home >>
stonecroft>>roho
mtakatifu yuko wapi?>>somo
la kwanza (1)>> somo la pili (2)
Stonecroft - Roho Mtakatifu yuko wapi? - Somo la pili (#2)
SOMO LA PILI (2)
KAZI ZA ROHO MTAKATIFU NI ZIPI?
The Guide has her own Guidebook
to help her lead and guide the lesson.
Download Swahili Lesson
#2 Swahili Guidebook
Download
Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #2
LENGO LA SOMO
• Kujifunza je agano la kale linasema nini kuhusukuhusu
Roho Mtakatifu.
• Kujifunza kazi za Roho Mtakatifu ndani ya maisha ya mkristo.
• Kujifunza kuhusu Roho Mtakatifu sehemu ambazo ziliandikwa
ndani ya Biblia.
• Kukubali ulinzi na uwezo war oho Mtakatifu ndani ya maisha
yetu.
MAOMBI
Mungu mwenyezi, asante kwa kutupatia Roho Mtakatifu wakati tunaokoka.
Fungua macho yetu ili tuweze kuona jinsi gani ambavyo anatusaidia
sisi. Tunaomba katika jina la Yesu…………AMEN………
Anza somo kwa kuwashirikisha watu katika kusoma
mistari ya Kibibilia amabyo waliweza kuichagua katika wiki iliyopita.
KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA
(Use your Bible or Africa Bible Verse
Handbook) Soma mistari ya Biblia ifuatayo na uchague ni mistari
mingapi ambayo unafikiri ni ya muhimu sana kwako katika
kila mstari unaousoma.
Yohana 3:1-13
Yohana 3:14-21
Matendo ya mitume 1:1-11
Matendo ya mitume 2:1-13
Matendo ya mitume 2:14-21
Matendo ya miitume 2:36-42 |
MAONI YA KIONGOZI
Tume,kuwa tukijifunza kuhusu maajabu na uhamasisho wa Mungu baba,
Mungu mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Ni Mungu mmoja tu ambaye anajifunuua
kwetu kwa kupitia njia hizi tatu.
Katika somo la kwanza, tulijifunza kuwa Roho Mtakatifualichukua
hatia zetu sana kuhusu dhambi zetu na kutusaidia kupata huu wokovu.
Kujua Roho ya Mungu, tunahitaji kuwa na ufahamu wa ziada sio mhuu
tu ambao tunao ili kuelewa kuwa Mungu yupo na kuwa Yesu alikufa
kwa ajili yetu. Tunatakiwa kumpokea Yesu kama mwokozi wetu. Tunapomkubali
yeye, Mungu yeye anatupatia Roho Mtakatifu.
Katika muda uliopita, Warumi 8:16 inakuwa kweli
katika maisha yetu………….
Tunapomkubali Yesu Kristo kama mwokozi wetu, tunakuwa watoto wa
Mungu. Roho ya Mungu iliyoko ndani yetu inaanza kubadilisa maisha
yetu ili kufanana na Yesu au ili kuwa kama Yesu.
ROHO YA MUNGU KATIKA AGANO LA KALE
Tunaona Roho m takatifu katika kitabu cha kwanza katika Biblia
yaani kitabu cha Mwanzo.
Tulisoma nini kuhusu kazi ya Roho Mtakatifu katika swali la kwanza
kabisa?
1. Tunatambulishwa Roho Mtakatifu
katika mstari wa pili (2) katika agano la kale. Aliitwaje na
alifanya nini? Mwanzo 1:2…………
(Roho ya Mungu ilikuwepo na ilikuwa imetawala
kila sehemu).
|
Biblia inasema kuwa Roho wa Mungu alikuwa na mzhango mkubwa sana
katika uumbaji wa hii dunia. Isaya 40:12-14……….
2. Watu tofauti tofauti walimtolewa Roho Mtakatifu
majina mengi sana ambayo yanafunua kazi yake ndani ya maisha
yetu pia.
Baada ya kila mstari, andika jina ambalo alipewa Roho Mtakatifu
na uoneshe kazi aliyoifanya :
a. Ayubu 33:4…..
Jina: (Roho wa Mungu)
Kazi: (Aliumba watu wote)
b. Ezekieli 36:27……
Jina: (Roho yangu)
Kazi: (Inasaidia watu kuweza kumtii Mungu)
c. Mika 3:8……
Jina: (Roho wa Bwana)
Kazi: (Anatoa nguvu kwa watu ili kuweza kufikisha ujumbe
wa Mungu kwa watu wengine)
d. 2 Samweli 23:2…..
