MWONGOZO UTAKAOTUONGOZA KATIKA KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA
YA STONECROFT.
LENGO:
Kuwafikia: Masomo haya yanatuwezesha
kupata njia ya kushirikiana kujua wokovu wa Yesu Kristo na watu
wengine.kwa wale ambao wana makundi wanaombwa kualika marafiki
zao, famila, wafanya kazi wenzao na pia majirani zao.
Uanafunzi: Wakristo wapya na wale
waliokomaa wanaweza kusoma saaana kuhusu MUNGU na kuweza kukua
naye katika uhusiano uliomzuri. Msomo haya yanatufundisha pia
jinsi gani unaweza kutupia kanuni za kiBiblia katika mazingira
ya kila siku.
UPEKEE:
Nini kinachofanya masomo ya stonecroft kuwa wa kipekee
sana kuliko masomo mengine ya kiBiblia katika soko la mafundisho
ya Biblia?
• Habari njema ya agano jipya: masomo haya
yameundwa katika mtindo wa kutumia agano jipya kwa sababu kurasa
zimewekwa katika vifungu vile unavyotakiwa kuvitafuta ndani ya
Biblia ili kuweka urahisi kwa wasomaji wa masomo haya. Kurasa
hizi zilizowekwa katika vifungu hivyo vimetoka katika Biblia ya
toleo la 4 good news new testament. na tafsiri hizi zinakubaliwa
sana na watu mbalimbali katika madhehebu tofauti tofauti.
• Masomo haya yameandikwa katika kwa mfumo
ambao ni rahisi wa kwamba hata Yule ambaye ni mara yake ya kwanza
kutumia Biblia basi anaweza kuyatumia vizuri tu. Na haya masomo
yanaweza kutafsiriwa kwa urahisi tu sana katika ulimwengu mzima
kwa kutumia lugha yeyote ile.
• Kiongozi ni mwezeshaji tu na sio mwalimu
wa Biblia.
VIFAA:
Masomo ya stonecroft ya kiBiblia ni rahisi sana
kusoma.
Maelezo kwa kiongozi yamefungiwa katika mistari
iliyowekewa nukta nukta. Kwa hiyo hayatakiwi kusomwa kwa sauti.
Maelezo mengine yameandikwa yakiwa ndani ya viboksi
yapo katika kitabu kile cha kujisomea au cha kusoma. Sehemu hii
inatakiwa kusomwa kwa sauti na wale wahisika wenyewe yaani wanafunzi
wa mmasomo haya.
Ukionna nukta zimeongozana namna hii (…..)
inaonyeshs ya kwamba kiongozi inatakiwa aruhusu kundi ili kuweza
kushiriki kwa kujibu maswali, kusma mistari ya Biblia, au kujadili
maada husika.
KABLA YA MASOMO :
Vitu vichache vya muhimu:
• Uhakikiwe kuwa wewe ni kiongozi wa stonecroft
kwa kukamilisha mchakato wa maombi katika Stonecroft.
• Soma malengo, na maelekezo ya masomo haya
husika.
• Pata vifaa mbalimbali utakavyo taka kwa
ajili ya masomo yako kutoka katika huduma hii ya Stonecroft _
(800) 525-8627.
• Vifaa vinavyohitajika katika mafunzo haya
ni :
a. Vitabu vya kujifunzia
b. Mwongozo
c. Kadi za taarifa
• Tafuta sehemu nzuri kwa ajili ya kujifunzia.
Kuwa na muda wa kujifunza ukiwa upo nyumbani, ofisini, kwenye
migahawa na katika sehemu mbalimbali.
KUJIANDAA KWA AJILI YA KUJIFUNZA:
• Maliza somo kwa kukamilisha kuandika majibu
yako kkatika kitabu chako cha kujifunzia ,kabla ya kusomo mwongozo.
Hii itakusaidiakatika kujua na kuelewa mafkirio yaw engine na
jinsi ambavyo majibu yako uliyoyajibu yapo.
• Fanya mazoezi ya kusoma kwa sauti kama inawezekana.
Pigia mstari maneno na vifungu ambavyo vitakusaidia katika kuelezea
mbele ya kundi lako. Kumbuka muda ambao unatakiwa kwa ajili ya
kusoma ujumbe wako, hii itakusaidia katika kujua muda gan uliobaki
wa majadiliano katika kipindi hicho.
• Thibitisha mahali, muda na ulinzi wa watoto
kama kutakuwa na uwezekano wa kufanya hivyo.
• Waombee wote wale ambao watakuwa wakihudhuria
katika masomo kujifunza.
WAKATI WA KUJIFUNZA/ WAKATI WA MASOMO:
Gawa vitabu vya kujifunzia na agano jipya na pia
kusanya malipo. Kusanya mapato au malipo na rudisha vile vitabu
vilivyobaki wakati ulikuwa unagawa.
