home >>stonecroft>>mwongoo
utakaotuongoza
Stonecroft Mwongoo Utakaotuongoza
MWONGOZO UTAKAOTUONGOZA KATIKA
KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA
YA STONECROFT
LENGO:
KUWAFIKIA: Masomo haya yanatuwezesha kupata njia ya kushirikiana
kujua wokovu wa Yesu Kristo na watu wengine.kwa wale ambao wana
makundi wanaombwa kualika marafiki zao, famila, wafanya kazi wenzao
na pia majirani zao.
Uanafunzi: Wakristo wapya na wale waliokomaa wanaweza
kusoma saaana kuhusu MUNGU na kuweza kukua naye katika uhusiano
uliomzuri. Msomo haya yanatufundisha pia jinsi gani unaweza kutupia
kanuni za kiBiblia katika mazingira ya kila siku.
UPEKEE:
Nini kinachofanya masomo ya stonecroft kuwa wa kipekee sana kuliko
masomo mengine ya kiBiblia katika soko la mafundisho ya Biblia?
• Habari njema ya agano jipya: masomo haya
yameundwa katika mtindo wa kutumia agano jipya kwa sababu kurasa
zimewekwa katika vifungu vile unavyotakiwa kuvitafuta ndani ya
Biblia ili kuweka urahisi kwa wasomaji wa masomo haya. Kurasa
hizi zilizowekwa katika vifungu hivyo vimetoka katika Biblia ya
toleo na tafsiri hizi zinakubaliwa sana na watu mbalimbali katika
madhehebu tofauti tofauti.
• Masomo haya yameandikwa katika kwa mfumo ambao ni rahisi
wa kwamba hata Yule ambaye ni mara yake ya kwanza kutumia Biblia
basi anaweza kuyatumia vizuri tu. Na haya masomo yanaweza kutafsiriwa
kwa urahisi tu sana katika ulimwengu mzima kwa kutumia lugha yeyote
ile.
• Kiongozi ni mwezeshaji tu na sio mwalimu wa Biblia.
VIFAA:
Masomo ya stonecroft ya kiBiblia ni rahisi sana kusoma.
Maelezo kwa kiongozi yamefungiwa katika mistari
iliyowekewa nukta nukta. Kwa hiyo hayatakiwi kusomwa kwa sauti.
Maelezo mengine yameandikwa yakiwa ndani ya viboksi
yapo katika kitabu kile cha kujisomea au cha kusoma. Sehemu hii
inatakiwa kusomwa kwa sauti na wale wahisika wenyewe yaani wanafunzi
wa mmasomo haya.
Ukionna nukta zimeongozana namna hii (…..)
inaonyeshs ya kwamba kiongozi inatakiwa aruhusu kundi ili kuweza
kushiriki kwa kujibu maswali, kusma mistari ya Biblia, au kujadili
maada husika.
KABLA YA MASOMO :
Vitu vichache vya muhimu:
• Uhakikiwe kuwa wewe ni kiongozi wa stonecroft kwa kukamilisha
mchakato wa maombi katika Stonecroft.
• Soma malengo, na maelekezo ya masomo haya husika.
• Pata vifaa mbalimbali utakavyo taka kwa ajili ya masomo
yako kutoka katika huduma hii ya Stonecroft _ (800) 525-8627.
• Vifaa vinavyohitajika katika mafunzo haya ni :
- Vitabu vya kujifunzia
- Mwongozo
- Kadi za taarifa
• Tafuta sehemu nzuri kwa ajili ya kujifunzia. Kuwa na muda
wa kujifunza ukiwa upo nyumbani, ofisini, kwenye migahawa na katika
sehemu mbalimbali.
KUJIANDAA KWA AJILI YA KUJIFUNZA:
• Maliza somo kwa kukamilisha kuandika majibu yako kkatika
kitabu chako cha kujifunzia ,kabla ya kusomo mwongozo. Hii itakusaidiakatika
kujua na kuelewa mafkirio yaw engine na jinsi ambavyo majibu yako
uliyoyajibu yapo.
• Fanya mazoezi ya kusoma kwa sauti kama inawezekana. Pigia
mstari maneno na vifungu ambavyo vitakusaidia katika kuelezea
mbele ya kundi lako. Kumbuka muda ambao unatakiwa kwa ajili ya
kusoma ujumbe wako, hii itakusaidia katika kujua muda gan uliobaki
wa majadiliano katika kipindi hicho.
• Thibitisha mahali, muda na ulinzi wa watoto kama kutakuwa
na uwezekano wa kufanya hivyo.
• Waombee wote wale ambao watakuwa wakihudhuria katika masomo
kujifunza.
WAKATI WA KUJIFUNZA/ WAKATI WA MASOMO:
Gawa vitabu vya kujifunzia na agano jipya na pia kusanya malipo.
