home >>vijana wa stonecroft>> yesy ni nani?
Yesy ni nani?
Utangulizi
YESU NI NANI? YEYE NI MTU WA AJABU SANA NA ANAISHI.
Unajua nini kuhusu yesu? Masomo haya ndio yatajadili kuhusu haya
yote kama-
Kujua kuwa yesu kiuhalisia ni nani,
Kwa nini alikuja duniani,
Ujio wake una uhusiano gani na sisi, na
Pia kujjua kama tutamuona tena Yesu .
Tunafikia hatua ya kumjua mungu kupitia kile alichokifanya yesu
kwetu kipindi alipokuja hapa duniani. Kuwa na uhusiano wa karibu
sana na mungu, ni vizuri kwanza kujua kuhusu yesu mwenyewe. Kwa
sababu hiyo inapaswa kujua kuwa yesu ni nani? Kuwa wa kwanza kusoma
mpangilio huu: Yesu ni nani? Mungu yukoje? Na Roho mtakatifu
yuko wapi?
Unapoendelea kujifunza kuhusu yesu, mwana wa Mungu, unaweza ukamjua
yeye kwelikweli na kukubaliana na kile alichojia ulimwenguni kukileta.
Mungu akubariki sana kwa upya na ufunuo mkubwa sana ulioupata kupitia
mwana wake na mwokozi wetu, Yesu Kristo.
“Lakini hizi zimeandikwa ili mmpate
kuamini ya kwamba yesu ndiye kristo, mwana wa Mungu; na kwa kuamini
mwe na uzima kwa jina lake”
Yohana 20:31
Lucille Fern Sollenberger
Huduma
ya Stonecroft
www.stonecroft.org
Toleo la rejeo
Lucille Sollenberger,BS,M.A
Kimechapishwa na huduma ya Stonecroft
Stonecroft Ministries, Inc.
Office Location: 10561 Barkley, Suite 500,
Overland Park, KS 66212
Phone: 1.800.525.8627
FAX: 816.763.5565
E-mail: connections@stonecroft.org
JINSI YA KUJIFUNZA MASOMO YA BIBLIA KATIKA
STONECROFT.
Kwa sababu hii ni shule ya biblia, lengo letu kuu
ni kujifunza kile ambacho biblia inasema na jinsi gani tunaweza
kutumia katika maisha yetu. Kijitabu hiki na biblia ndivyo vitakuwa
vitabu vyetu ambavyo tutavitumia katika masomo yetu.
Inatakiwa tujiandae kwa somo kwa kumaliza maswali
katika vijitabu vyetu hivi vya awali. Hii itatusaidia katika majadiliano
yetu ya wiki kufanya kwa urahisi na kuelewa vizuri kuhusiana na
somo husika kwa wakati huo. Tutajifunza somo la kwanza sote kwa
pamoja.
Masomo yetu haya ya biblia yataanza katika muda muafaka
na yatachukua muda wa dakika 60 mpka 90. Tutaondoka pale ambapo
somo letu husika tunalolisoma litakapokuwa limefikia mwisho kwa
hiyo hatutaacha kitu tutamaliza.
Kwa sababu tunatoka katika mazingira tofauti tofauti
na (ukijumuishatunatoka katika makanisa tofauti tofauti) kwa hiyo
tutaheshimu mawazo ya kila mtu na imani yake.
Katika wiki chache, tungependa kuanza masomo mapya ya biblia katika
maeneo mapya na kwa watu wapya. Hebu fikiria mtu ambaye ungependa
umwalike katika masomo haya.
Katika kitabu chako cha kusoma.
Katika kila mwisho wa somo kuna maandishi yanasomeka
hivi “Vitu ninavyotaka kukumbuka kutoka katika somo”.
Kwa kuanza na somo la pili, mistari imependekezwa
kwa ajili ya kusoma kipindi cha wikendi. Hii itakiusaidia wewe kujiandaa
na somo husika.
Masomo mengine ya ziada ambayo yanaweza kukusaidia
yapo nyuma ya hiki kitatabu. Appendices inakupa taarifa nzuri sana
kuhusu tipiki ambazo zimeshasomwa katika masomo haya ya biblia.
Kwa hiyo hata hapa katika ukurasa huu ni sehemu ya kuweka rekodi
ya mambi yako. Kama ungependa katika kuweka nyongeza ya kusoma biblia,
kwa hiyo rekodi agano jipya itakusaidia kuweka kumbukumbu katika
zile sura ambazo umeshazisoma.
|