home >>
stonecroft>>
mwongozo >>
somo 6 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #6
Nawezaje kumfurahisha Mungu?
Mistari ya Biblia
Swali #1
Warumi 1:20
20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana
kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika
wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.
2 Petro 1:20-21
20 Kwanza kabisa ni lazima muelewe kwamba hakuna unabii katika Maandiko
uliotokana na tafsiri ya nabii mwenyewe. 21 Kwa sababu hakuna unabii
uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka
kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Yohana 1:18
18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee,
ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha
Mungu kwetu.
Matendo 1:8
8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi
mwisho wa dunia.”
I Timotheo 1:19
19 ukishikilia imani na dhamiri njema. Watu wengine, kwa kukataa
kuisikiliza dhamiri yao, wameangamiza imani yao.
Yohana 5:26
26 Kama vile Baba alivyo chanzo cha uzima, hali kad halika amemwezesha
Mwanae kuwa chanzo cha uzima.
Ufunua wa Yohana 4:11
11 “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu
na heshima na uweza, kwa maana ni wewe uliyeviumba vitu vyote, na
kwa mapenzi yako vitu vyote viliumbwa na vinapata kuwapo.”
Swali #2
1 Yohana 4:16
16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi.
Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu
hukaa ndani yake.
Zaburi 107:1
Mshukuru BWANA kwakuwa ni mwema!
Kwa maana fadhiri zake ni za milele.
Zaburi 86:15
Lakini wewe Bwana u Mungu wa Rehema na neema,
Mvumilivu mwingi wa fadhili na kweli.
2 Petro 3:15
15 Hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni wokovu, kama ndugu yetu mpendwa
Paulo alivyokwisha kuwaandikieni kwa hekima aliyopewa na Mungu.
Mathayo 6:14
14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe
na ninyi;
Mathayo 11:29
29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni kutoka kwangu; kwa maana mimi
ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
Wafilipi 4:7
7 Na amani ya Mungu, ambayo inapita ufahamu wote, italinda mioyo
yenu na nia zenu kwa Kristo Yesu.
Swali #3
1 Petro 1:16
16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.”
Waebrania 12:14
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na utaka tifu,
ambao bila kuwa nao, hakuna mtu atakayemwona Bwana.
Swali #5
Yohana 13:34-35
34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi
nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana
hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”
Yohana 14:15
15 “Kama mnanipenda mtatimiza amri zangu.
Warumi 12:1
Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni
kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio
ibada yenu ya kiroho.
1 Thessalonike 4:3
3 Mungu anapenda ninyi muwe watakatifu, mjiepushe na maisha ya zinaa;
1 Thessalonike 5:16-18
16 Furahini wakati wote, 17 ombeni pasipo kukoma, 18 shu kuruni
katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili
yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.
Zaburi 25:4-5
Ee BWANA unifundishe njia zako; Unifundishe mapito yako.
Uniongoze katika kweli yako na kunifundisha, Maana wewe ndiwe Mungu
wa wokovu wangu; Nakungoja wewe mchana kutwa.
Swali #7
Isaya 43:7
7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya
utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.
Yohana 15:8
8 Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha
kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.
1 Petro 4:11
11 Mtu akisema kitu, basi na awe kama anayesema maneno halisi ya
Mungu. Mtu anayetoa huduma na ahudumu kwa nguvu apewayo na Mungu;
ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye
ni mwenye utukufu na uweza, milele na milele. Amina.
Zaburi 16:11
Utanijulisha njia za uzima;
Mbele za uso wako kuna furaha tele;
Na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele.'
Usomaji wa Biblia wa kila juma
Marko 12:28-31
28 Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona
kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri
zote, ni ipi iliyo kuu?”29 Yesu akamjibu, “Iliyo kuu
ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee.
30 Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako
yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ 31 Na sheria
ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi
yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”
Mathayo 4:10
10 Yesu akamwambia, “Ondoka hapa shetani! Kwa maana imean
dikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na utamtumikia yeye peke
yake.’ ”
Mathayo 12:50
50 Kwa maana ye yote anayefanya mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni,
ndiye kaka, dada na mama yangu.”
Yohana 14: 23
23 Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika mafundisho yangu
na Baba yangu atampenda, nasi tutafanya makao yetu kwake.
Wafilipi 1:9-11
9 Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka
siku hadi siku pamoja na maarifa na busara 10 ili mpate kutambua
mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi
siku ya Kristo. 11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo
kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa.
1 Wakorintho 10:31
31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo
yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
1 Mambo ya nyakati 16:23-29
23Mwimbieni BWANA, nchi yote;
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
24 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.
25 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26 Maana miungu yote ya watu si kitu;
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
27 Heshima na adhama ziko mbele zake;
Nguvu na furaha zipo mahali pake.
28 Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
29 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Leteni sadaka, mje mbele zake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
Wakolosai 3: 1-10
Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, elekezeni mioyo yenu
kwenye mambo ya juu, alikokaa Kristo, upande wa kulia wa Mungu.2
Yafikirini mambo ya juu na siyo mambo ya hapa duniani. 3 Kwa maana
ninyi mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo kwa Mungu.4
Wakati Kristo ambaye ni uzima wetu ataonekana, ndipo na ninyi mtakapoonekana
pamoja naye katika utu kufu.
5 Basi, yaangamizeni kabisa mambo yote yanayotokana na asili yenu
ya kidunia: uasherati, mawazo machafu, tamaa mbaya, nia mbaya na
choyo ambayo ni ibada ya sanamu. 6 Kwa sababu ya mambo haya, ghadhabu
ya Mungu inakuja. 7 Ninyi mlikuwa mkitenda mambo haya katika maisha
yenu ya zamani.
8 Lakini sasa ni lazima mwa chane kabisa na mambo kama haya: hasira,
ghadhabu, nia mbaya, matukano na maneno machafu kutoka vinywani
mwenu. 9 Msiambiane uongo kwa maana mmekwisha vua utu wenu wa zamani
pamoja na matendo yake 10 na kuvaa utu upya ambao unaendelea kufanywa
upya katika ufahamu ili ufanane na Muumba wake.
Swali #8
1Haleluya msifuni Mungu katika patakatifu
pake; msifuni katika anga la uweza wake.2 msifuni kwa Matendo yake
makuu; msifuni kwa kadri ya uwingi wa ukuu wake. 3 msifuni kwa mvumo
wa baragumu; msifuni kwa kinanda na kinubi;.4 msifuni kwa matari
na kucheza; msifunikwa zeze na filimbi; 5 msifuni kwa kwa matoazi
yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 kila mwenye pumzi
na amsifu Bwana haleluya.
Zaburi 150:1-6
|