home>> mwongozo >> somo 1 >> somo 2
Mwongozo Somo #2
SOMO LA PILI (2)
MUNGU ANA MW ONEKANO GANI?
LENGO LA SOMO
• Kugundua Mungu ambaye haonekani yukoje.
• Kuelewa jinsi ya kumjua yeye vizuri.
• Kujua na kutambua umilele wa Mungu ,na utakatifu wake.
MAOMBI
Mungu wa milele, tunakuabudu wewe,. Tumejifunza kuwa wewe huna Mwanzo
wala huna mwisho. Tunatambua kabisa kuwa wewe ndio muumbaji wa kila
kitu kinachoishi. Tusaidie jinsi ya kukufikiria vizuri wewe tunaposoma
neno hili. Tunaomba katika jina la Yesu ………..AMEN
MAONI YA UONGOZI
Unaweza ukawa umesikia kuhusu mwalimu mmja ambaye alijikita katika
picha aliyokuwa akiichoara:
“Unacora nini, Amina?” aliuliza.
“Ninachora picha ya Mungu” alijibu.
“Lakini, Amina,” mwalimu aliitikia, “hakuna,
mtu anaye jua Mungu alvyo”.
“Watajua pale nitakapo maliza kuchora picha
yangu hii,” Amina alijibu.
Hatutakiwi kuchora picha katika somo la leo, bali
kinachotakiwa ni kuwa na neno la Mungu kwa kufikiria kuwa hivi Mungu
yukoje.
1. Kwa kutumia maneno machache,
elezea ni nini unachokiona ukifikiri kuhusu Mungu? Kuwa mkweli
na sahihi unafikiri nini kuhusu Mungu. Mwisho mwa somo hili,
hili Sali litaulizwa tena. (Sisitiza kila mtu aweze kushiriki.) |
Fahamu zetu, sio kubwa kiasi kwamba tukamwelewa Mungu.
Yeye hayuko kama sisi hivi tulivyo. Hakuna kitu ambacho tunaweza
kulinganishwa nay eye. Hata kile tunachokifikiri kuhusu Mungu hakioneshi
jinsi Mungu alivyo.
Nini tunachofikiri kuhusu Mungu ni kitumuhimu sana
kwetu sisi.
Ili kufikiri vizuri kuhusu Mungu , inatakiwa sisi
tuache kufikiri kuwa Mungu ana mwili kama wa kwetu hivi ambao unaweza
ukaonekana. Tukiwa na mawazo kama hayo yana weka ukomo wa kuweza
kumwelewa Mungu kiundani zaidi.
Mungu hayupo kama sisi wanadamu hivi tulivyo, vitu
vini ambavyo tunavyo sisi vinatofautiana sana na vyake, kwa mfano
tabia, maadili yake, n.k. hatuwezi kumfahamu yeye mpaka yeye mwenyewe
aongee na sisi kuhusu yeye.
Biblia ndio chanzo kikuu kuhusu taarifa, za Mungu.
Yeye anataka sana tuweze kumfahamu yeye, kwa hiyo amekuwa akijifunua
sana ten asana kuhusu yeye mwenyewe hasa kwa kupitia Biblia.
Sasa tutazungumzia nini tulichhokisoma kuhusiana na
Mungu kutoka katika maosmo mya Biblia.
Kila mtu achague mstari wa kujisomea na asome kwa
sauti.
KUJISOMEA BIBLIA KWA
JUMA
(Use your Bible or Africa Bible Verse
Handbook)
Kila siku katika wiki hii, soma mistari ya Biblia,
kwa siku kutoka katika agano jipya, na ueleze kila kifungu
kinasema nini kuhusu Mungu.
