Stonecroft
Mafunzo wa Stonecroft
Mfululizo wa Utatu wa Stonecroft
Kitabu cha Mwongozo
Mistari ya Biblia
Stonecroft Kimataifa
Uinjilisti wa Mtoto
Mradi wa Mlonge
The International Team
YDT Teachings
|
|
home >>stonecroft>>
mwongozo
>> yesu
ni nani somo 3 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #3
SOMO LA TATU
YESU ALIFANYA NINI?
Kitabu mwongozo
Mistari ya Biblia
Kujisomea Biblia kwa Juma
Marko 1:16-28
6 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya Ziwa la Galilaya alimwona
Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa kutumia nyavu; ndugu
hawa wawili walikuwa wavuvi. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni,
nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” 18 Wakaacha nyavu zao
mara moja wakamfuata Yesu. 19 Alipokwenda mbele kidogo, akawaona
Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo. Wao walikuwa katika mashua wakitengeneza
nyavu zao. 20 Mara tu alipowaona akawaita, nao wakamwacha baba yao
na wavuvi wa kuajiriwa, wakamfuata Yesu.
21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda
katika sinagogi akaanza kufundisha. 22 Watu waliom sikiliza, walishangazwa
sana na mafundisho yake. Yeye hakufund isha kama walimu wao wa sheria.
Alifundisha kama mtu mwenye mam laka.
23 Wakati huo huo, mtu mmoja aliyekuwa na pepo 24 akapiga kelele
humo katika sinagogi akasema, “Mbona unatuingilia, Yesu wa
Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninafahamu wewe ni nani! Wewe ni
Mtakatifu wa Mungu.”25 Lakini Yesu akamkemea akamwambia, “Kaa
kimya! Mtoke!” 26 Yule pepo mchafu akamtikisa yule mtu kwa
nguvu kisha akamtoka akipiga kelele.
27 Watu wakashangaa, wakaanza kuulizana, “Haya ni mambo gani?
Ni mafundisho mapya? Huyu mtu anatoa amri kwa mamlaka na hata pepo
wanamtii!” 28 Sifa zake zikaenea upesi kila mahali katika
mkoa wote wa
Marko 1:29-39
29 Yesu na wanafunzi wake walipoondoka katika sinagogi, walikwenda
moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. Wanafunzi wengine
waliokuwepo ni Yakobo na Yohana. 30 Mama mkwe wake Simoni alikuwa
kitandani, ana homa. Na mara Yesu alipofika wakamweleza. 31 Yesu
akaenda karibu na kitanda, akamshika yule mama mkono, akamwinua;
homa ikamtoka, akawahudumia.
32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote
na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo
wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi
waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini
hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni
nani. 35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka
akaenda mahali pa faragha, akaomba. 36 Simoni na wenzake wakaenda
kumtafuta.37 Walipomwona wakamwambia, “Kila mtu ana kutafuta!”
38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani
nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.”
39 Kwa hiyo akazunguka Galilaya nzima akihubiri katika masinagogi
na kuponya watu waliopagawa na pepo.
Marko 3:13-19
13 Yesu alipanda mlimani akawaita wale aliowataka, nao wakaja.14
Akawachagua kumi na wawili wafuatane naye na awatume kuhubiri na15
wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16 Hawa ndio aliowachagua: Simoni,
ambaye alimwita Petro, 17 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo ambao
aliwaita Boanerge, yaani wana wa ngurumo; 18 Andrea; Filipo; Bartholomayo;
Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Thadayo; Simoni, Mkanaani;
na 19 Yuda
Marko 4:35-41
35 Siku hiyo, ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvuke,
twende ng’ambo ya pili.” 36 Wakawaacha wale watu wakaingia
katika ile mashua ambamo Yesu alikuwa amekaa. Pia palikuwa na mashua
nyingine.
37 Pakatokea dhoruba kali, mawimbi yakaipiga ile mashua waliyokuwa
wakivukia, ikaanza kujaa maji. Yesu alikuwa amelala akiegemea mto
sehemu ya nyuma kwenye ile mashua.
38 Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali
kwamba tuna zama?’ 39 Akaamka, akaukemea ule upepo, akaiambia
ile bahari, “Kaa kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia,
kukawa shwari. 40 Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini
mnaogopa? Je, bado hamna imani?” 41 Lakini wao walikuwa wamejawa
na hofu wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi
vinamtii?”
Marko 6:30-44
30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo
yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa
wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia
wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate
kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda
mahali pasipo na watu.
33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia
mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda.
Wakawahi kufika.
34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea
huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa
hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea
wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda.
36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba
na vijiji vya jirani.”
37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam
wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya
kutosha kulisha watu wote hawa.”
38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.”
Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”
39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye
nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini
hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili
akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa
wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki
wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya
vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya
wanaume waliokula walikuwa elfu tano.
Marko 10:2-16
2 Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakitaka kumtega, wakamwul iza,
“Ni halali mtu kumwacha mke wake?”
3 Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuruje?” 4 Wakamjibu,
“Musa aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati
ya talaka na kumwacha.”
5 Yesu akawaambia, “Musa aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu
ya ugumu wa mioyo yenu. 6 Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu
aliwaumba mume na mke. 7 Na kwa sababu hii mume atamwacha baba yake
na mama yake na hao wawili, watakuwa mwili mmoja.’ 8 Kwa hiyo
hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja. 9 Basi, alichokiun ganisha
Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”
10 Baadaye waliporudi nyumbani , wanafunzi wa Yesu walimwul iza
kuhusu jambo hili.
11 Akawajibu, “Mtu ye yote anayempa mkewe talaka na kuoa mke
mwingine, anazini kwa yule mke aliyempa talaka. 12 Na mwa namke
anayempa mumewe talaka na kuolewa na mume mwingine, anazini pia.”
13 Watu walikuwa wakimletea Yesu watoto wadogo ili awaguse lakini
wanafunzi wake wakawakemea. 14 Yesu alipoona yaliyokuwa yakitokea
alichukizwa, akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo
waje kwangu wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa watu
kama hawa! 15 Ninawahakikishieni kwamba, mtu ye yote ambaye hataukubali
Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”16 Akawakumbatia
wale watoto wadogo, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Yohana 2:13-22
13 Ilipokaribia sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka, Yesu alikwenda
Yerusalemu. 14 Alipoingia Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng’ombe,
kondoo na njiwa, na wengine wamekaa kwenye meza zao wakifanya biashara
ya kubadilishana fedha. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba akawafukuza
wote kutoka Hekaluni pamoja na kon doo na ng’ombe; akazipindua
meza za wale waliokuwa wakibadilish ana fedha na kuzimwaga fedha
zao.
16 Akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, “Watoeni hapa!
Mnathubutuje kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko?” 17
Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa Maan diko yalisema: “Upendo
wangu kwa nyumba yako utaniangamiza.”
18 Viongozi wa Wayahudi wakamwuliza, “Unaweza kutuonyesha
ishara gani kuthibitisha una mamlaka ya kufanya mambo haya?”
19 Yesu akawajibu, “Livunjeni hili Hekalu, nami nitalijenga
tena kwa siku tatu!”
20 Wale Wayahudi wakamjibu, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda
wa miaka arobaini na sita. Wewe unasema unaweza kulijenga kwa siku
tatu?”
21 Lakini yeye aliposema ‘Hekalu’ alikuwa anazungumzia
mwili wake. 22 Kwa hiyo alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi
wake walikumbuka maneno haya; wakayaamini Maandiko na yale maneno
ali yosema Yesu.
Marko 11: 15-17
15 Walipofika Yerusalemu, Yesu aliingia Hekaluni akaanza kuwafukuza
watu waliokuwa wakifanya biashara humo. Akapindua meza za waliokuwa
wakibadilisha fedha na viti vya watu waliokuwa wakiuza njiwa.16
Hakuruhusu mtu ye yote kuchukua bidhaa kupi tia ukumbi wa Hekalu.17
Akawafundisha akisema, “Je, haikuan dikwa katika Maandiko
kuwa: ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa watu wote’?
Mbona ninyi mmeigeuza kuwa pango la wany ang’anyi?”
Luka 1: 29,34
29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni,
maana ya salamu hizi ni nini.
34 Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba,
na mimi ni bikira?”
Luka 2: 19, 51
19 Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake, akayafikiria
mara kwa mara.
51 Akarudi pamoja na wazazi wake hadi Nazareti. Akawa aki watii,
na mama yake akayaweka moyoni mambo haya yote.
Yohana 1: 1-3, 14
Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo
Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu
mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala
hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba.
14 Neno akawa mwanadamu akaishi kati yetu akiwa amejaa utu kufu
na kweli. Tuliona utukufu wake, utukufu wa Mwana pekee wa Baba.
1. a. Luke 3:23
23 Yesu alikuwa na umri wa miaka kama thelathini hivi ali poanza
kazi ya kuhubiri. Yesu alijulikana kama mtoto wa Yusufu. Yusufu
alikuwa mwana wa Eli,
b. 1 Yohana 4:9
9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma
Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa
kupitia kwake.
2. a Yohana 5:17
17 Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya mema siku zote. Mimi
pia sina budi kufanya mema.”
