Project Hope     home >>stonecroft>> yesu ni nani? >> somo 1
Yesu ni nani? - Somo #1
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

Biblia inasemaje kuhusu Yesu?

Download Swahili Lesson #1 Student Study Book

Download Swahili Lesson #1 Bible Verses Handbook

Yesy ni nani?
Sauli, huyu alikuwa ni myahudi ambaye alikuwa anawafunga na kuwatesa wakrito wa awali, aliuliza swali la muhimu na zuri sana. Kiukweli na kwamba ni swali ambalo ni la muhimu sana na ambapo tunaweza hata sisi wenyewe tunaweza kujiuliza. Aliuliza, “wewe ni nani, Bwana?”

Alipokea jibu kwa haraka sana :
“Naye akasema mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe.……” (Matendo 9:5)

Wakati huu mtu (aliyeinua havoic katika kanis ala kwanza la yerusalemu) alipata taarifa taarifa sahihi, na aliweza kubadilika. Alikuwa anasukumwa na imani potofu. Alifikiri kuwa alikuwa anamfurahisha Mungu kwa Matendo yake mabaya lakini ukweli ni kwamba alikua anamkasirisha sana Mungu.

Nasi tunafanya vivyo hivyo, hasa pale tunapoamini vitu ambavyo ni vya uongo. Tunafanya vitu ambayo ni hatari kwetu sisi wenyewe na hata kwa watu wengine. Njia pekee ya kuwa na taarifa ambazo ni nzuri na za kumpendeza Mungu ni kugundua na kuamini kweli.

Kujifunza Biblia kutasaidia katika kujua taarifa ambazo ni za kweli. Kwa hiyo Biblia yenyewe ndio chanzo cha kweli yote, amabalo ni neno la Mungu ambalo ndio kweli yenyewe. Neno la Mungu linasema hivi

“mbingu nan chi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Mathayo 24:35

Neno la Mungu ni kweli na litasimama milele.

Watu wengi wana mitazamo tofauti sana kuhusu Yesu. Hii inatokana na kwamaba tabia zetu zinasukumwa na kile tunachokiamini, ni kweli kuwa tuna taarifa nzuri sana kuhusu Yesu kuwa ni nani, na Mungu yukoje na sisi kuwa tukoje. Tukimaliza kusoma somo hili utajua kuhusu Yesu zaidi na kiuhalisia.

Unaamini kuwa Yesu ni nani? Leo hii tunasikia mawazo tofauti tofauti kuhusu Yesu kuwa ni nani. Wengine wanasema kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa dini…… wengine wanasema kuwa yeye ndio kiongozi mkubwa sana wa waKristo….. wengine wana sema ni mwalimu wa maadili… wengine husema ndiye mtu katika karne ya kwanza aliyefanyiwa ukatili.
Tutaweza kupata ukweli woote pale tutakapo amini taarifa sahihi Kutoka katika chanzo sahihi. Kuna chanzo kimoja tu ambacho ambacho ni MUNGU. Mungu ametupatia kitabu , ambacho kinatuambia sisi jinsi ya kujua yeye na jinsi ya kuishi maisha ambayo yanapendeza yeye na sisi pia.

Yesu siyo tu kuwa ni kiongozi mkuu wa dini katika ulimwengu. Pia sio tu kuwa ni mtu mkubwa sana katika Biblia kama Abraham, musa, au mfalme Daudi. Mara nyingi huwa tunaandika tarehe na mwaka ,pia tunatambua kuwa miaka 2000 iliyopita Yesu Kristo alikuja duniani na alieneza historia katika njia kuu mbili. K.B –Kabla ya Kristo na B.K – Baada ya Kristo.

Biblioa inatumbia vitu vingi sana na tena vya kushangaza kuhusiana na Yesu Kristo. Kwa mfano Yesu alikuwepo tangu mwanzo hata kabla ya muda kuwepo. Sehemu mbalimbali ndani ya bbilia zinazungumzia kuiwa Yesu alikuwepo kabla ya mbingu na nchi kuumbwa. Biblia inaema

“ naye amekuwako kabla ya vitu vyote,
na vitu vyote hushikana katika yeye.”
Wakolosai 1:17

Jesus existed before He was born as a man. He has always existed and will live forever. No other religious leader everclaimed to be eternatl, but Jesus did, He said,

“… Before Abraham was born, ‘I Am’.”

