SOMO LA NNE (4)
MUNGU ANANIJUA MIMI?
LENGO LA SOMO
• Kutambua kuwa Mungu anatujua sisi, kila mtu Mungu anamfahamu
vizuri.
• Kuelewa kuwa upendo wa Mungu hauishi na wala haubadiliki.
• Hama ya kumwabudu Mungu na kuwa na ushirika naye.
MAOMBI
Mungu wa milele, asante kwa kutuambia kuhusu wewe mwenyewe katika
bilblia. Tusaidie ili tuweze kukuamini wewe katika kila siku na
klatika mahitaji yetu. Tunaomba utusaidie kuelewa kuwa wewe Mungu
una mipango chanya katika maisha yetu, tunaomba katika jina la
Yesu ……………AMEN
MAONI YA UONGOZI
Tunasoma biblia kwa sababu tunataka kumjua mungu. Tunataka kujua
kama mungu anatujua sisi. Kumbuka kichwa cha somo letu, kinasema
mungu ananijua mimi? Je unawezaje kuelezaje utofauti uliopo kati
ya sisi kumjua mungu na mungu kutujua sisi?............
Kwa sisi kumjua mungu ni lazima yeye ajifunue yeye
mwenyewe kwetu sisi. Sisi kumhua mungu inategemeana ni jinsi gani
tunatii na kuweza kuamini na kwa kufanya hivyo atajifunua kwetu
kwa kupitia neno lake. Tumekuwa na masomo mengi amabyo yalikuwa
yanatufundisha jinsi mungu alivyojifunua yeye mwenyewe kwetu sisi,
kwa hiyo tunatambua kuwa yeye mungu anataka sisis tuweze kumjua
yeye.
Siri ya kumjua mungu inatakiwa sisis wenyewe tuchukue
hatua kama tunaamini katika yeye.Je anaposema kuwa anataka sisi
tumjue yeye, je tunaamini anavyomaanisha? Je kuna utofauti wowote
unaoonekana pale tunapomuomba kuwa ajioneshe, tujue jinsi yeye
alivyo.
Mungu anatufahamu kuliko vile sisi tunavyojifahamu
sisi kama sisi au jinsi anavytufahamu mtu mwingine. Munguyeye
hana hata muda wa kunanza kutusoma sisi. Yeye alitujua hata kabla
ya kuja hapa dunianai.yeye kama yeye alikua ameshaandaa mpango
kwa ajili ya maisha yetu. Mungu anatutambua sisi mar azote. Uliposoma
somo lako ulisoma Zaburi 139. Inatuambia njia nyingi ambazo mungu
anatujua sisi kabla hatujazaliwa. Anajua kila kitu kuhusiana na
sisi.
Katika somo la nne kwenye kitabu cha kujifunzia,
katika kusoma na kujifunza biblia kwa wiki kunathibitisha kuwa
mungu anatujua sisi.
KUJISOMEA BIBLIA KWA JUMA
(Use your Bible or Africa Bible Verse
Handbook) Kila siku wiki hii, soma kifungu cha Biblia,
kwa wiki thibitisha kuwa Mungu anatujua sisi.
Yohana 6:37
Utakuwaje ukija kwa Yesu?...... (Hatakuacha peke yako)
Ayubu 34:21
Vitu vingapi tunavyovifany ana mujngu anaona?....... (Kila
kitu tunachokifanya)
Zaburi 139:1-4
Mistari hii inasemaje ukiunganisha na jinsi Mungu anavyojua
kuhusu watu wake?.......
(Anajua kila kitu kuhusu wao, hakuna kilichojificha
kwake)
Mithali 15:3, 11
Unajuaje kuwa Mungu anaweza kuona mawazo yako?.......
(Biblia inasema kuwa Mungu anaona kila kitu, hata kila mioyo
ya kila mtu)
2 Mambo ya nyakati 16:9
Mungu anataka kuona nini?......
(Watu ambao mioyo yao imemwelekea yeye na ina nia nay eye)
Waebrania 13:5
Ni wakati gani ambao Yesu atakuacha?.......
(Hatakuacha wewe kamwe)
Yohana 14:21
Kuna muunganiko gani kati ya pendo letu kwa Mungu na utii
wetu kwake?.......
Je Mungu anajibuje au anachukuliaje?......
(Yeye anatupenda sisi na amejiweka wazi kwetu)
• Chagua mstari ambao unaona kwako una maana sana
kutoka katika mistari iliyosomwa katika wiki hii. Jiulize
mstari huo ulivyo na maana kwako wewe kama wewe na utumie
katika maisha yako. |
Ni mstari gani ambao ulikua wa maana sana kwako?....... Je uliathirir
wiki yako? Tuambie nini ambacho kilitokea………
1. Hadithi katika Mathayo 18:12-14, inaonyesha
kuhusu mtazamo wa Mungu kuhusu kila mtu?....... (Mungu
anatafuata kile kilichotokea)
2. Waefeso 2:10, inatuambia nini kuhusu
Mungu alichokifanya kwa kila mtu?........ (Mungu ana
mpango mzuri wa maisha yetu, ambao anataka sisi tufanye) |
Mungu anampenda kila mmoja wetu na ana mpango maalumu kwa kila
mtu.
Soma katika kitabu chako cha kujifunzia, Zaburi 100:3……..
Mungu alituumba sisi. Mungu anataka kutubariki sisi na Baraka
za Rohoni. Anataka tuwe na ushirika nay eye. Biblia inathibitisha
ukweli kuw-a Mungu anatupenda sana sisi, anajua kila kitu kuhusu
sisi, na anataka sisi tujue mpango wake juu ya maisha yetu.
