Stonecroft
Mafunzo wa Stonecroft
Mfululizo wa Utatu wa Stonecroft
Kitabu cha Mwongozo
Mistari ya Biblia
Stonecroft Kimataifa
Uinjilisti wa Mtoto
Mradi wa Mlonge
The International Team
YDT Teachings
|
|
home >>stonecroft>>
mwongozo
>> yesu
ni nani somo 5 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #5
SOMO LA TANO
YESU YUKO WAPI KWA SASA
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Matendo 1:6-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia
kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni.
Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya
Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini
baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa
ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke
Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni
sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini
baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati
huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?” 7 Yesu akawaambia,
“Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na
Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho
Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea
yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na
wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho
yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa
mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu
wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu
huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda
mbinguni.”
Matendo 2:32-35
32 Huyu Yesu, Mungu alimfufua, na sisi ni mash ahidi wa tukio hilo.
33 “Basi akiwa ametukuzwa na kukaa upande wa kulia wa Mungu,
alipokea Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Baba yake. Huyo Roho Mtakatifu
ndiye aliyetumiminia haya mnayoyaona na kuyasikia.
34 Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini alisema, ‘Bwana alim
wambia Bwana wangu: kaa upande wangu wa kulia, 35 mpaka nitaka powafanya
maadui zako kiegemezo cha miguu yako.’
Waebrania 4:14-16
14 Hivyo basi, kwa kuwa tunaye kuhani mkuu aliyepitia mbingu, Yesu
Mwana wa Mungu, tushikilie kwa uthabiti imani yetu tunayoikiri.
15 Kwa maana huyu kuhani wetu mkuu si kuhani ambaye hawezi kutuhurumia
katika udhaifu wetu, bali ni kuhani ambaye kwa kila hali amejaribiwa
kama sisi, lakini pasipo kutenda dhambi. 16 Kwa hiyo basi, tusogelee
kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupokee rehema na kupata neema ya
kutusaidia wakati wa shida.
Wagalatia 2:15-20
15 Sisi tulio Wayahudi wa kuzaliwa na sio watu wa mataifa ‘wenye
dhambi,’16 tunafahamu kwamba mtu hawezi kuhesabiwa haki kwa
kutii sheria bali kwa kumwamini Yesu Kristo. Kwa hiyo sisi pia tumemwamini
Yesu Kristo ili tupate kuhesabiwa haki kwa kumwa mini Kristo, na
wala si kwa kuitii sheria. Maana hakuna mtu ata kayehesabiwa haki
kwa kutii sheria. 17 Lakini ikiwa sisi katika jitihada ya kuhesabiwa
haki katika Kristo, bado tunaonekana tun gali wenye dhambi, je,
hii ina maana kwamba Kristo amekuwa mwene zaji wa dhambi? La hasha!
18 Lakini ikiwa mimi nina jenga tena kile ambacho nimekwisha bomoa,
basi ninadhihirisha kwamba mimi ni mvunja sheria.19 Kwa maana mimi
kwa njia ya sheria, nimeifia sheria, ili nipate kuishi kwa ajili
ya Mungu.
20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni
Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa
kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake
kwa ajili yangu.
Waefeso 3:14-21
14 Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya Mungu Baba, 15 aliye baba
wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. 16 Namwomba Mungu
awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake
kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. 17 Na naomba kwamba, kwa
imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama
imara na kujengwa katika upendo, 18 mpate uwezo wa kuelewa, pamoja
na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo
wa Kristo;19 na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo
wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu
mwenyewe.
20 Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale
tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi
ndani yetu.21 Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu
kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina.
Wakolosai 1:27-29
27 Kwao, Mungu amependa kudhihirisha kati ya mataifa utukufu wa
utajiri wa siri hii, yaani, Kristo ndani yenu ndiye tumaini pekee
la utu kufu.
28 Kwa sababu hii tunamtangaza Kristo, tukiwaonya na kuwa fundisha
watu wote kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya
Mungu akiwa amekamilika katika Kristo. 29 Kwa shabaha hii nina fanya
kazi, nikijitahidi kwa nguvu kuu ya Kristo inay ofanya kazi kwa
uwezo mkuu ndani yangu.
1 Petro 3:22
22 Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja
na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.
Marko 6:31
31 Kisha Yesu akawaambia, “Njooni mnifuate peke yenu hadi
mahali patulivu na palipo mbali na watu wengine ili mpumzike kidogo”,
kwani pale walikuwepo watu wengi wakija na kutoka, nao hawakuwa
na nafasi ya kula.
2 Wathesalonike 3:10
10 Tulipokuwa nanyi, tuliwapa kanuni hii: “Yeyote asiyefanya
kazi asile.”
Mwanzo 3:15
Name nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, na kati ya uzao
wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Matayo 28:11-15
11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari
waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu
yote yaliyotokea. 12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana,
waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni,
‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’
14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata
shida yo yote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha
wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi
mpaka leo.
1. Matendo 1:1-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia
kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni.
Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya
Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini
baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa
ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke
Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni
sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini
baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati
huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”
7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira
ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu
akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na
wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho
yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa
mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu
wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni?
Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona
akienda mbinguni.”
Luke 24:36-44
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama
katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza,
“Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu?39
Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni
mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema
haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini
kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna
chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa
kuokwa,43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa
pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she
ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”
2. a. Yohana 20:14-18
14 Alipokuwa akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma
yake, lakini hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona
unalia? Unamta futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea
naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua
tafadhali nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita,
“Mar iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia
kwa Kiebrania, “Rabboni!’ 17 Yesu akamwambia, “Usin
ishike kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu
zangu ukawaambie, ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu
wangu na Mungu wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda
akawakuta wanafunzi akawaambia, “Nimemwona Bwana!”
b. Luka 24:13-15
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda
kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa
wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza,
Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao,
c. Yohana 20:26-29
26 Wakashindwa kumkamata kwa maneno aliyosema mbele ya watu. Jibu
lake liliwashangaza mno, wakakosa la kusema. Yesu Afundisha Kuhusu
Ufufuo
27 Baadhi ya Masadukayo , wale wanaosema kwamba hakuna ufu fuo wa
wafu, wakamjia Yesu wakamwuliza, 28 “Mwalimu, katika sheria
ya Musa , tunasoma kwamba kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila
mtoto, basi kaka yake amwoe huyo mjane ili amzalie marehemu watoto.
29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza akafa bila kuzaa mtoto.
d. 1 Wakorintho 15:5
5 Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili.
e. Yohana 21:1
Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando
ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi:
f.1 Wakorintho 15:6
6 Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja,
na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa.
g. 1 Wakorintho 15:7
7 Kisha akamtokea Yakobo, na ndipo akawatokea mitume wote.
3. Waebrania 12:2
2 Tumtazame Yesu aliyeanzisha na anayekamilisha imani yetu. Yeye,
kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, alivumilia kifo cha msalaba
bila kujali aibu, na sasa ameketi upande wa kulia wa kiti cha enzi
cha Mungu.
4. Waebrania 7:24-25
24 Lakini yeye anaendelea na ukuhani wake daima kwa maana anaishi
milele. 25 Kwa hiyo anaweza kwa wakati wote kuwaokoa wale wanaomkaribia
Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye anaishi daima ili kuwaombea.
Yohana 14:16-20
16 Nami nitam womba Baba, naye atawapeni Msaidizi mwingine akae
nanyi siku zote. 17 Huyo ndiye Roho wa Kweli ambaye watu wasioamini
hawawezi kumpokea. Watu kama hao hawamwoni wala hawamfahamu. Ninyi
mnamfahamu kwa kuwa anakaa ndani yenu na ataendelea kuwa nanyi.
18 Sitawaacha kama yatima. Nitarudi kwenu.
19 Baada ya muda mfupi watu wa ulimwengu hawataniona tena, ila ninyi
mta niona; na kwa kuwa mimi ni hai, ninyi pia mtakuwa hai. 20 Wakati
huo utakapofika mtajua ya kuwa mimi niko ndani ya Baba yangu na
ninyi mko ndani yangu.
Tito 3: 4-7
4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa,
5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda,
bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa
mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye
Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu.
7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi
wa uzima wa milele tunaoutumainia .
5. Warumi 5:8-9
8 Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa
tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.
9 Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, bila
shaka atatuokoa kutoka katika ghadhabu ya Mungu.
Warumi 5:10
10 Kwa kuwa kama tulipokuwa maadui wa Mungu tulipatanishwa kwa kifo
cha Mwanae, bila shaka sasa kwa kuwa tumepatanishwa, tutaokolewa
kwa uzima wake.
Yohana 6:37
37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote ajaye
kwangu, sitamtupa nje kamwe.
Matayo 11:28
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na mizigo, nami nitawapumzisha.
7. a. Wagalatia 2:20
20 Nimesulubiwa pamoja na Kristo; si mimi tena ninayeishi bali ni
Kristo anayeishi ndani yangu. Maisha ninayoishi sasa naishi kwa
kumwa mini Mwana wa Mungu, aliyenipenda hata akatoa maisha yake
kwa ajili yangu.
b.1 Korintho 3:16-17
16 Je, hamjui kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa
Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu
la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa sababu Hekalu la Mungu
ni takatifu, na ninyi ni Hekalu hilo.
1 Korintho 6:19
16 Hamjui kwamba mtu aushirikishaye mwili wake na kahaba ana kuwa
mmoja naye kimwili? Maandiko yanasema, “Hao wawili watakuwa
mwili mmoja.”
c. Warumi 8:9-11
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa
na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote
ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo
anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi,
roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na
ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi
ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia
uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye
anaishi ndani yenu.
Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele, ambaye jina lake
ni mtakatifu; asema hivi; nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo
patakatifu; tena pamoja nay eye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea,
ili kuzifufu roho za wanyenyekevu, na kuifufu mioyo yao waliotubu.
Matendo 4:12
Yesu peke yake ndiye anayeweza kuokoa watu. Jina lake ndiyo nguvu
pekee iliyotolewa kumwokoa mtu yeyote ulimwenguni. Ni lazima tuokoke
kupitia yeye!”
|
|