home >>
stonecroft>>roho
mtakatifu yuko wapi?>>somo la tatu>> mistari ya biblia
Roho
Mtakatifu yuko wapi? - Somo la Tatu #3 - Mistari ya Biblia
Somo 3
Je Roho mtakatifu anaweza kunisadia kukua?
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Yohana 14:1-14
Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu,
niaminini na mimi pia. 2 Katika nyumba ya baba yangu mna nafasi
nyingi. Kama sivyo, nisingeliwaambia kwamba nakwenda kuwaandalia
makao. 3 Na nikishawaandalia, nitarudi kuwachukua mkae pamoja nami;
ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. 4 Ninyi mnajua njia ya kufikia
ninakokwenda.”5 Tomaso akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda;
tutaijuaje njia?”6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia
na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.
7 Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu.
Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.”
8 Filipo akamwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe
Baba yako nasi tutaridhika.”9 Yesu akamjibu, “Filipo,
imekuwaje hunifahamu baada ya mimi kuwa pamoja nanyi muda wote huu?
Mtu ye yote ambaye ameniona mimi, amemwona Baba. Sasa inakuwaje
unasema, ‘Tuonyeshe Baba’? 10 Je, huamini ya kuwa mimi
niko ndani ya Baba yangu, na Baba yangu yuko ndani yangu? Mambo
ninayowaambia siyasemi kwa mamlaka yangu mwenyewe, bali yanatoka
kwa Baba yangu ambaye anaishi ndani yangu, na ndiye anayetenda haya
yote. 11 Niaminini ninapowaambia ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu
na Baba yangu yu ndani yangu. La sivyo, niaminini kwa sababu ya
haya mambo ninayotenda. 12 Ninawaambia hakika, mtu ye yote akiniamini
ataweza kufanya miujiza kama hii na hata zaidi, kwa kuwa mimi ninakwenda
kwa Baba yangu. 13 Kitu cho chote mtakachoomba kwa jina langu, nitawafanyia,
ili Baba yangu apate kutukuzwa kwa yale ambayo mimi Mwanae nitawafanyia.
14 Mkiniomba cho chote kwa jina langu nitawafanyia.”
Yohana 14:15-31
15 “Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu. 16 Nami nitam womba
Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae nanyi siku zote. 17
Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini hawawezi kumpokea.
Watu kama hao hawamwoni wala hawamfahamu. Ninyi mnamfahamu kwa kuwa
anakaa ndani yenu na ataendelea kuwa nanyi. 18 Sitawaacha kama yatima.
Nitarudi kwenu. 19 Baada ya muda mfupi watu wa ulimwengu hawataniona
tena, ila ninyi mta niona; na kwa kuwa mimi ni hai, ninyi pia mtakuwa
hai.
20 Wakati huo utakapofika mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba
yangu na ninyi mko ndani yangu. 21 Mtu anayezishika amri zangu na
kuziti miza ndiye anayenipenda. Na mtu anayenipenda, Baba yangu
atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” 22 Yuda,
siyo Iskariote, akamwuliza, “Bwana, itakuwaje ujidhihirishe
kwetu tu na si kwa ulimwengu mzima?”23 Yesu akamjibu, “Mtu
akinipenda atashika mafundisho yangu na Baba yangu atampenda, nasi
tutafanya makao yetu kwake. 24 Mtu asiyenipenda hayashiki mafundisho
yangu na mafundisho niliyowapeni si yangu bali yametoka kwa Baba
yangu aliyenituma.
25 “Nimewaambia mambo haya wakati nikiwa bado nipo nanyi.
26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu
atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha
yote niliyowaambia. 27 Ninawaachia amani. Nawapeni amani yangu;
amani hii ulimwengu hauwezi kuwapa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala
msiogope.28 Kumbukeni nilivyowaambia, ‘Ninakwenda, na nitarudi.’
