home >>vijana wa stonecroft>>
Vijana wa Stonecroft
Karibu katika masomo ya kiafrica ya biblia ya Stonecroft, maelezo
haya yanatokana na mtandao wa Stonecroft kwa ruhusa kutoka kwao
ili kutengeneza huu mwongozo ili utumike katika kufundishia Africa,
katika kitabu hiki mambo ya kitamaduni yamezingatiwa ili kuhakikisha
kuwa kinakubarika katika mazingira ya kiafrica na nchi zake.
Stonecroft ni shirika la kimataifa ambalo haliko chini ya kanisa
lolote.
MAELEZO YA KIUTUME YA STONECROFT:
Utume wa shirika la Stonecroft ni kuwezesha wakina mama ili nao
waweze kufikia jamii kwa kupitia injili ya Yesu Kristo, Kumuinua
Yesu na kuhakikisha kuwa Yesu anatukuzwa kwa kuhubiri injili ya
wokovu .
MAONO YA STONECROFT:
Ni kutoa mwongozo wa kimataifa katika kuwafikia wakina mama kwa
ajili ya Yesu, Stonecroft inawawezesha na kuwatia moyo wakina mama
ili wamuhubiri Yesu.
Uinjilist ndilo lengo letu kuu—Msingi wa kila jitihada za
huduma. Utume wetu ni kuwafikia wanawake wa kila umri, na kila kabila
kwa ajili ya injili ya Yesu Kristo.
Maombi ndio msingi wa kila jambo tunalo tunalotenda, Yesu alisema,
”Pasipo mimi, hamuwezi kufanya lolote” (Yohana
15:5).
Kumtegemea Mungu, Kutafuta mwongozo wake na Baraka,ni muhimu, uanafunzi
ni nyenzo muhimu katika uinjilisti, mwanamke anakuwa mfuasi wa Yesu,
wakati huo huo huduma ya Stonecroft inatoa nyenzo za kumuwezesha
huyu mwanamke kukua katika imani, na baada ya hapo ili aweze kuwaongoza
wengine kufuata na kuwa na mawasiliano na Yesu.
Kuwawezesha wanawake ndio msingi wa stonecroft,kuwasaidia ili waweze
kugundua vipawa Mungu alivyo viweka katika maisha yao.kuwawezesha
ili wawe viongozi makini, ambao wanaleta mabadiliko katika nyumba
zao, vijiji, jamii, na hata nchi zao na mwisho kabisa dunia nzima.
Lengo la stonecroft na masomo yake ya biblia ni uanafunzi na uinjilisti,
haya ni masomo rahisi ambayo mtu anaweza akajifunza katika makundi
madogo dogo, ili kuwatia moyo katika ukuaji wa kiroho.
Stonecroft inahubiri injili kwa kuwafikia wanawake dunia nzima.Zaidi
ya watu 25,000 ambao ni watu wa kujitolea wa Stonecroft wanafanya
kazi ya kuwafikia wanawake dunia nzima.
Watu wa kujitolea katika Nchi ya marekani na nchi nyingine zaidi
ya 30 wanatumia vitabu vya stonecroft, ili kuhubiri injili.
Kwa zaidi ya miaka 75 Stonecrift wamekuwa wakitegemea maombi katika
kueneza injili.
HISTORIA YA STONECROFT:
Kufikia leo hii,huduma ya Stonecroft inawafikia maelfu ya watu dunia
nzima kila mwaka, lakini historia ya Stonecroft ilianza na mwanamke
mmoja aitwaye— Helen Duff Baugh – mwanamke aliye na
imani isio teteleka, mwanamke wa Maombi, mwanamke ambaye aliguswa
sana na maisha yaw engine.
Kuanza hapo mwaka 1938, makundi kama hayo ya kiamama wafanyao
biashara yalianzishwa nnchi nzima, mnamo1948, Binti Mary E. Clark,
Mwanamke aliyekuwa mfanya biashara hapo kale na mmishenari, aliamua
kuitikia wito wa Mungu na kujiunga Mama Baugh katika kumsaidia kwenye
huduma yake ya uinjilisti ambayo ilikuwa inakuwa kwa haraka sana.
Katika mwaka 1952, Mungu kwa neema yake aliweza kuwapatia Jengo
katika mji wa Kansas,Missouri, ambapo hapo ndipo palikuwa ofisi
zao za kitaifa, Jengo hilo likaitwa Stonecroft, likiwa na maana
ya “Nyumba ya Mwamba”. Hii ilikuwa ni ukumbusho kuwa
Yesu Kristo ni Mwamba na ni jiwe kuu la msingi.
Kwa zaidi ya mika 70, Mungu kwa uaminifu amekuwa akilinda,kuwapatia
mahitaji yao, na kuongoza huduma ya Stonecroft, katika tamaduni
inayo badirika haraka sana, mambo mawili ni muhimu sana, kujitoa
kwetu katika maombi na Uinjilisti.
Stonecroft kwa sasa wamehamia ofisi ndogo maana ofisi zao za mwanzo
wameuza ili pesa za ziada wapate kuzipeleka katika uinjilisti.
UONGOZI WA STONECROFT:
Viongozi wa Stonecroft wanafanya majukumu yao katika ofisi ya kitaifa
na hata kazi ambazo ziko mbali na hapo.
