home >>
stonecroft>>roho
mtakatifu yuko wapi?>>
somo la pili (2)>>la tatu (3)
Stonecroft - Roho Mtakatifu yuko wapi? -La Tatu (#3)
SOMO LA TATU (3)
ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUNISAIDIA KUKUA?
The Guide has her own Guidebook
to help her lead and guide the lesson.
Download Swahili Lesson
#3 Guidebook
Download
Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #3
LENGO LA SOMO
• Kujifunza zaidi kuhusu ulinzi na uwezo war oho
Mtakatifu ndani ya maisha yetu.
• Kuanzisha mipango binafsi na maombia binafsi na kujifunza
Biblia.
• Kutambua uhuru kutoka katika himaya ya dhambia kwa nguvu
ya Roho Mtakatifu ndani ya maisha yetu.
MAOMBI
Baba uliye juu mbinguni, tunatambua kuwa siku zote hatuna nguvu
ya kushindana na dhambi katika maisha yetu. mara zote hatufanyi
kama vile wewe unavyotaka kama watoto wako kufanya. tusaidie sisi
kujua vitu mbali mbali ambavyovitatusababisha kuwa tofauti katika
maisha yetu. tunaoma katika jina la Yesu Kristo …….AMEN
MAONI YA KIONGOZI
Maeleze ya kina kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu yapo katika Yohana
14 -16. Sura hizi tatu ni mambo ambayo Yesu alikuwa akiwaambia wanafunzi
wake kabla hajaenda katika bustani ambako ndiko aliko kamatwa. Hizi
sura ndizo tutakazososma katika wiki hii ya ya kujisomea au kujifunza.
Watie moyo wana kikundi ili wataje mstari wa biblia walio uchagua.
KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA
(Use your Bible
or Africa Bible Verse Handbook)
Soma vifungu vya Biblia hivi hapa chini na
uweze kukopi mistari a,mbayo unafikiri ni ya muhimu sana
katika kusoma.
Yohana 14:1-14
Yohana 14:15-31
Yohana 15:1-17
Yohana 15:18-27
Yohana 16:1-15
Yohana 16:16-33
|
Kitu cha kushangaza tulichokisoma kutoka katika masomo yetu kuhusu
Roho Mtakatifu ni anaitwa Mungu, a na sifa za Mungu, na anafanya
kazi anazofanya Mungu.
Wiki iliyopita, tulijifunza kuwa Roho Mtakatifu anahusika katika
kuzaliwa kwetu ndani ya familia ya Mungu.
Ni kitu gani ambacho Roho Mtakatifu anafanya ili kutudsaidia sisi
kujua kuwa tunahitaji msaada baada ya kuokoka?.........(Roho
Mtakatifu anachukua hatia ya dhambi zetu kabla hatujaokolewa Yohana
16:8.)
Je anajishughulisha vipi na sisis baada ya kuwa Wakristo?........(Anaingia
ndani ya maisha yetu pale tunapomwamini yeye kama mkombozi wetu
na kuanza mafundisho yake na kazi ya kutulinda Yohana 16:13.)
Tunapompokea Yesu Kristo kama bwana na mwokozi wetu, tunakuwa tayari
tumepewa uhakika wa maisha ya milele na Mungu. Wokovu haungalii
kuishi kwetu vizuri, yaani mkuwa na nyumba nzuri, maisha mazuri
N.K lakini kwa kuwa na uhakika kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi
badala yetu hilo tu linatosha. Sisi kama waamini tuehakikishiwa
tayari kuingia mbinguni baada ya kufa.
Roho Mtakatifu ni alama tu moja wapo ya kwamba Mungu anatumiliki,
na kutufanya kufanya yale Mungu anayoyataka.sisi kama waumini au
washirika wake kristo tayari tumesha tiwa muhuri kuwa asisi ni wana
wa Mungu na wokovu upo kwetu.
Somo letu la leo linatuonyesha ya kwamba ni jinsi gani Roho Mtakatifu
anaishi ndani yetu na jinsi gani anavyotusaidia kuishi maisha ya
Kikristo yenye utii.