John 8:58

Yesu alikuwepo hata kabla hazaliwa kama mwanadamu wa kawaida. BIKO lilikuwa ni jina la MUNGU.

Katika kitabu cha Kutoka 3:14, miaka 2000 kabala Yesu hajazaliwa, MUNGUalijidhihirisha mwenyewe kwa musa kwamba “ MIMI NIKO AMBAYE NIKO”. Kwa waebrania hili jina linamaanisha kuendelea kuwepo.

Pia Yesu naye alisema sawasawa na Mungu katika (Yohana 5:18).

Kugundua ukweli

Fikiri vizuri na uombe sana kuhusiana na hili somo unalosoma.
Hebu ujiulize wewe mwenyewe haya maswali matatu:

Je kifungu hiki katika Biblia kinasemaje?
Gundua ukweli wa Mungu.

Je kifungu hiki cha Biblia kinamaanisha nini?
Elewe kile Mungu anachokisema.

Je Mungu anasemaje kuhususiana na mimi mwenyewe?
Tumia huo ukweli ulioupata ndani ya kusoma katika maisha yako.

Jinsi utakavyoomba ndiko kutasababisha Mungu akuangalie jinsi utakavyoweza kujibu.Je utatii amri au utabadili mtazamo wako.

Injili

Vitabu vya kwanza kabisa katika agano jipya havikuandikwa kuwa viweze kuelezea wasifu wa Yesu. Viliandikwa na watu tofauti tofauti na vikundi tofauti tofauti vya watu na kwa sababu malimbali. Hivi vitabu vine vya mwanzo katika agano jipya ni vitabu vya injili.

Vitabu viwili yaani injili ya Mathayo na injili ya Yohana viliandikwa na watu wawili ambao walitembea na Yesu kwa miaka mitatu. Walikuwa ni sehemu ya wale wanafunzi kumi na mbili ambao Yesu aliwachagua kama mitume.

Mathayo aliandika injili ya Mathayo ili kuwashawishi wayahudi kwamba Yesu ndiye alikuwa messia aliyeahidiwa kuja ambaye wao wayahudi walikuwa wakimngojea.

Yohana aliandika injili ya Yohana ili kuwashawishi viongozi wake kuwa Yesu alikuwa kweli ni mwana wa Mungu.

Katika injili ya Marko ambapo injili hii iliandikwa na kijana mdogo sana ambaye jina lake aliitwa Marko, ambaye alifanya kazi kama mmisionari na Paulo, Barnabas, na mtume Petro. Marko aliwaandikia mataifa kuwaambia kuhusu Yesu na nini Yesu alichokifanya.

Injili ya Luka iliandikwa na dactari wa kigiriki ambaye yeye alifanya utafiti na aliwauliza baadhi ya watu ambao walikuwa wanamjua Yesu.

Kwa sababu kila injili iliandikwa navikundi tofauti tofauti vya watu, kwa hiyo kila waandishi hao wameelezea vipengele vya maisha ya Yesu Kristo.

1. Yohana alisema nini mwisho wa injili yake?
Yohana 21:25

_________________________________________________

2. Je ni majina gani ambayo Yesu aliitwa katika kitabu cha Mathayo?
a) Mathayo 1:21
_________________________________________________

_________________________________________________

b)Mathayo 1:23

_________________________________________________

_________________________________________________

c)Mathayo 3:17

_________________________________________________

_________________________________________________

d)Mathayo 12:8

_________________________________________________

_________________________________________________

e)Mathayo 16:16

_________________________________________________

_________________________________________________

f)Mathayo 19:16

_________________________________________________

_________________________________________________


3. Yesu aliitwaje katika vitabu hivi vifuatavyo?
a. Marko 5:6-7
_________________________________________________

b. Luka 5:5
_________________________________________________

c.Yohana 1: 35-36
_________________________________________________

d. Yohana 1:49
__________________________________________________

e. 1 Korintho 1:6-7
_________________________________________________

Josephus (Joh-SEE-fus), mwanahistoria wa uyahudi aliyezaliwa mwaka A.D 37, amabaye alikuwa sio mwamini, alitupa ukweli kuhusu kusuluiwa kwa Yesu Kristo. Ingawa Josephus hakuwa anaamini kuwa Yesu ndiye messiah, aliandika taarifa zifuatazo kuhusiana na Yesu;

