Somo la 2
Roho mtakatifu ana kazi gani?
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Yohana 3:1-13
Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo,2
alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe
ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya
miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”
3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu
asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”
4 Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima
azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa
mara ya pili?”
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama
mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme
wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa
kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba
huna budi kuzaliwa mara ya pili.8 Upepo huvuma po pote upendapo.
Mvumo wake unausikia lakini huwezi ukafahamu utokako wala uen
dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
9 Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”10
Yesu akamwambia, “Wewe ni mwalimu mashuhuri wa Waisraeli
na huyaelewi mambo haya? 11 Ninakwambia kweli, sisi tunazungumza
lile tunalo lijua na tunawashuhudia lile tuliloliona, lakini hamtaki
kutu amini! 12 Ikiwa hamuniamini ninapowaambia mambo ya duniani,
mtaniaminije nitakapowaambia habari za mbinguni? 13 Hakuna mtu
ye yote ambaye amewahi kwenda juu mbinguni isipokuwa mimi Mwana
wa Adamu niliyeshuka kutoka mbinguni.
Yohana 3:14-21
14 Na kama Musa alivyomwi nua yule nyoka kule jangwani, vivyo
hivyo mimi Mwana wa Adamu sina budi kuinuliwa juu15 ili kila mtu
aniaminiye awe na uzima wa milele . 16 “Kwa maana Mungu
aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu
amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17 Maana Mungu
hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe ulimwengu.18
Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa
sababu hakumwamini Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hukumu yenyewe
ni kwamba: Nuru imekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza
kuliko nuru kwa sababu matendo yao ni maovu.20 Kwa kuwa kila mtu
atendaye maovu huchu kia nuru, wala hapendi kuja kwenye nuru ili
matendo yake maovu yasifichuliwe. 21 Lakini kila mtu anayeishi
maisha ya uaminifu huja kwenye nuru, kusudi iwe wazi kwamba matendo
yake yanatokana na utii kwa Mungu.”
Matendo 1:1-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia
kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni.
Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia
ya Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku
arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi
ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii,
“Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa
Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza
kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati
huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”
7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati
na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini
mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi
wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho
wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na
wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho
yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili
waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi
watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu
huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona
akienda mbinguni.”
Matendo 2:1-13
Ilipofika siku ya Pentekoste, waamini wote walikuwa wameku tana
mahali pamoja. 2 Ghafla, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliwashukia
kutoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wamekaa.
3 Pakatokea kitu kama ndimi za moto ambao uligawanyika
ukakaa juu ya kila mmoja wao.4 Wote walijazwa Roho Mtakatifu wakaamza
kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kusema.
5 Wakati huo walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha
Mungu kutoka nchi zote za dunia.
6 Waliposikia kelele hizi, walikusany ika kwa wingi.
Wote walishangaa kwa sababu waliwasikia waamini wakiongea lugha
ya kila mmoja wao.
7 Wakastaajabu sana, wakasema, “Hawa wote
wanaozungumza ni Wagalilaya. 8 Imekuwaje basi tunawasikia wakinena
lugha ya kila mmoja wetu? 9 Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami,
wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia,
Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni
kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi. 11
Watu wen gine wametoka Krete na Uarabuni. Sisi sote tunasikia
watu hawa wakisema katika lugha zetu wenyewe mambo makuu ya ajabu
aliyofa nya Mungu.” 12 Wakiwa wameshangaa wakaulizana, “Ni
nini maana ya mambo haya?” 13 Lakini wengine waliwadhihaki
wakasema, “Hawa wamelewa divai mpya!”
Matendo 2:14-21
14 Ndipo Petro akasimama na wale mitume kumi na mmoja, aka hutubia
ule umati wa watu kwa sauti kuu akasema, “Wayahudi wen zangu
na ninyi nyote mkaao Yerusalemu. Nisikilizeni kwa makini niwaambie
jambo hili maana yake ni nini! 15 Hawa watu hawakulewa kama mnavyodhania,
kwa maana sasa ni mapema mno, saa tatu asu buhi. 16 La, jambo
hili lilitabiriwa na Nabii Yoeli aliposema, 17 ‘Mungu alisema,
siku za mwisho nitawamiminia binadamu wote Roho yangu: wavulana
wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee
wataota ndoto. 18 Ndio, hata watumishi wangu wa kiume na wa kike
nitawamiminia Roho yangu, nao watata biri. 19 Nami nitafanya maajabu
angani, na duniani nitaonyesha ishara, damu na moto na moshi mnene.
20 Jua litageuka kuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,
kabla ya siku ya Bwana kuwa dia, siku ambayo itakuwa ya kutisha.
21 Lakini ye yote ata kayetubu na kukiri jina la Bwana, ataokoka.’
Matendo 2:36-42
36 “Basi nataka niwahakikishie Waisraeli wote ya kuwa, Mungu
amemfanya huyu Yesu ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa ndiye
37 Watu waliposikia maneno haya yaliwachoma moyoni, wakawau liza
Petro na wale mitume wengine, “Tufanye nini ndugu zetu?”
