Project Hope     home >>stonecroft>> mwongozo >> yesu ni nani somo 2 >> mistari ya biblia
Mistari ya Biblia - Somo #2
Women's Empowerment  Program
Sports Bible Club
Living Water Bible Club

SOMO LA PILI

YESU ALISEMA NINI?

Kitabu mwongozo

Mistari ya Biblia

Kujisomea Biblia kwa Juma

Mathayo 5:1-12
1 Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, 2 naye akaanza kuwafundisha akisema:
3 “Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. 4 Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. 5 Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. 6 Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. 7 Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. 8 Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. 9 Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 10 Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.

Mathayo 5:13-16
13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezekani kuwa chumvi tena. Haifai kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kwenye mlima haufichiki.15 Wala hakuna mtu anayewasha taa kisha akaifunika. Badala yake, huiweka mahali pa juu ili itoe mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya nyumba. 16 Hali kadhalika, nuru yenu iwaangazie watu ili waone matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbin guni.’

Mathayo 6:1-15
“Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 “Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao.
3 Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; 4 ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”
5 “Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6 Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.
7 “Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 8 Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.” 9 Basi msalipo ombeni hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku. 12 Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea. 13 Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,’ [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.] 14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15 lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

Mathayo 6:24-34
24 “Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”
25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege?27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?
28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo.
29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo.
30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”

Mathayo 7:1-12
1 Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. 2 Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. 3 Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? 5 Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.
6 “Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”
7 “Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.
9 “Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Mathayo 7:13-20
13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”
15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

Mathayo 7:21-27
21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’
24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

Yohana 8:56-59
56 Baba yenu Ibrahimu alifurahi sana kwamba angeiona siku nilipokuja duniani. Hakika aliiona na akafurahi sana.”

57 Wayahudi wakamwambia Yesu, “Ati nini? Wawezaje kusema ulimwona Ibrahimu? Wewe bado hujafikisha hata umri wa miaka hamsini!”

58 Yesu akajibu, “Ukweli ni kwamba, kabla Ibrahimu hajazaliwa MIMI NIPO.” 59 Aliposema haya, wakachukua mawe ili wamponde. Lakini Yesu akajificha, na kisha akaondoka katika eneo la Hekalu.

1. a. Yohana 13:19
19 Ninawaambia mambo haya kabla hayajatokea ili yatakapotokea mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye Kristo.

b. Yohana 8:12
12 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.”

c. Yohana 10:9
9 Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho.

d. Yohana 10:11
11 Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo.

e. Yohana 10:36
36 itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni?

f. Yohana 11:25
25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi;

g. Yohana 6:48
48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa.

h. Yohana 14:6
6 Yesu akawaam bia, “Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu.

3. Mathayo 5:21-26
21 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usiue; na ye yote atakayeua atastahili hukumu.’ 22 Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena. 23 “Basi, kama ulikuwa tayari kutoa sadaka yako madhaba huni, ukakumbuka kuwa ndugu yako amekukasirikia, 24 acha sadaka yako hapo hapo, uende kwanza ukapatane naye, kisha urudi kumtolea Mungu sadaka yako. 25 “Mtu akikushtaki, patana naye kabla hamjafika mahaka mani; ili mshtaki wako asije akakukabidhi kwa hakimu, na hakimu akamwamuru askari akufunge gerezani; 26 nami nawaambia hakika, hutatoka huko mpaka deni lako lote litakapolipwa.”

Mathayo 5:3-12
3 “Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. 4 Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. 5 Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. 6 Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. 7 Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. 8 Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. 9 Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 10 Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.

Mathayo 5:13-16
13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezekani kuwa chumvi tena. Haifai kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.
14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kwenye mlima haufichiki.15 Wala hakuna mtu anayewasha taa kisha akaifunika. Badala yake, huiweka mahali pa juu ili itoe mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya nyumba. 16 Hali kadhalika, nuru yenu iwaangazie watu ili waone matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbin guni.’

Mathayo 5:17-20
17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19 Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18 Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii a taitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20 Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Mathayo 5:27-30
27 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usi zini’. 28 Lakini mimi nawaambia: ye yote atakayemwangalia mwa namke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kulia likikufanya utende dhambi, ling’oe ulitu pilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena. 30 Na kama mkono wako wa kuume ukiku fanya utende dhambi, ukate uutupilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena.

Mathayo 5:31-32
31 “Pia mliambiwa kwamba, ‘Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.’32 Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la uasherati, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini.”

Mathayo 5:33-37
33 “Tena mmesikia watu wa kale waliambiwa kwamba, ‘Usi vunje kiapo chako bali umtimizie Mungu kama ulivyoapa kutenda.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu,35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”

Mathayo 5:38-42
38 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia;40 na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili. 42 Mtu akikuomba kitu mpe, na usikatae kumsaidia mtu anayetaka kukukopa.”