1 Wakorintho 1:9…….. (Mungu
anatakiwa kuaminiwa)
Warumi 16:27……. (Ni mmoja
tu ambaye ni mwelewa zaidi)
Luka 1:37……… (Hakuna
jambo ambalo hawezi kulifanya)
Yohana 3:16……. (Alitupenda
sisi na kutupatia mwanae kufa kwa ajili yetu, ili tupate na
tuwe na uzima wa mmilele)
Hesabu 23:19……… (Yeye
sio mwanadamu, hata aseme uongo, anafanya chochote anachotaka
kufanya)
Ufunuo 15:3-4……… (Mungu
ni mtakatifu, kweli. Mataifa yatakuja kusujudu yeye kwa sababu
ya haki na kazi yake kubwa )
Funuo 1:8……… (Ni wa
milele. Yeye ni Mwanzo na mwisho)
Chgua mstari ambao wewe kwako una maana sana kutoka mistari
tuliyosoma hapo juu. Fikiria kuhusu ukweli huo una maanisha
kwako binafsi na uweze kuutumia ndani ya maisha yako. |
Je mstari uliuchagua umefanyiaje mazoezi ?..........Je uliatiri
vipi wiki yako? Tuambie nini kilitokea…………
Rudi katika aganoo jipya, soma wako; Losai 1:15-16………
Inasema nini kuhusu Mungu? Katika mstari wa 15 unasemaje kuhusu
Mungu?.......(Mungu haonekani)
Mungu hana mwili kama wa kwetu. Fikra zetu
zina makosa mengi sana, pale tunapofikiri kuwa Mungu yuko
kama sisi, au ana ukomo kama sisi. Ukiangalia sisi hatukujiumba,
wala hatukuamua sisi kwamaba tuanze kuishi, pia tunatakiwa
tujiulize je tuliumba nywele, chakula?, au maji? Ambavyo hivi
vinafanya maisha yetu yasonge mbele. Pia Mungu yeye ni mkamilifu
yeyey kama alivyo. Yeyey hata msaada hataki kwa kuwa yeye
ndio kila kitu.
Kila kitu tunachokiona katika dunia hii kilumwa au kilitengenezwa.
Lakini Mungu hakuumbwa, wala hakujtengenezwa. Mungu ni wa
tofauti katika kila kitu. Jina lake ni NIKO. Yeye yupo na
atakuwepo milele yote. Yeye hatakuwa na mwisho wowote ule.
Utofauti mwingine ambao tunatofautiana na Mungu ni kwamba
sisi ni binadamu nay eye ni Mungu. Kwa hiyo sisi ni vitu vinavyoonekana. |
Swali la pili linatuambia vitu vingine zaidi kuhusu Mungu.
2 . Katika Yohana 4:24 inasema nini kuhusu
Mungu?.........(Mungu nni Roho) |
Mungu hana ukomo. Yeye ni Roho na anaweza kuwa mahali opote na
kwa muda huohuo.
Biblia inatufundisha kuwa Mungu hana ukomo yeye ni wa milele.
Mistari mingi sana ndani ya Biblia inatuambia kuhusu hili. Mingi
mistari imetolewa katika kitabu cha kujifunzia (Unaweza ukamweleza
mtu ili aweze kusoma mistari hiyo)
MUNGU WETU HANA UKOMO
Sulemani alioma,
“Lakini Mungu je? Atakaa, kweli kweli juu ya nchi?
Tazama, mbingu za mbingu semmbuse nyumba hii niliyojenga!”
- 1 Wafalme 8:27.
Je wewe waweza kuvumbua ukuu wa Mungu?
Waweza kufikiria upeo wa huyo mwenyezi?
Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe?
Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?
Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, ni kipana zaidi ya bahari.
- Ayubu 11:7-9.
YEYE NI ZAIDI YA UFAHAMU WETU
“Mungu huunguruma kwa kustaabisha kwa sauti yake; hufanya
mambo makuu, amabyo hatuwezi kuelewa nayo. - Ayubu
37:5
“Maana mawazo yangu si mawazo yenu,
wala njia zenu si njia zangu; asema bwana.
Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi,
kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu,
na mawazo yangu kuliko mawazo yenu”. - Isaya
55:8-9. |
Ufahamu wetu sisi una ukomo lakini wa Mungu hauna ukomo. Sisi ni
wenye dhambi, yeye hawezi tenda dhambi, yeye ni mkamilifu katika
kila njia. Yeye ni mkuu t hata tusengenye vipi.
Katika agano lako jipya rudi katika Warumi 11:33-36………
Biblia inazungumzia kuhusu mfalme au bwana. Zaburi 145:5
inasema “Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, na
Matendo yako yote ya ajabu”.
Fahamu zetu haziwezi kuwa na Mungu kwa kuwa yeye han a ukomo. Kw
ahiyo kuhusu siri ya Mungu kwetu kwa sababu ya ukomo wetu katika
mambo mengi hatuwezi kuelewa Mungu maana yeye hana aukomo. Kwa hiyo
tunaweza kupokea vitu ambavyo hatuvielewi kwa imani ambavyo Mungu
anasema, kwa sababu tuna kitu cha kuangalia ambacho ni Biblia. Mungu
alitupatia kitabu ili tukitumie katika kumwellewa kuwa yeye ni nani.
3. Sifa ya uungu ya Mungu ni sifa bora sana
ambapo ndio tunatambua ukweli wa Mungu. Katika kila mtari
wa Biblia ufuatao unaambatanisha siafa ya uungu ya Mungu ndani
yake. Soma mistari hiyo na uandike sifa katika kila mstari.
a. 1 Yohana 4:8…….. (Upendo)
b. 2 Wathethalonike 3:3………
(Mwaminifu)
c. Yakobo 1:17……… (Habadiliki)
d. Marko 10:18……… (Mwema)
e. Waebrania 1:8……… (Haki
ya milele)
f. Luka 1:78……… (Mwenye
huruma)
g. 1 Petro 1:15-16………
(Mtakatifu) |
Ukutaka kujua zaidi kuhusu Biblia inasemaje kuhusu sifa hizi za
Mungu, rudi katika baadhi ya kurasa katika agano jipya ili ujue
vizuri kuhusu hili.
SIFA ZA MUNGU
MUNGU NI PENDO
Upendo ni sifa ya Mungu, lakini sio ufafanuzi wa Mungu. Mungu
anafafanua upendo sio upendo unamfafanua Mungu. Hii inaonyesha
tu jinsi Mungu alivyo.
Uaminifu, wema, huruma haki vyote hivi vinamwakilisha Mungu.
Yeye yupo katika hivi lvitu tulivyovitaja. Upendo wa Mungu
mara zote ni mtakatifu. Na mara zote umekuwa mwema, mwamnifu,
na wa haki. |
Hatuelewi namna sahihi ya kuelezea upendo,lakini tunaelewa upendo
umefunuliwaje.upendo hutamani kutenda mema daima na wala hautaki
baya limKumbe yeyote.upendo hutoa vyote bule kwa aliyependwa ,na
Mungu hutupenda sisi sote mmoja mmoja.
Upendo ndio unaowafanya wakristo kuwa wa tofauti kwa kuwa upendo
huo huwa unaleta mabadiliko ambayo ni chanya. Ambapo kama ni upend
waMungu upo kwa kila mtu Yule aliye ndani ya kristo kwa hiyo atakuwa
tofauti na watu ambaohawako nadni ya kristo.
Soma katika 1 Yohana 4:7-16……….
Ni vizuri kusoma zaidi kuhusu upendo wa Mungu . Soma katika Waefeso
2:4 -5……….
MUNGU NI MWAMINIFU
Tunaweza kumtegemea Mungu kwa kuwa Mungu ni mwaminifu. Anatimiza
ahadi zake.tunaweza kuishi katika tumaini kwa maisha ya baadae
kwa kuwa uaminifu wa Mungu haushindwi. |
Tunapozungumzia uaminifu wa Mungu , tunaona umoja wa sifa zake.