Lorraine Potter Kalal: Raisi
Lorraine Potter Kalal Huduma yake iliyo jawa na mafanikio, Pamoja
na upendo wake wa Stonecroft na maono na historia, Yeye kama raisi
hujiona kuwa ndie Mtumwa mkubwa, Lorrain anahitaji kuona kuwa huduma
ya Stonecroft ikimtegemea Mungu ili kukamilisha mahitaji yote.
Doris Thompson anawasaidia wanawake kufikia maono
yao na mawazo yao katika matendo, akiwa kama makamu wa Raisi, Doris
anataka kuwafikia wanawake wengi zaidi katika ulimwengu huu,na anawasaidia
wanawake wengi kupitia Stonecroft, na anawasaidia wale wanao jitolea
kuwafikia wengine katika maeneo mengi zaidi. Anafanya kazi ya kuibadiri
Stonecroft ili iweze kuwafikia watu walio katika maeneo mapya zaidi,
Pia kuna watu wengi zaidi katika uongozi ambao hamuwezi kuwa na
mawasiliano nao.
Huduma ya Stonecroft inatamani kuwaunganisha wanawake kwa Mungu
na kwa wanawake wenzake na katika jamii zao.
Stonecroft inawatia moyo wanawake,kuwa na mawasiliano na wenzao
na hata katika jamii zao, na pia kuwaalika katika masomo ya biblia
katika vijiji vyao na miji yao.
Haya masomo ni rahisi kuyafuata, na pia ni makundi yanayo leta
uzima wa kiroho katika maeneo mkakati wa muda mrefu katika maisha
ya waumini.
Hili toleo la kiafrica litaleta matokeo mawili tofauti,la kwanza
ni mkakati wa Stonecroft wa kuwafikia wasio fikiwa, na la pili ni
mkakati wa Stonecroft wa masomo ya kibiblia.katika madarasa ya kujisomea
biblia, mwongozo wa vitabu vya Stonecroft utatungwa ili kuwa na
vikundi vya kujisomea biblia na kuwafikia wasio fikiwa, wasio amini
na wanao amini, watatiwa moyo ili wajiunge katika makundi haya .makundi
haya yataundwa na wanawake ambao wamemaliza kujisomea vitabu vya
“Utatu” lakini hawajafikia kiwango cha kuongoza lakini
wanataka kuendelea kujisomea, hili litawezesha ukuwaji na kutanuka
kwa stonecroft katika bara la Africa.
Huduma ya Stonecroft inaelewa na kushukuru huduma ya mwanamke mmoja,
ukimfikia mwanamke nae akakokoka basi umeweza kuifikia jamii, mume
wake, watoto, marafiki, majirani, na anao fanya nao kazi.
Askofu David Akondowi, ambaye ni muwakilishi wa United Caribbean
Trust’s (UCT) Tanzania na muasisi wa mafunzo ya wachungaji
katika chuo kitwacho Training Bible School (ATBS) na mchungaji wa
House of Freedom – Tanzania, ambapo UCT wana mradi wa kuwawezesha
wanawake uitwao ‘Women's Empowerment Sewing Project’
yeye anazungumzia juu ya mithari ya Kiswahili isemayo, ’Ukimuwezesha
mwanamke umeiwezesha jamii’."
Stonecroft wanawawezesha wanawake ili waweze kufikia jamii zao
ki ukamilifu.
MAELEZO YA IMANI YA STONECROFT:
• Huduma ya Stonecroft inaamini katika utendaji wa kiroho,na
uvuvio wa neno la Mungu,na tunaamini kuwa biblia haina kosa, inafaa
kwa mafundisho na ndio yenye maamuzi ya mwisho na usemi wa mwisho.
• Tunaamini katika utatu wa Mungu – yani Mungu baba,
Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu;
• Tunaamini katika utu wa Mungu; Utu na uungu ya Yesu (Yesu
na Mungu ni Mtu mmoja, Yesu Kristo ni Mungu aliyekuwa katika mwili)
aliyezaliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu na mtu aliyekuwa bikra,
yeye ni Mungu halisi na ni Mwanadamu halisi, na ni utu wa Roho mtakatifu.
• Tunaamini katika ufufuo wa Yesu kristo,—kuwa mwili
wake ulifufuliwa kutoka katika wafu,sawasawa na maandiko, na pia
akapaa kwenda mbinguni na kuketi katika mkono wa kuume wa Mungu
baba kama wakili wa waamini.
• Tunaamini katika hali ya dhambi ya mwanadamu—kuwa
kila mwanadamu anazaliwa na asili ya dhambi, na hawawezi kujiokoa
wenyewe bali wanamuhitaji mkombozi ili awaokoe kutoka dhambini;
• Tunaamini katika utakaso—Kuwa Yesu alifanyika kuwa
dhambi pale alipotoa dhabihu ambayo ni damu yake mwenyewe ili dunia
nzima wapate msamaha wa dhambi.
• Tunaamni katia umuhimu wa kuzaliwa upya—wokovu ni
kwa neema .kwa imani.na sio kwa matendo, imani iokoayo itaimalisha
matendo mema katika maisha yetu.
• Tunaamini katika ufufuo halisi wa mwili wa waaminio na wasio
amini.
• Tunaamini katika Baraka za umilele kwa walio amini na adhabu
ya milele kwa wasio amini.
