Stonecroft
Mafunzo wa Stonecroft
Mfululizo wa Utatu wa Stonecroft
Kitabu cha Mwongozo
Mistari ya Biblia
Stonecroft Kimataifa
Uinjilisti wa Mtoto
Mradi wa Mlonge
The International Team
YDT Teachings
|
|
home >>stonecroft>>
mwongozo
>> yesu
ni nani somo 4 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #4
SOMO LA NNE
KWA NINI YESU ALIKUJA?
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Mathayo 5:1-2, 17-20
Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi
wake wakamjia, 2 naye akaanza kuwafundisha akisema: 17 “Msidhani
kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii.
kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi
moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19 Kwa
hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri
zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa
katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18 Kwa
maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha
wengine kuzitii a taitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20 Kwa
maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa
sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”
Yohana 6:35-38
35 Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima. Ye yote ajaye
kwangu hataona njaa kamwe, na ye yote aniaminiye, hataona kiu kamwe.
36 Lakini kama nilivyokwisha waambia, mnaniona lakini bado hamtaki
kuamini. 37 Wale wote ambao Baba amenipa watakuja kwangu na ye yote
ajaye kwangu, sitamtupa nje kamwe. 38 Kwa maana sikushuka kutoka
mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu, bali nitimize mapenzi yake
yeye aliyenituma.
Matendo 2:23-24
23 Huyu Yesu ali tiwa mikononi mwenu kwa mpango na makusudi ya Mungu
aliyoyafahamu tangu awali. Nanyi mlimwua kwa kumtundika na kumpigilia
misumari msalabani, mkisaidiwa na watu waovu. 24 Lakini Mungu alimfufua
kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu hata kifo
kisingaliweza kumzuia.
1 Yohana 3:5-6
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa
kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu
huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho
wa Mungu.
Waebrania 2:14-15
14 Basi, kwa kuwa watoto hao wana mwili na damu, yeye pia alishiriki
katika ubinadamu wao, ili kwa kufa kwake apate kumwan gamiza yule
mwenye mamlaka juu ya kifo, yaani shetani; 15 na hivyo awaweke huru
wale ambao walikuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa
kifo.
Ufunuo 3:20-21
20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti
yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye,
naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja
nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi
pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi.
Ufunuo 5:9-10
9 Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati
na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako
ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha;
watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme
na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.”
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume;
na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa
Amani.
Isaya 35:4-6
….jipeni moyo, msiogope; tazama, mung wenu atakuja na kisasi,
na malipo ya mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.
Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa.
Ndipo mtu aliye kilema ataruka ruka kama kulungu, na ulimi wake
aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito
jangwani.
1.a. Mathayo 5:17
17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho
ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna
hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike.
b. Yohana 1:18
18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Lakini Mwanae pekee,
ambaye ana uhusiano wa karibu sana na Baba yake, amemdhihirisha
Mungu kwetu.
c. Mathayo 20:28
28 kama vile ambavyo mimi Mwana wa Adamu sikuja ili nitumikiwe bali
kutumika na kutoa maisha yangu kuwa fidia kwa ajili ya watu wengi.”
d. Luka 4:42-43
42 Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha.
Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, na walipom wona wakajaribu
kumzuia asiondoke. 43 Lakini yeye akawaambia, “Ninao wajibu
wa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu sehemu nyingine pia.
Hii ndio sababu nilitumwa.”
e. Luka 19:10
10 Kwa maana mimi Mwana wa Adamu nimekuja kutafuta na kuokoa waliopotea.”
f. Yohana 3:17
17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae kuuhukumu ulimwengu bali auokoe
ulimwengu.
g. Yohana 10:7-10
7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango
wa kupitia kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi.
Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. 9 Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia
zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka
na kupata malisho. 10 Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu.
Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili.
h. 1 Timotheo 1:15
15 Neno hili ni la hakika tena linastahili kukubalika kabisa, kwamba
Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi, ambao kati yao,
mimi ni mwenye dhambi kuliko wote.