Tunaweza kusema kuwa sifa za Mungu zinaelezeana kila moja inaeleza
sifa ya mwenzake. Tunaweza kusema kuwa kila sifa ya Mungu inaelezea
nyenzake na kuvumvua ukamilifu wa Mungu.
Kutambua kuwa agano la kale linasemaje kuhusu uaminifu wa Mungu
soma katika kitabu cha kumbukumbu la Torati 7:9 na Zaburi 92:1-2………….
MUNGU HABADILIKI
Kati ya sifa za Mungu ni kuwa yeye habadiliki. Tunatambua
ya kua Mungu hawezi kuwa sio mwamifu kwa sababu angekuwa sio
mwaminifu ingembidi yeye kubadilika. Mungu ni mkamilifu. Hawezi
kushindwa hata siku moja.
Soma Malaki 3:6…… |
Sifa nyingine ni wema. Tunajua kuwa ili kuwa mwema zaidi ni kuwa
mkarimu, mpole, mwenye maadili mazuri, mwenye upendo, na mtakatifu.
Tunaelewa ubora wa wema kwa sababu kuna muda mwingine tunaweza kuona
kuwa sisi kama sisi ni wema .
MUNGU NI MWEMA
Wema wa Mungu ni tofauti na wema wa mwanadamu, kwa sababu
Mungu ni mkamilifu kila eneo.” Mungu peke yake ndio
mwema”
Soma Zaburi 107:1...… |
MUNGU NI WA PEKEE
Mungu yeye pekee amejikamilasha, na hawezi kuwa kitu kingine.
Yeye ni wa pekee. Soma katika kumbukumbu la Torati
32:4……… |
Hakuna kitu katika haki ya Mungu ambacho kinachomzuia yeye kwamba
asiwe mwenye huruma. Sifa zake zote hazifarakani.
MUNGU NI MWENYE HURUMA
Huruma na sifa ya Mungu. Yeye ni Mungu mwenye huruma sana
na ni Mungu wa haki sana. Mungu aluwa mwenye huruma tangu
Mwanzo .
Hata katika kutenda haki,yeye ni mwenye huruma,mara zote
anaposhughulika na mwana damu huonyesha upedno wa hali ya
juu sana,Upendo upitao sio tabia ya muda mfupi ya Mungu bali
ndiyo alivyo ,Mungu alikuwa ni mwenye huruma hata kabla saa
hazijakuwepo na mwenye huruma hata leo hii.
Soma 2 Wakorrintho 1:3……… |
MUNGU NI MTAKATIFU
Mungu yeye hana uhafu wowote yaani yeye ni msafi sana, na
mwenye maadili ya hali ya juu sana.
Kwa sababu Mungu ni mtakatifu, kwa hiyo hata sifa zake pia
ni takatifu. Kwa hiyo kila kitu tunachofikiria kinachohusuiana
na Mungu, Mungu inatakiwa tufikiri kuwa ni kitakatifu. |
Biblia inasema nini kuhusu utakatifu? Soma 1 Samweli 2:2
na Zaburi 99:9
4. a. Mungu anategemea nini kutoka kwa wakristo?
1 Petro 1:13-16……… (Kuwa
watakatifu katikakila kitu tunachokifanya)
b. Kulingana na 1 Wakorintho 1:30, tunawezaje
kuwa watakatifu?........ (Kwa kukaa na Mungu kupitia Yesu
kristo) |
Tunajua ya kuwa sisi sio watakjatifu na hatuwezi kuwa watakatifu
kama Mungu alivyo. Lakini tunapompokea Yesu kristo, tunapokea kila
kitu ambacho Mungu yuko. Katika 1 Wakorintho 1:30 tunaambiwa ya
kwamba kristo ambaye yupo ndanni yetu ni hekima yetu, na utakatifu.
Tunakuwa karibu na Mungu na ana tuweka huru. Kristo ndiye mtakatifu
wetu.