Kama kweli mngalinipenda mngefurahi, kwa kuwa nakwenda kwa Baba;
na Baba yangu ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nimewaambia mambo
haya kabla hayajatokea ili yataka potokea mpate kuamini. 30 Sitasema
tena mengi nanyi kwa sababu mtawala wa dunia hii anakuja. Yeye hana
uwezo juu yangu. 31 Lakini ninatii amri ya Baba ili ulimwengu upate
kujua kwamba nampenda Baba. Simameni tuondoke hapa.’ ’
Yohana 15:1-17
‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila
tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila
tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. 3
Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa.
4 Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza
kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi
msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote. 5 Mimi ni mzabibu;
ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa
matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote.
6 Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi
hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani
yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo
nanyi mtatendewa. 8 Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa,
na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu. 9 “Kama
Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivy owapenda ninyi;
dumuni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa ndani
ya pendo langu kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa
katika pendo lake.
11 “Nimewaambia haya kusudi furaha yangu iwe ndani yenu,
nanyi mpate kuwa na furaha iliyokamilika.
12 “Amri yangu ni hii: pendaneni kama nilivyowapenda. 13
Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa
ajili ya rafiki zake.14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza.
15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli
za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia
kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha. 16 Hamkunichagua, bali mimi
nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda
yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu,
awatimizie. 17 Hii ndio amri yangu: pendaneni.
Yohana 15:18-27
18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia
mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu
huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi
si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu.
20 “Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi
aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi na ninyi
pia watawatesa; kama wamelishika neno langu na neno lenu watalishika
pia. 21 Lakini yote haya watawatendea kwa ajili yangu kwa sababu
hawamfahamu Baba yangu ambaye amenituma. 22 Kama sikuja na kusema
nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi
zao. 23 Mtu ye yote anayenichukia mimi anamchukia na Baba yangu.
24 Kama nilikuwa sikuwafanyia miujiza ambayo haijapata kufanywa
na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini
wameona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25
“Hali hii imetokea kama ilivyoandikwa katika Sheria kwamba,
‘Walinichukia pasipo sababu.’ 26 Lakini atakapokuja
yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho
wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Na ninyi
pia ni mashahidi wangu kwa maana tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.”
Yohana 16:1-15
Nimewaambia mambo haya yote ili msipoteze imani mtakapokutana na
matatizo. 2 Watu watawafukuza mtoke katika masinagogi[a] na msirudi
humo tena. Hakika, unakuja wakati watapofikiri kuwa kwa kuwaua ninyi
watakuwa wanatoa huduma kwa Mungu. 3 Watafanya hivyo kwa sababu
hawajamjua Baba, na hawajanijua mimi pia. 4 Nimewaambia haya sasa
ili kuwaandaa. Hivyo wakati wa mambo haya kutimia utakapofika, mtakumbuka
kwamba niliwapa tahadhari mapema.
Kazi za Roho Mtakatifu
Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo, kwa sababu bado nilikuwa pamoja
nanyi. 5 Sasa narudi kwake yeye aliyenituma, ingawa hakuna hata
mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ 6 Nanyi mmejawa
na huzuni kwa vile nimewaambia mambo haya yote. 7 Hakika nawaambieni,
ni kwa faida yenu mimi nikiondoka. Nasema hivi kwa sababu, nitakapoondoka
nitamtuma kwenu Msaidizi. Lakini nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja.
8 Ila huyo Msaidizi atakapokuja, atawaonesha watu wa ulimwengu
jinsi walivyofanya dhambi. Atawaonesha nani ana hatia ya dhambi,
nani ana haki mbele za Mungu, na nani anastahili kuhukumiwa na Mungu.
9 Huyo Msaidizi atawaonesha kuwa wana hatia ya dhambi kwa sababu
hawaniamini mimi. 10 Atawaonesha jinsi wasivyoelewa mtu anavyohesabiwa
haki na Mungu. Hakika mimi nina kibali kwa sababu naenda kwa Baba
nanyi hamtaniona tena. 11 Naye atawaonesha watu wa ulimwengu huu
jinsi hukumu yao isivyo sahihi, kwa sababu mkuu wao ulimwenguni[b]
amekwisha hukumiwa.
