Somo la 5
Kuishi katika nguvu za Roho mtatifu
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Wagalatia 5:16-26
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute
kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana
na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana,
na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18 Lakini
kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria. 19 Basi matendo
ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi,20
kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano,
uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana
na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu
watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu. 22 Lakini
tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu, wema, fadhili,
uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga mambo kama
haya.
24 Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili
pamoja na tamaa zake.25 Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho
wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26 Tusiwe watu wenye maji
vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo
Warumi 6:1-11
Tusemeje basi? Tuendelee kutenda dhambi ili neema izidi kuongezeka?2
Hata kidogo! Itawezekanaje sisi tuliokufa kwa mambo ya dhambi,
tuendelee tena kuishi humo? 3 Au hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa
katika Kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? 4 Kwa hiyo tulikufa
na kuzikwa naye kwa njia ya ubatizo ili kama vile Kristo alivyofufuliwa
kutoka kwa wafu kwa nguvu na utukufu wa Baba, sisi pia tupate
kuishi maisha mapya. 5 Kwa maana ikiwa tumeunganika naye katika
kifo chake, basi tutaunganika naye katika kufufuka kwake. 6 Tunafahamu
kwamba mwili wetu wa asili ulisulubiwa msalabani pamoja na Kristo
ili mwili wetu wa dhambi uharibiwe kabisa na tusiwe tena watumwa
wa dhambi.
7 Kwa maana mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi. 8 Lakini
ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja
naye.
9 Kama tujuavyo, Kristo alikwisha kufufu liwa kutoka
kwa wafu kwa hiyo hafi tena; kifo hakina mamlaka juu yake tena.
10 Alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, lakini maisha anayoishi
anamwishia Mungu.
11 Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kujihesabu kuwa
wafu kwa mambo ya dhambi bali hai kwa Mungu mkiwa ndani ya Kristo
Yesu.
Warumi 6:12-19
12 Basi, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ambayo
ni ya muda, iwafanye mzifuate tamaa za mwili. 13 Msiku bali kutoa
sehemu yo yote ya miili yenu itumike kama vyombo vya uovu kutenda
dhambi. Bali jitoeni kwa Mungu kama watu waliotolewa kutoka katika
kifo wakaingizwa uzimani. Pia toeni sehemu zote za miili yenu
zitumike kama vyombo vya haki. 14 Kwa maana dhambi haitakuwa na
mamlaka juu yenu kwa sababu hamtawaliwi na sheria bali mnatawaliwa
na neema. Watumwa Wa Haki
15 Tufanyeje basi? Tuendelee kutenda dhambi kwa
kuwa hatutawa liwi na sheria bali tuko chini ya neema? La , sivyo!
16 Hamfahamu kuwa kama mkijitoa kumtumikia mtu na kumtii kama
watumwa basi mnakuwa watumwa wa huyo mnayemtii? Mnaweza kuwa watumwa
wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti au mnaweza kuwa watumwa
wa utii ambao huleta haki.17 Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa
ninyi ambao mlikuwa watumwa wa dhambi mmetii kwa moyo wote mafundi
sho mliyopewa. 18 Mmewekwa huru, mbali na dhambi na mmekuwa watumwa
wa haki. 19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu
wenu wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa
ajili ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na
zaidi, sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.
Warumi 6:20-23
20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 21
Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea
aibu? Mwisho wa mambo hayo ni kifo. 22 Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa
huru kutokana na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata
ni utakaso, na hatimaye, uzima wa milele. 23 Kwa maana mshahara
wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika
Kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 8:1-8
1 Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani
ya Kristo Yesu.
2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka
huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile
ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili
wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake
wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili
ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya
haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na
wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.
5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili
yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale
waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya
Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni
kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani.
7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa
Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa
kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza
Mungu .
Warumi 8:9-17
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa
na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye
yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini
kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa
sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa
haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka
kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka
kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo
Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu,
hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana
mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza
matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu
ni wana wa Mungu.15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa
wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho
huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho
mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana
wa Mungu.
17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa
Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye
ili pia tutukuzwe pamoja naye.
2. Waefeso 1:18-20
18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate
kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu
wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika
ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu
kuu 20 ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka
akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni.
2 Wakorintho 13:4
4 Kwa maana alisu lubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu
za Mungu. Hali kadhalika sisi ni wadhaifu ndani yake, lakini kwa
nguvu za Mungu tutaishi pamoja naye ili tuweze kuwahudumia.
Waefeso 2:10
10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika
Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa,
tuishi katika hayo.
3. Waefeso 5:18-20
18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho.
19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za
rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati
wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana
wetu Yesu Kristo.
1 Wakorintho 3: 1-3
1Lakini ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho,
bali kama watu wa mwili, na kama watoto wachanga katika Kristo.2
Niliwalisha maziwa, sio chakula kigumu; kwa kuwa mli kuwa hamjawa
tayari kukipokea. 3 Kwa maana ninyi bado mnatawaliwa na mambo
ya mwili. Je, wakati kuna wivu na kugombana kati yenu, ninyi si
watu wa mwili wenye tabia kama za watu wa kawaida?
Matendo Ya Mitume 9: 17; 20
17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani. Akaweka mikono yake
juu ya Sauli akasema, “Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea
njiani ame nituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.”
20 bila kukawia akaenda katika sinagogi akawash
uhudia watu kwamba, “Yesu ni Mwana wa Mungu.”
4. Warumi 6:19
19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu wenu
wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa ajili
ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi,
sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.
Warumi 12:1
1 Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu,
jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu,
ambayo ndio ibada yenu ya kiroho.
1 Petro 4:19
19.Basi wale wanaoteswa kufuatana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi
kwa Muumba wao aliye mwaminifu.
Warumi 12:2
2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia
zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi
ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.
Warumi 8:1-5
1 Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani
ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo
Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu
amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu
wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana
wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa
ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa
ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho
na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.