Jina: (Roho wa Bwana)
Kazi: (Anaongea kupitia watu. Mstari huu unasema kuwa
alisema na daudi, ambaye aliandika Zaburi kwa asilimia kubwa
ndani ya Biblia)
|
Ili kurudia, sikiliza tena kuwa kazi ya Roho Mtakatifu katika agano
la kale ilikuwaje. Roho Mtakatifu aliumba watu wote, aliwapa uwezo
wa wao kumtii Mungu, aliwapa watu nguvu ya kusambaza ujumbe wa Mungu,
na aliongea kupitia mtu binafsi.
Agano la kale linafunua zaidi kuhusu Roho Mtakatifu. Anaitwa Roho
ya Bwana, na Roho ya rehema, na Roho ya dua. Majukumu mmengi ya
Roho Mtakatifu yapo katika agano la kale. Soma Isaya 11:2……
ROHO MTAKATIFU KATIKA
AGANO LA KALE Ni Roho wa kweli,
Anafunua ufahamu wa Mungu. |
Ni Roho wa utakatifu,
Huonesha usafi na utakatifu wa Mungu.
Ni Roho wa nguvu,
Kuwatia nguvu kwa wale wote walichagua kazi yake.
Ni Roho wa hekima,
Anaonesha utu halisi wa Mungu.
Ni Roho wa ahadi,
Kuonesha mambo yajayo au wakati ujao. |
Roho Mtakatifu aliwajilia watu katika agano la kale, na kuwatia
nguvu watu hao kwa kazi aliyokuwa Mungu amewapa. Kwa mfano, Mungu
aliruhusu Roho Mtakatifu kumsaidia Bezalel, kwa kazi aliyokuwa amepewa
na katika hema. Soma kuhusu sifa ambazo Mungu alimpa mtu huyu katika
Kutoka 31:3…………
Roho Mtakatifu pia katika agano la kale aliwapa nguvu ya ajabu,
uwezo mkubwa wa kuweza kungoza taifa kubwa .
Agano la kale halisemi kuwa Roho Mtakatifu alikuja kukaa ndani
ya mtu moja kwa moja. Na ndio maana daudi aliomba kwa kadri ya uwezo
wake katika Zaburi 51:11………..
katika nyakati za agano la kale. Mungu alichukua Roho yake kutoka
kwa mtu wakati kazi yake ikiwa imeshakwisha. Katika Zaburi 51 inatuambia
kuwa kutubu kwa daudi na kwa maombi yake akiomba kuwa Mungu asimtoe
Roho wake kutoka kwake.
ROHO MTAKATIFU KATIKA AGANO JIPYA
Ufunuo mkuu kuhusu Roho Mtakatifu ndio umejifunua katika
agano jipya.
Kipindi cha agano jipya, Roho Mtakatifu aliendela na kazi
aliyokuwa nayo tangu alipokuwa katika agano la kale. Aliongea
na watu binafsi, aliwapa ulinzi, na kuwawezesha watu kufanya
vitu ambavyo wamembiwa na Mungu kuvifanya. Lakini kwa nyongeza
tu, katika nyakati za agano jipya na sasa, Roho Mtakatifu
akiingia ndani ya mtu anakaa humu milele yote.
Soma katika Yohana 14:16…..
|
Kwa sasa ukweli kwamba Roho Mtakatifu anakaa ndani ya watu moja
kwa moja (milele), hii ndio tofauti iliyopo kati ya kazi ya Roho
Mtakatifu katika agano la kale na kazi ya Roho Mtakatifu katika
agano jipya.
Hakuna kazi yeyote ya Roho Mtakatifu ambayo iumerekodiwa katika
kipindi cha miaka 400 kati ya kitabu cha mwisho cha agano la kale
na kitabu cha kwanza cha agano jipya. Hakukuwa na nabii aliyekuwa
akiongea au akinena neno la Mungu.
Lakini, baadae mara rooho Mtakatifu akaanza kazi tena ya huduma
, kuandaa kwa kuja kwa Yesu Kristo. Tangu ilipotungwa mimba ya Yesu
Kristo na mpaka mwisho wake Roho Mtakatifu ndiye alikuwa akiongoza
kazi hii ili kufanikiwa na mpango kutimilika.
ROHO MTAKATIFU KATIKA
MAISHA YA KRISTO
3. Agano jipya linaweka wazi kuwa Roho Mtakatifu alikuwa
na kazi ya ziada katika maisha ya kristo. Oanisha mistari
ifuatayo na kazi za Roho Mtakatifu katika maisha ya kristo.
Luka 4:16-18……
Luka 4:1…..
Warumi 8:11……
Matendo 1:1-2……
Mathayo 1:18-20……
a. Kutungwa kwa mimba ya Yesu ilikuwa ni kwa uwezo war oho
Mtakatifu. (Mathayo 1:18-20)
b. Yesu alijazwa na aliongozwa na Roho wa Mungu. (Luka
4:1)
c. Yesu alitiwa mafuta na Roho Mtakatifu ili kuhubiri, kuponya
wagonjwa na vipofu na kuokoa, na kuwajali waliodhulumiwa.