Isaya 14:12-14
Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, ewe nyota ya alfajiri, mwana
wa asubuhi, jinsi ulivyokatwa kabisa, ewe uliyewaangusha mataifa.
Nawe ulisema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbiguni, nitakiinua kiti
change juu, kuliko nyota za mungu; name nitaketi juu yam lima wa
mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini.
Nitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana nay eye aliye juu.
Warumi 5:12
12 Kwa hiyo kama vile ambavyo dhambi iliingia ulimwenguni kupitia
kwa mtu mmoja, na dhambi ikaleta kifo, na kwa njia hiyo kifo kikawajia
watu wote kwa kuwa wote walitenda dhambi -
Matendo Ya Mitume 4:11-12
11 Huyu Yesu ndiye ‘lile jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa,
ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.’ 12 Wokovu unapatikana
kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa
wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake
tunaweza kuokolewa!”
Mark1:11
11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa;
nimependezwa nawe.”
2. a. Luka 18:29-33
29 Yesu akajibu, “Nawaam bia hakika, hakuna hata mmoja aliyeacha
nyumba yake, au mke, ndugu, wazazi au watoto kwa ajili ya Ufalme
wa Mungu,
30 ambaye hatapewa na Mungu mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha
haya na kupata uzima wa milele katika maisha yajayo.” 32 Nitatiwa
mikononi mwa watawala wa Kirumi. Watu watanizomea, watanitukana
na kunitemea mate. 33 Watanipiga na kuniua, lakini siku ya tatu
nitafufuka.”
b. Mathayo 12:38-40
38 Kisha baadhi ya waandishi wa sheria na Mafarisayo wakam wambia,
“Mwalimu, tunataka kuona ishara kutoka kwako.” 39 Lakini
yeye akawajibu, “Kizazi cha watu waovu na wasiowaami nifu
hutafuta ishara; lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile
ya nabii Yona. 40 Kwa maana kama vile Yona alivyokaa katika tumbo
la nyangumi kwa muda wa siku tatu mchana na usiku, vivyo hivyo mimi
Mwana wa Adamu nitakaa siku tatu, mchana na usiku ndani ya ardhi.
c. Marko 8:31-32a
31 Akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa yeye, Mwana wa Adamu,
atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, na makuhani wakuu na
walimu wa sheria; na kwamba atauawa na baada ya siku tatu atafufuka.32
Aliyasema haya wazi wazi.
3. Luka 23:4
4 Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni
sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!”
4. Marko 14:61-64
61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu
akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?”
62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu
nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu
ya mbinguni.”
63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani
tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu
gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.
Isaya 53:3-6
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye
sikitiko; na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa
na wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; lakini
tulimzania ya kuwa amepigwa,amepigwa na mungu na kuteswa. Bali alijeruhiwa
kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu
ilikua juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama
kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe;
na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.
5. Marko 14:43-15:47
43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi
kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na
marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, waandishi,
na wazee. 44 Yuda, yule msaliti, alikuwa amewapa ishara wale watu
kuwa, “Yule nitakayembusu, ndiye mnayemtaka, mkamateni na
kumchukua akiwa chini ya ulinzi.”
45 Kwa hiyo Yuda alipofika, alimwendea Yesu akamwambia, “Mwalimu,”
akambusu. 46 Wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. 47 Lakini
mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo aka chukua upanga akampiga
mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 48 Kisha Yesu akasema,
“Mbona mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu? Kwani mimi
ni jambazi?49 Siku zote nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni
wala hamkunikamata. Lakini Maandiko lazima yatimie. ” 50 Ndipo
wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. 51 Kijana mmoja aliyekuwa
amevaa shuka tu alikuwa akimfuata Yesu. Walipomkamata, 52 alikimbia
uchi, akaacha shuka lake.
53 Kisha wakampeleka Yesu nyumbani kwa kuhani mkuu ambapo makuhani
wakuu, wazee, na walimu wa sheria walikuwa wamekuta nika. 54 Petro
aliwafuata kwa mbali, akaingia barazani kwa kuhani mkuu, akaketi
pamoja na walinzi akiota moto. 55 Makuhani wakuu na wajumbe wote
wa Baraza walijaribu kutafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu ili wapate
kumwua, lakini hawakupata. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo, lakini
ushahidi wao haukupatana.
