home >>
stonecroft>>roho
mtakatifu yuko wapi?>>
la nne (4)>>la tano (5)
Stonecroft - Roho Mtakatifu yuko wapi? - La Tano (#5)
SOMO LA TANO (5)
KUISHI KATIKA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU
The Guide has her own Guidebook
to help her lead and guide the lesson.
Download Swahili Lesson
#5 Guidebook
Download
Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #5
LENGO LA SOMO
• Kuhjifunza umuhimu na kuruhusu Roho Mtakatifu kuwa ndani
yetu.
• Kutambua kuwa maisha ya ushindi ya mkrishto yanatokana na
Roho wa Mungu kuwa ndani yetu.
• Kuelewa kwa nini utii na uzao ni muhimu sana katika kujazwa
kwa Roho Mtakatifu.
Kwa sababu ya utata uliopo ndani ya hili somo, itakuwa vizuri kurudia
mwongozo unaotuongoza katika mafunzo haya. Kama majibu yaliyotolewa
yana kinzana kwa kukubali majibu kwa kutolea ufafanuzi hata kidogo
basi unaweza ukaendelea na somo. Kama mtu "akizungumzia kunena
kwa lugha"unaweza ukasema kuwa,“ kwa sababu makanisa
yanatofautiana katika mafundisho juu ya hili, lakini ngoja nikupe
kifungu ambacho kinajibu swali lako . Tafuta muda ukasome katika
1 Wakorintho 14:1-40 utakapo kuwa nyumbani"
MAOMBI
Baba uliyejuu mbinguni, asante kwa kutupa neema ya kuishi maisha
ya Kikristo. Tufundishe sisi umuhimu wa kukutii wewe. Katika jina
la Yesu, AMEN
MAONI YA KIONGOZI
Unaweza ukawa umegundua kuwa kuna vifungu vingine ndani ya masomo
haya yaliyopita vimekuwa vikijirudia.Lakini ni kwamba vifungu vya
Biblia vikijirudia katika kusomwa haina tatizo bali tutakuwa tunaongeza
ufahamu juu yay ale tuyamayo.
KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA
(Use your Bible or Africa Bible Verse
Handbook) Andika rejea ya mstari ambao umekusaidia wewe
kwa umuhimu mkubw asana katika vifungu vifuatavyo.
Wagalatia 5:16-26
Warumi 6:1-11
Warumi 6:12-19
Warumi 6:20-23
Warumi 8:1-8
Warumi 8:9-17 |
Uwepo war oho Mtakatifu ndani ya maisha yetu na zawadi au vipawa
anavyo tupatia, vinatufanya sisi kuwa kama Wakristo ambao tunafanana
na kristo mwenyewe. Kama waamini, tunaye Roho Mtakatifu kila mara
ambaye anayetulinda kila mara, anatufundisha, na kutupatia nguvu
ya kuweza kushinda katika hali mbalimbali. Kwa kuwa Roho yupo kwa
ajili yetu na kufanya kazi kwa ajili yetu basi tutakua tunaona ushindi
mara kwa mara.
1. Kukaa kwa Roho Mtakatifu ndani
yako kumekusaidiaje ndani ya wiki hii? ....... (Waruhusu
watu kushirikiana majibu yao watakayo toa.) |
Mwandishi Charles Swindoll alitoa msaada juu ya ufafanuzi war oho
Mtakatifu ndani ya maisha yetu.
Alizungumzia kuhusiana na kijana mdogo amabye jina lake alikua
mtenda Dhambi, ambaye alipokea gari kkutoka kwa baba yake, lilikuwa
gari jekundu na lilikuwa linaitwa Wokovu. Lilikuwa ni gari jipya
na zuri sana. Muda mwingi Yule kijana alikuwa anawaeleza watu wengi
kuwa amepata zawadimkutoka kwa baba yake, alikuwa hatarajii kuwa
na gari kama lile, na asingeweza kulilipia, yaani hiyo ilikuwa ni
zawadi tu ya moja kwa moja kutoka kwa baba yake.
Hili gari lilimfanya yeye kubadilika na kuwa na furaha sana, a
mbapo likabadili hata jina lake kutoka mtenda Dhambi mpaka jina
la Kuokolewa.
