Project Hope     home >>vijana wa stonecroft>> maelekezo kwa mwongozo >> wakati wa kujifunza
Wakati Wa Kujifunza
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

KABLA YA MAFUNZO YA BIBLIA:

Vitu muhimu –

Unaweza ukawa kiongozi uliye thibitishwa na Stonecroft wetu kwa kujaza fomu iliyo tafsiriwa kwa Kiswahili.

Tunataka kujiridhisha kuwa baada ya kusoma kanuni na sheria pamoja na maelezo yetu ya imani, huna wasiwasi tena nasi.

Vitu vinavyo hitajika katika kujisomea:

1. Vitabu vya utangulizi vya utatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili vinaweza patikana ,katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

2. Vitabu vya mwongozo vinapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

3. Biblia ya Kiswahili inapatika 'Tanzania Bible Society', na madukani.

4. Je unaweza kuamini hili? Nacho kimetafsiriwa kwa Kiswahili kinapatikana katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

5 Kadi ya maelezo nayo imetafsiliwa inapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.

6. Fomu ya maombi ya kiongozi nayo inapatika katika makao makuu ATBS, Mbeya, Tanzania.

Tafuta eneo zuli kwa ajili ya kujisomea biblia, labda nyumbani, kanisani, shuleni, nyumbani katika kivuli chini ya mti.

MAANDALIZI YA KIONGOZI KABLA YA MASOMO:

Hakikisha unajibu maswali yote ya kijitabu cha mwongozo kabla ya kuanza kusoma vitabu, hii itakuwezesha kuelewa watakao kuwa na wajibu wanapitia katika wakati gani kabla ya kupata majibu halisi.

• Fanya zoezi la kusoma hayo masomo kwa sauti, ikiwezekana,pigia msitali maneno muhimu utakayo ongelea katika kundi lako, masomo hayo yasizidi saa moja na nusu1 – 1 1/2 hasa pale ambapo masomo haya yanaendeshwa katika kuwezesha wakina mamam yani 'Mpango wa Uwezeshaji Wanawake Afrika' (MUWA) maana wanawake watahitaji kuondoka na kuanza kujifunza kushona.

• Wakati huo huo wanafunzi wa MUWA wanapofurahi masomo yao,watoto wao watakuwa wakihudhulia 'Powerclub' wakijifunza njia za Mungu kupitia 'Kids in Ministry International' (KIMI) pamoja na watoto wengine kutoka katika mkakati wa 'Kids Evangelism Explosion' (Kids EE)..

Maeneo haya kwa wakatio huu yatakuwa;
Tanzania – Africa Training Bible School (ATBS) – Mbeya, Tanzania.
Uganda – Hope Community Centre, Kampala, Uganda.
Malawi – Africa Training Bible School (ATBS) – Uluwa and Vulwa, Malawi.

• Omba juu ya wale watakao kuwa wanakuja.

WAKATI WA KUJIFUNZA:
Gawa vitabu vya kujifunzia na agano jipya na pia kusanya malipo. Kusanya mapato au malipo na rudisha vile vitabu vilivyobaki wakati ulikuwa unagawa.

Anza kipindi kwa maombi. Kukiwa na mtu yeyote anayeuliza, utamruhusu kuwa aandike swali lake nyuma ya kitabu chake sehemu ya maombi (prayer request page) ili iwe kama kumbukumbu yay ale maombi ya katikati ya wiki. Kama swali lililoulizwa linataikiwa kjibiwa kwa wakati huo liambatanishe na kulijibu wakati unaanza kipindi.

Kumbuka kuwa katika kipindi cha awali yaani cha kwanza, kila mtu ataandika majibu katika kitabu chake ha kujifunzia wakati wa kujifunza, au wakati wa masomo. Hamasiha makundi yote kusoma kabla ya kuonana ili kuweka kumbukumbu ya somo hilo.

Soma na uwakilishe taarifa katika kitabu kile cha mwongozo kwa njia ya kujadiliana, hapo ukiwa unawaangalia kwa sana wanafunzi wanachokifanya. Jifunze na soma na makundi yaliyopo; hutakiwi kuwa wewe ndio mjuaji sana wa Biblia.

Kiongozi anaseti toni na kasi ya kujifunza kwa:
• Kuanza na kumaliza kwa wakati uliopangwa.
• Kutumia mwongozo na Biblia kama vitabu vya kurejea. Vifaa vingine havitakiwi ambavyo havina maana yeyote katika kipindi hicho.
• Kuhamasiha kila mtu katika kushiriki katika majadiliano na kuangalia kuwa hakuna mtu anayetawala kundi kwa kuzunumza yeye peke yake.
• Kuweka hisia kwa Yesu Kristo, iswe kisiasa, au kimaandishi, au katika mambo ya kijamii.

Kumbuka kuwa mabo ya kisiasa, mambo ya kijamii yote haya yana mazingira yake ya kuweza kuyaelezea.

Mara zote angalia wale ambao wako ndani ya kundi hilo unalowafundisha ambao hao ndio watakuwa viongozi wazuri kwa masomo ya baadae.

Kama kiongozi, kuwa wa mfano kwa wale unaowaangoza. Kataza watu kuzungumza vitu sirini, mbali na kundi lenyewe husika, omba pamoja nao na uwahamasishe katika kutafuta ushauri mzuri wa kiMungu.

Waulize wahusika wenyewe yaani wanafunzi katika kufikiria ni watu gani ambao wanaweza kuwaalika kwenye masomo mengine. Wahamasishe katika kuwaombea watu wengine kwa majina yao.

VITU MUHIMU VYA KUKUMBUSHA:
Kama huwezi kuongoza masomo kwa sababu yeyote ile, kama kuna mtu anayeweza kufanya hiyo kazi vizuri basi anaweza kufanya hiyo kazi badala yako.
Kwa taarifa zaidi kuhusu taratibu, vifaa, au au jinsi gani uanaweza kuongoza wasiliana nasi kupitia stonecroft bible studies at (800) 525-8627.

“Kesheni, simameni kimara katika imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo”
1 Wakorintho 16:13-14.

 
     
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us