Project Hope     home >> stonecroft>>roho mtakatifu yuko wapi?>>la tatu (3) >> la nne (4)
Stonecroft - Roho Mtakatifu yuko wapi? -La nne (#4)
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA NNE (4)
NAWEZAJE KUWA MKRISTO WA KUZAA MATUNDA?

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #4 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #4

LENGO LA SOMO
• Kutambua kuwa maisha ya ushindi kwa mkristo yanawezekana pale ambapo Roho Mtakatifu anaishi ndani yetu na kutawala maisha yetu.
• Kurusu matunda ya Roho Mtakatifu kuonekana ndani ya maisha yetu.
• Kumruhusu Roho Mtakatifu kuendeleza na kutumia vipawa vya kiRoho ambavyo tumepewa.

MAOMBI
Baba yetu uliye juu mbinguni, wewe ni wa muhimu sana kwetu. Hatuwezi kuishi katika mipango yako bila msaada wako. Asante kwa kutupatia Roho Mtakatifu kuishhi ndani yetu. Tusaidie kujishusha chini ya utawala wake kwa sababu tunajua kuwa ndio njia pekee ambayo tunaweza kuishi kama Wakristo wa kweli. Tunaomba katika jina la Yesu……AMEN…..

KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA

(Use your Bible or Africa Bible Verse Handbook)

Soma mistari uliyopewa hapa chini na uandike mstari ambao unaona kuwa ni wa muhimu sana katika kila ms tari utakaosoma.

1 Wakorintho 13:1-13
Warumi 8:1-8
Warumi 8:9-17
1 Wakorintho 12:1-11
1 Yohana 4:7-21
Wagalatia 5:16-26


MAONI YA KIONGOZI

Mungu ametupa sisi ili kwamba tuwe na maisha bora. Kila mara maisha yetu yanatakiwa tuishi katika mwelekeo wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Kwani inakuwa inaleta furaha ya moyo wako. 1 Petro 5:14b inasema “ Amani kweni nyonte mlio ndani ya Kristo.”

Wakati ule tulipookolewa, Mungu akagtupatiua zawadi ambayo itakuwa inatulinda na tukae ndani ya uwepo wake ambaye ni Roho Mtakatifu. Na pia anatusamehe haraka sana pale ambapo tunashindwa katika kufan ya kazi yake vizuri. Soma 1 Yohana 1:9………

Hatutakiwi kusubiri mpaka kuwa katika eneo muhimu sana ili kutubu kama tumekosea, ni kuhakikisha kuwa pale tunapoona kuwa tumefanya ndivyo ,sivyo muda huohuo ni kutubu naye Mungu anatusamehe kwa wakati huo huo. Tunaweza tukatubu dhamb zetu kwa Mungu na wakati huohuo tukasamehewa, na kuwa safi tena .

Waklristo wengi wamekuwa wakiishi katika maisha ambayo hayana mwelekeo kabisa na kutokutambua kuwa Mungu yupo kwa ajili yao. Katika mtazamo wa kiMungu ni kuwa maisha ya mkristo yako chini ya utawala wa Roho matakatifu. Matokeo yak ni maisha ambayo yanazaa matunda ya roho, amabayo ndio topic yetu au maada yetu ya leo.

Katika soma la 3, tulijifunza kuwa Roho Mtakatifu ana kazi kubwa katika maisha yetu haya ya kukua kiroho. Anatusaidia kuomba, kuelewa Biblia, na kutii kile tunachokisoma. Katika somo hili, tutasoma matokeo chanya ya kutiii ulinzi war oho makatifu.

1. Roho ya Mungu inazalisha matokeo ya ajabu katika maisha yetu pale tunapomtii yeye.

Andika vitu tisa hapa ambavyo ni mazao au matokeo ya Roho mtakatuifu katika maisha ya mkristo. Wagalatia 5:22-23……… (upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.)

Matunvda haya yote ya ndani ambayo wote tunataka kuyamiliki, lakini sio mazao ya asili ya maisha ya mwanadamu. Haya yanazalishwa na Mungu peke yake. Haya ni matundaambayo yanakuja yanatokea kwa nje na watu kuyaona hasa pale ambapo tunatembea sana na Roho ya Mungu.