ROHO MTAKATIFU NDANI YA MAISHA YETU
Sisi kama watu tuliokoka, sio wafungwa tena wa dhambi. Shetani
aliuwa ni Bwana mkatili, lakini sasa Yesu ndiye BWANA wetu mpya
na anatupenda sana sisi.
Kwa sasa tuko tofauti na tunajua ni jinsi gani ambavyo tunaweza
kuishi maisha ya kiMungu.
Je unajuwa rasilimali hizo tulizonazo ni zipi?...... ( Uwepo
war oho Mtakatifu, ulinzi wake, neno la Mungu, na maombi.)
Maisha yetu ya Kikristo yanakuwa
pale tunapoendelea kumtii Roho Mtakatifu. Anatusaidia kuachana
na tabia mbaya, anatusaidia kuelewa Biblia, na kujifunza jinsi
ya kuomba. Maisha ya Kikristo ni maisha ambayo kila siku inakuwa
ni kukua ambayo yanaanza pale ambapo Roho Mtakatifu anaingia
ndani yetu. Kuna mida mingi sana ya majaribu, kutokutii na uasi.
Kwa kuwa Roho wa munu yu ndai yetu anaendela kutusaidia kuendelea
kukua katika kimo kingine.
1. Nini annachokifanya Roho Mtakatifu kwetu, kutusaidia ili
kukua kiroho?
a. 1 Yohana 2:27……. (Atatufundisha.)
b. Yohana 16:13-14…… (Sikiliza
vitu hivi viwili.)
(1. Ataonyesha au atafunua ukweli kuhusu Mungu.)
(2. Ataleta utukufu kwa kristo, sio kujitangaza yeye kama
yeye.)
c. Warumi 8:14..…(Roho ya Mungu
itakuongoza).
d. Wagalatia 5:22-23..… (Atazalisha
matunda yake katika maisha yetu.)
e. Matenndo ya mitume 1:8…. (Anatupatia
nguvu ili tuweze kumtambua yeye.)
|
Kazi ya roo Mtakatifu ni kutufanya sisi, kama kristo kwa kutufundisha,
kufunua ukweli,kumtukuza kristo, kutuongoza, kuzaisha matunda na
kutupatia nguvu ili kuwa na nguvu ya kuweza kumtambua yeye na kumhisi.
MAOMBI
Maombi ni nguzo muhimu sana katika kutaka kuwa kama kristo. Je
maombi ya kriso yalikuwaje?..........mstari ambao unatupa au unatukumbusha
kuwa maisha ya kristo yalikua ya maombi sana upo katika ukurasa
wa 90, ma rko 1:35.
Kama mwanadamu, Yesu alijua kabisa kuwa kuna muda ambao alitakiwa
kuwasiliana na baba, kuzungumza naye, kutafuta mapenzi yake na na
Baraka zake.
1. Je, Roho Mtakatifu anatusaidiaje
sisi kuomba? Warumi 8:26…... (Anatusaidia
katika madhaifu yetu ,na anatuombea sana sisi kwa yale mambo
hatuwezi kuyapeleka) |
Mungu aliumba wau ili awe na ushirika pamoja naye. Alituumba sisi
kwa mfano wake ili kwamba tuwe na uwezo wa kumwelewa na kumfurahia
yeye. Tunazungumza na Mungu kwa njia ya maombi. Anaongea na sisi kwa
kupitia kitabu alichokiandika ambacho ni Biblia.
Soma 1 Yohana 5:14-15…..
Muda mwingine Wakristo hawaombi kisawasawa,
wanabakia kusema tu maombi. Maombi yetu thabiti yanatoka ndani
ya mioyo yetu. Kwa hiyo yanaunganisha ya moyo wa Mungu, ambaye
anawasiliana na sisi kupitia Roho wake Mtakatifu. Kwa kuwa Yesu
amtupa uhuru wa wa kuomba kwa Baba kwa jina lake, tunaomba na
Mungu anatujibu, kwa sababu tunaomba kwa mapenzii yake.
3. a. Mungu alituambia nini sisis kuhusu muda gani au wakati
gani tunaotakiwa kuomba?