• Tunaamini katika uinjilisti wa dunia nzima,—Agizo
kuu la Mungu ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo kwa watu wote wa
kila rika.
• Tunaamini juu ya ujio wa mara ya ili wa Yesu sawa sawa na
maandiko.
MASOMO YA BIBLIA YA STONECROFT:
Karibu katika masomo ya kibiblia ya Stonecroft, tunajitahidi kumpatia
kila mmoja neno la Mungu haijalishi ana kiwango gani katika safari
hii ya Kiroho.
Ni maombi yetu kuwa masomo haya yatatoa fursa kwako ili upate kuwezeshwa
na neno la Mungu ili uweze kuifikia jamii yako na injili ya Yesu
Kristo.
MTAZAMO:
Masomo ya biblia ya stonecroft yaliandaliwa kwa msingi wa kufuatilia
mikutano ya kuwafikia wasio fikiwa, lakini kwa sasa masomo haya
yamekuwa mpaka kuwafikiwa magerezani na makanisani, maofisini, na
maeneo mengine.
SIFA MUHIMU:
Masomo ya biblia ya Stonecroft yameandaliwa ili kufanya uinjilisti
na uanafunzi, na injili hii imejumuishwa maeneo yote ambayo Stonecroft
inafanya kazi.
Kila somo limeandaliwa maalum kabisa ili wale ambao hawamjui Mungu
nao wapate kushiriki,kwa bahati mbaya wanawake wa Africa sio wote
walio na biblia na ndio maan kulasa za biblia zimetolewa na kuacha
vipengele vya biblia tu ili kuwawezesha nao kushiriki vizuri.na
hii imeandaliwa katika mpangilio maalum wa kimatukio.
Masomo ya biblia ya Stonecroft yanaendeshwa katika nyumba, maeneo
ya kazi, makanisani, mashuleni, hata chini ya mti katika vivuri
huku Africa.
Masomo haya yameandaliwa katika, kufundisha juu ya kichwa furani
cha somo lakini hata hivyo masomo yanayo husu vitabu vya biblia
yanapatikana katika hatua ya juu.
Masomo ya biblia ya Stonecroft ni rahisi kujisomea katika makundi
madogo na hata makundi makubwa, na masomo haya yanaanzia (4-14 masomo).na
utatu masomo 6 kwa hiyo kitabu kimoja kna masomo 18.
Masomo mengi yanakuwa na kitabu cha mwongozo wa masomo, kitabu
hiki hutumika pamoja na biblia na kila anae shiriki masomo haya
Majadiliano ni njia mojawapo katika ukuaji wa kiroho.
USHAURI WA KUJISOMEA:
Katika maeneo mengi ya Stonecroft washiriki hutumia kitabu cha mwongozo
na biblia ya Kiswahili, ambayo hupatikana madukani, lakini kama
nilivyosema kitabu cha mkononi cha biblia kinapatikana kwa wale
wasio na biblia.
Vikundi hivi vya kujisomea hukutana mara moja kwa wiki, kwa dakika
60-90 .kama dakika ni chache kundi wanaweza kuamua kugawa masomo
haya nusu, kwa kugawana maswali na kusoma andiko.ili kutanua kazi
ya uanafunzi tunashauri kuwa vikundi lazima vitafute njia za kuongeza
washiliki ili ufanisi wake uonekane katika jamii.
MAELEZO YA MASOMO:
Kuna aina tatu za masomo ya biblia ya Stonecroft:
•Masomo ya Utangulizi wa utatu.
• Masomo ya wakristo wanao kuwa.
• Na masomo yahusuyo vichwa vya somo.
Stonecroft waanze na somo la Utangulizi, ambalo linasema “Yesu
ni nani” Mungu yukoje?’ na Je Roho mtakatifu yuko wapi.haya
ni masomo muhimu sana kwa wakristo wapya na hata wale wa zamani
maana ni muhimu hata kwa wale wanao taka majibu ya maswali yao.
Haya masomo yote yamekwisha tafsiliwa Kiswahili na kazi bado inaendela
ya kutafsiri huko Congo na Malawi pia.
KANUNI NA SHERIA ZA MASOMO YA KIBIBLIA YA STONECROFT
Huduma ya Stonecroft imejiwekea kanuni kwa jili ya masomo yake ya
kibiblia, ni muhimu kwa mtu yeyote anae hudumu katika huduma hii
ya Stonecroft afuate hizosheria na kanuni
Injili ya Yesu ambayo imeandikwa katika kila somo la Stonecroft
ni muhimu kuwa ihunbiriwe kwa uhakika na umakini mkubwa.
Huduma ya Stonecroft hawana msimamo mwingine wa imani, au msimamo
wa kisiasa nje ya maelezo yao ya imani.
Wote ambao wanajihusisha na Stonecroft watafanya haya yafuatayo:
• Kukubariana na msingi wa imani ya huduma ya Stonecroft.
• Kutenda kazi kwa ushiriano na kanisa lako.
• Kila neno litakalo nenwa katika mjadala au mazungumzo wakati
wa masomo huo sio msiomamo wetu kama huduma ya Stonecroft.