38 Petro aliwajibu, “Tubuni, muache dhambi
na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe
dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 39 Kwa maana
ahadi hii ilitolewa na Mungu kwa ajili yenu na watoto wenu, na
wale wote walio nchi za mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu
wetu anamwita kwake.”
40 Petro aliwasihi kwa maneno mengine mengi na kuwaonya
akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kiovu.” 41 Wote
waliopokea ujumbe wa Petro walibatizwa na zaidi ya watu elfu tatu
wal iongezeka katika kundi la waamini siku hiyo.
42 Waamini hawa walitumia muda wao wakifundishwa
na mitume, wakiishi pamoja katika ushirika, wakila pamoja na kusali.
43 Watu wote wakajawa na hofu kwa maana miujiza mingi na maajabu
yalifanywa na mitume.
Warumi 8:16
16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi
ni wana wa Mungu.
1. Mwanzo 1:2
Nayo nchi ilikuwa ukiwa nayo tupu, na giza lilikuwa juu ya uso
wa vilindi vya maji, Roho wa Mungu akatulia juu ya uso wa maji
Isaya 40:12-14
Ni nani aliye yapima maji kwa konzi ya mkono wake? Na kuzikadiri
mbingu kwa shubiri? Na kuyashika mavumbi ya dunia katika pishi,na
kuipima milima kwa uzani, na vilima kama kwa mizani, ni nani aliye
mwongoza Roho wa Bwana na kumfundisha kwa kuwa mshauri wake? Alifanya
shauri na nani ni nani aliye mwelimisha na kumfunza njia ya hukumu
na kumfunza maarifa.
2. a. Ayubu 33:4
Roho wa Mungu ameniumba, na Pumzi ya mwenyezi hunipa uhai.
b. Ezekiel 36:27
Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria
zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu na kuzitenda.
c. Mika 3:8
Bali mimi hakika nimejaa nguvu kwa Roho ya Bwana, nimejaa hukumu
na uwezo nimhukumu yakobo kosa lake, na Izraeli dhambi zake.
d. 2 Samweli 23:2
Roho wa Bwana alinena ndani yangu na neno lake likawa ulimini
mwangu.
Isaya 11:2
Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho wa hekima na ufahamu, Roho
wa ushauri na uweza, Roho wa maarifa na kumcha Bwana.
Kutoka 31:3
Nami nimemjaza Roho wa Mungu katika hekima na maarifa na ujuzi
na mambo ya kazi ya kila aina.
Zaburi 51:11
Usinitenge na uso wako,
Wala Roho wako Mtakatifu usiniondolee.
Roho Mtakatifu katika agano jipya
Roho Mtakatifu katika agano jipya
Yohana 14:16
16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae
nanyi siku zote
Luka 4:16-19
16 Baadaye Yesu akaenda Nazareti, mahali alipokulia. Siku ya sabato
alikwenda katika sinagogi kama kawaida yake. Akasimama ili asome
Maandiko. 17 Akapewa kitabu cha nabii Isaya, akakifun gua mahali
palipoandikwa: 18-19 “Roho wa Bwana yu juu yangu. Amenichagua
kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatan gazia wafungwa
kuwa wako huru, kuwaambia vipofu kuwa wanaweza kuona tena; na
kuwaweka huru wanaoonewa, na nitangaze mwaka ambao Bwana atawabariki
watu wake.”
Luka 4:1-2a
Kisha Yesu, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akarudi kutoka Yordani
akaongozwa hadi jangwani. Alikaa huko jangwani siku arobaini 2
akijaribiwa na shetani.
Warumi 8:11
11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu
anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu
ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho
wake ambaye anaishi ndani yenu.
Matendo 1:1-2
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia
kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni.
Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia
ya Roho Mtakatifu.
Mathayo 1:18-20
18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake,
alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Mar ia akiwa
bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa
kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake
Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri.
20 Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa
Bwana akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi,
usisite kumwoa Maria mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata
kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
4. 2 Petro 1:21
21 Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu,
bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho
Mtakatifu.
1 Wakorintho 2: 13
13 Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa
na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho,
nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho.
Roho Mtakatifu katika maisha yetu
5. Wagalatia 3:27
27 Kwa maana nyote mliobatizwa katika Kristo, mmemvaa Kristo.
Warumi 8:15
15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini
mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza
kumwita Mungu, “Abba! Baba!”
2 Wakorintho 3:18
18 Na sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa tunaonyesha, kama
kwenye kioo, utukufu wa Bwana. Nasi tunabadilishwa tufanane naye,
kutoka utukufu hadi utukufu wa juu zaidi, ambao unatoka kwa Bwana
ambaye ni Roho.
1 Wakorintho 3:16-17
16 Je, hamjui kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu, na kwamba Roho
wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu
la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa sababu Hekalu la Mungu
ni takatifu, na ninyi ni Hekalu hilo.
Yohana 6:63
63Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai
kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima.