home >>
stonecroft>> je
mungu yokoje? >>
somo 1 >> somo 2
Je Mungu yokoje? - Somo #2
Je Mungu yukoje?
Download
Swahili Lesson #2 Student Study book page 1-2
Download
Swahili Lesson #2 Student Study book page 3-4
Maombi
Mungu uishie milele, nakuabudu.nimejifunza kuwa haukuwa na mwanzo
wa hautakuwa na mwisho, nasadiki kuwa wewe ni muumbaji wa kila kitu
tukionacho. Naomba unisaidie kufikilia vizuri kuhusu wewe na neno
lako,naomba katika jina la Yesu. Amen.
1. Kutumia maneno rahisi elezea unafukilia nini kuhusu Mungu, uwe
mkweli na dhahili kuhusu jambo hili la kumhusu Mungu na jinsi unavyo
mfikilia, katika mwisho wa masomo haya swari hili litaulizwa tena.
________________________________________________________________
Kujisomea Biblia kwa Juma
Kila siku katika juma hili jisomee neno la MUngu hili na elezea
kila kipengele kinasema nini kumhusu Mungu.
1 Wakorintho 1:9
Je kifungu hiki kinasema nini kumhusu Mungu?
________________________________________________________________
Warumi 16:27
Neno hili linamuelezeaje MUngu?
________________________________________________________________
Luka 1:37
Neno hili linatuambia nini kuhusu Mungu?
________________________________________________________________
Yohana 3:16
Je neno hili linasema nini kumhusu Mungu.
_______________________________________________________________
Hesabu 23:19
Ni sifa zipi za Mungu zimetajwa?
_______________________________________________________________
Ufunuo 15:3-4
Je ni sifa zipi za Mungu zinatajwa hapa?
_______________________________________________________________
Ufunuo 1:8
Je hili nalo linasema nini kuhusu Mungu?
_______________________________________________________________
. Chagua kifungu ambacho
kinaleta maana zaidi kwako katika vifungu vya kujisomea vya juma,
tafakari ukweli huo unamaana gani katika maisha yako na utendee
kazi.
Mungu hana mwili kama tulivyo sisi,
tukifikilia hivyo tutakuwa tunafanya kosa kubwa sana maana tutafikilia
kuwa Munguana mapungufu kama tulivyo sisi wanadamu.
Hatukujiumba wala hatukuumba hata upepo, chakula,
au maji, ambavyo tunaviihitaji ili maisha yetu yasonge mbele.
Lakini Mungu huishi kama yeye na haitaji msaada wowote ili maisha
yake yapate kusomnga mbele
.Kila kitu tukionacho katika dunia kilifanywa
au kuumbwa lakini yeye Mungu hakuumbwa, wala hakufanywa huyu
Mungu ni tofauti kabisa na vitu tuvionavyo yeye NDIYE, yeye
amekuwako na atakuwako yeye yupo milele na huishi milele.
|
Jambo jingine la kumtofautisha Mungu na sisi
ni kwamba yeye ni Roho wakati sisi husihi katika mwili.
2. Je Yohana 4:24 inasema kumhusu Mungu?
(If you do not have
a Bible, look up the verses in the Bible Verse Handbook)
Download Bible Verses Handbook |
Mungu wetu hazuiliwi na kitu
Sulemani aliomba.
“Lakini Mungu je atakaa kweli kweli juu ya nchi? Mbingu hazikutoshi
wala mbingu za mbingu sembuse hii nyumba niliyo ijenga!”
1 Wafalme 8:27
Je wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu?
Waweza kuufikilia upeo wa huyo mwenyezi?
Ni juuu mno kama mbingu waweza kufanya nini wewe?
Ni wenye kina kuliko kuzimu waweza kujuoa nini wewe?
cheo chake ni kirefu kuliko dunia
Ni kipana kuliko baharo
Ayubu 11:7-9
Nizaidi ya upeo wetu
Mungu huunguruma kwa kustaaajabisha kwa sauti yake;
Hufanya mambo makuu ambayo hatuwezi kuelewa.
Ayubu 37:5
“Maana mawazo yenu si mawazo yangu,
Wala njia zenu si njia zangu” asema BWANA.
“Maana kama mbingu zilivyo juusana kuliko nchi,
Kadharika nia zangu zi juusana kuliko niia zenu,
Na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.”
Isaya 55:8-9
3. Sifa za kiroho ndizo sifa za kweli zimhusuzo Mungu,kila kifungu
utakachosoma hapa kina sifa
Ya Mungu soma na andika sifa hiyo mbele ya kifungu
a. 1 Yohana 4:8 ____________________________________________________________
b. 2 tesalonike 3:3 ____________________________________________________________
c. Yakobo 1:17 _____________________________________________________________
d. Marko 10:18 _____________________________________________________________
e. Waebrania 1:8 _____________________________________________________________
f. Luka 1:78 _____________________________________________________________
g. 1 Petro 1:15-16 _____________________________________________________________
Sifa za Mungu
Mungu ni Upendo
Upendo ni sifa ya Mungu lakini sio tafsiri ya Mungu, inaelezea MUngu
jinsi alivyo kama sifa nyingine zinavyoelezea, uaminifu, uzuri,
huruma, haki, utakatifu, zote hizi zinaeleza Mungu alivyo.
