home >>stonecroft>>
mwongozo >> somo 1
Mwongozo Somo #1
MUNGU ANA MWONEKANO GANI?
Marekebisho Toleo.
Lucille Sollenberger. B.S., M. A.
SOMO LA KWANZA(1)
MUNGU YUPO
Stonecroft Ministries
www.stonecroft.org
P.O.Box 9609, Kancas City, MO 64134-0609
SOMO LA KWANZA(1)
MUNGU YUPO
LENGO LA SOMO
• Anza kuelewa Mungu kuwa yukoje na anakuwa kama nini.
• Tambua kuwa Mungu mara zote ana furaha
• Ikubali Biblia kama ndiyo chanzo cha majibu.
MAOMBI
Baba yetu uliye juu, tunataka kujifunza kitabu hiki ulichokiandika
mwenyewe ili sisi tukuelewe wewe. Fungua macho yetu, masikio yetu,
na mioyo yetu ili tuweze kuelewa kile unachotaka sisi kujifunza
kutoka kwako. Twaja kwako kwa jina laYesu kristo …….AMEN
MAONI YA KIONGOZI
Kutusaidia sisi kufaidika kutoka katika haya masomo, kuna mwongozo
ambao tutaufuata.
JINSI YA KUJIFUNZA
MASOMO YA BIBLIA KATIKA STONECROFT
Kwa sababu hii ni shule ya Biblia, lengo letu kuu ni kujifunza
kile ambacho Biblia inasema na jinsi gani tunaweza kutumia
katika maisha yetu. Kijitabu hiki na Biblia ndivyo vitakuwa
vitabu vyetu ambavyo tutavitumia katika masomo yetu.
Inatakiwa tujiandae kwa somo kwa kumaliza maswali katika
vijitabu vyetu hivi vya awali. Hii itatusaidia katika majadiliano
yetu ya wiki kufanya kwa urahisi na kuelewa vizuri kuhusiana
na somo husika kwa wakati huo. Tutajifunza somo la kwanza
sote kwa pamoja.
Masomo yetu haya ya Biblia yataanza katika muda muafaka na
yatachukua muda wa dakika 60 mpka 90. Tutaondoka pale ambapo
somo letu husika tunalolisoma litakapokuwa limefikia mwisho
kwa hiyo hatutaacha kitu tutamaliza.
Kwa sababu tunatoka katika mazingira tofauti tofauti na (ukijumuisha
tunatoka katika makanisa tofauti tofauti) kwa hiyo tutaheshimu
mawazo ya kila mtu na imani yake.
Katika wiki chache, tungependa kuanza masomo mapya ya Biblia
katika maeneo mapya na kwa watu wapya. Hebu fikiria mtu ambaye
ungependa umwalike katika masomo haya. |
Mungu yeye ni nani? Swali limekuwa linasumbua sana watu kwa karne
nyingi sana zilizopita. Wametafuta katika historia, wakajaribu ,kujua
kuiwa Yesu ni nani na anafanyaje kazi.
Lengo la masomo haya ni:
• Kujifunza Biblia inavyosema kuhusu Mungu.
• Kutambua jinsi maisha ambavyo yatakuwa baada ya kumjua Mungu
na kuwa na ushirika na yeye.
• Kutumia tuliyojifunza na kuendeleza kwa undani zaidi, uhusiano
tulionao na Mungu.
Ili kuchochea kufikiria kwetu, kumbuka yafuatayo:
MUNGU YUPO
Biblia inatuambia ukweli kuwa Mungu yupo. Hakuna utuibitisho mwingine
kuwa Mungu hayupo, Mungu yupo. Hakuna mjadala juu ya hili. Mtu anayechukua
Biblia kwa mara ya kwanza na kuisoma ni kwamab atajua kaisa kuwa
Mungu yupo na bila hata mashaka yeyote yale. Mungu, ni kweli na
ni Mungu mwenyezi yupo. Ni yeye aliyefanya kila kitu katika dunia
hii.
Mungu ,muda wote amekuwapo,
na atakuwepo,
uweza wake unawakilishwa na maneno mawili tu:
Mungu yupo. |
Unaweza ukawa na mwitikio upi katika maelezo haya?
(Jadiri, tambua na tia moyo mawazo)
Mwenyezi , huwakilisha Mungu, ambaye anajua
kila kitu, yuko mahali hapa. Mara zote atakuwepo, kwa sababu
Mungu yupo .