Kusanya mapato au malipo na rudisha vile vitabu vilivyobaki wakati
ulikuwa unagawa.
Anza kipindi kwa maombi. Kukiwa na mtu yeyote anayeuliza,
utamruhusu kuwa aandike swali lake nyuma ya kitabu chake sehemu
ya maombi ili iwe kama kumbukumbu yay ale maombi ya katikati ya
wiki. Kama swali lililoulizwa linataikiwa kjibiwa kwa wakati huo
liambatanishe na kulijibu wakati unaanza kipindi.
Kumbuka kuwa katika kipindi cha awali yaani cha
kwanza, kila mtu ataandika majibu katika kitabu chake ha kujifunzia
wakati wa kujifunza, au wakati wa masomo. Hamasiha makundi yote
kusoma kabla ya kuonana ili kuweka kumbukumbu ya somo hilo.
Soma na uwakilishe taarifa katika kitabu kile cha
mwongozo kwa njia ya kujadiliana, hapo ukiwa unawaangalia kwa
sana wanafunzi wanachokifanya. Jifunze na soma na makundi yaliyopo;
hutakiwi kuwa wewe ndio mjuaji sana wa Biblia.
Kiongozi anaseti toni na kasi ya kujifunza
kwa:
• Kuanza na kumaliza kwa wakati uliopangwa.
• Kutumia mwongozo na Biblia kama vitabu vya kurejea. Vifaa
vingine havitakiwi ambavyo havina maana yeyote katika kipindi
hicho.
• Kuhamasiha kila mtu katika kushiriki katika majadiliano
na kuangalia kuwa hakuna mtu anayetawala kundi kwa kuzunumza yeye
peke yake.
• Kuweka hisia kwa Yesu Kristo, iswe kisiasa, au kimaandishi,
au katika mambo ya kijamii. Kumbuka kuwa mabo ya kisiasa, mambo
ya kijamii yote haya yana mazingira yake ya kuweza kuyaelezea.
Mara zote angalia wale ambao wako ndani ya kundi
hilo unalowafundisha ambao hao ndio watakuwa viongozi wazuri kwa
masomo ya baadae.
Kama kiongozi, kuwa wa mfano kwa wale unaowaangoza.
Kataza watu kuzungumza vitu sirini, mbali na kundi lenyewe husika,
omba pamoja nao na uwahamasishe katika kutafuta ushauri mzuri
wa kiMungu.
Waulize wahusika wenyewe yaani wanafunzi katika
kufikiria ni watu gani ambao wanaweza kuwaalika kwenye masomo
mengine. Wahamasishe katika kuwaombea watu wengine kwa majina
yao.
VITU MUHIMU VYA KUKUMBUSHA:
Kama huwezi kuongoza masomo kwa sababu yeyote ile, kama kuna mtu
anayeweza kufanya hiyo kazi vizuri basi anaweza kufanya hiyo kazi
badala yako.
Kwa taarifa zaidi kuhusu taratibu, vifaa, au au jinsi gani uanaweza
kuongoza wasiliana nasi kupitia stonecroft bible studies at (800)
525-8627.
“Kesheni, simameni kimara katika
imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. Mambo yenu yote na yatendeke
katika upendo”
1 Wakorintho 16:13-14.
Bibliography
Enns, Paul, The Moody Handbook of Theology. Chicago:
Moody Press, 1989.
Eerdmans, Wm. B., Eerdmans’ Handbook to Christian
Belief. Grand Rapids: WM. B. Eerdmans Publishing Co., 1982.
Elwell, Walter, A., Evangelical Dictionary of Theology.
Grand Rapids: Baker Book House, 1996.
Harrison, Everett F., Editor and Chief, Baker’s
Dictionary of Theology. Grand Rapids: Baker Book House, 1960.
Hodge, Charles, Systematic Theology. Grand Rapids:
Baker Book House, 1992.
McDowell, Josh. Evidence That Demands a Verdict.
Arrowhead Springs, CA: Campus Crusade for Christ, International,
1972.
Moody.November-December, 1998. Chicago: Moody Bible
Institute, 1998.
New Geneva Study Bible, Nashville: Thomas Nelson
Publishers, 1995.
Packer, J.I., Knowing God. Downers Grove, IL: InterVarsity
Press, 1973, 1993.
Ryrie, Charles C., Basic Theology. Wheaton: Victor
Books, 1986.
Sproul, R.C., Pleasing God. Wheaton: Tyndale House
Publishers, 1988.
Tozer, A.W., The Knowledge of the Holy—The
Attributes of God: Their Meaning in the Christian Life. New York:
Harper Collins Publisher, 1961.
Willmington, H.L., Willmington’s Guide to
the Bible. Wheaton: Tyndale House, 1986
|