Yeye ni kila kitu kilichotajwa hapa chini na wakatai huo huo upendo
wa Mungu mara zote ni mzuri na mtakatifu,wa uamini fu na wa haki.
Mungu ni mwaminifu
Tunaweza kumtegemea Mungu wetu maana ni mwaminifu na hutunza agano
lake mara zote, tunaweza kuishi kwa matumaini ya hata kesho maana
Mungu ni mwaminifu.
Mungu habadiriki
Moja ya sifa za Mungu ambazo bado hatujazisema ni kwamba Mungu habadiriki,
tunjua kuwa Mungu wawezi kutokuwa mwaminifu maana hili litamfanya
abadirike. Malki 3:6
Mungu ni mwema
Huu wema wa Mungu ni tofauti na wema wetu maana Mungu ni mwema katika
kila jambo ambalo analifanya tofauti na wanadamu. Yesu alisema Mungu
pekee ndiye aliye mwema. Zaburi 107:1
Mungu ni wa haki
Mungu atendapo haki hatendi haki kama kumtuliza au kumpongea mwanadamu
kwa yale aliyotenda bali hutenda haki kama yeye jinsi alivyo, Mungu
ni Mungu na ataendelea kuwa Mungu hawezi akawa kitu kingine zaidi
ya kuwa Mungu Kumbukumbu la Torati 32:4
Mungu ni wa huruma
Huruma ni sifa mojawapo ya Mungu na mara zote huyu Mungu amejawa
na huruma na pia pamoja na huruma na pia yeye ana haki, hata atendapo
haki hua na huruma pia, huwa anaonyesha huruma isiyokuwa na kipimo
mara zote anaposhughulika na mwanadamu, hii huruma sio ya kitambo
tu bali ndivyo Mungu alivyo, Mungu alikuwa na huruma hata kabla
nyakati za muda hazijaanza na ataendelea kuwa na huruma, soma 2
Wakorintho 1:3
Mungu ni mtakatifu
Huu utakatifu unajitegemea,ni wabila mawaa,ni wa tofauti na ni mkuu
sana,utakatifu wa Mungu unapita hata fahamu zetu,utakatifu wa Mungu
hupita fahamu zote na huu utakatifu anao yeye mwenyewe.
4. a Mungu anahitaji wakristo wafanye nini?
1 Petro 1:13-16
______________________________________________________________
b.Kutokana na msingi wa 1 Wakorintho 1:30 tunawezaje kuwa
kuwa watakatifu.
______________________________________________________________
BWANA asema hivi mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake,
wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri
asijisifu kwa sababu ya utajiri wake, bali ajisifu kwa sababu hii
kwamba ananifahamu mimi, na kunijua kuwa mimi ni BWANA nitendaye
mema, na hukumu, na haki katika nchi, maana mimi napendezwa na mambo
hayo asema BWANA.
Yeremia 9:23-24
Sifa taytu za tofauti
Mungu ana nguvu zote aliviumba vyite vitu vionekanavyo na visivyo
onekana kwa kutamka tu neno lake, ana vitawala vyote na ana nguvu
za kutendea miujiza na ndio maana tunasema Mungu ana nguvu zote
- Ominipotent.
Mungu huyajua mambo yote, hakuna jambo asilo lijua hivyo nguvu
za Mungu na ufahamu wake huwezi ukavitenga, tunaliita jambo hili
Omniscient.
Mungu yupo popote katika muda mmoja, anapatikaka popote katika
muda huo huo mmoja, tunasema yeye ni - Omni present.
5. Soma vifungu hivi vifuatavyo na andika katika vifungu hivyo
ni sifa gani ya Mungu inazungumziwa hapo. Omnipotence,omnipresence,omniscience.
“……….na ntakuwa nanyi mpaka mwisho wa dahari.”
---------Mathayo 28:20
“……Mimi ni Mungu mkuu….Je kuna jambo gumu
la kumshinda BWANA?”
---------Mwanzo 17:1.18:14
“Hakuna jambo ambalo linajificha mbele za Mungu, kila jambo
katika viumbe vyake vi wazi kabisa mbele zake,na kwake tu ndiko
tutakako toa hesabu ya matendo yetu.”
---------Waebrania 4:13
MAOMBI
Mungu mwenye nguvu nashukuru yote niliyo jifunza ya kukuhusu.nashukuru
kuwa unapatikana mahali popote, na pia una nguvu zote, na unatambua
mambo yote.
Wewe ni Mungu wa ajabu. Nashukuru kuwa unawapenda na kuwaelewa watu
ulio waumba.
Nakushukuru kwa sababu ya Baraka zetu zote, katika jina la Yesu.
Amen.
This is a translation of Lesson #2 Students
Study Book, the English version of -
What is God like is
available online from their website.
The Guide has her own Guidebook to help her
lead and guide the lesson.
View Guidebook online
Download
Swahili Lesson #2 Guidebook
Download
Swahili Guidebook Bible Verses Lesson #2
|