57 Ndipo watu fulani wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo wakisema,58
“Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitabomoa Hekalu hili
lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga lin gine
ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59 Lakini hata hawa,
ushahidi wao ulipingana.
60 Kuhani Mkuu akasimama mbele ya Baraza akamwuliza Yesu, “Huwezi
kujibu mashtaka haya ambayo watu hawa wameleta juu yako?”
61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu
akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?”
62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu
nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu
ya mbinguni.”
63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani
tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu
gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.
65 Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa
usoni wakampiga na kumwambia, “Toa unabii, utuambie nani amekupiga!”
Maaskari wakampokea kwa mapigo.
66 Petro alikuwa bado yuko barazani. Kisha akaja mtumishi mmoja
wa kike wa kuhani mkuu. 67 Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama
sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.”
68 Lakini Petro akakataa, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema,”
akaondoka akaenda mlangoni. 69 Yule mtumi shi wa kike akamwona,
akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama pale, “Huyu mtu
ni mmoja wao.” 70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda
kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika
wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 71 Petro
akaanza kulaani na kuapa, akawaambia, “Simjui huyo mtu mnayemsema.”
72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno
ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara
mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji
Yesu
Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee
na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga
Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza,
“Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe
ndiye uliyesema maneno hayo.” 3 Makuhani wakuu wakamsh taki
kwa mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?
5 Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.
6 Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa
ye yote ambaye watu walimtaka . 7 Wakati huo, mtu mmoja aitwaye
Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa
makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. 8 Basi watu
waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa
desturi wakati wa Pasaka. 9 Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue
huyu mfalme wa Wayahudi?” 10 Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu
wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki
kwake. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie
Baraba.
12 Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita
mfalme wa Wayahudi?” 13 Wakapiga kelele, “Msulub ishe!”
14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini
wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”
15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba;
na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.
16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu
iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika
Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika.
18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!”
19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki
kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha
kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake.
Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.
21 Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja
aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda
na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe
msalaba wa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa
Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.
23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa.
24 Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura
kuamua kila mtu achukue nini.
25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo
la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.”27
Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa
kulia na mwingine upande wa kushoto. [ 28 Na kwa njia hii yale Maandiko
yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia.]
29 Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao
kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja
Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? 30 Shuka msalabani basi, ujiokoe
mwenyewe!”31 Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria
walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa
kujiokoa mwenyewe.32 Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani
ili tupate kuona na kuamini!” Na wale waliosulubiwa pamoja
naye pia walimtukana.
33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa
tatu.34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi,
Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu,
mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu
waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita
36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki,
akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu
tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”
37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka
vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi
alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa
Mungu!”
40 Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa
mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao
Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41 Hawa walifuatana na Yesu
alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine
wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.
42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi, siku moja
kabla ya Pasaka, 43 Yusufu wa Arimathea alijikaza akamwendea Pilato
akamwomba auchukue mwili wa Yesu. Yeye alikuwa ni mjumbe wa Baraza
aliyeheshimika, ambaye alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu.
44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu amekwisha kufa. Kwa hiyo
akamwita askari amhakikishie kuwa kweli amekufa. 45 Baada ya kuhakikishiwa
na yule askari kwamba kweli amekufa, Pilato alimpa Yusufu ruhusa
ya kuuchukua mwili wa Yesu. 46 Basi Yusufu alinunua sanda ya kitani,
akautoa mwili wa Yesu msalabani; akamzungushia sanda, akamweka ndani
ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe
akaufunika mlango wa kaburi.47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama
wa Yose walipaona mahali alipozikwa Yesu.
Mathayo 27:27-28:15
27 Kisha askari wa gavana wakampeleka Yesu kwenye makao makuu ya
gavana wakakusanya kikosi cha askari, wakamzunguka Yesu.