3. a. Marko 1:21
21 Wakaenda mpaka Kapernaumu. Ilipofika siku ya sabato, Yesu akaenda
katika sinagogi akaanza kufundisha.
b. Marko 1:32-34
32 Jioni ile, baada ya jua kutua, watu wakawaleta wagonjwa wote
na wengine waliopagawa na pepo kwa Yesu. 33 Watu wote wa mji huo
wakakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 Yesu akawaponya watu wengi
waliokuwa na magonjwa ya kila aina. Akawatoa pepo wengi; lakini
hakuwaruhusu pepo hao wazungumze, kwa sababu wal ifahamu yeye ni
nani.
c. Marko 1:35
35 Kesho yake alfajiri, kabla hapajapambazuka, Yesu akaamka akaenda
mahali pa faragha, akaomba.
d. Marko 1:38
38 Yesu akawajibu, “Twendeni kwenye vijiji vingine vya jirani
nikahubiri huko pia; kwa sababu hicho ndicho kilicho nileta.”
e. Marko 6:7-12
7 Akawaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili
wawili na akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu.
8 Akawaagiza wasichukue cho chote safarini isipokuwa fimbo tu. Wasichukue
mkate, wala mfuko, wala fedha. 9 Ila wavae viatu lakini wasichukue
nguo ya kubadili. 10 Pia akawaambia, “Mkiin gia nyumba yo
yote, kaeni hapo hapo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 Na mahali
po pote ambapo hamtakaribishwa wala kusikili zwa, mtakapoondoka
hapo, kung’uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, kama onyo
lenu kwao.”
12 Kwa hiyo wakatoka, wakaenda wakihubiri kwamba watu wat ubu, waache
dhambi.
Yohana 21: 25
25 Jesus did many other things as well. If every one of them were
written down, I suppose that even the whole world would not have
room for the books that would be written.
4. a. Luka 4:33-36
33 Alikuwepo mtu mmoja katika sinagogi aliyekuwa ame pagawa na pepo
mchafu, naye alianza kupiga kelele kwa nguvu akisema, 34 “Unataka
kutufanya nini, Wewe Yesu wa Nazareti? Ume kuja kutuangamiza? Nakufahamu
wewe ni nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 35 Yesu akamwamuru
yule pepo: “Nyamaza! Mtoke!” Yule pepo akamwangusha
chini yule mtu mbele yao, akamtoka pasipo kumd huru. 36 Watu wote
wakashangaa wakaambiana, “Mafundisho ya mtu huyu ni ya ajabu.
Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka!
b. Luka 5:4-10
4 Alipokwisha zungumza na watu akamwambia Simoni, “Sasa ipe
leke mashua hadi mahali penye kina kirefu, kisha mshushe nyavu zenu
nanyi mtapata samaki.”
5 Simoni akamjibu, “Bwana, tumekesha usiku kucha tukivua na
hatukuambulia kitu cho chote. Lakini, kwa kuwa wewe umesema, tutazishusha
nyavu.” 6 Nao walipofanya kama Yesu alivyowaagiza, nyavu zao
zikajaa samaki, zikaanza kuchanika! 7 Wakawaashiria wavuvi wa ile
mashua nyingine waje kuwasaidia. Mashua zote mbili zikajaa samaki
hata karibu kuzama.
8 Simoni Petro alipoona yaliyotokea alipiga magoti mbele ya Yesu
akamwambia, “Bwana,tafadhali uniache kwa maana mimi ni mwe
nye dhambi.” 9 Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wamesh
angazwa sana na wingi wa samaki waliopata. 10 Hali kadhalika wavuvi
wa ile mashua nyingine, Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo walishangazwa
pia. Ndipo Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangu sasa utakuwa
mvuvi wa watu.”
c. Marko 1:40-42
40 Akaja mtu mwenye ukoma, akapiga magoti mbele ya Yesu akamsihi,
“Ukitaka, unaweza kunitakasa.” 41 Yesu akamwonea huruma,
akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka upone,
takasika.” 42 Mara ukoma wote ukaisha akapona kabisa.
d. Mathayo 15:1-9
Baadhi ya walimu wa sheria na Mafarisayo kutoka Yerusalemu walikuja
kwa Yesu wakamwuliza, 2 “Mbona wanafunzi wako hawafu ati mafundisho
ya wazee wetu? Kwa maana wao hawanawi mikono ka bla ya kula!”