“lakini pasipo imani haiwezekani
kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba
yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.
- Waebrania 11:6 |
Agano jipya linazungumzia ukweli kwamba “Mungu yupo”
kwa kutumia neno linguine badala ya “yupi” au “ni”.
(Use your Bible or Africa Bible Verse
Handbook)
1. Usome Waebrania 11:6……..
je ni neno gani ambalo linatumika katika mstari huu kuonesha
ukweli kuwa Mungu yupo? ……(anaishi, au yu
hai). |
Mungu amekuwa akiishi au yu hai na ataendelea kua hai tu. Watu
wanaishi nawe pia unaishi. Miili yetu ina Mwanzo na ina mwisho wake.
Lakini, Mungu han a Mwanzo wala mwisho. Kusema kuwa, Mungu yu hai
ni sahihi. Hakuna muda, ambao Mungu hakuwepo. Alikuwepo na atakuuwepo
tu.
MUNGU NI MUUMBAJI
Tangu Mwanzo hakukuwa na kitu ; lakini Mungu pekee yake ndiye
aliyekuwepo. Kulikuwa hakuna mbingu, dunia, jua, mwezi, au
nyota. Mungu alisema tu na mambo yote yakatokea na uumbaji
ukaanzia hapo. Alianza kujaza utupu uliokuwepo, kuumba vitu
kutoka katika sehemu ya utupu. Mungu yeye ni muubaji wa kila
kitu katika ulimwengu huu. |
Je agano la kale linasema nini kuhusu kuwa Mungu ni muumbaji?
2. Soma mistari ifuatayo ya Bibblia, na ueleze
kwa amaneno yako mwenyewe ukweli wa kila mstari kuwa unafundisha
nini?
(Kumbuka maandiko ya agano la kale yanaandikwa katika
kila mwisho wa somo.)
Nehemia 9:6…….
WakoLosai 1:15-16……..
Ukweli ulioandikwa katika mistari hii ni (Mungu ndiye
muumbaji wa vitu, vyote.) |
Mungu ni muumbaji wa vitu vyote. Mwanzo , kuitabu cha kwanza katika
Biblia, inatuambia kuwa Mungu akasema tu na vitu vikatokea. Neno
lake lina nguvu sana. Alisema na kukawa na nuru. Alisema na vitu
ambavyo havkuwepo vikatokea ambavyo havikuwwepo. Kwa hiyo kila kitu
unachokiona Mungu alisema tu na kikatokea, na kuhusiana na sisi
wanandamu Mungu alitufanya kwa mikono yake mwenyewe. Je ni Mungu
gani wa ajabu, huyu ambaye tunaye. Aliumbakila kitu kinachoonekana
katika ulimwengu huu ambao tupo.
MUNGU NI WA MILELE
Maneno haya mawili kuwa Mungu yupo yanaonesha kuwa Mungu
ni wa milele. Umilele ni wazo ambalo ni vigumu sana kulielewa,
kwa kuwa tunaishi kwa muda.
Sis ni wafungwa wa muda. Muda tulipozaliwa ulirekodiwa, ,kwa
hiyo kuna ,muda ambao tutakufa. Kila kitu tunachokifanya katika
maisha yetu haya, kuanzia Mwanzo mpaka mwisho, vinapimwa na
muda yaani miaka, siku, masaa, na dakika. Tuliumbwa kwa ufahamu
wa mjuda, kwa hiyo ni vigumu sana sisi kulewa kablaya wakati.
3. Soma mistari ifuatayo ya Biblia na uandike kwa maneno
yako mwenyewe, ukweli unaofundishwa katika mistari hiyo.
Zaburi 102:12, 25-27…………
(Mungu ni wa milele)
Mungu yeye alikuwepo kabal ya wakati, hana Mwanzo na wala
hana mwisho. Anaishi milele.
Tunaishi katia nyakati tatu, wakati uliopita, wakati uliopo,
na wakati ujao. Tumeshaishi wakati, uliopita kwa sasa tunaishi
katika wakati uliopo, na tutaishi wakati ujao. Mungu alikuwa
akiishi hata kabla ya kila kitu kuwepoi hapa duniani na ataishi
milele. |
Mungu hana Mwanzo wala mwisho. Ila sisi tuna mwanazo na tuna mwisho,
lakini cha ajabu zaidi ni kuwa hatutakuwa na mwisho. Miili yetu
hii itakufa, lakini nafsi zetu na Roho zetu zitaishi milele.