28 Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu ya rangi nyekundu.29 Wakasokota
taji ya miiba wakamvika kichwani. Wakamwekea fimbo mkono wake wa
kulia, wakapiga magoti mbele zake wakamdhihaki wakisema, “Uishi
maisha marefu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate, wakachukua
ile fimbo wakampiga nayo kich wani. 31 Baada ya kumdhihaki, walimvua
ile kanzu, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka kumsulubisha.
32 Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye
Simoni, wakambebesha ule msalaba kwa nguvu. 33 Na wali pofika sehemu
iitwayo Golgotha, maana yake mahali pa Fuvu la Kichwa, 34 wakampa
divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini baada ya kuionja,
akaikataa.
35 Walipokwisha kumsulubisha wakagawana nguo zake kwa kuzi pigia
kura.36 Kisha wakaketi, wakamchunga. 37 Juu ya kichwa chake, kwenye
msalaba, wakaandika shtaka lake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA
WAYAHUDI.’38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja
naye, mmoja kulia kwake na mwingine kushoto kwake.
39 Watu waliokuwa wakipita njiani walimtukana, wakatikisa vichwa
vyao 40 na kusema, “Si ulisema ungevunja Hekalu na kulijenga
kwa muda wa siku tatu? Jiokoe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu
shuka msalabani.” 41 Hali kadhalika, makuhani wakuu, walimu
wa sheria na wazee walimdhihaki, wakisema, 42 “Aliwaokoa wengine,
lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye si Mfalme wa Israeli? Ashuke
kutoka msalabani nasi tutamwamini.
43 Anamwamini Mungu; basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka. Kwa
maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 44
Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa naye walimtukana kwa
njia hiyo hiyo.
45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza.
46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama
sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona
ume niacha?”
47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema,
“Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta
sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo
moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata
kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni,
pakatoka maji na damu].
50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho. 51 Wakati
huo huo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, kuanzia juu hadi
chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52 Makaburi yakafunguka
na miili ya watakatifu waliofariki ili fufuka. 53 Walitoka makaburini
na Yesu alipofufuka walikwenda Mji Mtakatifu wakawatokea watu wengi.
54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa naye wakimlinda Yesu walipoona
lile tetemeko na yote yaliyotokea, waliogopa wakasema, “Hakika,
huyu alikuwa
55 Wanawake wengi walio kuwa wamefuatana na Yesu tangu Gali laya
wakimhudumia, nao walikuwapo wakitazama kwa mbali yote yali yotokea.56
Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo
na Yusufu na mama yao wana wa Zebedayo.
57 Ilipofika jioni, alifika tajiri mmoja kutoka Arimathea aitwaye
Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akaenda kwa Pilato
akaomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59-60 Yusufu alichukua
mwili wa Yesu akauweka katika sanda safi akauzika katika kaburi
lake jipya ambalo lilikuwa limechongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha
jiwe kubwa akafu nika mlango wa kaburi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena
na yule Mariamu mwingine walikuwa wamekaa mbele ya kaburi.
62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi
ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia,
“Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku
tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe
ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja
wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili
likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.”
65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke
ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda
wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka
askari walinzi.
Baada ya Sabato, alfajiri mapema siku ile ya Jumapili, Mari amu
Magdalena na yule Mariamu mwingine walikwenda kuliangalia kaburi.
2 Ghafla pakatokea tetemeko kubwa la ardhi; kwa sababu Malaika wa
Bwana alikuja kutoka mbinguni akalisogeza lile jiwe, akalikalia.
3 Malaika huyo alifanana kama umeme na mavazi yake yalikuwa meupe
kama theluji. 4 Wale walinzi wa kaburi walipomwona walitetemeka
kwa hofu, wakawa kama wamekufa.
5 Lakini yule malaika akawaambia wale wanawake, “Msiogope.
Ninajua kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulubiwa. 6 Hayupo hapa. Amefu
fuka kama alivyosema. Njooni muone pale alipokuwa amelazwa. 7 Kisha
nendeni upesi mkawaambie wanafunzi wake hivi, amefufuka kutoka kwa
wafu naye amewatangulia kwenda Galilaya, mtamwona huko. Sasa nimekwisha
waambia.” 8 Wakiwa wamejawa na hofu na furaha nyingi, wale
wanawake waliondoka upesi pale kaburini, wakaenda mbio kuwaeleza
wanafunzi habari hizo.
