home >>
stonecroft>>
mwongozo >>
somo 5 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #5
Nani awezaye kumjua Mungu?
Mistari ya Biblia
Usomaji wa Biblia wa kila juma
Yohana 14:21-23
21 Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda.
Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha
kwake.” 22 Yuda, siyo Iskariote, akamwuliza, “Bwana,
itakuwaje ujidhihirishe kwetu tu na si kwa ulimwengu mzima?”23
Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika mafundisho yangu na
Baba yangu atampenda, nasi tutafanya makao yetu kwake.
Warumi 5:6-9
6 Yesu alipomwona amelala hapo, na akijua kwamba amekuwa katika
hali hiyo kwa muda mrefu, alimwul iza, “Unataka kupona?”7
Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, sina mtu wa kuniingiza bwawani
maji yanapotibuliwa. Ninapoanza kwenda bwawani, mgonjwa mwingine
huniwahi akaingia kabla yangu.” 8 Yesu akamwambia, “Simama,
chukua mkeka wako, utembee!” 9 Mara moja yule mtu akapona,
akachukua mkeka wake, akaanza kutembea! Jambo hili lilitokea siku
ya sabato.
1 Timotheo 2:1-6
Basi, kwanza kabisa, naagiza kwamba dua, sala, maombezi na shukrani
zitolewe kwa ajili ya watu wote: 2 kwa ajili ya wafalme na wote
wenye mamlaka, ili tupate kuishi maisha ya utulivu na amani, tukimcha
Mungu na kuwa wenye heshima kwa kila njia. 3 Jambo hili ni jema
na linampendeza Mungu Mwokozi wetu 4 ambaye anapenda watu wote waokolewe
na wapate kuijua kweli. 5 Maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja
kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Kristo Yesu, 6 aliyejitoa
mwenyewe kuwa fidia kwa ajili ya wote. Yeye ni uthibitisho wa mambo
haya, uliotolewa kwa wakati wake.
Yakobo 4:7-10
7 Kwa hiyo, jinyenyekezeni kwa Mungu . Mpingeni shetani, naye atawakimbia.
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Takaseni mikono yenu, ninyi
wenye dhambi; na takaseni mioyo yenu, ninyi wenye nia mbili.9 Huzunikeni,
ombolezeni na kulia. Kicheko chenu kiwe kilio na furaha yenu iwe
huzuni. 10 Jinyenyekezeni mbele za
2 Petro 3:9
9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama watu wengine wanavyochukulia
kukawia, bali yeye anawavumilia, maana hapendi mtu ye yote aan gamie,
bali wote waifikie toba.
Waebrania 11:6
6 Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu
anayemjia ni lazima aamini kuwa yupo na kwamba yeye huwapa tuzo
wale wanaomtafuta kwa bidii.
Mathayo 11:27-30
27 Nimekabidhiwa vitu vyote na Baba yangu: na hakuna mtu amjuaye
Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na mtu ye yote
ambaye Mwana anapenda kumdhihirisha Baba kwake.”
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni
kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi
mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na
mzigo wangu ni mwepesi.”
Swali #1
Zaburi 46:10
Acheni mjue ya kuwa mimi ni Mungu, Nitatukuzwa katika mataifa nitatukuzwa
katika nchi.
Zaburi 145:18-19
Bwana yu karibu na wote wamwitao, Na wote wamwitao kwa uamnifu.
Atawafanyia wamchao matakwa yao; Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Isaya 55:3
Tega sikio lako na uje kwangu. Sikieni na nafsi zenu zitaishi…
Waebrania 10:22
22 basi tumkaribie Mungu kwa moyo wa kweli na imani timilifu, mioyo
yetu ikiwa imenyunyizwa na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya na
miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi.
Swali #2
Yohana 14:6-7
6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu
hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7 Kama mngekuwa mnajua
mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba
yangu na mmemwona.”
1 Yohana 1:5
5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake, ambao tunawatan gazia:
Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza kamwe.
Warumi 3:20-24
20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki
mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue
dhambi.
21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria,
njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa.
22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo.
Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua,
23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa
Mungu;24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi
ulioletwa na Yesu Kristo.
Ezekiel 18:32
“Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye”
Asema Bwana “Mungu,basi ghairini mkaishi!”
Warumi 3:23
23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa
Mungu;
Matendo Ya Mitume 4:12
12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani
ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina
hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”
Swali #3
Yohana 6:29
29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii:
mumwamini yeye aliyenituma.”
Yohana 5:24
24 Ninawaambia hakika, ye yote anayesikiliza maneno yangu na kumwamini
yule aliyenituma, anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Amevuka
kutoka kwenye mauti, na kuingia katika uzima.
1 Yohana 5 :10-12
10 Mtu anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake.
Mtu asiyemwamini Mungu, amemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kwa sababu
hakuamini ushuhuda alioutoa Mungu kuhusu Mwanae. 11 Na ushuhuda
wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu
umo kwa Mwanae. 12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana
wa Mungu hana uzima.
Swali #4
Yohana 3:1-8
Kiongozi mmoja wa Wayahudi wa kundi la Mafarisayo aitwaye Nikodemo,2
alimjia Yesu usiku akamwambia, “Rabi, tunafahamu kuwa wewe
ni mwalimu uliyetumwa na Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kufanya
miujiza hii uifanyayo, kama Mungu hayupo pamoja naye.”
3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara
ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.” 4 Nikodemo akasema,
“Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika
tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?” 5 Yesu akamwambia,
“Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho
hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na
wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa
hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya
pili.8 Upepo huvuma po pote upendapo. Mvumo wake unausikia lakini
huwezi ukafahamu utokako wala uen dako. Ndivyo ilivyo kwa kila mtu
aliyezaliwa kwa Roho.”
Swali #5
Yohana 3:36
36 Ye yote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele; asiyemtii Mwana
hatauona uzima bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake daima.”
Yohana 16:24
24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa
ili furaha yenu ipate kukamil ika.
Warumi 4:7-8
7 “Wamebarikiwa wale ambao makosa yao yamesame hewa, ambao
dhambi zao zimefunikwa.8 Amebarikiwa mtu ambaye Bwana hamhesabii
dhambi zake.”
Warumi 5:1
Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani
na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Wakorintho 5:17
17 Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya
kale yamepita, tazama, mapya yamekuja.
Efeso 1:13
13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli,
Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho
Mtakatifu ambaye mliahidiwa.
Waebrania 13:5
5 Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike
na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia
kamwe wala sitakuacha.”
Waefeso 1:3-6
3 Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki
sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya
Kristo. 4 Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla
ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio
na lawama mbele zake. 5 Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo
yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa
mapenzi yake mwenyewe; 6 na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema
yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake.
Wafilipi 3:8-9
8 Zaidi ya hayo, nahesabu mambo yote kuwa hasara tupu yakilinganishwa
na faida kubwa ninayopata kwa kumjua Kristo Yesu aliye Bwana wangu.
Kwa ajili yake nilikubali kupoteza kila kitu na kuona mambo hayo
yote kuwa ni takataka ili nipate faida ya kuwa na Kristo; 9 na nikiwa
kwake nisionekane kama mtu mwenye haki yake mwenyewe, inayotokana
na kushika sheria, bali niwe na ile haki inayotokana na kumwamini
Kristo, ambaye yeye ni haki itokayo kwa Mungu inayopatikana kwa
imani.
|