12 Ninayo mambo mengi ya kuwaeleza, lakini ni magumu kwenu kuyapokea
kwa sasa. 13 Hata hivyo atakapokuja huyo Roho wa kweli, Yeye atawaongoza
hadi kwenye kweli yote. Hatasema maneno yake mwenyewe bali atayasema
yale tu anayosikia na atawajulisha yale yatakayotokea baadaye. 14
Roho wa kweli atanipa mimi utukufu kwa kuwaeleza ninyi yote aliyopokea
kutoka kwangu. 15 Yote aliyonayo Baba ni yangu pia. Ndiyo sababu
nilisema kwamba Roho atawaeleza yote anayopokea kutoka kwangu.
Yohana 16:16-33
Huzuni Itageuzwa Kuwa Furaha
16 Baada ya kipindi kifupi hamtaniona. Kisha baada ya kipindi kingine
kifupi mtaniona tena.”
17 Baadhi ya wafuasi wake wakaambiana wao kwa wao, “Ana maana
gani anaposema, ‘Baada ya kipindi kifupi hamtaniona tena.
Kisha baada ya kipindi kifupi kingine mtaniona tena?’ Tena
ana maana gani anaposema, ‘Kwa sababu naenda kwa Baba’?”
18 Wakauliza pia, “Ana maana gani anaposema ‘Kipindi
kifupi’? Sisi hatuelewi anayosema.” 19 Yesu alitambua
kuwa wafuasi wake walitaka kumwuliza juu ya jambo hilo. Hivyo akawaambia,
“Je, mnaulizana ninyi kwa ninyi kwamba nilikuwa na maana gani
niliposema, ‘Baada ya kipindi kifupi hamtaniona. Kisha baada
ya kipindi kifupi kingine mtaniona tena’? 20 Hakika nawaambia,
ninyi mtapata huzuni na kulia, bali ulimwengu utakuwa na furaha.
Ndio, mtapata huzuni, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
21 Mwanamke anapojifungua mtoto, hupata maumivu, kwa sababu wakati
wake umefika. Lakini baada ya mtoto kuzaliwa, huyasahau maumivu
yale. Husahau kwa sababu huwa na furaha kwa kuwa mtoto amezaliwa
ulimwenguni. 22 Ndivyo ilivyo hata kwenu pia. Sasa mna huzuni lakini
nitawaona tena, nanyi mtafurahi. Mtakuwa na furaha ambayo hakuna
mtu atakayewaondolea. 23 Katika siku hiyo, hamtapaswa kuniuliza
mimi kitu chochote. Nami kwa hakika nawaambia, Baba yangu atawapa
lo lote mtakalomwomba kwa jina langu. 24 Hamjawahi kuomba lo lote
kwa namna hii hapo awali. Bali ombeni kwa jina langu nanyi mtapewa.
Kisha mtakuwa na furaha iliyotimia ndani yenu.
Ushindi Dhidi ya Ulimwengu
25 Nimewaambia mambo haya kwa kutumia maneno yenye mafumbo. Isipokuwa
utakuja wakati ambapo sitatumia tena maneno ya jinsi hiyo kuwaeleza
mambo. Nami nitasema nanyi kwa maneno ya wazi wazi juu ya Baba.
26 Kisha, mtaweza kumwomba Baba vitu kwa jina langu. Sisemi kwamba
nitapaswa kumwomba Baba kwa ajili yenu. 27 Baba mwenyewe anawapenda
kwa sababu ninyi mmenipenda mimi. Naye anawapenda kwa sababu mmeamini
kwamba nimetoka kwa Mungu. 28 Mimi nimetoka kwa Baba kuja ulimwenguni.