9 Mara, Yesu akawatokea, akawasalimia, “Salamu!” Wale
wana wake wakamwendea wakajitupa chini wakaishika miguu yake, wakam
wabudu.10 Ndipo Yesu akawaambia, “Msiogope. Nendeni mkawaambie
ndugu zangu waende Galilaya, wataniona huko.”
11 Wakati wale wanawake walipokuwa wanakwenda, baadhi ya wale askari
waliokuwa wanalinda kaburi, wakaenda mjini kuwaeleza makuhani wakuu
yote yaliyotokea. 12 Baada ya kufanya mkutano na wazee na kushauriana,
waliwapa wale askari kiasi fulani cha fedha na 13 kuwaambia, “Semeni,
‘Wanafunzi wake walikuja wakamwiba usiku sisi tukiwa tumelala.’
14 Kama habari hizi zikimfikia gavana, sisi tutamridhisha na hamtapata
shida yo yote.” 15 Kwa hiyo wale askari wakazipokea hizo fedha
wakafanya kama walivy oagizwa. Na habari hii imeenea kwa Wayahudi
mpaka leo.
Yohana 19:16-21:25
16 Ndipo Pilato akawaka bidhi Yesu wamsulubishe.
17 Kwa hiyo wakamchukua Yesu, naye akatoka akiwa amebeba msalaba
wake kuelekea mahali palipoitwa, ‘Fuvu la kichwa,’ au
kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja
naye walisulubishwa watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto
na mwingine upande wa kulia wa Yesu. 19 Pilato aliandika maneno
yafuatayo kwenye kibao, kikawekwa juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU
WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI”
20 Kwa kuwa mahali hapo palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi
walisoma maneno haya ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania,
Kilatini na Kigiriki. 21 Makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike,
‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali ‘Mtu huyu alisema,
Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.”’ 22 Pilato akawajibu, “
Nilichokwisha andika, nimeandika.”
23 Maaskari walipokwisha msulubisha Yesu, walichukua mavazi yake
wakayagawa mafungu manne; kila askari akapata moja. Ila wal ikubaliana
wasipasue ile kanzu yake kwa maana ilikuwa imefumwa tangu juu hadi
chini na haikukatwa mahali po pote. 24 Wakaam biana, “Tusiipasue
ila tupige kura tuone ni nani aichukue.” Hii ilitimiza yale
Maandiko yaliyosema, “Waligawana mavazi yangu, na kanzu yangu
wakaipigia kura.” 25 Kwa hiyo wakapiga kura. Karibu na msalaba
wa Yesu walikuwa wamesimama: Mariamu mama yake, shan gazi yake,
Mariamu mke wa Klopa na Mariamu Magdalena.26 Yesu alipomwona mama
yake na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, alimwambia
mama yake, “Mama, huyo ni mwanao!”27 Kisha akamwambia
yule mwanafunzi, “Na huyo ni mama yako.” Tangu wakati
huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.
28 Baada ya haya Yesu alifahamu ya kuwa mambo yote yameka milika,
kwa hiyo, ili kutimiza Maandiko, akasema, “Naona kiu.”
29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji
iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo
wakampandishia mdomoni.30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema,
“Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.
31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka
miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya
pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru
miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani.
32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa
na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni,
na mara pakatoka damu na maji. 35 Mambo haya yamehakikishwa na mtu
aliyeyaona, na ushahidi wake ni wa kuaminika. Yeye anajua ya kuwa
aliyosema ni kweli, naye ametoa ushuhuda huu ili nanyi mpate kuamini.
36 Kwa maana mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema,
“Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Na pia
Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma
kwa mkuki.” 38 Baada ya haya, Yusufu wa Arimathea aliyekuwa
mfuasi wa siri wa Yesu, maana aliwaogopa Wayahudi, akamwomba Pilato
auchukue mwili wa Yesu; naye akamruhusu. Kwa hiyo akaja, akauchukua
mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye alimwen dea Yesu kwa
siri usiku, alikuja na mchanganyiko wa manukato zaidi ya kilo thelathini.