(Luka 4:16-18)
d. Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu kwa uwezo wa Roho ya Mungu.
(Warumi 8:11)
e. Baada ya kufufuka, Yesu aliwafundisha mitume wake kwa uwezo
war oho Mtakatifu.
( Matendo 1:1-2)
|
Mistari hii ya kiBiblia inatuambia kuwa Roho Mtakatifu ana uongozi
mkubwa sana katika maisha ya kristo alipokuwa hapa duniani. Ingawa
Yesu alikuwa na nguvu ndani yake yeye mwenyewe kwa ajili ya kuikamilisha
kazi aliyopewa na Mungu, lakini Yesu aliishi maisha yake hapa duniani
kwa msaada war oho Mtakatifu. Aliisi kama mwanadamu na kutuonesha
kuwa mipango ya Mungu kwetu ikoje na tuweze kuishi kwa namna gani.
Kama Roho ilivyomuongoza Yesu, pia vile vile atatungoza na kutuwezesha
kuishi kama Wakristo kama tutamruhusu kuingia ndani yetu.
KAZI YA ROHO MTAKATIFU KATIKA UANDISHI WA BIBLIA 4.
Tumembiwa kuwa ni jinsi gani ambavyo Biblia 2 Petro
1:21…..
a. nani aliwaambia watu waliondika Biblia kuwa waandike nini?.........
(Roho Mtakatifu)
b. Je, ujumbe ulitokea wapi ?........ (Kwa Mungu) |
Roho Mtakatifu alliwaongoza wote walinadiika vitabu ndani ya Biblia.
Ona kile alichokizungumza Paulo mwandisha wa kitabu cha Wakorintho,
1 Wakoritjo 2:13…..
Roho Mtakatifu alimfundisha Paulo kitu gani afundishe. Je Roho
Mtakatifu alimpa Paulo maneno au mawazo aliyotakiwa kuandika?.......(Roho
Mtakatifu alimpa kila neno kuandika).
Nani alimpa Roho Mtakatifu maneno? Jibu linapatikana katika mstari
tuliousoma katika swali la 4……….(Mungu).
Hii ndiyo sababu tunaita Biblia kuwa ni neno la Mungu. Roho Mtakatifu
alikuwa na waadisha ambao na waume, Mungu alisema.
Biblia ni kitabu pekee ambacho mwandishi yupo muda wowote unapokisoma.
Elezea sentensi hii ina maanisha nini….. (Roho Mtakatifu,
mwandishi wa Biblia, wapo muda wote unaposoma Biblia, au Biblia
inaposomwa).
ROHO MTAKATIFU NDANI YA MAISHA YETU
5. Kila mstari ufuatao wa Biblia, unaonesha hatua Fulani
ya kazi ya Roho Mtakatifu.katika wokovu wetu. Oanisha mistari
hii na sentesi sahihi.
Wagalatia 3:27
Warumi 8:15
2 Wakorintho 3:18
1 Wakorintho 3:16-17
Yohana 6:63
a. Mungu ni mpaji wa maisha, Roho anatupa maisha ya kiroho.
(Yohana 6:63)…….
b. Roho ya Mungu inayoishi ndani yako, inakwambia kuwa wewe
ni m wana wa Mungu. (Warumi 8:15)…….
c. Roho Mtakatifu anakubatiza wewe katika umoja na kristo
unapookolewa.
(Wagalatia 3:27)……..
d. Roho wa Mungu anayeishi ndani yako anakufanya wewe kuwa
hekalu la Mungu.
(1 Wakorintho 3:16-17)…..
e. Roho wa Bwana anabadilisha maisha yetu ili kuonesha utukufu
wa Mungu.
(2 Wakorintho 3:18)……..
6. Cagua aliyeyote ile ndani ya maisha yako ambayo unahitaji
ulinzi war oho Mtakatifu. Eleza mahitaji yako, na kasha andika
maombi yako ukimuomba Roho wa Mungu kukupatia ulinzi unaoutaka
katika eneo hilo ulitakalo katika maisha yako………
|
Chagua mtu ambaye atasema ombi lake mbele ya kundi ili kundi la
mjadala liwe la kuwajibika,baada ya maombi,buni na andika maombi
yako mwenyewe au au tumia haya yafuatayo katika kuhitimisha.
MAOMBI
Baba yetiu uliye juu mbinguni, asante kwa kutuipatia Roho wako
Mtakatifu, ambaye anatupaia nguvu, uwezo wa kufanya yale wewe uyatakayo.
Tusaidie tuweze kutambua sauti yake pale anapoongea na sisi katika
kujibu maombi yetu. Tunataka kuishi maisha ambayo yanakufurahisha
wewe Mungu. Katia jina la Yesu…………
AMEN
|