Katika kujisomea haya masomo ya biblia ya Stonecroft, ni muhimu
wahusika wote wakatumia vitabu ambavyo vimethibitishwa na Sonecroft,
katika somo la utangulizi inashauliwa kuwa wahusika wote watumie
aina moja ya biblia ya Kiswahili.
Watu wote ambao watakuwa wanaisimamia au kuongoza haya masomo ya
kibiblia ya Stonecroft ni lazima watume maombi,waongozaji na wakufunzi
hufundishwa na kiongozi wa eneo husika, video ya masomo hayo imekwisha
andaliwa na Stonecroft Barbados ili kuwezesha kuwafunza wale watu
ambao wako Tanzania, Malawi, Uganda na nchi nyingine za Kiafrica,hii
video ya dakika 15 itarecodiwa kwa Kiswahili na lugha nyingine za
kiafrika, hii yote ni katika kuhakikisha kuwa tunawafunza wale ambao
watakuwa viongozi, ukiambatanisha na Mwongozo hii itawapa uwezo
mkubwa katika huduma.
MKAKATI WA MWONGOZO WA KUFUNZA:
Kazi ya huyu mwongozaji ni kuongoza masomo haya ya kibiblia,na
wakati huo huo washiliki watakuwa na muda wakuleta mabadiliko katika
jamii ya kuwaleta watu kwa Yesu, katika kundi hilo pia wanaweza
kuona ni nani anafaa kuanzisha kundi jingine la kujisomea biblia,
hii ni baada ya kumaliza vitabu vyote vya utatu.
Masomo ya kibiblia ya Stonecroft na mwongozo wake:
• Kuwaombea wote ambao wanakuja katika masomo ya kibiblia.
• Anza masomo haya ya biblia kwa maombi.
• Kiongozi wa masomo haya ya kiungozi, ambaye atampa majukumu
ya kusimamia kikundi husika lakini yeye ataendela kupewa taarifa.
• Huyu kiongozi atahakikisha kuwa anafuata kanuni na sheria
za huduma ya huduma ya Stonecroft kwa kufuata maelekezo yaliyoko
katika video.
• Anandaa kundi lake kwa kupitia kitabu cha mwongozo, atawakumbusha
wana kikundi juu ya umuhimu wa siri katika kundi na kundi kuelekrza
maswali yao katika maandiko.
• Masomo ya kibiblia ya Stonecroft pamoja na mwongozo wake
unatoa fursa kwa wanakikundi kuielewa vizuri huduma ya Stonecroft,
na nafasi za kujiunga nao.
• Atateua watu ambao watajaribu kupata majibu ya maswari yahusuyo
imani, majadiliano yanhimizwa juu ya nini biblia inasema na sio
nini makanisa yetu yanasema au kufundisha.
• Atahakikisha anakwepa majadiliano yote yahusuyo imani na
misimamo ya watu, siasa, kanisa lipi linapinga au kukubali.
SIFA ZA KUWA KIONGOZI
1. Kiongozi lazima awe kaokoka.
2. Awe ni mtu anae itanga nguvu ya mabadiliko kupitia neno.
3. Akubaliane na sheria na kanuni za Stonecroft.
4. Anawasiliana na kufanya kazi na wenzake.
5. Ana shauku ya kuona watu wanakuwa katika maisha yao ya kiroho
na kumjua Mungu.
JINSI YA KUMHOJI MTU AMBAYE UNADHANI ANAWEZA AKAWA KIONGOZI.
KUMCHAGUA KIONGOZI
Wachungaji (kutoka Africa Training Bible School) ambao walifunzwa
kuwa viongozi watawatambua viongozi hao kiurahisi, kwa kuomba, kwa
hekima, na watoke katika makanisa yao, hawa baada kuwateuwa hao
viongozi, watawezesha katika ukuaji na kutanuka kwa masomo ya ka
kibiblia ya Stonecroft.
Ni muhimu sana katika kumtafuta Yule kiongozi atakae kuwa na sifa
zitakazo endana na sifa zilizotajwa katika sehemu hii.
Maelezo yafuatayo ni muhimu sana unapotaka kumteua kiongozi.
Omba kabla hujaonana na mtu husika, omba ili Bwana awapeni nyote
hekima Roho ya kupambanua .
1. Pangeni muda, muwe tayari kukubaliana juu ya masomo ya kibiblia
ya Stonecroft na huduma.(ikihitajika).
2. Kwa yale maeneo tu ambayo yameolodheshwa katika fomu ya maombi
ya Stonecroft.
o Toa maelezo juu ya huduma ya Stonecroft—mwelekezeke akasome:
• Kijitabu cha masomo ya biblia cha Stonecroft.
• Tembelea mtandao www.stonecroft.org kwa maelezo zaidi.
o Mwambie akupatoe ushuhuda wake wa kumwanini Yesu tu katika wokovu
wake na akupe maandiko ya biblia.
o Muulize je anaweza akajibu nini iwapo ataulizwa Yesu ni nani .
o Muulize kwanini anataka kujiunga na masomo ya kibiblia ya Stonecroft
.
o Chunguza juu ya utayari wake wa kufanya kazi na watu, wa imani
tofauti na tamaduni tofauti
o Muulize juu ya mambo mengine anayo yafanya, na pia anafurahishwa
na nini katika kusoma neon na kuwaongoza wengine katika kujisomea
biblia.
o Hakikisha anazielewa sheria na kanuni za Stonecroft na imani.