40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakau vika sanda iliyokuwa na manukato,
kama ilivyokuwa desturi ya Way ahudi. 41 Karibu na pale walipomsulubisha
palikuwa na bustani yenye kaburi ambalo lilikuwa halijatumika. 42
Kwa hiyo ili kuka milisha mazis
Jumapili asubuhi na mapema, kukiwa bado giza, Mariamu Mag dalena
alifika kaburini akakuta lile jiwe lililokuwa limeziba mlango wa
kaburi limeondolewa. 2 Kwa hiyo akaenda mbio kwa Simoni Petro na
yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akawaambia, “Wameu chukua
mwili wa Bwana kutoka mle kaburini na hatujui wameuweka wapi!”
3 Petro na yule mwanafunzi wakaondoka mara kuelekea kabu rini. 4
Wote wawili walikuwa wanakimbia lakini yule mwanafunzi akakimbia
mbio zaidi kuliko Petro, akawahi kufika kaburini. 5 Alipofika akainama
na kuchungulia mle kaburini akaona ile sanda, lakini hakuingia ndani.
6 Ndipo Petro akaja akimfuata nyuma akaenda moja kwa moja hadi ndani
ya kaburi. Naye akaona ile sanda 7 na kile kitambaa kilichokuwa
kichwani mwa Yesu kimekunjwa na kuwekwa kando ya ile sanda. 8 Kisha
yule mwanafunzi aliyewahi kufika kaburini naye akaingia ndani; akaona,
akaamini. 9 Kwa maana mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa
yale Maandiko yaliyotabiri kuwa angefufuka kutoka kwa wafu. 10 Wale
wanafunzi wakaondoka wakarudi nyumbani kwao.
11 Lakini Mariamu akakaa nje ya kaburi akilia. Na alipokuwa akilia
akainama kutazama mle kaburini. 12 Akaona malaika wawili wamevaa
nguo nyeupe, wamekaa pale mwili wa Yesu ulipokuwa, mmoja upande
wa miguuni na mwingine upande wa kichwani! 13 Wakamwuliza Mariamu,
“Mama, mbona unalia?” Akawaambia, “Nalia kwa kuwa
wamemchukua Bwana wangu na sijui wamemweka wapi.” 14 Alipokuwa
akisema haya akageuka, akamwona Yesu amesimama nyuma yake, lakini
hakumtambua! 15 Yesu akamwambia, “Mama, mbona unalia? Unamta
futa nani?” Mariamu alidhani aliyekuwa anaongea naye ni mtunza
bustani, kwa hiyo akajibu, “Kama ni wewe umemchukua tafadhali
nionyeshe ulipomweka ili nimchukue.” 16 Yesu akamwita, “Mar
iamu.” Ndipo Mariamu akamgeukia Yesu, akamwambia kwa Kiebrania,
“Rabboni!’ 17 Yesu akamwambia, “Usin ishike kwa
maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini nenda kwa ndugu zangu ukawaambie,
ninakwenda kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu
wenu.” 18 Kwa hiyo Mariamu Magdalena akaenda akawakuta wanafunzi
akawaambia, “Nimemwona Bwana!”
19 Jumapili hiyo jioni, wakati wanafunzi walikuwa pamoja huku milango
ikiwa imefungwa kwa kuwaogopa Wayahudi, Yesu aliwato kea! Akasimama
kati yao akasema, “Amani iwe nanyi.” 20 Baada ya kusema
haya, aliwaonyesha mikono yake na ubavu wake. Wanafunzi walifurahi
sana walipomwona Bwana! 21 Yesu akawaambia tena, “Amani iwe
nanyi. Kama Baba alivyonituma, mimi pia nawatuma ninyi.”
22 Na alipokwisha kusema haya akawavuvia pumzi yake akawaambia,
“Pokeeni Roho Mtakatifu.23 Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake,
atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”
24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi
wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.”
Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari
katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari
na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”
26 Siku nane baada ya haya, wanafunzi walikuwa pamoja tena katika
chumba kimoja na Tomaso pia alikuwepo. Milango ilikuwa imefungwa,
lakini Yesu akawatokea akasimama kati yao akawaambia, “Amani
iwe nanyi.”27 Ndipo akamwambia Tomaso, “Weka kidole
chako hapa; tazama mikono yangu halafu nyoosha mkono wako uguse
ubavu wangu. Usiwe na mashaka bali uamini.” 28 Tomaso akasema,
“Bwana wangu na Mungu wangu!” 29 Yesu akamwambia, “Umeamini
kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”
30 Yesu alifanya ishara nyingine nyingi mbele za wanafunzi wake
ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki. 31 Lakini hizi zimeandikwa
ili muweze kuamini ya kuwa Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na
kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.
Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando
ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: 2 Simoni Petro, Tomaso aitwaye
Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi
wengine wawili walikuwa pamoja. 3 Simoni Petro aka waambia wenzake,
“Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda
pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini
usiku ule hawakupata cho chote. 4 Kulipopambazuka, Yesu alisimama
ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. 5 Yesu akawaambia,
“Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.”
6 Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu
nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki
wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika
mashua! 7 Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia
Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga
nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa
baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. 8 Wale wanafunzi wengine wakaja
kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa
wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja
hivi.
9 Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa
juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya
samaki mliovua.”11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu
ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta
ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja
wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua
hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na
baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu
kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.
15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni
mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu,
“Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia,
“Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu
akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?”
Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.”
Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu
Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?”
Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’
Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku
penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia
wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa
mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka
usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro
jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu
akamwambia Petro, “Nifuate.” 20 Petro akageuka akamwona
yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi
ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula
cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’
21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana,
na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi
mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa
sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba
huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa.
Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi,
inakuhusu nini?”
24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye
ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake
ni wa kweli.
Luka 23:26-24:52
26 Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni
wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha
atembee nyuma ya Yesu.
27 Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake
waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28 Lakini Yesu akawageukia,
akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi
bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu.
29 Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa
akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’
30 Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima,
‘Tufunikeni’. 31 Kwa maana kama watu wanafanya mambo
haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”
32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na
Yesu.33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,”
wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa
kulia na mwingine upande wa kushoto.
34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali
tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35 Watu wakasi
mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema,
“Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye
ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36 Askari nao wakam wendea,
wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37 wakamwambia, “Kama
wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”
38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake:
“HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39 Mmoja kati ya wale
wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si
ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”
40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe
humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu
ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini
huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana
Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu
akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”
44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka
saa tisa, 45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu
likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46 Yesu akapaza sauti
akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.”
Baada ya kusema haya, akakata roho.
47 Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema,
“Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48 Na watu wote
waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona
hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.
49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa
wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo
haya. Yesu Azikwa Kaburini
50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya,
ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe
wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika.51 Lakini
yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo
cha kumsulubisha Yesu. 52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba
apewe mwili wa Yesu. 53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia
sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi
hilo lilikuwa halijatumika bado. 54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku
ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze. 55 Wale wanawake
waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu,
wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo. 56 Kisha
wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili.
Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.
Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua
yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini. 2 Wakakuta
jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi. 3 Lakini walipoingia
ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa wanashangaa juu
ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa
sana, wakasimama karibu nao. 5 Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha
nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta
aliye hai mahali pa wafu? 6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia
alipokuwa Gali laya, 7 kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe
mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.”8
Wakayakumbuka maneno ya Yesu. 9 Waliporudi kutoka huko kaburini
wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na
wengine wote. 10 Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana
na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao.11
Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini. 12 Bali
Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile
sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia
yaliyotokea.
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda
kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa
wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza,
Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao, 16 lakini wao hawakumtambua.
17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?”
Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni.18 Mmoja wao, aliyeitwa
Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi
Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”
19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo
yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu
katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu.
20 Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha.
21 Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa
Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.
22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda
kaburini leo alfajiri23 lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi
walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai.