Kuna mistari miwili yenye nguvu katika Yeremia 9 ambayo ni muhimu
kwa maisha haya ya kila siku
Bwana asema hivi, "Mwenye hekima asijisifu kwa
sababu ya hekima yake, Wala mwenye nguvu aijisifu kwa sababu
ya nguvu zake, Wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wak;
Bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, Ya kwamba ananifahamu
mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni bwana nitendaye wema, na hukumu,
na haki, katika nchi; Maana mimi napendezwa na mambo hayo,"
asema Bwana. - Yeremia 9:23-2 |
Tumeshaanza kuona jinsi gni Mungu Mungu alivyo.
SIFA TATU (3) ZA KIPEKEE
Mungu ana nguvu zote. Aliumba ulimwengu huu na kila kitu
kilichomo ndani yak e kwa kuongea tu. Na anatawala vyote.
Ana nguvu ya kufanya miujiza. Kwa hiyo tuna sema kuw aMungu
nijalali (yaani anaweza kufanya lolote atakalo).
Mungu anajua kila kitu katika ulimwengu huu. Hakuna kitu
ambacho tunaweza kusema uwa hakijui. Nguvu ya Mungu na maarifa
yake hayatengani. Hii tunaita omniscience (yaani utu).
Mungu yuko kila mahali na kwa muda mmoja. Yeye anapatikana
karibu kila eneo au kila sehemu muda wote. Tunasema kuwa Mungu
yupo kila mahali (omnipresent).
|
5. Soma mistari ifuatayo ya Biblia na uandike
sifa hizo tatu za Mungukila sehemu ya mstari utakao soma.
Maana mistari hiyi inaonesha omnipotence, omnipresent na omniscience.
Mathayo 28:20………………...…..
(Omnipresence)
Mwanzo 17:1; 18:14………………..(Omnipotence)
Waebrania 4:13…………………….(Omniscience) |
MUHTASARI
Kwa kile tulichokijadili katika somo la 1 na somo la 2, oredhesha
maneno yanayomwelezea Mungu. Unaweza kuandika maneno yafuatayo katika
ukuras aambao upo wazi mwisshoni mwa somo hili.
Maneno yanayomwelezea Mungu
Roho
Yupo kila mahali- omnipresent
Ni zaidi ya ufahamu wetu
Mwaminifu
Hana ukomo
Mtakatifu
Ana nguvu zote- omnipotent
Mwenye huruma Habadiliki
Anajua kila kitu- omniscient
Mwenye haki
A.W. Tozer muandishi maarufu sana,”Mungu tunae paswa kumjua
ana nguvu za ajabu sana na yupo mbinguni,Mungu baba muumba wa Mbingu
na nchi,Mungu mwenye hekima na mkombozi.
Yeye ndie akaaye katika mzunguko wa ulimwengu,yeye akunjuaye mbingu
kama hema.
Je umeanza kuelewa kuwa Mungu ni nani? Je unahisi utakatifu wake,
usafi, na hekima yake? Je unaweza ukathibitisha kuwa yeye hana ukomo?
Katiak somo la tatu na la sita andika mwenyewe maombi ya kufungia
baada ya masomo yako, hii itakusaidia wewe ili kupeleka haja zako
mbele za Mungu na kumwomba Mungu katika kila jambo wewe utakalo
litaka. Maombi yako binafsi hayatasomwa au kushirikishwa katika
kundi itakuwa ni siri yako.
MAOMBI
Mungu mwenyezi, asante kwa hiki tulichokisoma. Asante Mungu kwa
kuwa upo kila mahali, na kwamba una nguvu zote, na unajua kila kitu.
Wewe ni Mungu wetu mwema. Tuna furaha kwa kuwa wewe unatupenda na
una tulewa sana. Tunakusifu wewe kwa Baraka zako zote. Katika jina
la Yesu kristo……….AMEN
MAELEZO
_______________________________________________________________
_______________________________________________________________
|