Baadae, alionekana akisukuma lile gari lake chini ya njia kuu,
mtu mmoja jina lake alikuwa anaitwa Msaada, alikuwa akitembea alijitambulisha
yeye mwenyewe, na kumuuliza yula kijana kama angetaka msaada wowote.
Tle kijana akamwambia “hapana asante sana nashukuru “
Aliyeokolewa akajibu
“Umesukuma gari lako tokea mbali?” Msaada akauliza.
“Kama maili 200 hivi.Imekuwa inaniwia vigumu, lakini hii
yote nafanya kwa sababu baba alinipatia hili gari.” Aliyeokolewa
akajibu
Msaada akasema, “Niruhusu mimi nikusaidie, kuna kitu ambacho
wewe hukielewi”.
Msaada akafungua mlango wa gari, na yule kijana akashtuka kidogo,
kw ahiyo Yule msaada akaingia ndani ya gari, kwani tangu Yule kijana
alipopewa lile gari alikuwa amelipumzisha tu.
Msaada akazunguka kwa upande mwingine, na akakaa katika kiti cha
dereva, na akawasha gari ambapo likaanza kutembea mara wakaingia
barabarani na kuanza kuondoka vizuri kabisa bila tatizo lolote.
Kwa hiyo Yule kijana akakaa pale kwenye gari akiwa anashangaa.Alikuwa
akimruhusu sasa hata Yule aliyetoa Msaada kufanya kile ambacho hakutaka
hata kukifanya. Alifikiri kuwa kufika mwisho wa ile barabara ilikuwa
nndio mwisho wa majukumu yaka. Alitabasamu saana, na akagundua Yule
kijana kuwa tangu amepata ile zawadi kutoka kwa baba yake ile ilikuwa
ndio tabasamu lake la kwanza tangu kupokea ile zawadi.
Hiyo ni picha halisi ya Wakristo wengi.tunajua kabisa kuwa kulikua
hakuna njia ambayo tungeweza kulipa kwa ajili ya wokovu huu. Hii
ilikuwa ni zawadi tu, lakini pia hatujui kuwa nguvu yenyewe ya kuishi
maisha ya Kikristo pia ni zawadi.
Swindoll alihitimisha kwa kusema “ mtu aliyekupa gari, alikupa
na dereva. Anaweza kumiliki vizuri tu. Unapotaka kutoa tairi juu
ya mikono yake weqe utakuwa una matatizo”.
Ili kuendelea kuishi katika maisha mazuri ya Kikristo ni kuw ana
Roho Mtakatifu, anapoishi ndani yetu na kupitia wewe.
Kua wakati ni vigumu san kukubaliana na ukweli kuwa, tunaweza tusifanye
kitu chochote, ili kufanya wokovu wetu ukawa imara zaidi kuliko
siku ile ambayo tulipmpokea Yesu kama mkombozi wetu. Tunataka kufanya
kitu kwa aji.li ya Mungu., lakini badala yake Mungu alifanya hicho
kwa ajili yetu. Wokovu ni zawadi ya upendelea ambayo haina malipo
yeyote, kwa hiyo ni maisha yetu mapya.
Kifo cha Yesu Kristo pale msalabani, kilileta zawadi
kwetu sisi ya wokovu, lakini ni ufufuo wake, ambao ulileta nuvu
zaidi kuishi katika maisha ya utii. Soma katika Warumi 5:8-10……
Kuokolewa kwa kifo cha Yesu Kristo,
lakini nguvu ya kuishi ni ufufuo wake.
2. Kifo cha Yesu kilikuokoa wewe, je ufufuo wake umekufanyia
nin I wewe?
Waefeso 1:18-20…………
2 Wakorintho 13:4………..
(Unatupatia sisi nguvu ya kuishi vile Mungu anavyotaka sisi
tuendelee kuishi). |
Masiha yetu ya kila sisku na shughuli za kila wakati zote zinatolewa
kwa sanbabu ya kufufuka kwa Yesu Kristo. Tunakubali na kupokea zawadi
ya wokovu kwa imani. Pia tunaishi maisha ya Kikristo kwa imani.
