Somo la 4
Nawezaje kuwa mkristo nizaae matunda?
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea biblia katika Juma
1 Wakorintho 13:1-13
Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za
malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au
toazi. 2 Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na
maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha
milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3 Kama nikitoa mali yote
niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina
upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna
wivu au majivuno.
5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti
kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya.
6 Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia
yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.
8 Upendo hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma; zikiwepo
lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha. 9 Kwa maana tunafa
hamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu. 10 Lakini uka
milifu utakapokuja, yale yasiyo kamili yatakwisha. 11 Nilipokuwa
mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo,
nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo
ya kitoto. 12 Kwa maana sasa tunaona sura kama ya kwenye kioo,
lakini wakati huo tutaona uso kwa uso. Sasa nafahamu kwa sehemu,
wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile ninavyo faha mika
kikamilifu.
13 Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini
na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.
Warumi 8:1-8
Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya
Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo
Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu
amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu
wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana
wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa
ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa
ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho
na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.
5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili
yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale
waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya
Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni
kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani.
7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa
Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa
kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza
Mungu .
Warumi 8:9-17
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa
na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye
yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini
kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa
sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa
haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka
kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka
kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo
Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu,
hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana
mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza
matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu
ni wana wa Mungu.15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa
wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho
huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho
mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana
wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi
wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja
naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.
1 Wakorintho 12:1-11
Sasa kuhusu karama za Roho Mtakatifu ndugu zangu, sipendi mkose
kufahamu. 2 Mnajua kwamba mlipokuwa hamumjui Mungu mlivutwa na
kupotoshwa na sanamu bubu.
3 Kwa hiyo napenda mfahamu ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa
na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu alaaniwe.”
Pia hakuna mtu awezaye kukiri, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa
ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4 Basi kuna aina mbalimbali za karama,
lakini Roho ni mmoja. 5 Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini
Bwana ni mmoja. 6 Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini
ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu.7 Roho Mtakatifu
hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote. 8 Maana mtu mmoja
hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la
ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani
na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho
humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine
uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina
za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho
huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila
mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.
1 Yohana 4:7-21
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu
mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye
na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo
Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa
pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake.
10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba
yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia
dhambi zetu.11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho,
sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona
Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo
wake unakamilika ndani yetu. 13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani
yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake.
14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe
mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana
wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu.
16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi.
Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na
Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili
tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu
huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo
ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na
adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda
kwa sababu yeye alitupenda kwanza.
20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na
huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda
ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona.
21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda
Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.
Wagalatia 5:16-26
16 Kwa hiyo nasema, mruhusuni Roho atawale maisha yenu na msitafute
kutimiza tamaa za mwili. 17 Kwa maana tamaa za mwili hushindana
na Roho; na Roho hushindana na tamaa za mwili. Roho na mwili hupingana,
na kwa sababu hiyo ninyi hamwezi kufanya yale mnayotaka. 18 Lakini
kama mkiongozwa na Roho, hamko tena chini ya sheria.
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya:
uasherati, uchafu, ufisadi,20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi,
wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi
na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha
waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi
Ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani,
uvumili vu, wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria
inayopinga mambo kama haya.
24 Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili
pamoja na tamaa zake.25 Kwa kuwa tunaishi kwa kuongozwa na Roho
wa Mungu, basi tufuate uongozi wake. 26 Tusiwe watu wenye maji
vuno, tusichokozane na wala tusioneane wivu. Kuchukuliana Mizigo
1 Yohana 1: 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwa minifu na wa haki na atatusamehe
dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.
1. Wagalatia 5: 22-23
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumili vu,
wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi. Hakuna sheria inayopinga
mambo kama haya.
1 Wakorintho 13:13
13 Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo.
Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.
Matayo 22: 34-40
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha
Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu
wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu,
ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?” 37 Yesu akamjibu, “Mpende
Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na
kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza.
39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani
yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa
sheria zote na Maandiko ya manabii.”
3, Walosai 3:19
19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu wala msiwe wakali juu yao.