Ukursa 523, 1 Wathethalonike 5:17……..(Omba
kila mara na kila wakati)
b. Ni sifa gani ya Mungu ambayo inatufanya sisi kuomba kila
mara na sehemu yeyote?..........(Yeye yupo sehemu yeyoteile
na muda wote, yupo kila mahali)
4. a. Mungu alisema nini kuhusu maombi katika Mathayo 6:5-6?..........
(Usifanye kama maonesho katika maisha yako, unaweza kuomba
peke yako ukiwa katika chumba chako na Mungu wako)
b. Nini alichokisema daudi kwamba angezungmza na Mungu? Zaburi
55:17……
(Asubuhi, mchana,na jioni)
c. Kama una muda wa mara kwa mara wa kuomba kila siku, anzisha
sasa . Andika plani yako ya maombi ya kila siku kama ulikuwa
hufanyi hivyo.
|
KUOMA BIBLIA
Kama Wakristo tuna faida kubwa sana ambayo haikuwepo tangu hapo
awali kabla hatujawa Wakristo. Roho Mtakatifu anatufundisha na anatusaidia
kuelewa nini Biblia inasema. Soma 1 Wakorintho 1:18……..
Wengi wetu tulikuwa hatuelewi Biblia kabla hatujawa Wakristo. Je
unahisi tofauti yeyote na kipindi ambapo ulikuwa hujapata msaada
huu war oho Mtakatifu?......
5. Kukua katika Ukristo inatakiwa
tuanzishe ratiba ya mara kwa mara ya kusoma Biblia. Tafuta muda
ambao wewe unaona kuwa wewe utakufaa katika kukamilish a hili…………… |
Itakuwa ni vizuri hata ukiwa unaamka mapema au unachelewa kulala
kwa ajili ya kusoma Biblia na kuomba kwa manuafaa yako na maisha
yako kiujumla. Lakini kuwa na ushirika na Mungu kila mara ni kitu
cha muhimu sana katika maisha ya kila siku ya muumini hasa pale
unapokuwa unakuwa katika maisha ya Kikristo, kama vile rho mtgakatifu
navyo tufundisha sisi kwa kupitia neno la Mungu.
Kuwa na ushirika na Mungu ni kitu kinachofanya maisha yetu ya Kikristo
kama kujua utatu ndani ya ma isha ya Kikristo. Kwa kupitia maombi,
na vile Mungu a navyotupa kupitia umakini wetu tunaposoma neno,
tunafikia hatua ya kuelewa kuwa Mungu ndiye anayeyaa ngalia maisha
yetu. Kuishi chini ya ulinzi war oho Mtakatifu inamaanisha kuwa
sisi tunaishi na kukua katika uhusiano mzuri na kristo.
UTII
6. Ni ushauri gani ambao Mungu anatupa
kuhusu kusoma Biblia? Yakobo 1:22-25…..
(Tii kile unachokisoma, na kifanyie mazoezi). |
Tunapotii kile tunachokisoma katika neno la Mungu, tunaweza kuzuia
kufanya maamuzi ambayo sio sahihi, na utabarikiwa sana na Mungu.
Utii kwa munu ndio utakao tuwezesha sisi kukua kama Wakristo. Maarifa
ya neno la Mungu ni muhimu sana, lakini kujua bilia na kutokuitii
ni hatari sana.
Roho Mtakatifu anachukua dhambi zetu au hatia yetu katika maisha
yetu kabla hatujawa Wakristo. Na bado anaendfelea kuchukua hatia
yetu na kutukumbusha kutokutenda vibaya, kuwa na mawazo potofu,
kuwa na mitazamo mibaya ,ambapo haya yote yanatusababisha sisi kutokukua
kiroho.
Soma Wagalatia 5:17…..
Ukweli ni kuwa hatuwezi kutii mapenzi ya Mungu kwa nguvu zetu sisi
wenyewe. Tunamhitaji Roho Mtakatifu kutupatia nguvu na uwezo wa
kufanya hivyo.
