uct >>stonecroft
>> mwanamitindo wa kiafrika
Mwanamitindo wa Kiafrika:
Huu mfumo wa kiafrica wa ambao ni wa
kugawanya na kuzidisha ni muhimu kuliko wa kuongeza!
1. Mfumo huu utaanzishwa kwanza Tanzania kupitia, "Africa
Training Bible School" (ATBS) ambao lengo lao la kwanza ni
kuwa funza wachungaji kutoka makanisa 280 ambao wamo katika mpango
wa ATBS ili wajiunge na masomo ya kibiblia ya Stonecroft. Watafundishwa
kwa kupitia video na ktabu cha kiafrica cha kufundishia, hawa wachungaji
watakuwa viongozi wa kwanza wa Stonecroft Tanzania, na Bwana akipenda
kila mmoja wao atapatiwa kitabu ca utatu 10 - Mungu yukoje? 10 -
Yesu ni nai? na 10 - Je Roho mtakatifu yuko wapi? Na kitabu ambacho
kimejumuisha vitabu vyo hivi vitatu.
2. Hawa wachungaji watachukua taarifa hii na kwenda nayo katika
vijiji vyao ambao nao watachagua mwanamke mmoja, labda kiongozi
wa kinamama, na baada ya hapo atamfundisha huyu mama,na mchungaji
atabaki kuwa mwangalizi wakufuatilia kazi inaendaje tu.
3. Watapatiwa kitabu cha mwongozo cha Stonecroft na vitabu 10 vya
Stonecroft ‘Mungu anaonekanaje?’ vyote hivi vimetafsiriwa
katika lugha yake anayo ielewa,na atapewa vitabu vingine 10, naye
atatafuta wenzake 5 katika kanisa ili waanze kujifunza.
Na hawa 5 nao walete mmoja kila mmoja wao, katika huduma ya Stonecroft,
na wataanza kujifunza utatu, ‘Mungu anaonekanaje?’ baada
ya hapo ataendelea na "Yesu ni nani?” Na atahitimisha
na "Roho mtakatifu yuko wapi?" Na atatumia videa na kitabu
kuwafundisha ili nao wakawafikie wengine.
4. Na akifikia hapo atakuwa kiongozi wa wenzake hao 5. Na atakacho
kifanya ni kurudia masomo ya Stonecroft kwa wanawake watano wengine
tena kanisani hawa watano wa sasa watatiwa moyo kuwaletwa watu wasio
okoka kanisani, sasa ataanza kuwafikia wasio fikiwa.
5. Mchungaji kwa wakati huu atakuwa ni mtu wa kutoa ushauri na
mwangalizi.
6. Hawa viongozi wapya 5 pamoja na mwana maombi wao,watamtafuta
mtu mmoja kanisani au kijijini ambaye ana sifa za kuwa kiongozi,
wamfundishe kwa ruhusa ya mchungaji wao.
7. Kwa pamoja hawa wakina mama 5 watawasihi wasio mwamini Mungu
wajiunge na masomo ya Stone croft,ya utatu, kwa kawaida kila mmoja
awe na wakina mama 2, kumbuka masomo haya yawe na wakina mama10
- 12 women.
8. Wakisha kujifunza masomo haya ya utatu basi huyu mwangalizi
atawafundisha wakina mama 2, mmoja toka kanisani kwake na mwingine
kanisa jingine ambao watakuwa viongozi wa Stonecraft wa kizazi cha
nne. Wana maombi wake watabaki na darasa hili katika kulifundisha.
9. Mtindo huu utandelea katika kanisa ambalo limejifunza mkakati
huu.
10. Iwapo kuna swali ambalo huyu kiongozi hawezi kulijibu basi
amuhusishe mwangalizi wake.
11. Kwa kadri muda unavyo zidi kuendelea tutapata waangalizi wengi
zaidi kwa kadri mtandao huu unavyozidi kutanuka na video nyingi
sana zitatengenezwa.
12. Kumbuka - kugawa na kuzidisha !
13. Kuzidisha ni bora kuliko kuongeza!
‘Uwe macho, Simama imara katika imani,
Uwe jasiri,uwe mwenye nguvu. Fanya kazi zote kwa upendo ’
1 Corinthians 16: 13 – 14
|