Luka 6:27-28
27 “Sikieni niwaambie, wapendeni adui zenu. Watendeeni mema
wanaowachukia. 28 Wabarikini wanaowalaani, waombeeni mema wanaowaumiza.
Tito 2:3-4
3 Hali kadhalika akina mama wazee wawe na mwenendo wa unyenyekevu.
Wasiwe wachonganishi, wala wasiwe watumwa wa pombe; bali waonyeshe
mfano mwema. 4 Hivyo wawafundishe akina mama vijana kuwapenda
waume zao na watoto wao
Yohana 13:34-35
34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi
nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana
hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”
Mathayo 22:39
39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani
yako kama nafsi yako.’
Waefeso 5:2
2 Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa
kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.
Warumi 12:9-10
9 Upendo wenu uwe wa kweli. Chukieni uovu, mshikilie yaliyo mema.10
Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine
kuliko mnavyojiheshimu wenyewe.
Warumi 5:5
5 Tukiwa na tumaini hatuwezi kukata tamaa kwa sababu Mungu amekwisha
kumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu
ambaye ni zawadi tuliyopewa na Mungu.
Wafilipi 4:4
4 Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini!
Wafilipi 4:6-7
6 Msifadhaike juu ya jambo lo lote; lakini katika kila jambo mjulisheni
Mungu haja zenu, kwa kusali na kuomba pamoja na kushu kuru 7 Na
amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo yenu
na nia zenu kwa Kristo Yesu.
Yohana 14: 27
27 Ninawaachia amani. Nawapeni amani yangu; amani hii ulimwengu
hauwezi kuwapa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.
4. Warumi 15:5
5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo
wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu,
5. Wakolosai 3:12
12 Basi, kwa kuwa ninyi ni wateule wa Mungu, wapendwa na watakatifu,
vaeni moyo wa huruma, wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
6. Waefeso 2:10
10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika
Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa,
tuishi katika hayo.
Luka 16:10-12
10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa
mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu
katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11
Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni
nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa
waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu
wenyewe?
2 Wathesalonike 3:3
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana
na yule mwovu.
7. Wafilipi 2:3-8
3 Msifanye jambo lo lote kwa ajili ya ubinafsi au kwa kujiona,
bali kuweni wanyenyekevu, mkiwahesabu wengine kuwa bora kuliko
ninyi.
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu ajishughulishe
pia kwa faida ya wengine. 5 Muwe na nia kama ile aliyokuwa nayo
Kristo Yesu; 6 yeye kwa asili alikuwa sawa na Mungu, lakini hakuona
kwamba kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kush ikilia sana. 7 Bali
alikubali kuacha vyote, akachukua hali ya mtumishi, akazaliwa
na umbo la wanadamu. 8 Alipochukua umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza
akawa mtii mpaka kufa, tena kifo cha msalaba.
Tito 2:11-12
11 Kwa maana neema ya Mungu iletayo wokovu imedhihirishwa kwa
watu wote. 12 Neema hiyo inatufundisha kukataa uovu na tamaa za
dhambi, tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu,
katika ulimwengu huu. Wakati huo huo.
1 Wakorintho 12:11
11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa
karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.
1 Wakorintho 12:11
11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa
karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.
8. 1 Petro 4:10
10 Kila mmoja na atumie kipawa alichopewa kuwahudumia wengine,
kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu.
9. 1 Wakorintho 12:8-10
8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine
hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine
hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo
huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii,
mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine
aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha.
Wafilipi 1:11
11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo,
ili Mungu apewe utukufu na sifa.
Warumi 12: 6-8
6 Tumepewa vipawa tofauti kulingana na neema tuliy opokea kutoka
kwa Mungu. Kama mtu ana kipawa cha kutoa unabii basi akitumie
kulingana na imani yake. 7 Kama kipawa chake ni kuwahudumia wengine,
basi awahudumie. Kama ni kufundisha, basi na afundishe. 8 Kama
kipawa chake ni kuwatia moyo wengine, na afanye hivyo. Kama ni
ukarimu, basi na atoe kwa moyo. Mwenye kipawa cha uongozi na afanye
hivyo kwa bidii. Mwenye kipawa cha huruma na aonyeshe huruma yake
kwa furaha.