Hatuwezi kuishi maisha ya Kikristo kwa nguvu zetu wenyewe. Ni
kwa nguvu ya Mungu pekee ambapo tunaweza kuishi na kutii kile
ambacho Mungu ametruagiza kwa mapenzi yake. Nguvu ya Roho Mtakatifu
katika maisha yetu inatakiwa iwe ni ya kumtumikia Mungu na watu
wengine. Haitakiwi kutumika kama faida yetu sisi wenyewe. Tumejazwa
na Roho Mtakatifu, kwa hiyo tuna uwezo wa kuishi kama vile Mungu
alivypanga mipango yake kwetu sisi.
Soma katika Waefeso 2:10…………
|
Sisi kama sisi,hatuwezi kufanya kile kitu ambacho Mungu amekipanga.hiyo
itakuwa kama kusukuma gari, usije ukajichanganya. Tunatakiwa pia
tuendelee kutoa nguvu ya kumalizia kazi , lakini inafanywa chini
ya uangalizi wa roho.
Wakristo wamepokea Roho Mtakatifu (Warumi 8:9-10). Sasa kwa nini
Biblia inatuambia kuwa tujazwe na Roho Mtakatifu?
Kujjazwa na Roho haimaanishi kuwa inatakiwa kupata kile kitu ambacho
hatunacho. Inamaanisha kuwa sisi kama sisi inatakiwa tujazwe na
Roho Mtakatifu.
Tujishushe kwake kjila mara. Ili kufanya hili, tujishushe sana kwake
nan a sio kujikontrol sisi wenyewe. Tunatakiwa tuache saizi ,kusukuma
gari letu la kiroho, badala yake tunatakiwa kutii na kufurahia mahala
,popote pale ambapo Roho Mtakatifu atatuongoza.
Soma Waefeso 5:18….. kwa nini unatakiwa kujazwa
na Roho wa Mungu inafananishwa na kulewa ?.........(Kwa sababu
Matendo yestu yanasukumwa na Yule .mtu anaye ishi ndani yetu.)
Watu wakiwa wamelewa, wanakuwa wako cini ya utawala wa pombe waliyoinywa.
Kwa njia hiyo hiyo, Wakristo ambao wamejazwa na Roho Mtakatifu,
wana uwezo wa kufanya vitu katika njia ya Mungu, na sio katika njia
tuzitakazo sisi wenyewe.
3. Elezea mtu ambaye amejazwa na Roho Mtakatifu. Waefeso
5:18-20……
(Mtu ambaye amejazwa na Roho Mtakatifu, anajishusha chini ya
ugtawala war oho Mtakatifu, kuongea kwa lugha ya kristo kwa
watu wengine, kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu, na kumpa shukrani
kwa kila kitu). |
Mungu anatulazimisha sisi kujazwa na Roho Mtakatifu sababu kuu
mbili: ili kukua na kumtumikia Mungu katika njia nzuri zaidi.
Mmkristo mpya anapewa Roho Mtakatifu, lakini hiyo ,haimaanishi
kuwa tayari kakua kiroho. Kukua kiRoho kunakuja pale anapojazwa
na kuishi maisha ya utii kwa muda mrefu tu.
Wakristo wa korintho hakua wamekua, Biblia inasema na inaeleza kwa
uzuri kabisa kuwa kwa nini hawakuwa wamekua ilikuwa na kwa sababu
ya uchanga wao. Soma katika Wakorintho 3:1-3……..
Tumejazwa na Roho Mtakatifu ili kuweza kukamilisha kazi ambayo
Mungu ametupatia sisi. Soma Matendo 9:17 na 20………
Paulo alijazwa na Roho ili kukamilisha kazi ambayo alipewa na Mungu
na vile Mungu alivyokuwa amepanga juu ya kazi yake.
Tunapompokea Yesu Kristo kama mkombozi wetu, Roho Mtakatifu anakuja
ndani yetu, hakuna masharti ya kumpokea Roho wa Mungu. Lakini kuna
masharti ya kujazwa na Roho Mtakaytifu, ambapo inatakiwa tumtii
sana Mungu ndipo tutajazwa na Roho Mtakatifu.
4. Ni masharti gani ambayo yameainishwa
katika kumtii Roho Mtakatifu?
