni hatua inayochukua
muda mrefu sana.
Faida mojawapo ya kujifunza Biblia, ni jinsi ya kujifunza kutumia
neno la Mungu katika maisha yetu ya kila siku. Katika kutumia masomo
haya ya Roho Mtakatifu mtazamo wetu ndio unatakiwa kuwa yakinifu
na sio tabia yetu. Kubadilisha mawazo ni vigumu sana kuliko kubadilisha
tabia ya mtu.
MUNGU NI MMOJA
Majina na maandiko ya Roho Mtakatifu yanafunua uhusiano uliopo
kati ya Mungu na Yesu Kristo. Soma Warumi 8:9 ,uoneshe
majina mawili ambayo Roho Mtakatifu aliitwa…… (Roho
ya Mungu na Roho ya kristo) kwa hiyo Roho Mtakatifu ana majina
mengi sana ambayo ni tofauti tofauti.
Tunapo jifunza kuhusu Yesu Kristo, tunajifunza kuwa moja kati ya
majina yake ni NIKO, ambapo Biblia ndiyo inayosema kuwa ni jina
la MUNGU. Soma Yohana 10:30……. Hii
itakuwa ngumu sana kwa fahamu zetu kuelewa .pia tunaposoma mistari
inayozungumzia kuhusu Roho Mtakatifu na Mungu ni kitu kimoja, ni
rahisi kuelewa kwa sababu wote hawa ni Roho.
Biblia inatufundisha tangu Mwanzo mpaka mwisho kuwa Mungu, Yesu
na Roho Mtakatifu wana tabia moja. Ni kitu kimoja na kufanya
kazi pamoja tena kwa umoja.
Tuna Mungu mmoja aambaye ana kazi tatu tofauTito fauti na
katika yeye tuna uhusiana katika utatu.
|
Kwa yote kuelewa hili ni vigumu sana .Yesu yeye hana mwisho, laini
mawazo yestu yana ukomo. Haiwezekani kumwelewa Mungu kuwa yukoje.
Nahiyo ilikuwa nisababu mojawapo ya Mungu kumtuma Yesu ulimwenguni
ili kuweza kutoa na kutujulisha asili ya Mungu na ukuu wake katika
njia ambayo tunaweza kumuelewa.
Tunapomwamini Yesu kama mwokozi wetu, Mungu anatupa Roho wake ili
kutufundisha na kutuongoza sisi. Tunapozidi kusoma na kujifunza
neno la Mungu, ndivyo tutakavyoelewa umoja uliopo kati ya Baba,
Mwana na Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ana kila kitu cha uuungu ambacho Mungu anacho. Swali
linalofuata linathibiftisha sifa zote hizo jinsi zilivyo.
7. Roho Mtakatifu anazo sifa zote ambazo Mungu
na Yesu Kristo wanazo.
Sifa hizo tatu zipo zimeorodheshwa hapa chini katika mistari
ifuatayo.
Sifa zifuatazo je zinadhihilrisha kuhusu rioho Mtakatifu?
Mpaji wa maisha
Anaishi milele
Maarifa yote, amniscience.
1 Korontho 2:11…….
(Maarifa yote - omniscience)
Waebrania 9:14…….
(Uzima wa milele)
Warumi 8:2,10……..
(Mpaji wa maisha)
|
Mungu alituokoa sisi kupitia Roho Mtakatifu, anyetupa kuzaliwa
upya na kuwa na maisha mapya. Roho Mtakatifu anatuwezesha sisi kukamilisha
mipango ya Mungu katika maisha yetu. Hatujui mipango ya Mungu kwamba
ikoje, lakini tunapomkaribisha yeye ili awe ndani ya maisha yetu
na kumruhusu kudhibiti maisha yetu, atatimiza mipango yake aliyoiweka
juu yetu sisi.
Pale tunapokuwa Wakristo, tunashangazwa tunapoona kwa kujua, kuwa
na Yesu katika maisha yetu kunabadilisha tabia zetu na pia inasababisha
kufikiri kitofauti, tuna hamu ya kusikia kuwa Mungu anasema nini
na kitu gani anakitarajia kutoka kwetu.
Mara nyingi tunafanya makosa katika kuangalia Wakristo wengine,
na kuanza kushawishi maisha yetu badala ya yale ya kwao. Au tunaweza
kusukumwa na kile watu ambao ni Wakristo wanachohitaji kutoka kwetu.
