home >>
stonecroft>>
mwongozo >>
somo 2 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #2
Je Mungu yukoje?
Mistari ya Biblia
Usomaji wa Biblia wa kila juma
1 Wakorintho 1:9
9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae,
Yesu Kristo, Bwana wetu.
Warumi 16:27
27 Mungu aliye pekee mwenye hekima, atukuzwe milele na milele kwa
njia ya Yesu Kristo! Amina.
Luka 1:37
37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”
Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Hesabu 23:19
19 Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema,
hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
Ufunuo 15:3-4
3 Nao waliimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu na wimbo wa Mwana-Kondoo
wakisema, ‘ ‘Matendo yako Bwana Mungu Mwenyezi, ni makuu
na ya ajabu! Njia zako wewe Mfalme wa Mataifa ni za haki na za kweli!
4 Ni nani asiyekucha wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa
wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu
kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha dhihirishwa.”
Ufunuo 1:8
8 “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Aliyeko
na aliyekuwako na ata kayekuja, Mwenyezi.”
Wakolosai 1: 15-16
15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo
kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. 16 Yeye ndiye ali yeumba vitu
vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana;
kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka:
vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake.
Swali #2
Yohana 4:24
24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika
roho na kweli.”
Warumi 11: 33-36
33 Jinsi utajiri wa Mungu ulivyo mkuu! Hekima yake na maarifa yake
hayana mwisho. Njia zake na maamuzi yake hayachu nguziki! 34 Kwa
maana ni nani amepata kufahamu mawazo ya Mungu au kuwa mshauri wake?
35 Au ni nani amewahi kumpa cho chote ili arudishiwe? 36 Kwa maana
vitu vyote vyatoka kwake na vipo kwa ajili yake na vyote vinadumu
kwake. Utukufu ni wake milele. Amina.
Swali #3
1 Yohana 4:8
8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo.
2 Tesalonike 3:3
3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana
na yule mwovu.
Yakobo 1:17
17 Kila kipawa chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni, ikishuka
kutoka kwa Baba wa nuru za mbinguni ambaye habadiliki kama kivuli.
Marko 10:18
18 Yesu akamwambia, “Mbona unaniita mwema? Hakuna ali yemwema
isipokuwa Mungu peke yake.
Waebrania 1:8
8 Lakini kuhusu Mwana, anasema: “Kiti chako cha enzi, Wewe
Mungu, kitadumu milele na milele, na haki takuwa fimbo ya ufalme
wako.
Luka 1:78 - 79
78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia
kutoka mbinguni na
1 Petro 1:15-16
15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe
watakatifu katika mwenendo wenu;16 maana imeandikwa: “Muwe
watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.”
SIFA ZA MUNGU
1 Yohana 4: 7-16
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye
upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo
hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu
alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni
ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio
upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda
sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu.11 Wapendwa,
kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana.
12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu
anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu
kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia
kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu
anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na
yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo
alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo
hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.
Waefeso 2: 4-5
4 Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake
mkuu ambao alitupenda nao, 5 japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho
kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo
Yesu. Mmeokolewa kwa neema.
GOD IS FAITHFUL
Kumbukumbu la Torati 7:9
Basi jueni ya kuwa BWANA Mungu wenu Ndiye Mungu, ashikaye agano
lake na rehema zake kwao wale wampendao, na kushika amri zake hata
vizazi elfu.
Zaburi 92:1-2
Nineno jema kumshukuru BWANA ,
Na kulumbia jina lako, ee uliye juu,
Kuzitangaza rehema zako asubuhu
Na uaminifu wako wakati wa usiku.
GOD IS UNCHANGING
Malaki 3:6
Kwa maana mimi BWANA sina kigeugeu;
Ndio maana ninyi hamku angamizwa ninyi wana wa Jakobo.
GOD IS GOOD
Zaburi 107:1
1 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni
za milele.
GOD IS JUST
Torati 32:4
4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki.
Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.
GOD IS MERCIFUL
2 Wakorintho 1:3
3 Ashukuriwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma
na Mungu wa faraja zote.
GOD IS HOLY
1
Samweli 2:2
Hakuna aliye mtakatifu kama Mungu,
Kwa maana hakuna yeyote ila wewe,
Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
Zaburi 99:9
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;Maana
BWANA, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Swali #4
1 Petro 1:13-16
13 Kwa hiyo, ziandaeni nia zenu, muwe na kiasi, wekeni tumaini lenu
lote katika neema ile mtakayopewa wakati ule Yesu Kristo atakapodhihirishwa.14
Kama watoto watiifu, msikubali kutawaliwa na tamaa mbaya mlizokuwa
nazo wakati mkiishi katika ujinga. 15 Bali kama yeye aliyewaita
alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe watakatifu katika mwenendo
wenu;16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu kwa sababu mimi
ni mtakatifu.”
1 Wakorintho 1:30
30 Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya
yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi
Yeremia 9:23-24
23 Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima
yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala
tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake;
24 bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu
mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu,
na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema
Bwana
Swali #5
Mathayo 28:20
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama,
mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mwanzo 17:1
Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu,
akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Hebrews 4:13
|