Mathayo 5:43-48
43 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo. 47 Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo. 48 Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Mathayo 6: 1 – 4
“Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 “Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao. 3 Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; 4 ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Mathayo 6: 5 – 15
5 “Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. 6 Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.
7 “Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. 8 Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.” 9 Basi msalipo ombeni hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku. 12 Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea. 13 Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,’ [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.] 14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15 lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

Mathayo 6: 16 – 18
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao. 17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni.

Mathayo 6: 19 – 21
19 “Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba.21 Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”

Mathayo 6: 22 – 23
22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zuri, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Kwa hiyo kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hakika utakuwa na giza la kutisha.”

Mathayo 6: 24 – 24
24 “Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”
25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege?27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?
28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”

Mathayo 7: 1 – 6
Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. 2 Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. 3 Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? 4 Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? 5 Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.
6 “Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”

Mathayo 7: 7 – 12
7 “Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.
9 “Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Mathayo 7: 13 – 14
13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”

Mathayo 7: 15 – 20
15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

Mathayo 7: 21 – 23
21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’

Mathayo 7: 24 – 27
24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

Mathayo 7: 28 – 29
28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.

1 Wakorintho 2: 13-16
13 Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho. 14 Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu kwa sababu mambo hayo ni upuuzi kwake; na hawezi kuyaelewa kwa kuwa hayo yanaeleweka tu kwa msaada wa Roho.
15 Mtu wa kiroho anao uwezo wa kupima kila kitu, lakini yeye hapimwi na mtu. 16 “Kwa maana ni nani amefahamu mawazo ya Bwana ili apate kumshauri?” Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