Tunawezatukajisifu kwamba tuna ubora wa kuwa na hiv vitu lakini kumbe hakuna. Na haya matunda hayawezi kugawanyika. Kusoma katika mistari hii kunaonyesha ya kwamba hivi vitu ni kitu kimoja. Hayawezi kugawanyika. Pia, ubora huu wa vitu hivi inatakiwa kupatika kwa kila mkristo

2. Matun day a rooho yameoredheshwa hapa chini. Andika au orodhesha matunda hayo kama yalivyo tajwa kutoka katika, Wagalatia 5:22-23.

MATUNDA YA ROHO

Mtazamo
Hatua

Maombi

(Upendo)
(Uvumili vu)

(Uaminifu)

(Furaha)
(Wema)

(Upole)

(Amani)
(Fadhili)
(Kiasi)

J. Sidlow Baxter, mwalimu wa kingereza wa Biblia na mzungumzaji katika mikutano, alisema matunbda matatu ya Mwanzo yanatuhusus na yanazungumzia sana kuhusu sisi. Mengine hayo matatu yanayoendelea kwa hapo mbele yanahusu watu wengine. Matendo yao yanaangalia nje. Mengine hayo matatu ya mwisho yanaangali juu. Ni muhimu sana haya matunda kuyaelewa. Kwa hiyo haya makundi matatu yanajumuisha mahusiano yetu yote tuliyonayo ndani ya maisha yetu.

UPENDO

Ni ukweli kuwa upendo umeandikwa wa kwanza kabisha .ina maanisha kuwa upendo ni kitu cha msingi sana. 1 Wakorintho 13:13……. Kupenda watu wate kwa kuhusianisha upendo uliopo kati yetu na Mungu. Soma Mathayo 22:34-40……

3. Maisha ya mkristo ni maisha ya upendo. Oanisha vifungu vifuatavyo na rejea sahihi za Biblia.

a. Wakolosai 3:19……
b. Luka 6:27-28…..
c. Tito 2:3-4……
d. Yohana 13: 34-35……
e. Mathayo 22:39……
f. Waefeso 5:2……

……d……. Pendaneni ninyi kwa ninyi.
……f……. Mtawaliwe na upendo.
……c……. Mpende mume wako na watoto wako.
……a……. Mpende mke wako.
……e……. Mpende jirani yako.
……b……. Wapende maadui zako.


Roho Mtakatifu ni pendo. Anatoa upendo kwa wana wa Mungu wote.

Upendo sio tu kama mtazamo, ni Matendo au tendo .upendo hauko s awa na hisia na muda mwingine upendo unaendana sana na hisia za mtu mwenyewe. Lakini upendo ni Matendo ambayo yanahuishwa na msukumo w amtu mwenyewe.
Soma Warumi 12:9-10……

Upendo ni kujitoa, kuna gharama ya kuonesha upendo. Inajumuisha Matendo, kujitoa, muda, umakini au usikivu. Lakini sio lazima .kupenda kama hivi haya yanavyosema haya maeno lakini pia unaweza ukapenda kata kwa kutumia njia nyingine.
Soma Warumi 5:5…… Mungu anatoa pendo lake kwa kupitia Roho Mtakatifu. Hii inatusaidia kumpenda sana kama yeye alivyo tupenda.

FURAHA
Furaha huonekana pale ambapo tunapata bahati nzuri. Tunakuwa na furaha pale ambapo mabo yetu yanakwenda kama ilivyotakiwa kwa upande wetu. Lakini furaha yetu inapotea pale ambapo hali inabadilika katika maisha yetu.

Sisi kama Wakristo tuna fuuraha n dani ya mioyo yetu bila kujali hali gani tunayopitia. Mahusiano yetu na Mungu ni ndio msingi mkuu wa wa ma hhusiano yetu na Mungu. Kwa hiyo furaha haishi na haifikii kikompo. Soma Wafilipi 4:4……

AMANI

Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu am bayo ilipatikana pale Yesu alipokufa msalabani. Inajumuisha amani na Mungu. , amani na watu wengine, na pia amani kwako wewe mwenyewe. Soma Wafiipi 4:6-7……

Rudi katika Yohana 14:27……

4. Ni hali gani katika maisha yake inakusababisha amani alilyokupatia mung kutoweka? Unaweza ukafanya nini ndani ya wiki hii ili usaidiwe kuelewa Mungu zaidi?