Mtu yeyote anaetarajia kuwa kiongozi lazima aelewe Kanuni na sheria
za Stonecroft, na mwongoz wake.
Majukumu ya mchungaji ambaye atakuwa Coordinator (Muunganishaji)
Uwe umekwisha pata fomu ya maombi ya mtu anaye taka kuwa kiongozi.
Kwa umakini wa hali ya juu soma fomu ya maiombi na hakikisha kuwa
ushuhuda wa kiongozi uko sahihi.
Kwa maombi unapaswa kumuuliza huyo mtu maswali machache kuhusiana
na Yesu, kwa mfano.
1. “Ninashauku ya kusikia safari yako na Mungu, hivi Yesu
ana nafasi gani?
2. Iwapo mshiriki wa Stonecroft kakuuliza kuwa anawezaje kuwa na
uhusiano na Yesu utajibu nini?
3. Unaelewa nini kuhusu injili na unawezaje kuihubiri?
Unaweza ukataka kusoma kupitia hili neon je unaweza amini?
Kitabu na mwongozo.
Panga muda wa kumfundisha muhusika kama kiongozi, tumia nyenzo
zifuatazo.
Kitabu cha kibiblia cha Stonecroft cha Africa.
Iwapo hajawahi kukisoma kitabu cha Sonetabu kama “Yesu ni
nani”ili wapate kuelewa ni kitu gani kinahusika katika haya
masomo.
Mchungaji au mkurugenzi atakuwa na fomu za maombi katika faili
lake.
Kumbuka kwamba sio kila mtu yuko tayari kwa ajili ya kuongoza,ukihisi
kuwa huyo mtu hawezi akaepukana na mambo yanayoweza kuleta mkanganyiko
kama vile siasa na mambo mengine ya kijamii ,basi mtie moyo kuwa
yeye asiwe kiongozi bali abaki kama mshiriki tu, wa hicho kikundi.
Baada ya kumaliza haya mafunzo ya uongozi wasiliana na kiongozi
wa Stonecroft wa Africa kwa barua pepe na mawasiliano mengine ya
ziada.
Kiongozi wa Stonecroft wa kijimbo ambaye ni Mchungaji David Akondowe,
atawasiliana na huduma ya Stonecroft ya Marekani, anaweza akafanya
hivi kwa barua pepe: connections@stonecroft.org.
Atuma anuani ya kiongozi iliyo kamili, namba ya simu, na barua
pepe.
Nao Stonecroft wakisha pokea hayo maelezo watamkaribisha huyo kiongozi
mpya kwa barua pepe, ambayo itatafsiriwa katika lugha ya eneo husika,
na kuanzanzia hapo huyu kiongozi ataunganishwa katika mtandao wa
watu wakujitolea na anaweza kunza kupikea barua na majarida katika
barua pepe.na anaweza kutembelea mtandao wa viongozi, na kujipatia
mambo mengi ya kujisomea katia mtandao wa Stonecroft Ministries
website. (www.stonecroft.org)
Hawa viongozi wapya watatambuliwa kama viongozi kwani tunatambua
mchango wa kila mmoja wetu katika kazi hii muhimu ya kuufikia ulimwengu
na injili ya Yesu.
KUWAWEZESHA VIONGOZI WA STONECROFT:
Walimu waliofunzwa vizuri ni muhimu sana katika hii kazi ya kuwafundisha
watu katika imanina hata wale ambao wako katika masomo ya kibiblia
kwa miaka mingi.
Hawa viongozi wengi hutuma majarida mara kwa maana ili kuwa na
mawasiliano na watu,hata mawasiliano ya kuhusu kongamano iwapo wapo
katika Skype, na mawasiliano mengine ya mtandao wa kijamii.
Hawa wakurugeni waandae mikutanio ambayo wanaweza kukutana na viongozi
hawa kwa mwaka mara moja ili watiane moyo na kuweshana ili Stonecroft
ipate kusonga mbele.
Mambo mengi yana shuhudiwa katika mawasiliano, kuwa na maono mamoja,
na kujifunza kwa pamoja,na namna ya kujibu maswali magumu.
Kuwafundisha walimu wapya kunaweza kupangwa katika kipindi maalum
kama vile, muda wa Krismass, na likizo nyingine.
Haya ni mawazo muhimu iwapo unajipanga kuwa na mafunzo ya viongozi:
• Muda maalum kwa ajili ya maombi na ushirika na Mungu.
• Changamoto ya maandiko au maombi.na kuwatia moyo;
• Utangulizi na kushuhudia matokea chanya ya kujisomea biblia.
Muda wa kujifunza: i.e. namna unavyo shuhudia inasadia kuongeza
namna ya kuwafikia wengine, kuanzisha Stonecroft katika makanisa,na
huu uwe muda wa kujifunza kutoka hata wkwa wengine, tuwe na kiongozi
ambae anaelezea namna anavyo waalika wengine, matatizo waliyo kutana
nayo.na eneo lipi walimwona Mungu akiwatetea. Hitimisha kwa maombi
na kuwatia moyo.