4. Mathayo 13:1-58
1 Siku hiyo hiyo Yesu alitoka nyumbani akaketi kando ya bahari. 2 Umati mkubwa mno wa watu wakasongamana hata ikabidi aingie katika mashua akaketi humo; na wale watu wakakaa ukingoni mwa bahari. 3 Kisha akawaambia mambo mengi kwa mifano, akasema: “Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. 4 Alipokuwa akitawanya mbegu, baadhi zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila.
5 Nyingine zikaanguka kwenye mawe, ambapo hapakuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka kwa sababu udongo ulikuwa kidogo. 6 Lakini jua kali lilipowaka, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikwenda chini. 7 Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba. Miiba hiyo ikakua ikazisonga.
8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri zikatoa mazao, nyingine mara mia moja zaidi ya mbegu zilizopandwa, nyingine mara sitini na nyingine mara the lathini.9 Mwenye nia ya kusikia na asikie.”
10 Wanafunzi wake wakamwendea wakamwuliza, “Kwa nini unazungumza na watu kwa mifano?” 11 Akawajibu, “Ninyi mmejal iwa kuzifahamu siri za Ufalme wa mbinguni, lakini wao hawakujal iwa.
12 Kwa maana mtu aliye na kitu ataongezewa mpaka awe navyo tele; lakini mtu asiye na kitu, hata kile alichonacho atany ang’anywa. 13 Hii ndio sababu nazungumza nao kwa mifano; wanata zama lakini hawaoni, wanasikiliza lakini hawasikii, wala hawae lewi. 14 Hali yao inatimiza ule utabiri wa nabii Isaya ali posema:’Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa, na pia mtatazama lakini hamtaona. 15 Kwa maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, wakanigeukia, nami nikawaponya.’16 Lakini macho yenu yame barikiwa, kwa maana yanaona, na masikio yenu yamebarikiwa kwa maana yanasikia. 17 Nawaambieni kweli, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona mnayoyaona, na hawakuyaona; na kusikia mnayosikia lakini hawakuyasikia.”
18 “Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi aliyepanda mbegu. 19 Mtu anaposikia neno la Ufalme na asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake; hii ndio mbegu iliyopandwa njiani. 20 Mbegu iliyopandwa kwenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na kulipokea mara moja kwa furaha. 21 Lakini kwa kuwa hana mizizi ndani yake, neno hilo hukaa kwa muda mfupi;
Na inapotokea dhiki au mateso kwa ajili ya hilo neno, yeye mara moja huanguka. 22 Mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno na mahangaiko ya maisha haya na anasa za mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. 23 Lakini mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu ambaye hulisikia neno na kulielewa. Naye hakika huzaa matunda, mara mia, au mara sitini, au mara thelathini zaidi ya mbegu iliyo pandwa.”
24 Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbi nguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.25 Lakini watu walipokuwa wamelala, adui yake aka ja akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Ngano ilipoota na kuzaa, magugu nayo yakachipua. 27 “Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwul iza, ‘Bwana, si ulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Imekuwaje kuna magugu?’ 28 Akawajibu, ‘Adui ndiye amefanya jambo hili’. Wale watumishi wakamwuliza, ‘Sasa unataka tukayang’oe?’ 29 Lakini akasema, ‘Hapana msiyang’oe, kwa maana huenda katika kung’oa magugu mkang’oa na ngano pia. 30 Acheni ngano na magugu yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavu naji wayang’oe magugu kwanza wayafunge katika mafurushi tayari kwa kuchomwa moto, lakini wavune ngano na kuikusanya ghalani mwangu.’ ”
31 Akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na punje ndogo ya haradali ambayo mtu aliichukua akaipa nda shambani mwake. 32 Ijapokuwa mbegu hiyo ni ndogo kuliko mbegu zote, lakini inapokua, mmea wake huwa mkubwa kuliko mimea yote bustanini; nao huwa mti mkubwa ambao ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
33 Akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika vipimo vitatu vya unga mpaka wote ukaumuka.”
34 Haya yote Yesu aliwaeleza umati wa watu kwa kutumia mifano. Na hakika hakuwaambia lo lote pasipo kutumia mfano.
35Hii ilikuwa kutimiza utabiri wa nabii, kwamba, ‘Nitazungumza nao kwa mifano; nitatamka mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.’
36 Kisha Yesu akaagana na huo umati wa watu, akaingia nyum bani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.”
37 Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni mimi Mwana wa Adamu.38 Shamba ni ulimwengu, na mbegu nzuri ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. 39 Yule adui aliyepanda magugu ni shetani. Mavuno ni mwisho wa ulimwengu; na wavunaji ni malaika. 40 Kama vile magugu yanavyong’olewa na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa ulimwengu. 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika wake wang’oe kutoka katika Ufalme wake kila kitu kinachosababisha dhambi na watenda maovu wote.
42 Nao wata watupa katika tanuru la moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno. 43 Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Mwenye nia ya kusikia, na asikie.”
44 “Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani ambayo mtu mmoja aliigundua akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akanu nua lile shamba.”
45 Tena, Ufalme wa mbinguni unafanana na mfanya biashara aliyekuwa akitafuta lulu safi,46 ambaye alipo pata lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza vyote alivyo kuwa navyo akainunua.”
47 “Na tena Ufalme wa mbinguni ni kama wavu wa kuvulia samaki ambao ulitandazwa baharini ukakamata samaki wa kila aina. 48 Ulipojaa, wavuvi waliuvuta ukingoni, wakachagua samaki wazuri wakawaweka kwenye vyombo safi, lakini wale samaki wabaya wakawat upa.
49 “Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. 50 Na watawatupa hao waovu katika tanuru ya moto ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
51 Je, mmeyaelewa haya yote?” Wakam jibu, “Ndio.” 52 Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa sheria aliye mwanafunzi wa Ufalme wa mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka katika ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”
53 Yesu alipomaliza kutoa mifano hii, aliondoka. 54 Alipo fika mji wa kwao, aliwafundisha watu katika sinagogi lao. Nao wakastaajabu, wakauliza, “Mtu huyu amepata wapi hekima hii na uwezo huu wa kufanya miujiza? 55 Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si anaitwa Mariamu, na ndugu zake ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake si wako hapa nasi Amepata wapi basi mambo haya yote?” 57 Wakakataa kumpokea. Lakini Yesu aka waambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika nchi yake na nyumbani kwake.”
58 Na hakufanya miujiza mingi huko kwa sababu ya kutokuamini kwao.

5. Luka 8:11-15
11 Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. 12 Ile njia zilipoanguka baadhi ya mbegu, ni mfano wa watu wanaolisikia neno la Mungu lakini shetani huja akalichukua kutoka katika mioyo yao, ili wasiamini na kuokolewa.
13 Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao.
Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao. 14 Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua. 15 Bali ule udongo mzuri ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mwema na wa utii, wakavumilia na kuzaa matunda.”

7. Marko 8:38
38 Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu, na mimi, Mwana wa Adamu, nitamwonea aibu wakati nitakapokuja katika utu kufu wa Baba yangu na malaika watakatifu.”

Marko 14:72
72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji Yesu

Luka 24:5-7
5 Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu?
6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya, 7 kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.”

Yohana 5:25-29
25 Nina waambia hakika, wakati utafika, tena umekwisha timia, ambapo wafu wataisikia sauti ya Mwana wa Mungu; na wote watakaoisikia wata kuwa hai.26 Kama vile Baba alivyo chanzo cha uzima, hali kad halika amemwezesha Mwanae kuwa chanzo cha uzima. 27 Na amempa Mwanae mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.
28 “Msishangae kusikia haya. Wakati unakuja ambapo wafu wataisikia sauti yake, 29 nao watatoka makaburini; wale waliot enda mema watafufuka na kuwa hai, na wale waliotenda maovu, wata fufuka na kuhukumiwa.

Yohana 12:32-33
32 Nami nitakapoinuliwa kutoka ardhini, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 Alisema haya ili kuonyesha jinsi atakavyokufa.