24 Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea
wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”
25 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona
ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii? 26 Je, haikumpasa
Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?”
27 Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na
maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.
28 Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama
anaendelea na safari. 29 Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa
hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi
akaingia ndani kukaa nao. 30 Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate,
akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa,
wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.
32 Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha
alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”
33 Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi
kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika 34 wakisema,
“Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.” 35 Kisha
wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua
Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama
katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza,
“Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu?39
Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni
mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema
haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini
kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna
chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa
kuokwa,43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa
pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she
ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”
45 Akawapa uwezo wa kuyaelewa Maandiko, 46 aka waambia, “Haya
ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka
kwa wafu. 47 Habari hii ya wokovu itatan gazwa kwanza Yerusalemu
hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msa maha wa dhambi kwa wote
watakaotubu na kunigeukia mimi.48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.
49 Na sasa nitawapelekea Roho Mtaka tifu kama alivyoahidi Baba yangu;
lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapopewa nguvu ya Roho Mtakatifu
kutoka mbinguni.”
50 Kisha akawaongoza nje ya mji mpaka Bethania, akainua mikono yake,
akawabariki. 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.52
Wakamwabudu na kisha wakarudi Yerus alemu wamejawa na furaha;
Matendo Ya Mitume1: 1-11
Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia
kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, 2 hadi wakati alipopaa mbinguni.
Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya
Roho Mtakatifu. 3 Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini
baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa
ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.
4 Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke
Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni
sikia nikiizungumzia. 5 Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini
baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6 Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati
huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”
7 Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira
ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. 8 Lakini mtapokea nguvu
akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”
9 Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na
wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho
yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa
mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu
wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu
huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda
mbinguni.”
2 Wakorintho 5: 21
21 Mungu alimfanya yeye ambaye hakujua dhambi, awe dhambi kwa ajili
yetu ili ndani yake tupate kuwa haki ya Mungu.
1 Yohana 3: 8-10
8 Kila atendaye dhambi ni wa shetani; kwa maana shetani ametenda
dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alikuja ili aziangamize kazi
za shetani.
9 Mtu aliyezaliwa na Mungu haendelei na tabia ya kutenda dhambi,
kwa maana ana asili ya Mungu; hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa
sababu amezaliwa na Mungu.
10 Na hivi ndivyo tunavyoweza kutambua wazi kati ya walio watoto
wa Mungu na walio watoto wa shetani. Mtu ye yote asiyet enda lililo
haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu.
Waefeso 1: 18-22
18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate
kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu
wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao
ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20 ambayo
aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono
wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. 21 Hapo alipo ni juu sana,
kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita
cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi,
bali pia katika nyakati zijazo. 22 Na Mungu ameweka vitu vyote viwe
chini ya mamlaka yake na akamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili
ya kanisa.
Ufunua wa Yohana 20:1-3, 7-10
Kisha nikaona malaika akija kutoka mbinguni akiwa ameshika ufunguo
wa lile shimo la kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi. 2 Akalishika
lile joka, yule nyoka wa kale ambaye ni Ibilisi au Shetani, akamfunga
kwa muda wa miaka elfu moja. 3 Akamtupa kuzi muni; akamfungia huko
na kumzibia kabisa, asipate nafasi ya kudanganya mataifa tena mpaka
hiyo miaka elfu moja iishe. Baada ya hapo ataachiliwa kwa muda mfupi.
7 Miaka hiyo elfu moja itakapokwisha, shetani atafunguliwa kutoka
kifungoni mwake, 8 naye atakuja kuyadanganya mataifa yali yopo katika
pembe nne za dunia, yaani, Gog na Magog na kuwakusa nya tayari kwa
vita. Idadi yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Nao walitembea juu
ya eneo lote la dunia, wakaizunguka kambi ya wata katifu na ule
mji mwema, lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza.
10 Na yule Ibilisi aliyewadanganya alitupwa katika ziwa la moto
na kiberiti walipokuwa yule mnyama na yule nabii wa uwongo. Nao
watateseka huko usiku na mchana, milele na milele.
7. Matendo 4:12
12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani
ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina
hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”
|
|