Kama Wakristo tunajaribiwa kwa kufanya
vitu kwa njia zetu wenyewe bila kumshirikisha Roho Mtakatifu
kama kiongozi wetu. Sisi tuna panga sisi wenyewe kukupambana
na majaribu ambapo kwa wakati mwingine inaonekana ni njia nzuri
sana ya kuweza kupambana na majaribu. Lakini Mungu anatuia moyo
kuwa kukaa nay eye itasaidia zaidi kuliko kuaa peke yestu kwa
atatusadia katika kusimama imara katika mambo tofauti tofauti,
hata ikiwa ni katika majaribu atatusaidia. Yeye ametupa ahadi
kuhusu hili, soma 1 Wakorinntho 10:13…….
Huu mstari ni vizuri kukariri. Andika hapa
7. je inawezekanaje kwetu sisi kumhuzunisha Roho Mtakatifu?.
Waefeso 4:25-32……… (Roho
Mtakatifu anahuzunika pale tunaposhindwa kumtiii yeye)
|
Tunapo sema uongo, unapokuwa na hasira, tunapowafanyia watu wengine
mabaya, kuwa na machukizo, au kuwa na mioo migumu, tunamkasirisha
Roho Mtakatifu. Hii, inatika kwa sababu hatujali maonuyo yake. Kwa
hiyo ili sisi tuweze kukua inatakiwa haya mambo yote tuachane nayo
ili tuweze kukua kiroho.
Soma Waefeso 4:30 tena.. Huu mstari unaodhihilrisha
ukweli mwingine. Kukaa kwa Roho Mtakatifu ndani yetu ni ishara ya
kwamba Mungu a natumiliki sisi. Sisi hatuko peke yetu. Tumenunuliwa
kwa ,gharama kubwa sana. Soma 1 Wakorintho 6:19-20...
8. Umeumbwa ili kumtukuza Mungu.
Kazi kubwa ya Roho Mtakatifu ni kuhakikisha kuwa anakusaidia
katika kuishi maissha ya kuweza kumtukuza Mungu.
a. oredhesha baadhi ya maeneo ambapo Roho Mtakatifu anafanya
kazi ndani ya maisha yako ili kukufanya wewe kama kristo……..
b. orodhesha maeneo ndani ya maisha yako ambayo Mungu tayari
ameshakupatia ushindi………..
|
Wagalatia 5:16…………
Wakati Roho Mtakatifu anadhibiti maisha yetu, badala yetu sisi
wenyewe, anatufanya kuwa kama kristo.
U funguo wa kuweza kubaki na kuwa kama Yesu ni kukazana kusoma
neno la Mungu yaani Biblia na kuweka muda juu ya Mungu kwa maombi
sana. Tunapotaka au tunapounda urafiki na watu mara nyingi tunakaa
pamoja, hivyo basi inatakiwa hata kwa upande wetu tufanye hivo kuwa
na urafiki wa karibu na Mungu, kwa kusoma bib lia na kuomba ili
tujue anasema nini kuhusu sisi. Roho Mtakatifu atakuwa mwaminifu
katika kutufundisha sisi, endapo tukiwa wakrimu na kufanya kwa nafasi
yetu kile kinachotakiwa kufanywa kwa matakwa yake, na kwa kumsikiliza
na kumtii Mungu.
Maombi ni mrejesho wa kile ambacho Mungu amesema. Kila asubuhi
tunaweza kuomba kuhusu kazi zetu, kumuomba Mungu kufunua mipango
yake kwa ajili yetu juu ya siku husika. Tunaweza kumuomba yeye kutupa
hekima ili tuweze kukamilsha vitu katika njia ya kumpendeza Mungu.
Unapoishi ndani ya uwepo wa Mungu kila mara, maisha yetu yatabadilika
na kuwa na maana mpya sana. Kila siku tutaona ukuu wa Mungu ukiwa
unafanya kazi ndani yetu.
9. Fikiria majibu yako katika swali
la 8 na andika maombi yako ya kumshukuru Mungu kwa maendeleo
ambayo unayaona ndani ya maisha yako……….. |
MAOMBI
Baba yetu, asante kwa kutupatia Roho Mtakatifu wa kutufundisha
sisi na kutusaidia kuelewa ukweli wa neno lake. hamu ya mioyo yetu
ni kukutii wewe. asante kwa kutusaidia katika kukua tunapokuheshimu
wewe. katika jina la Yesu Kristo…..AMEN…..
|