“Sasa, kulikuwa muda kama huu Yesu, mtu mwenye busara, ingekuwa halali hata kumwita mtu, kwani alikuwa anafanya kazi nyingi za ajabu, na mwalimu anayefundisha kweli na unaipokea kwa furaha. Aliweza kuwa pamoja na wayahudi hata mataifa pia wasio wayahudi. Alikuwa ni Kristo, hata pale pilato alipo amua kumhukumu kwa kuangikwa msalabani, kwa wale waliompenda tangu mwanzo hawakuweza kumuacha , na pia akawatokea siku ya tatu tangu alipokufa kwa sababu utabili ulitakiwa kutimia maana aliwaambia ya kuwa siku ya tatu baada ya kufa atafufuka na aliwwambia kuhusu vitu vingi sana vya ajabu kuhusiana nay eye mwenyewe. Na ukoo wa kiKristo ambao uliitwa jina hilo nay eye mwenyewe hauko tena leo hii."

- Antiquities

Unabii mchache kati ya mwingi kuhusu messiah.

 
 
Unabii
Kutimia kwa unabii
Atazaliwa kwa mwanamke bikira.
Isaya 7:14 (742 B.C).
Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanaume, naye atamwita jina lake Immanuel.
Yesu anazaliwa Kutoka kwa mwanamke bikira.
Mathayo 1:22-23.
Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, tazama, bikira atachukua mimba, naye atazaa mwana; nao watamwita jina lake Immanuel yaani Mungu pamoja nasi.
Eneo atakapozaliwa.
Mika 5:2 (710 B.C)
Bwana anasema “ Ewe Bethlehemu efrata uliye mdogop kuwa miongoni mwa elfu za yuda; Kutoka kwako wewe utanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.”
Yesu anazaliwa bethlehemu.
Mathayo 2:1a
Yesu alipozaliwa katika bethlehemu ya uyahudi zamani za mfalme Herode.
Atakataliwa na watu wake.
Isaya 53:3 (712 B.C)
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Yesu alikataliwa.
Yohana 1:11
Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
Usaliti.
Zaburi 41:9 (1062 B.C)
Msiri wangu tena niliyemtumaini, aliyekula chakula change, ameniinulia kisigino chake.
Yesu alisalitiwa.
Marko 14:10
Yuda iskariote, Yule mmoja katrika wale thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani apate kumsaliti kwao
Atafufuka Kutoka kwa wafu
Zaburi 16:10 (1040 B.C)
Maana hatukuachia kuzimu nafsi yangu, wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
Yesu alifufuka Kutoka katika wafu baada ya siku tatu Kutoka kaburini.
Mathayo 28:5-6
Malaika akajibu akawaambia wale wanawake, msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliYesulubiwa, 6 hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.

4. Maneno na marejeo yafuatayo ya vitabu yanazungumzia vizuri kuhusu Yesu. Angalia maswali haya ambayo yanajitosheleza na uonisha na maneno yatokayo katika vitabu vya mrejeo ya Biblia .
a. Ukoo wake
b. Ubatizo wake
c. Muujiza wake wa kwanza.

________________ Mathayo 1:1-17.
________________ Yohana 2:1-11.
________________ Marko 1:9-11.

“Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana,
mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote….”

Wakolosai 1:15

Maombi
Asante Mungu, nimejifunza sana kuhusu Yesu katika somo hili. Namba Mungu unifundishe zaidi ninapoendelea na masomo haya. Naomba unisaidie kupata muda wa kuweza kufika wiki ijayo kwa ajili ya kuendelea kujifunza. Ninaomba katika jina la Yesu Kristo. AMEN.

Maelezo

_________________________________________________

_________________________________________________

This is a translation of Who is Jesus? Stonecroft's Students Study Book Lesson #1 in Swahili, the English version of Who is Jesus? is available online from Stonecroft's website.

Download Swahili Lesson #1 Student Study Book

Download Swahili Lesson #1 Bible Verses Handbook

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Guidebook Introduction

Lesson #1 Swahili Guidebook (To be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #1

YESY NI NANI?

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us