home >>
stonecroft>>
mwongozo >>
somo 4 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #4
Je Mungu ana nijua?
Mistari ya Biblia
Usomaji wa Biblia wa kila juma
Yohana 6:37
37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye
kwangu, sitamtupa nje kamwe.
Ayubu 34:21
Macho yake yako katika njia za wanadamu, na anaona hatua zake zote.
Zaburi 139:1-6
Ee BWANA umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo lanhu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na nia zangu
zote.
Maana hamna neno ulimini mwangu, usilolijua kabisa BWANA.
Umenizingira nyuma na mbele, ukaniwekea mkono wako.
Maarifa yako ni ya ajabu yanishinda mimi; hayadilikiki ni ya ajabu
siwezi kuyafikilia.
Mithari 15:3,11
Macho ya BWANA yako kila mahali,
yakimchunga mbaya na mwema.
Kuzimu na uharibifu vi wazi mbele za BWANA;
Si zaidi basi mioyo ya wanadamu.
2 Nyakati 16:9
Kwa maana macho ya BWANA huzunguka duniani kote, ili ajionyeshe
mwenye nguvu kwa ajili ya hao walio kamilika mioyo kuelekea kwake,kwa
hayo umetenda upumbavu kwani tangu sasa utakuwa na vita.
Waebrania 13:5
5 Maisha yenu yasitawaliwe na tamaa ya kupenda fedha, na mridhike
na mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, “Sita kupungukia
kamwe wala sitakuacha.”
Yohana 14:21
21 Mtu anayezishika amri zangu na kuziti miza ndiye anayenipenda.
Na mtu anayenipenda, Baba yangu atam penda; nami nitampenda na kujidhihirisha
kwake.”
Swali #1
Mathayo 18:12-14
12 “Mnaonaje? Kama mtu ana kondoo mia moja na mmoja wao akapotea,
hatawaacha wale tisini na tisa mlimani aende kumtafuta yule aliyepotea?13
Na akisha mpata, nawaambia kweli, anafurahi zaidi kwa ajili ya huyo
kondoo mmoja kuliko kwa wale tisini na tisa ambao hawakupotea. 14
Hali kadhalika, Baba yenu wa mbin guni hapendi hata mmojawapo wa
hawa wadogo apotee.”
Waefeso 2:10
10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika
Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa,
tuishi katika hayo.
Zaburi 100:3
Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliye tuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake na kondoo wa malisho yake.
Swali #4
Zaburi 139:7-18
7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso
wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda
changu, Wewe uko. 9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande
za mwisho za bahari; 10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono
wako wa kuume utanishika. 11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika,
Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu,
Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa
mama yangu. 14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu
ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana,
15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa
kwa ustadi pande za chini za nchi;
16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa
zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado.
17 Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa
jumla yake!
18 Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo nikali
pamoja nawe.
Swali #5
Zaburi 139:23-24
23 Ee Mungu, unichunguze, uujue moyo wangu, Unijaribu, uyajue mawazo
yangu; 24 Uone kama iko njia iletayo majuto ndani yangu, Ukaniongoze
katika njia ya milele.
Swali #6
Mathayo 6:25-34
25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu:
mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini.
Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni
ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote
ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si
wa thamani zaidi kuliko ndege?27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha
kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?
28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi
tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini
nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi
kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha
hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha
ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe
na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa
nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay
owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni
anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza
Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa
hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe.
Kila siku ina shida zake za kutosha.”
1 Petro 5:6-7
6 Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu wenye nguvu, ili wakati
wake ufaao utakapotimia, awainue.
7 Mwekeeni yeye fadhaa zenu zote kwa maana yeye hujishughul isha
sana na mambo yenu.
Mathayo 6:8
8 Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata
kabla hamjaomba.”
Warumi 8:28-29
28 Tunajua kwamba katika kila kitu Mungu[f] hufanya kazi ili kuwapa
mema wale wanaompenda. Hawa ni watu aliowachagua Mungu, kwa sababu
huo ndiyo ulikuwa mpango wake. 29 Mungu aliwajua kabla hajauumba
ulimwengu. Na aliamua hao wangekuwa kama Mwanaye. Na Yesu angekuwa
mzaliwa wa kwanza wa watoto wake wengi.
Swali #7
Zaburi 37:4-5
4 Nawe utajifurahisha kwa Bwana, Naye atakupa haja za moyo wako.
5 Umkabidhi Bwana njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya.
MIthari 3:5-6
Umtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako
mwenyewe; kat ika njia zako zote mkiri yeye, naye atazinyoosha njia
zako zote.
Yeremia 29:13
Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakapo nitafuta kwa moyo wenu wote.
Swali #9
Yeremia 29:11
Maana najua mawazo niwawaziayo ninyi ni mawazo ya amani asema BWANA,
wala si mabaya kuwapa ninyi tumaini katika sku zenu za mwisho.
Swali #10
Warumi 5:6-9
6 Tulipokuwa tungali wanyonge, wakati aliochagua Mungu, Kristo aliwafia
wenye dhambi. 7 Ni vigumu sana kwa mtu kujitolea kufa kwa ajili
ya mwenye haki, ingawa yawezekana mtu akajitolea kufa kwa ajili
ya mtu mwema.8 Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba:
tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.
9 Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, bila
shaka atatuokoa kutoka katika ghadhabu ya Mungu.
Swali #11
Zaburi 147:5
BWANA wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu; Akili zake hazina mpaka.
|