3 Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnazivunja amri za Mungu kwa
ajili ya mafundisho yenu? 4 Kwa maana Mungu alisema: ‘Waheshimu
baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtukanaye baba
yake au mama yake, na auawe.’ 5 Lakini ninyi mnasema kwamba
mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza
kuku saidia nacho nimekitoa kwa Mungu,’ basi hana wajibu tena
wa kum saidia baba yake. 6 Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja
amri ya Mungu. 7 Ninyi wanafiki! Isaya alisema sawa juu yenu alipotabiri
kwamba: 8 ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo
yao iko mbali nami. 9 Kuniabudu kwao ni bure, na mafundisho yao
ni maagizo ya wanadamu.’
e. Luka 7:11-17
11 Baada ya siku hiyo, Yesu alikwenda mji mmoja uitwao Naini. Wanafunzi
wake na umati wa watu waliongozana naye. 12 Alipokaribia njia ya
kuingia mjini alikutana na watu wal iobeba maiti wakitoka nje ya
mji. Marehemu alikuwa mtoto wa kiume wa pekee wa mama mmoja mjane
na umati wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mama. 13 Bwana
Yesu alipomwona yule mjane moyo wake ulijaa huruma, akamwambia,
“Usilie.” 14 Kisha akalisoge lea lile jeneza akaligusa
na wale waliolibeba wakasimama. Ndipo akasema: “Kijana nakuambia,
amka!” 15 Yule aliyekuwa marehemu akaamka, akakaa na akaanza
kusema! Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16 Watu wote wakajawa na hofu. Wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii
mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kutuokoa sisi watu wake.”17
Habari hizi za mambo aliyofanya Yesu zikaenea Uyahudi nzima na sehemu
za jirani.
Luka 3:21-22
21 Baada ya watu wote kubatizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa
akiomba, mbingu zilifunguka. 22 Roho Mtakatifu akash uka juu yake
kama hua; na sauti ikasikika kutoka mbinguni ikisema: “Wewe
ni Mwanangu mpendwa, ninapendezwa nawe.”
5. a. Yohana 6:38
38 Kwa maana sikushuka kutoka mbinguni nije kutimiza mapenzi yangu,
bali nitimize mapenzi yake yeye aliyenituma.
b. Yohana 7:16-17
16 Yesu akawajibu , “Mafundisho yangu hayatoki kwangu. Yanatoka
kwake yeye aliyenituma. 17 Mtu ye yote akipenda kufanya mapenzi
ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema
kwa mamlaka yangu mwenyewe.
c. Wafilipi 2:13
13 Kwa maana ni Mungu ambaye anatenda kazi ndani yenu, akiwapa nia
ya kutimiza mapenzi yake na kuwawezesha kutenda yale yanayompendeza
1
6. Warumi 12:2
2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu
zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya
Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.
Mwanzo 1:27-28
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimuumba mwanamume
na mwanamke alimuumba. Mungu akawabarikia, mungu akawaambia, zaeni,
mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini,
na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya
nchi.
Mwanzo 2:15
Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya edeni,
ailime na kuitunza.
Mwanzo 3:17
Akamwambia adamu, kwa kuwa umesikiliza sauti ya mke wako, ukala
matunda ya mti aambao nalikuagiza, nikasema, usiyale; ardhi imelaaniwa
kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha
yako.
7. a. 2 Wathethalonike 3:10
10 Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa
mtu hatafanya kazi, basi asile.”
b. Warumi 12:11
11 Juhudi yenu isipungue, moto wenu wa kiroho uendelee kuwaka mkimtumikia
Mungu.
8. Waefeso 6:5-8
5 Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima
na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. 6
Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama
watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo.
7 Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na
sio watu. 8 Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana
na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru.
9. a. 1 Wakorintho 10:31
31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo
yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
b. 1 Wakorintho 16:14
14 Fanyeni kila kitu katika upendo.
c. Wakolosai 3:23
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia
Bwana na siyo wanadamu.
Yohana 13: 34-35
34 Nina waachia amri mpya: pendaneni ninyi kwa ninyi. Kama mimi
nilivy owapenda, na ninyi mpendane vivyo hivyo. 35 Kama mkipendana
hivyo, watu wote watafahamu ya kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”
Exodus 31:15
15 For six days work is to be done, but the seventh day is a day
of sabbath rest, holy to the Lord. Whoever does any work on the
Sabbath day is to be put to death.
Matayo 5: 17
17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho
ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna
hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike.
Marko 6: 31
31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa
nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni
peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.”
Matayo 11: 28-30
28 “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu; jifunzeni
kutoka kwangu; kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi
mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni rahisi, na
mzigo wangu ni mwepesi.”
10. a.Yohana 6:29
29 Yesu akawajibu, “Kazi anayotaka Mungu muifanye ni hii:
mumwamini yeye aliyenituma.”
b. Yohana 3:16
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele
1 Corinthians 3: 13-15
13 kazi yake itaonekana; kwa kuwa ile siku itaidhihirisha kazi yake.
Itadhihirishwa kwa moto, na moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu.
14 Kama alichojenga hakitaharibiwa kwa moto, atapokea tuzo. 15 Kama
kazi ya mtu itateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa,
lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto.
|
|