3. Ninapoongeza maarifa juu ya Mungu ninajifunza vitu vifuatavyo……
(Mungu anaishi, yeye ni wa milele, ana uweza na nguvu,
Mungu anajua kila kitu, yeye yupo kila mahali, yeye ana
haki, hekima, mtakatifu, ni mfalme, ni wa ajabu)
4. Zaburi 139:1-18 ni uthibitisho tu kwamba
Mungu yeye ana ufahamu thabiti juu ya kila mtu. Unaposoma
Zaburi hii, kopi mstari unaokuletea changamoto na utoe ni
mstari gani ambao unafaraja kubwa sana……
5. Soma mambi ambayo yapo katika Zaburi 139:23-24………
Andika maombi yako mwenyewe kwa kutumia mawazo yaliyopo
ndani ya hiyo mistari kama maombi maalumu.
6. a. Kwa kuwa Mungu anajua kila kitu kuhusu mahitaji yako,
sasa kuna kitu gani ambacho kinakusababisha uogope?
Mathayo 6:25-34…… (Hakuna
kitu) |
b. Mungu anataka ufanye nini na vitu unavyoogopa?
1 Petro 5:6-7…… (Mwachie Mungu
ashughulike nayo)
c. Ni wakati gani ambao Mungu anajua kuhusu mahitaji yako ya
kila siku?
Mathayo 6:8…… (Kabla hata hujaomba)
Sasa kwa nini tunaomba wakati Mungu anajua yote kabla hata hatujaomba?
Kwa sababu Mungu yeyey anataka sisi tuweze kuongea naye.
Maombi ni kazi ambayo inaonesha kuwa Mungu sisi tunamtegemea
na kupeleka mahitaji yetu. Majibu ake ndiyo yanayotupa nguvu nakujua
kuwa Mungu kweli yupo na anatusikia na anajibu maombi yetu.
Kuna wakati mwingine jibu ni “ndiyo” na wakati mwingine
tunaweza kugundua kuwa Mungu alishajibu kabla hatujaomba. Kuna
wakati mwingine jibu ni “subiiri” kuna wakati mazingira
yanaweza yasiwe rafiki kwa kutoa majibu Mungu. Kuna wakati mwingine
jibu ni “hapana” kwa sababu jibu chanya linaweza likaathiri
kazi anayofanya ndani ya maisha yetu.
Warumi 8:28:39 inatuambia kuhusu uimara tulionao
katika kristo………
Mungu hawezi kufanya kitu kinyume na mapenzi yake. Kwa kinachohitajika
hatutakiwi kuogopa ndani ya maisha yetu kwa kuwa Mungu ameshapanga
juu ya maisha yetu. Kwa kuwa yeye ni mtakatifu, anajua kila kitu,
ni mkamilifu, na anatupenda kwa dhati, tunajua kuwa Mungu anataka
mengi mazuri kwa ajili ya watoto wake.
7. Ili kumjhua vizuri Mungu tafuta kila ahadi aliyokuahidi
Mungu katoka rejea za Agano la Kale.
Zaburi 37:4-5…..
(Unapojikita kwake, ukimwamini, atakupa moyo wa hamu)
Zaburi 3:5-6……
(Jitoe kwake na yeyey atakulinda )
Yeremia 29:13……
(Tukimtafuta Mungu kwa moyo wetu wote, tutamuona)
8. Fikiria kuhusu mambo ya baadae katika maisha yako, je
ahadi hizi zinawezaje kuathiri au kuandaa mabo yako yajayo?
9. Mungu ana mipango gani juu ya maisha yako ya baadae?
Soma Yeremia 29:11…….
(Anatuwazia mema na baadae yetu kuwa yenye tumaini)
Mungu anajionesha mwenyewe katika upendo wa kihalisia na
wenye uthibiti. Usiwe na shaka na upendo wake. Tunaweza
kujua kuwa plani yake mar azote ni njema sana. |
10. Kwa kuwa Mungu anakujua wewe binafsi, amaeonyesha upendo
kwa kufanya yale mabo ambayo ilikua sio rahisi kwako wewe
kuyafanya.
Je Mungu alifanya nini kulingana na Warumi 5:6-9?.......
(Anatuilinda kutoka kwenye dhambi na ametuokoa kutoka
katika hasira ya Mungu kwetu kwa sababu ya dhambi zetu,
na kwa wale ambao walikua hawamtii yeye)
11. Tunapoachiilia maisha yetu kwa Mungu yaani (omnipotent)
au mwenye nguvu, kwa nini tusiwe na kujiamini kwamba sisi
tuko salama katika mikono yake?
Somakatika Zaburi 147:5……
(Mungu anajua ni nini ambacho kinafaa kwetu na ana uwezo
wa kutuweka sisi salama, anaona hatari ambazo hatuwezi kuziona
sisi)
12. Andika maombi yako kwa Mungu kwa kuelezea uwepo wake
ambao ni endelevu. Kumbuka kuwa haya maombi hayatashirikishwa
katika kundi. Kwa hiyo andika maombi yako hapa: |
Tutaomab kwa ajili ya somo hili na kwa upendo wa Mungu mkuu kwa
kutulinda.
MAOMBI
Mungu wetu uliye juu mbinguni, tunakushukuru kwa yote na kwa kutujua
sisi jinsi tulivyo. Na bado pendo lako halijapoa kwetu. Asante
Mungu kwa mipango yako mizuri juu yetu. Tusaidie kufanya haya
mambo tuliyosoma kuwa ni sehemu ya maisha yetu. Tunaomba katika
jina la Yesu kristo…………..AMEN
MAELEZO
_______________________________________________________________
_______________________________________________________________