UVUMILIVU

Ni kuweza kuvumilia au kutokuwa na kujutia juu ya jambo Fulani. Uvumilivu unajumuisha na huruma. Soma Warumi 15:5…..

5. kuna hali yeyote ndani ya maisha yako ambayo inahitaji uvumilivu?

Uvumilivu ni tabia ya Mungu tunayoikubali sana. Mungu ambaye amekuwa mvumilivua sana na sisi, yuko tayari na Roho wake Mtakatifu kutupatia uvumilivu kila mara tunapo muomba yeye.

WEMA

Wema muda mwingine unaweza ukasema ni upole. Soma Wakolosai 3:12…..

Mungu ni wema kwetu na anatutaka sana na sisi kuwa wema katika mahusiano yetu. Wema wetu kwa watu wengine unamfurahisha Mungu.

Muhimu:katika maswali yafuatayo ,wanapaswa kupanga mipango,na sio maelezo ya tukio au majina ya wahusika.

6. Fikiria hali gani ambayo huwa inakufanya kutokuwa mwema juu ya mafikirio yako au katika majibu yako. Muombe Mungu akupe njia nzuri ya kuwa mwema na kuweza kuwa kama yeye anavyotaka uwe katika hali zote. Andika kuwa majibu yako yatakuwaje .

UKARIMU

Ukarimu au wema ni jumla ya sifa zote za Mungu, kujionesha utakatifu wake, na uuungu wake. Soma Waefeso 2:10………

Mungu ni mwema. Sisi kama watoto wake, tunaweza tukafanya sisi kama sisi ,ili kuona wema wa Mungu unaonekana kwetu, kwa kuwa Roho Mtakatifu yeye anaendelea kuonesha na kukuza zile tabia za kiMungu ndani yetu.

UAMINIFU

Imani inaonesha ujasiri m kub wa tu kwa Mungu. Kwa hio hii inaonehs uwepo wa Mungu katika maisha ya Wakristo. Uaminifu unajionehs mooja kwa moja kwa mtu ambaye ni mwamini. Luka 16:10-12…….

7. ni maeneo gani katika maisha yako unaitaji Roho Mtakatifu kukusaidia ili uwe mwaminifu?..........

Tunapoonesha uaminifu katika maisha yetu, tunaonesha kwa watu wngine kuwa tunamwamini Mungu katika kiila kitu na kujua ukweli. 2 Wathethalonike 3:3……… Je ni sifa zipi ambazo mtu mwaminifu huwa anakuwa nazo?........

(Hakikisha majibu yanajumuisha haaya yafuatayo, kujitoa, kutegemewa, utiifu, uaminifu, hakika, kutegemewa, halisi,anatimiza ahadi)

UNNYEYEKEVU

Unyenyekevu ni kujishusha mbele za Mungu. Mfano halisi ni Yesu.
Soma Wafilipi 2:3-8……..
Unyenyekevu unajumuisha kutokuwa na kujisifu na kuwa na majivuno.

Kama Roho Mtakatifu anapozalisha matuncda ya unyenyekevu , tunajifunza kujisahau. Unyenyekevu kuelewa kuwa Mungu anaweza kufanya kazi kwa kupitia watu wengine ili kutimiza mapenzi yake.

KUJIZUIA

Wakati maisha yetu yapo chini ya utawala wa Roho Mtakatifu, tutaoneha kujizuia hata wakati tunataka, kujaribiwa. Tunatakiwa tusioneshe mazao ambayo hayana mwelekeo. Tunaweza kupata ushindi kwa kuwa ndani yetu tuna Roho wa Mungu ambaye anatuongoza na kutupatia nidhamu. Soma Tito 2:11-12……

Mwandishi Elizabeth George alisema ”Katika Biblia yote, neno tunda linajumuisha kile kitu ambacho kipo ndani. Kama kilichpo ndani ni kizuri, basi matunda ya huyo mtu yatakawa mazuri. Kama kilichomo ndani ni kibaya asi matunda ya huyo mtu yatakuwa ni mabaya tu”.