Biblia inatuambia sisis katika Mwanzo 2:7 jinsi
Mungu alivyomfanya mwanadamu ili kuishi milele. Inasema kuw Mungu
aliweka pumzi ya milele kwa mwanadamu au katika maisha ya mwanadamu,
na akawa nafsi inayoishi.
Mungu aliumba watu ili wamjue yeye. Na hilo ndio lengo la somo
hili, kumjua Mungu na kujifunza kuwa yukoje. Katika somo hili tumejifunza
kuwa:
- Mungu yupo. Hana Mwanzo na hana mwisho.
- Yeye ni muumbaji wa kila kitu katika mbingu na duniani.
- Yeye ni wa milele- yeye yupo hivyo na ataishi hivyo.
Kitu kingine cha muhimu ambacho Biblia inatuambia kuhusu Mungu
nui kuwa yeye ni wa pekee na yuko peke yake.
MUNGU MMOJA TU PEKE YAKE
4. Soma mistari ifuatayo na ujibu swali hili. Unaamini kuwa
kuna Mungu mmoja tu anayeishi?........
Toa sababu juu ya jibu lako……..
Isaya 44:6………..
Isaya 45:5………..
(Kuna Mungu mmoja tu kwa sanbabu Biblia inatuambia hivyo,
na kwa sanbabu Mungu anasema ni Mwanzo na mwisho. Hakuna Mungu
mwingine na hakutakuja kutokea Mungu mwingine). |
JE BIBLIA NI KWELI?
Tangu tumekuwa tukijibu maswali kutoka kattika Biblia, sasa unaweza
kukawa unajiuliza maswali mengi kwa nini Biblia ni kutegemewa sana
juu ya majibu yetu.
Waandishi wa Biblia wnasema kuwa walikuwa wanarekodi kila neno
la Mungu. Kitu cha kushangaza ni kuwa, ingawa hiki si ma dai ya
waandishi, waaandishi wote 40, walizungumzia msukumo. Takribani
mara 3000 waandishi tofauti tpfauti wa Biblia, kwa njia moja ama
nyingine, walikuwa wanawapa watu neno la Mungu.
Kitu cha kushangaza kingine ni kuwa hawa waandishi wa Biblia walitokea
katika mabara matatu yaani Asia, Afrika na Ulaya. Maandishi yao
yalitawanyika kwa zaidi ya miaka1500. Walikuwa wakitembea kwa muda
tofautitofauti na waliandika maandishi hayo katika lugha tau tofauti
tofauti. Lugha zilizotumika katika kuandika zilikuwa ni Kiebrania,
Aramaic na Kigiriki.
Biblia tangu Mwanzo mpaka mwish o ni kweli kabisa. Ingawa inatoa
mafundisho magumu kweli kweli. Kila kijisehemu kinataka kijisehemu
kingine ili kuweza kukamilisha hadithi, inayotakiwa. Biblia ni Ufunuo
uliojitosheleza, jinsi Mungu alivyotoa wokovu kwa watu wote na kupokea
zawadi kuu ya ajabu.
Vitabu vingine ndani ya Biblia viliandikwa
na ma nabii. Hawa walikuwa ni watu waliokuwa wanaongea neno
la Mungu kwa watu. Waliwaambia vitu vitakavyotokea kabla havijatokea.
Len go la unabii ndani ya Biblia ni kutukumbusha tu kuwa
Mungu anaishoi na kwamaba ana mpango na huu ulimwengu na kwa
kila mtu ana mpango wake mzuri kabisa. Pia kwa ajili ya hawa
manabii Mungu anatukumbusha tu kuwa .nini kitatokea wakati
ujao. |
Katiaka agano la kale .tunaona unabii ambao ulikuja kutimia wakati
wa agano jipya. Kwa mfano unabii kuhusu kuzaliwa, kufa kuishi, na
kufufuka kwa Yesu kristo. Hatuwezi kukaa kuangalia kila unabii kwa
sababau ya muda. Kuna nabii mbili tu ambazo tutaangalia katika maswali
mawili yanayofuata.
5. Tunaweza kuangalia kama utabiri kweli ulikuwa
sahihi.
Nabii mika, alitabiri sehemu ambapo Yesu atazaliwa miaka
700 kabla hajazaliwa.