MWONGOZO KWA KIONGOZI:
DHUMUNI:
Kuwafikia wasio fikiwa – haya masomo yanawezesha kuhubiri
wokovu kwa kupitia Yesu,
Tunataka kutanua huduma ya Stonecroft kupitia makanisa 280 ambayo
yana wanafunzi wake katika chuo cha ‘Africa Training Bible
School’ (ATBS) katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na
DR Congo na pia kupitia Hope Community Centre, Kampala, Uganda.
Pia tunamwamini Mungu tunaweza kujumuisha haya kupitia mradi ule
wa kuwezesha wanawake
‘Stonecroft Women’s Empowerment Program’ (SWEP)
ambao mtajifunza mengi hapo baadae. Mradi huu wa kuwawezesha wanawake
utatumia vitabu vya Stonecroft kuanzia vile vijitabu vya utatu,
Mungu yukoje? Yesu ni nani? na Roho Mtakatifu yuko wapi?
Katika kuhakikisha kuwa tunaukuza mradi wa SWEP mafunnzo ya kiafrica,
hawa wanawake watahimizwa kuwa viongozi, watatumia Video ya mafunzo
ya kiafrica, na pia kitabu hiki ambacho kitawawezesha kuanzisha,
Stonecroft katika nyumba zao, makanisa na hata vijiji vyao, kwa
kupata ruhusa maalum kutka kwa mchungaji wao.
Uanafunzi – wakristo wapya na hata wale wa kale wanaweza
kijifunza habari za Yesu na kuweza kuwa na mahusiano ya karibu na
Mungu, masomo haya yanatufundisha namna ya kutumia biblia katika
mazingira yetu ya kila siku, kuna vitabu vingi ambavyo navyo vitatafsiliwa
katika lugha nyingine. ‘Africa Training Bible School’
watatumia masomo haya kama nyenzo moja wapo za kufundishia katika
mitahara yao. Kwa mfano, maisha mapya, kuishi maisha yangu, wafilipi,
Yakobo, Warumi na vingine vingi.
UFAUTI:
Fautisha masomo ya kibiblia ya Stonecroft na masomo mengine ya biblia?
• Masomo haya yameandaliwa mahususi ili yatumike katika agano
jipya ambalo linapatikana sana katika nchi ya Tanzania, lengo kuu
ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo, na kuwatia moyo watu ili wapate
kujisomea maandiko kila siku, hatujajumuisha namba ya kila ukulasa
katika biblia maana wengine wanaweza wasiwe na biblia.
• Masomo haya ni rahisi hata kw wale ambao ndio wanaanza kujisomea.
• Kumbuka kuwa kiongozi sio mwalimu wa biblia lakini wote
wanasoma pamoja na washiriki wa kikundi.
.
NYENZO:
Masomo ya kibiblia ya Stonecroft hisi kuyasoma.
Kuna maeneo ambayo yamefungiwa ambayo hupaswi kuyasoma kwa sauti.
Maneno yaliyo chapishwa katika boksi unapaswa kuyasoma kwa sauti
ili washiriki wapate kusikia.
Kwa mfano nucta zikifululiza (.....) inakwambia kuwa kiongozi awaruhusu
washiriki wachangie kwa kuuliza maswali, kusoma biblia au kujadili
somo.
Ukiona wino umekolezwa unao ambatana na nucta Tano, ina maanisha
mstari wa biblia usome kwa sauti kubwa na msomaji.
Ikiwa kama kifungu kilicho nukuliwa kimeandikwwa katika maandishi
ya kawaida ina maana, hakihitaji majibu au ni kirefu sana kusoma
hadhatrani.
KABLA YA MASOMO YA BIBLIA
Vitu muhimu –
Unaweza ukawa kiongozi uliye thibitishwa na Stonecroft wetu kwa
kujaza fomu iliyo tafsiriwa kwa Kiswahili.
Tunataka kujiridhisha kuwa baada ya kusoma kanuni na sheria pamoja
na maelezo yetu ya imani, huna wasiwasi tena nasi.
Vitu vinavyo hitajika katika kujisomea:
1. Vitabu vya utangulizi vya utatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili vinaweza patikana, katika makao makuu ya ATBS, Mbeya,
Tanzania.
2. Vitabu vya mwongozo vinapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya,
Tanzania.
3. Biblia ya Kiswahili inapatika Tanzania Bible Society.na madukani.
4. Je unaweza kuamini hili? Nacho kimetafsiriwa kwa Kiswahili kinapatikana
katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.
5. Kadi ya maelezo nayo imetafsiliwa inapatikana makao makuu ya
ATBS, Mbeya, Tanzania.
6. Fomu ya maombi ya kiongozi nayo inapatika katika makao makuu
ATBS, Mbeya, Tanzania
Tafuta eneo zuli kwa ajili ya kujisomea biblia, labda nyumbani,
kanisani, shuleni, nyumbani katika kivuli chini ya mti.
MAANDALIZI YA KIONGOZI KABLA YA MASOMO:
Hakikisha unajibu maswali yote ya kijitabu cha mwongozo kabla ya
kuanza kusoma vitabu, hii itakuwezesha kuelewa watakao kuwa na wajibu
wanapitia katika wakati gani kabla ya kupata majibu halisi.