Kama Wakristo, tunapoendelea kutembea katika roho, tunakuwa kama Yesu Kristo, Yesu alipokuwa hapa d uniano aliweza kufanya mabo mengi sana ambayo alituachia ,ili tuyafuate. Tunapoonehs matunda mazuri ya roho, basi tunauthbitishia ulimwengu kuwa Mungu anaishi ndani yetu usome katika Wafilipi 1:11……

VIPAWA VYA ROHO

Vipawa vya Roho ni tofauti na matunda ya roho. Kila mkristo anapokea kila tunda la roho. Ambapo vipawa vya Roho ni tofauti kidoogo. Kila mkristo ana kipawa angalau kimoja ndani yake lakini sio kila muumini ana kipawa. (1 Wakorintho 12:11).

Angalia ukinzani au utofauuti huu mwingine hapa. Matunda ya Roho yanaimarisha uhusiano na Mungu na watu wengine. Lakini kipawa kinatumika katika kumtumikia Mungu. (1 Petro 4:10).

Vipawa vya kiRoho hivi vinatumika katika kumtumikia Mungu.

8. Lengo la vipawa vya kiRoho ni nini? 1 Petro 4:10……….. ( Tuumia hivy vipawa, kwa ajili ya mazuri kwa wengne)

9. Orodhesha vipawa vilivyotajwa katika mistari ifuatayop.

1 Wakorintho 12:8-10……… (Neno la hekima,maarifa,imani,karama ya kuponya,matendo ya miujiza,unabii,kupambanua Roho,aina za lugha,tafsiri za lugha)

Warumi 12:6-8……… (Kuongea ujumbe wa Mungu,kuhudumia,kufundisha,kuwatia moyo wengine,na kujitoa kwa moyo,kuwa na mamlaka na utu wema)

Roho mtakatifu hutupatia mambo ambayo yanatufaa katika maisha yetu.
1 Wakorintho 12:11………

Hatuhitaji kuwa na wasiwasi kuwa ni karama ipi tunayo au ni karama ipi tunahitaji,lakini tutaendelea kutumia karama hizi kwa kadri tunavyotenda kazi.

Hii haimanishi kuwa tumsubirie Mungu atuambie kuwa karama zetu za rohoni ni nini.tunapoendelea kumtii Mungu kila siku tutajikuta tunaanza kutumia karama za rohoni,mara zote tunagundua tunatumiwa katika eneo lipi pale ambapo Roho wa Mungu hututumia zaidi katika hhuduma furani.na ndipo tunapogundua tunaweza kutumika katika hali ya kimungu kama ya hali ya kawaida kabisa.

10. Andika maombi yako ya kumshukuru Mungu hapa kwa kukupa kipawa na matunda ya kiroho. Mwambie akusaidie ili Roho Mtakatifu aen delee kuleta mengine na kuimariha yaliyopo.

MAOMBI

Baba yetu ulikye mbinguni, asante kwa .kutupa matunda ya kiRoho , ambayo tunaweza kuyaonehs kwa watu wengine tuna poendela kuishi katika dunia hii. As nate kwa kutupa viapawa kwa kila mmoja wetu hapa. Tusaidie ili ,tuweze kufuata mipango yako kw aajili ya utukufu wako. Tunaomba kwa jina la Yesu Kristo……AMEN.

 

 
 

 

This is a translation of 'Who is the Holy Spirit?' Stonecroft's Guide Book Lesson #4 in Swahili, the English version of Who is the Holy Spirit? is available online from Stonecroft's website.

This transforming study will reveal who Jesus is, what He does, and what life is like when He lives within you. Learn what the Holy Spirit does in the life of a Christian and how He can help you grow to be more like Christ. (6 lessons)

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Download Swahili Lesson #4 Guidebook

Download Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #4

Download Swahili Lesson #4 Student Study Book

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us