Warumi 6:19…….. (Achilia
maisha yako chini ya Mungu baba)
Warumi 12:1…….. (Imejikita
katika kumtumikia Mungu)
1 Petro 4:19……… (Kutii,
hata kama itaonekana kuna mateso. Amini kile Mungu anachokisema;
mtegemee Mungu peke yake)
|
Kuna wakati mwingine sisi kama Wakristo tunatakiwa kujishusha katika
utawala wa Mungu. Kujishusha kwetu kunatakiwa kuwe hivyo kwa Mungu
wetu mara kwa mara. Tunatakiwa kumwambia Mungu au kumwoma Mungu
kubadilisha maisha yetu. Soma katika Warumi 12:2….
Mungu anatubadilisha sisi kutoka ndani, anasafisha fahamu zetu
ili kutufanya kufikiri tofaiti na watu wengine. Tunapokuwa karibu
na Mungu, tunajipeleka ili kwamab yeye atutumie sisi apendavyo.
Kwa sababu Roho Mtakatifu anamtii Mungu baba, lakini mioyo yetu
inataka sana kufanya mambo yenyewe bila msaada wowote ule, kwa kuwa
kuna mgogoro wa ndani. Lakini tunapo mruhusu Roho Mtakatifu kutusaidia
sisi kujishusha kwa Mungu, ina maana tunachagua kuwa Mungu afanye
mambo yote kwa niaba yetu.
Tunapomtegemea Mungu peke tunafanya kile ambacho Mungu anataka
sisi tufanye, kuliko kile tunachotaka kufanya sisi kama sisi. Biblia
inatuambia sisi kuhusu hili katika Warumi 8:1-5…..
Tunapokua katika kujishusha chini ya mamlaka ya Mungu, tunakua
watii, amabapo hii inatusaidia kujazwa na Roho yake.
5. Ni maeneo gani muhimu katika maisha
yako yanahitaji wewe kujazwa na Roho wa Mungu ili kukamilisha
matokeo yanayotakiwa?............ (Hakikisha kila mmoja
anatoa jibu lake) 6. Elezea ukweli kuhusu Roho wa Mungu
katika maisha yako katika mitazamo na majukumu/ kazi yafuatayo.
Ushahidi kuwa umejazwa
na Roho ya Mungu
|
Napanga nini pale ambapo mabadiliko
yanatakiwa
|
Kujua kuwa nimeokolewa |
|
Kuwa na muda wa maombi kila mara |
|
Kusoma Biblia mara kwa mara |
|
Kushinda tabia zinazoleta dhambi |
|
Kuwapenda waumini wengine |
|
Kuwa na mitazamo na wasioamini |
|
Hatuwezi kuishi maisha yay a mutii kw anguvu zetu wenyewe bila
kupata msaada wowote kutoka kwa Mungu. Tunataka nguvu ya ziada
ya kutusaidia sisi. Na ndio maana tukapewa zawadi ya Roho Mtakatifu.
Tukifuata utawala wake nasi tutaweza kuishi maisha ya kumpendeza
sana Mungu.
Matokeo ya somo hili, jiulize mwenyewe swali hili. Je, nimefikia
wapi katika kukaa na Roho Mtakatifu?
Gharama ni kujitoa
Sharti ni utii.
Roho mtakatifu alipoingia katika maisha yangu
Nilimpokea yeye katika utimilifu wake.
Kujazwa na Roho mtakatifu,
Ananiohitaji katika ukamilifu wangu.
7. Andika maombi yako, ambapo ukionesha jinsi ulivyo na hamu
ya kuweza kujazwa na Roho ya Mungu.
|
Kwa kuwa maombi katika somo la 7 ni maombi binafsi,sio muhimu wao
kulisema labda wakipenda kufanya hivyo.
MAOMBI
Baba yetu uliye mbinguni tunakushukuru kwa wema wako, na kutufanya
kuwa katika mahusiano mazuri na wewe. Asante kwa kutupa nguvu ya
kuishi maisha yenye kukupendeza wewe na kushi chini ya utawala wako,
tunataka kuwa wako kabisa. Katika jina la Yesu Kristo. AMEN
|