Inatakiwa twende ndani ya neno la Mungu na kusoma na kujua neno
linasema nini kuhusu tunachotakiwa kukifanya na tunafanyaje. Tunatakiwa
kuwa na hamu binafsi ya kukua kiimani na katika utii katika mwongozo
wa Mungu Roho Mtakatifu. Atatusaidia katika kuelewa neno lake. Hii
itatusaidia sisi katika kujizuia na watu kutaka kujua kile ambacho
kipo ndani yetu, na sio vile Mungu anatarajia kutoka kwetu.
Wakati Yesu Kristo ni muhimiri wa maisha yetu na tunampenda sana
kwa moyo wote. Na tunapotaka kufanya jambo Fulani ambacho hakihitaji
uangalifu sana, mara zote akili zetu na mafikilio yetu yanaelekeza
moja kwa moja kwenye maombi, au katika kuimba au kwenye nyimbo za
kuabudu. Tunafikilia kkuhusu uhusiano wetu na Mungu au nini ambacho
unaweza kumfanyia mtu ambaye tunatakia kumtumikia na tunataka kufikia
pendo lake.
Majibu ya maswari 8 yatatofautiana,mpe kila mmoja nafasi ya
kujieleza.
8. a. Je unatambuaje uwepo war oho
Mtakatifu ndani yako na analeta madhara gani pale unaposema
na unapofanya kitu Fulani?..... b. Kuwa na utambuzi juu ya
Roho Mtakatifu kuna athiri vipi muunganiko wako wewe na Yesu
Kristo?..... |
Tumia ukweli huu ndani ya aisha yako katika wiki hii, kuwa na ufahamu
au fahamu kuwa Mungu yuko pamoja na wewe. Kuna kuwa na furaha isiyoelezeka
pale unapoishi ndani ya ushirika wa Mungu.
Kwa kiurudia. Fikiria kuhusu tulichokisoma kuhusu Roho Mtakatifu:
Kutoka katika swali la 1:
Majina gani mengine ambayo Yesu aliweza alimpa Roho Mtakatifu?.....................(Msaidizi)
Nani alimtuma ………….(Mungu baba).
Alitakiwa kuja kufanya nini………(Kuwafundisha
wanafunzi na kuwakumbusha kwa kile alichokisema Yesu)
Kutoka katika swali la 4 na la 5:
Je Roho Mtakatifu alihusika vipi kabla ya kuwa Wakristo?......(Sisi
tulikuwa hatiana na alituonyesha kuwa sisi tunahitaji ukombozi ili
tutoke katika dimbwi la dhambi tuliyonayo)
Kutoka katika majadiliano:
Ni wakati gani ambapo Roho Mtakatifu anaingia ndani ya maisha ya
mtu?.......(Pale mtu anapokubali kumpokea Yesu Kristo kuwa bwana
na mwaozi katika maisha yake)
Kuutoka katika swali la 7:
Tumejifunza kuwa Roho Mtakatifu ni mtu ambaye ana sifa kama zile
alizonazo Mungu na Yesu Kristo. Hebu taja zile sifa tatu tulizozitaja
walati tunajadili katika somo hili…..(Maarifa yote, uzima
wa milele, na mpaji wa uzima)
Mmoja na anayeishi Mungu wetu wa mbinguni, muumbaji wa mbingu na
dunia, alimtuma Roho wake Mtakatifu ili aweze kuingia ndani yetupale
tunapompokea, anaigia kama zawadi ambayo Mungu anatupatia kwa ajili
ya wokovu. Tunapomalizia tunaweza kumshuru Mungu kwa kutupa Roho
Mtakatifu ambaye anatulinda.
Juma lijalo,somo 2 inatutamburisha katika juma la kujisomea biblia,kila
siku,soma mstari wa biblia katika biblia yako au kitabu cha biblia
ambacho kinakuja na masomo haya.biblia inaeleza sana kuhusu Roho
mtakatifu na inajibu maswari mawili,tambua mambo mapya uliyojifunza
kuhusu Mungu,katika kulasa ya mwisho.
MAOMBI
Baba yetu uliye mbinguni, asante kwa Roho wako Mtakatifu. Tusaidie
sisi kumsikia rohoo Mtakatifu anapoongea nasi. Hatuwezi kusikia
kila kitu tuliyoyaongea leo, lakini tunajua ya kuwa kitu ambacho
tunatakiwa kujua sisi sota ni kuamini. Tusaidie sisi kujifunza nini
kile tunachotakiwa kujua tutakapoendelea kujifunza na kusoma somo
linalofuata wiki hii. Tunaomba katika jina la Yesu …….
AMEN
|