Matayo 24: 1-3
Yesu aliondoka Hekaluni na alipokuwa akienda zake, wana funzi wakamwendea ili wakamwonyeshe majengo ya Hekalu. 2 Lakini yeye akawaambia, “Mnayaona haya yote? Nawaambieni kweli, hakuna hata jiwe moja hapa litakalobaki juu ya jingine, yote yatatupwa chini.”
3 Yesu alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni wanafunzi wake walimwendea faraghani, wakamwuliza, “Tueleze, mambo haya yatatokea lini na ni dalili gani zitaonyesha kuja kwako na mwisho wa dunia?”

Matayo 24: 36-39
36 “Hakuna ajuaye siku wala saa, hata malaika mbinguni wala Mwana, isipokuwa Baba peke yake. 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu.
38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina. 39 Nao hawakujua ni nini kitatokea mpaka gharika ilipokuja ika wakumba wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa nitakapokuja mimi Mwana wa Adamu.

8. Yohana 17:5-8.
5 Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe hata kabla dunia haijaumbwa.6 Nimewafahamisha jina lako wale ambao umenipa kutoka katika ulimwengu. Wao wametii neno lako. 7 Sasa wamefahamu ya kuwa vyote ulivyonipa vinatoka kwako ; 8 kwa kuwa nimewapa ujumbe ulionipa, nao wameupokea. Wamefahamu hakika ya kuwa nimetoka kwako na wameamini kwamba ulinituma.

9. a. Marko 1:10-11
10 Yesu alipo toka kwenye maji aliona mbingu zikifunuka na Roho wa Mungu anam shukia kama njiwa.11 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni mwanangu mpendwa; nimependezwa nawe.”

b. Yohana 1:32-33
32 Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akish uka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake.
33 Mimi nisingem tambua, lakini Mungu ambaye alinituma nibatize watu kwa maji ali kuwa ameniambia kwamba, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia kutoka mbinguni na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’

c. Matendo Ya Mitume 11: 4-9
4 Ndipo Petro akaanza kuwaeleza mambo yote yalivyotokea akasema, 5 “Nil ikuwa nikiomba katika mji wa Jopa, nikaona katika ndoto kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kwa ncha zake nne, kutoka mbinguni, nayo ikanifikia. 6 Nilipotazama kwa makini nikaona wanyama wa kila aina, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani. 7 Nikasikia sauti ikiniambia, ‘Amka Petro, chinja, ule!’8 Nami nikasema, ‘La, Bwana! Sijawahi kula kitu cho chote kili chokatazwa na sheria zetu.’ 9 Lakini ile sauti kutoka mbinguni ikasema kwa mara ya pili, ‘Usiite kitu cho chote alichokitakasa Mungu kuwa ni uchafu.’

Matendo Ya Mitume 10: 3-6
3 Alasiri moja, mnamo saa tisa, malaika wa Mungu alimjia katika ndoto na kumwita, “Kornelio!” 4 Kornelio akamtazama yule malaika kwa hofu akasema, “Ni nini Bwana?” Malaika akasema, “Sala zako na sadaka ulizotoa kwa maskini zimefika mbinguni, na Mungu amezikumbuka. 5 Sasa tuma watu Jopa wakamlete Simoni ait waye Petro. 6 Yeye hivi sasa anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi kando ya bahari.”

Matendo Ya Mitume 13: 2-3
2 Wal ipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu aliwaambia, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi maalumu niliyowaitia.” 3 Kwa hiyo baada ya kufunga na kuomba, waliwawekea mikono Sauli na Barnaba wakawaaga.

Waebrania 1: 1-2a
Hapo zamani Mungu alisema na baba zetu mara nyingi na kwa namna mbali mbali kwa kuwatumia manabii. 2 Lakini katika siku hizi za mwisho, amesema na sisi kwa njia ya Mwanae, ambaye alim chagua kuwa mrithi wa vitu vyote

Mithali 8:34-35
“34ana heri mtu Yule anisikilizaye, akisubiri siku zote malangoni pangu, akingija penye vizingiti vya milango yangu.35 maana yeye anionaye mimi auona uzima, naye atapata kibali kwa Bwana.”

1 Wathesalonike 2: 13
13 Nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma pia kwa sababu mlipo lipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu. Bali mlilipokea kama lilivyo hasa, yaani, neno la Mungu, ambalo linafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.

 

 
 

The Guide has her own Guidebook to help her lead and guide the lesson.

Swahili Lesson #2 Guidebook (to be translated)

Download Swahili Guidebook Bible Verses Swahili Lesson #1

Mistari ya Biblia

 
 
Copyright ©  2023 www.UnitedCaribbean.com. All rights reserved. Disclaimer Click to Contact us