• Fanya zoezi la kusoma hayo masomo kwa sauti,ikiwezekana,pigia
msitali maneno muhimu utakayo ongelea katika kundi lako,masomo hayo
yasizidi saa moja na nusu1 – 1 1/2 hasa pale ambapo masomo
haya yanaendeshwa katika kuwezesha wakina mamam yani ‘Stonecroft
Women’s Empowerment Program’ (SWEP) maana wanawake watahitaji
kuondoka na kuanza kujifunza kushona
• Wakati huo huo wanafunzi wa SWEP wanapofurahi masomo yao,watoto
wao watakuwa wakihudhulia “Powerclub” wakijifunza njia
za Mungu kupitia ‘Kids in Ministry International’ (KIMI)
pamoja na watoto wengine kutoka katika mkakati wa ‘Kids Evangelism
Explosion’. (Kids EE)
• Maeneo haya kwa wakatio huu yatakuwa;
Tanzania – Africa Training Bible School (ATBS) – Mbeya
Tanzania
Uganda – Hope Community Centre, Kampala
Malawi – Africa Training Bible School (ATBS) – Uluwa
and Vulwa, Malawi
• Omba juu ya wale watakao kuwa wanakuja.
WAKATI WA MASOMO:
Mara zote anza masomo haya kwa maombi, ikiwa kama kuna mtu ana hoja
basi kundi liandike hiyo hoja yake na mtaiombea katikati mwa juma.
Ikiwa kama hitaji lake ni maombi ya dhalula basi yajumuishwe siku
hiyo hiyo.
Kumbuka kila mara uanzapo somo la “Yesu ni nani” kila
mshiriki ataandika jibu lake katika kijitabu cha kujisomea, na uwakumbushe
kuwa ni vizuri wakawa wanajaza majibu kabla ya kuja darasani.
Soma na kuwapatia washiliki maelezo katika mtindo wa uwazi huku
ukiwangalia usoni, Kiongozi huwa najifunza na kusoma na kundi lote
la washiriki, hutakiwi kuwa umeisimea sana biblia.
KIONGOZI ANAHAKIKISHA NAFASI NA SAUTI HUTUMIKA VIZURI KATIKA
KUJISOMEA:
• Kuanza na kumaliza kwa muda mzuri, kumbuka masomo haya ya
biblia yatakuwa pamoja na shule ya kuwawezesha wanawake.ambao watahitajika
kwenda kushona.
• Tumia kitabu cha kiongozi na biblia ya Kiswahili hakita
hitajika ktabu cha ziada.
• Watie moyo kila mtu ili ashiliki katika kujadili, na hakikisha
hakuna ambaye anaongea kuliko wenginehakikisha unawatia moyo unapowasihi
wajadili.
• Mtazamo wako umuelekee Yesu, na usijadili misimamo ya mafundisho
ya kikanisa, au misimamo ya kisiasa, maswali ya misimamo na mafundisho
ya makanisa yashughurikiwe maeneo mengine.
Tafuta watu ambao watakuwa viongozi wa baadae wa kundi.
Kama kiongozi ni lazima uwe mifano wa kundi, hakikisha watu hawajadili
mambo ambayo yanapaswa kuwa siri, kwa mfano mambo yale ya nyumbani.
Uombe pamoja nao na kuwasihi watafute mwongozo wa Mungu.
Baada ya masomo ya Stonecroft yakina mama kufikia tamati, kila
mtu ambaye anaoneka kuwa ni kiongozi basi apitie mafunzo maalum
ya uongozi, kwa kutumia video na kitabu maalum cha uongozi, ili
waweze kupeleka stonecroft nyumbani kwao. Na katika makanisa yao.
Uwaulize washiriki wafikilie watu ambao wanaweza kuwaarika, uwahimize
waanze kuwaarika watu katika masomo, na pia waanze kuwaombea kwa
kuwataja majina yao.
Mambo muhimu ya kukumbuka.
• Iwapo huwezi kuongoza masomo haya ya biblia kwa sababu yeyote
ile, basi kiongozi aliyethibitiswa aje na kuchukua nafasi hiyo.
• Hutakiwi kumpatia mwenzako kitabu cha mwongozo mtu yeyote
Yule hata kama uko nae katika dara moja.
MKAKATI WA STONECROFT WA KUWAWEZESHA WANAWAKE
‘STONECROFT WOMEN’S EMPOWERMENT PROGRAM’ - (SWEP)
Masomo haya ya kibiblia ya stonecroft yanapangiliwa kutenda kazi
pamoja na mpango wa kuwawezesha wakina mama kupitia mradi wao wa
kujishonea (SWEP) huu ni ushirikiano wa mashirika mawili yani Stonecroft
and United Caribbean Trust (UCT), shirika la Kibarbados ambalo limesajiliwa
kama shirika la huduma za kijamii. Tunaamini kuwa mwanamke mwenye
uwezo wa kupata elimu, na akijua haki zake, anaweza kubadirisha
dunia hii.
Wakina mama ambao wanapitia mpango wa kushona wa Stonecroft watakuwa
katika mafunzo kwa muda wa mwaka mmoja.
Kila wiki atakuwa akihudhuria ‘Kukutana na Mungu’ huu
ni wakati wa kuomba, na tutatumia vitabu vya kujisomea vya Stonecroft
vilivyo tafsiriwa katika lugha za maeneo husika.
Na pia atahudhuria dalasa la kushona nguo na mitindo, masomo ya
computer, na kujifunza moringa na ufugaji wa wanyama.
