Somo la 1
Kutambua uwepio wa Roho Mtakatifu
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
1. Yohana 14:26
26 Lakini yule Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu
atamtuma kwenu kwa jina langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha
yote niliyowaambia.
Yohana 4: 24
24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika
roho na kweli.”
2. Yohana 15:26
26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa
Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia
mimi.
Matendo 13:2
2 Umati mkubwa mno wa watu wakasongamana hata ikabidi aingie katika
mashua akaketi humo; na wale watu wakakaa ukingoni mwa bahari.
Warumi 8:14
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu.
Warumi 8:26
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu
hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu
usioelezeka kwa maneno.
3. 2 Wakorintho 1:21-22
21 Ni Mungu mwenyewe ambaye anatuwezesha sisi na ninyi kusimama
imara katika Kristo. Ametuweka wakfu; 22 ametutia mhuri wake juu
yetu, akatupa Roho wake mioyoni mwetu kama uthibitisho.
4. Yohana 16:7-11
7 Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu
kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda
nitamtuma aje kwenu. 8 Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu
dhambi, haki na hukumu. 9 Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini;
10 kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena;
11 na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha
kuhukumiwa.
Yuda 1: 14-16
14 Henoki, ambaye alikuwa wa kizazi cha saba baada ya Adamu, alitoa
unabii kuhusu watu hawa akasema, “Sikilizeni! Nilimwona
Bwana akija na watakatifu wake maelfu kwa maelfu 15 kutoa hukumu
kwa wote na kuwaadhibu wasiomcha Mungu, kwa ajili ya matendo yao
maovu waliyoyatenda na kwa ajili ya maneno makali ambayo hao waovu
wasiomcha Mungu walisema juu yake.”
16 Watu hawa ni wanung’unikaji, wakaidi, wenye
kufuata tamaa zao, wenye majivuno, wenye kujigamba na ambao huwasifu
watu wen gine ili mambo yao yafanikiwe.
Warumi 6: 23
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu
ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
5. Yohana 3:5-7
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa
kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6
Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho
na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna
budi kuzaliwa mara ya pili.
Tito 3:4-7
4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa,
5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda,
bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa
mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye
Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu.
7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi
wa uzima wa milele tunaoutumainia.
Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa
Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima
wa milele.
6. Ufunuo 22:17
17 Roho na bibi harusi wanasema, “Njoo!” Na kila mtu
asi kiaye na aseme, “Njoo!” Na mtu ye yote mwenye
kiu na aje, na kila anayetaka na apokee zawadi ya maji ya uzima
bure.
Yohana 10:30
30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.
7. I Wakorintho 2:11
11 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye
ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya
Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.
Waebrania 9:14
14 damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe
kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu
zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia
Mungu aliye hai.
Warumi 8:2, 10
2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka
huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti.
10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa
miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa
sababu mmek wisha kuhesabiwa haki.