Sasa naondoka ulimwenguni na kurudi kwa Baba.”
29 Kisha wafuasi wake wakasema, “Tayari unaongea nasi wazi
wazi. Hutumii tena maneno yanayoficha maana. 30 Sasa tunatambua
kuwa unajua mambo yote. Wewe unajibu maswali yetu hata kabla hatujayauliza.
Hii inatufanya tuamini kwamba ulitoka kwa Mungu.”
31 Yesu akasema, “Kwa hiyo sasa mnaamini? 32 Basi nisikilizeni!
Wakati unakuja mtakapotawanywa, kila mmoja nyumbani kwake. Kwa hakika,
wakati huo tayari umekwisha fika. Ninyi mtaniacha, nami nitabaki
peke yangu. Lakini kamwe mimi siko peke yangu, kwa sababu Baba yupo
pamoja nami.
33 Nimewaambia mambo haya ili muwe na amani ndani yangu. Katika
ulimwengu huu mtapata mateso. Lakini muwe jasiri! Mimi nimeushinda
ulimwengu!”
1. a. 1 Yohana 2:27
27 Lakini yule Roho Mtakatifu mliyempokea anakaa ndani yenu wala
hamhitaji mtu kuwafundisha. Lakini kama vile huyo Roho Mtakatifu
anavyowafundisha mambo yote, naye ni wa kweli wala si wa uongo;
kama alivyowafundisha, dumuni ndani yake.
b. Yohana 16:13-14
13 Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye
hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia.
Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa
maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.
c. Warumi 8:14
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.
d. Wagalatia 5:22-23
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema,
fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo
kama haya
e. Matendo 1:8
8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi
mwisho wa dunia.”
Marko 1: 35
35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda
mahali pa faragha, akaomba.
2. Warumi 8:26
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu
hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu
usioelezeka kwa maneno.
1 Yohana 5: 14-15
14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho
chote sawa na mapenzi yake, atatusikia.15 Na tukijua kwamba anatusikia
kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale
tuliyomwomba.
3. a. 1 Tessalonike 5:17
17 ombeni pasipo kukoma,
4. a. Mathayo 6:5-6
5 “Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda
kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane
na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6 Unaposali,
nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini.
Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.
b. Zaburi 55:17
Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua,Naye ataisikia
sauti yangu.
1 Wakorintho 1: 18
18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini
kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
Utiifu
6. Yakobo 1:22-25
22 Basi muwe watendaji wa neno na wala msiwe wasikilizaji tu, ambao
wanajidanganya wenyewe. 23 Kwa maana kama mtu ni msi kilizaji tu
wa neno na wala hatekelezi alilosikia, atafanana na mtu ajitazamaye
uso wake katika kioo, 24 na baada ya kujiona alivyo, huenda zake
na mara moja husahau anavyofanana. 25 Lakini mtu anayeangalia kwa
makini katika sheria kamilifu, ile sheria iletayo uhuru, na akaendelea
kufanya hivyo bila kusahau alichosi kia, bali akakitekeleza, atabarikiwa
katika kile anachofanya.
Wagalatia 5:17
17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana na Roho; na Roho hushindana
na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana, na kwa sababu hiyo ninyi
hamwezi kufanya yale mnayotaka.
1 Wakorintho 10:13
13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu.
Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu.
Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.
7. Waefeso 4:25-32
25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu
yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26 Mkikasirika,
msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa
she tani nafasi. 28 Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa
mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada.
29 Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo
yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji
yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30 Na msimhuzunishe
Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa
siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira,
ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32 Muwe wema na wenye
mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe
kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru.
Waefeso 4:30
30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu
wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi.
1 Wakorintho 6:19-20
19 Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa
ndani yenu, ambaye mme pewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe;
20 mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili
yenu.
8. Wagalatia 5: 16
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute
kutimiza tamaa za mwili.
|