US $40 kila mwezi itatumika katika kuwawezesha wanawake ambao watakuwa
wakihudhuria hayo masomo, ambapo yatamsaidia katiak kupata elimu,
masomo ya kazi za mikono, na vifaa vitakavyo muwezesha kuwa na mradi
utakao muwezesha kujipatia kipato.
Lakini zaidi ya yoote, haya mambo yatafungua mlango ili mwanamke
ajifunze uongozi kupitia masomo ya ya Stonecroft.
Na pia atapatiwa nafasi ya kumleta mtoto mmoja atakae kuwa anaingia
katika mradi uitwao ‘After School Feeding Club’ ambao
utatoa chakula cha kimwili na kiroho.
Ni shauku yetu katika kuwafikia wanawake wa Tanzania, Malawi,
Zambia, DR Congo na Uganda, kwa kuwaonyesha upendo wa Mungu na kuwafungua
kutoka katika umaskini.
Tunawashukuru Stonecroft kwa kujitoa kwao katika kuwafikia wanawake
katika maeneo yaitwayo 10/40 window (wasio fikiwa).
MFUMO WA UANAFUNZI WA KIAFRICA:
Huu mfumo wa kiafrica wa ambao ni wa kugawanya na kuzidisha ni muhimu
kuliko wa kuongeza!
1. Mfumo huu utaanzishwa kwanza Tanzania kupitia, ‘Africa
Training Bible School’ (ATBS) ambao lengo lao la kwanza ni
kuwa funza wachungaji kutoka makanisa 280 ambao wamo katika mpango
wa ATBS ili wajiunge na masomo ya kibiblia ya Stonecroft. Watafundishwa
kwa kupitia video na ktabu cha kiafrica cha kufundishia, hawa wachungaji
watakuwa viongozi wa kwanza wa Stonecroft Tanzania, na Bwana akipenda
kila mmoja wao atapatiwa kitabu ca utatu 10, Mungu yukoje? 10 Yesu
ni nai? 10 na Roho Mtakatifu yuko wapi? Na kitabu ambacho kimejumuisha
vitabu vyo hivi vitatu.
2. Hawa wachungaji watachukua taarifa hii na kwenda nayo katika
vijiji vyao ambao nao watachagua mwanamke mmoja, labda kiongozi
wa kinamama, na baada ya hapo atamfundisha huyu mama,na mchungaji
atabaki kuwa mwangalizi wakufuatilia kazi inaendaje tu.
3. Watapatiwa kitabu cha mwongozo cha Stonecroft na vitabu 10 vya
Stonecroft ‘Mungu anaonekanaje?’ Vyote hivi vimetafsiriwa
katika lugha yake anayo ielewa, na atapewa vitabu vingine 10 ,naye
atatafuta wenzake 5 katika kanisa ili waanze kujifunza.
Na hawa 5 nao walete mmoja kila mmoja wao, katika huduma ya Stonecroft,na
wataanza kujifunza utatu, ‘Mungu anaonekanaje?’ Baada
ya hapo ataendelea na “Yesu ni nani?” Na atahitimisha
na “Roho Mtakatifu yuko wapi?” Na atatumia videa na
kitabu kuwafundisha ili nao wakawafikie wengine.
4. Na akifikia hapo atakuwa kiongozi wa wenzake hao 5. Na atakacho
kifanya ni kurudia masomo ya Stonecroft kwa wanawake watano wengine
tena kanisani.hawa watano wa sasa watatiwa moyo kuwaletwa watu wasio
okoka kanisani, sasa ataanza kuwafikia wasio fikiwa. .
5. Mchungaji kwa wakati huu atakuwa ni mtu wa kutoa ushauri na mwangalizi.
6. Hawa viongozi wapya 5 pamoja na mwana maombi wao, watamtafuta
mtu mmoja kanisani au kijijini ambaye ana sifa za kuwa kiongozi,
wamfundishe kwa ruhusa ya mchungaji wao.
7. Kwa pamoja hawa wakina mama 5 watawasihi wasio mwamini Mungu
wajiunge na masomo ya Stone croft,ya utatu,kwa kawaida kila mmoja
awe na wakina mama 2, kumbuka masomo haya yawe na wakina mama 10
- 12 wanawake.
8. Wakisha kujifunza masomo haya ya utatu basi huyu mwangalizi atawafundisha
wakina mama 2, mmoja toka kanisani kwake na mwingine kanisa jingine
ambao watakuwa viongozi wa Stonecraft wa kizazi cha nne. Wana maombi
wake watabaki na darasa hili katika kulifundisha.
9. Mtindo huu utandelea katika kanisa ambalo limejifunza mkakati
huu.
10. Iwapo kuna swali ambalo huyu kiongozi hawezi kulijibu basi amuhusishe
mwangalizi wake.
11. Kwa kadri muda unavyo zidi kuendelea tutapata waangalizi wengi
zaidi kwa kadri mtandao huu unavyozidi kutanuka na video nyingi
sana zitatengenezwa.
12. Kumbuka - kugawa na kuzidisha !
13. Kuzidisha ni bora kuliko kuongeza!'
‘Uwe macho, Simama imara katika imani, Uwe jasiri,uwe mwenye
nguvu. Fanya kazi zote kwa upendo ’
1 Corinthians 16: 13 – 14
|