Anza kipindi kwa maombi. Kukiwa na mtu yeyote anayeuliza,
utamruhusu kuwa aandike swali lake nyuma ya kitabu chake sehemu
ya maombi (prayer request page) ili iwe kama kumbukumbu yay ale
maombi ya katikati ya wiki. Kama swali lililoulizwa linataikiwa
kjibiwa kwa wakati huo liambatanishe na kulijibu wakati unaanza
kipindi.
Kumbuka kuwa katika kipindi cha awali yaani cha
kwanza, kila mtu ataandika majibu katika kitabu chake ha kujifunzia
wakati wa kujifunza, au wakati wa masomo. Hamasiha makundi yote
kusoma kabla ya kuonana ili kuweka kumbukumbu ya somo hilo.
Soma na uwakilishe taarifa katika kitabu kile cha
mwongozo kwa njia ya kujadiliana, hapo ukiwa unawaangalia kwa
sana wanafunzi wanachokifanya. Jifunze na soma na makundi yaliyopo;
hutakiwi kuwa wewe ndio mjuaji sana wa Biblia.
Kiongozi anaseti toni na kasi ya kujifunza
kwa:
• Kuanza na kumaliza kwa wakati uliopangwa.
• Kutumia mwongozo na Biblia kama vitabu vya kurejea. Vifaa
vingine havitakiwi ambavyo havina maana yeyote katika kipindi
hicho.
• Kuhamasiha kila mtu katika kushiriki katika majadiliano
na kuangalia kuwa hakuna mtu anayetawala kundi kwa kuzunumza yeye
peke yake.
• Kuweka hisia kwa Yesu Kristo, iswe kisiasa, au kimaandishi,
au katika mambo ya kijamii. Kumbuka kuwa mabo ya kisiasa, mambo
ya kijamii yote haya yana mazingira yake ya kuweza kuyaelezea.
Mara zote angalia wale ambao wako ndani ya kundi
hilo unalowafundisha ambao hao ndio watakuwa viongozi wazuri kwa
masomo ya baadae.
Kama kiongozi, kuwa wa mfano kwa wale unaowaangoza.
Kataza watu kuzungumza vitu sirini, mbali na kundi lenyewe husika,
omba pamoja nao na uwahamasishe katika kutafuta ushauri mzuri
wa ki Mungu.
Waulize wahusika wenyewe yaani wanafunzi katika
kufikiria ni watu gani ambao wanaweza kuwaalika kwenye masomo
mengine. Wahamasishe katika kuwaombea watu wengine kwa majina
yao.
VITU MUHIMU VYA KUKUMBUSHA:
Kama huwezi kuongoza masomo kwa sababu yeyote ile,
kama kuna mtu anayeweza kufanya hiyo kazi vizuri basi anaweza
kufanya hiyo kazi badala yako.
Kwa taarifa zaidi kuhusu taratibu, vifaa, au au
jinsi gani uanaweza kuongoza wasiliana nasi kupitia stonecroft
bible studies at (800) 525-8627.
“Kesheni, simameni kimara katika
imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke
katika upendo”
1 Wakorintho 16:13-14
UTANGULIZI
ROHO MTAKATIFU YUKO WAPI?
Watu wengi wanaweza kuzungumzia maisha ya Kikristo
katika njia tofauti tofauti, kwamba kuna mambo amabayo ya naweza
kubadilika badilika. Wanafurahia muda ule wanapokuwa karibu na
Mungu, lakini wanashindwa kujizuia mara zote hasa wakati wa mateso
au wakati wanapopitia magumu.
Jonathan Edwards, ambaye anajulikana kuwa ni mwanatheolojia
mkubwa sana huko marekani, alisema kuwa, maisha ya mkristo sio
mwendelezo wa mawazo yaliyo juu ya mlima. Lakini ni kuishi na
uwazi wa Mungu, na uwepo wawake nyumbani, shuleni, katika sehemu
za kazi, kanisani, na katika jamii. Ni kuwa na Mungu katika maisha
yetu.
Hicho ndicho ambacho masomo haya ya Biblia yanajiusisha
nayo. Tunataka kumjua Roho matakatifu katika ma isha yetu kila
siku. Juu ya yote, kama ingewezekana kuishi maisha ya Kikristo
sisi wenyewe, Munu asingeweza kutupatia Roho Mtakatifu katika
maisha yetu. Ni nguvu zake na uwezo wake ambao unaongeza uwezo
wa kuwa naye bila tatizo lolote lile.
Hatumtumii Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu anatutumia sisi.
Roho Mtakatifu yuko wapi? Anaishi na anafanya kazi na pia anaishi
ndani ya wale wote wanaomwamini Yesu Kristo. Uendelee kufurahia
uwepo wake ndani ya maisha yako.
Lucille Fern Sollenberge.
The Guide has her
own Guidebook to help her lead and guide the lesson.