Mika 5:2………
“Bali wewe , Bethelehemu Efrata, uliye mdogo kuliko
miongoni mwa elfu za yuda;
kutoka kwako wewe atanitokeammoja atakayekuwa mtawala katika
Israeli;
ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele”.
Unabii huu ulitimia soma katika Mathayo 2:4-6……….
Yesu ilitakaiwa azaliwe wapi?.............. (Bethelehemu)
Maria aliishi mashariki mwa palestina, katika Nazareth katika
ujauzito wake. Na bethelehemu ilikuwa kusini mwa palestina.
Na pia serikali ya kirumi iliamuru kuchukua hesabu ya watu
kwa ajili ya kukusanya kodi. Kwa hiyo kila mmoja alitakiwa
kurudi katika sehemu yake yaani nyumbani kwao alikotoka ili
waweze kuhesabiwa. Yufusu na maria walitoka katika ufalme
wa daudi, ambapo wao kwao kulikuwa ni bethelehemu (1
Samweli 16:1……). Andiko lilitimia kwa
sababu Yesu alizaliwa wakiwa tayeri wameshafika bethelehemu,
na sio nazareth. Kwa hiyo Mungu peke yake angeweza kuwaweka
pamoja na sio mtu mwingine.
6. Daudi alizungumzia sana maswala ya kuteswa katika shairi
lake aliloliandika miaka 1000 kabla ya kristo. Kwa mfano :
Zaburi 22:18……………
“Wanagawanya nguo zangu,
na vazi langu wanalipigia kura.”
Tunaona kutimia kwa unabii huu katika Yohana 19:23-24……..
Je akari walifanya nini?...........
(Waligawa mavazi katika makundi manne, na kuyapigia kura.)
Utabiri huu ulimtimizwa na askari wa kirumi ambao walikuwa
hawajui ya kwamba walikuwa wanatimiza utabiri wa wayahudi.
Walikuwa hawajafungamanishwa na mtu ambaye tayari wamesha
mtesa.
7. Andika ufupisho kwa kile Yesu alisema kuhusu agano la
kale.
Luka 24:27, 44……….
(Kila kitu ambacho kimendikawa kuhusu Yesu katia agano
kale inatakiwa yatimie.)
|
Wakati wa kuja kwake Messiah, kifo chake, kuharibiwa kwa yerusalemu,
kuharibiwa kwa hekalu yote haya yalitabiriwa katika kitabu cha danieli
miaka 100 kabla hayajatokea haya yote. Haya yote yalitimia ili unabii
utimie na ndipo unajua kuwa Biblia ni kitabu ambacho kimehuishwa.
8. Je 2 Timotheo 3:16, inasema
kuhusu msukumo wa Biblia?.........
(Maandio yote yamehuishwa na Mungu, na yanatumika katika
kufundisha ukweli.) |
MUHTASARI
Katika kila mwisho wa kulasa kuna eneo unaloweza kuandika. Tunaweza
kutumia ukurasa huu kuandika vitu ambavyo tunataka kuvikumbuka.
Labda unapoendelea unaweza ukaendelea kuandaa notsi kuhusu mambo
ambayo unataka Mungu akutendee au ayafanye. Katika ukurasa huu,
unaweza pia ukarekodi mawazo mbalimbali kuhusu jinsi gani ambavyo
unaweza ukjatumia mawazo haya ya kiBiblia katika maisha yako. Huu
ni ukurasa wako. Tumia jinsi uwezavyo, kuleta maana nzuri kwa upande
wako.
Kwa mfano unaweza ukaandika baadhi ya haya mambo ambayo tumejjifunza
leo.
Tumejifunza nini kuhusu Mungu tunaposoma Waebrania 11:6?........(Mungu
yu hai, au Mungu yupo.)
Tunaposoma Nehemia 9:6, tumegundua au tumehekikisha ukweli gani?..........(Mungu
ni muumbaji wa kila kitu, ndaani ya mbingu na dunia pia.)
Mungu hana Mwanzo na wala hana mwisho. Je ni neno gani linguine
ambalo linatumika badala ya hilo………….. (Milele.)
Biblia imekuwa ikirudia rudia na kutuambia kuwa Mungu wako wako
wangapi?.......... (Ni mmoja tu.)
Sabababu moja ambayo ambayo tunaweza kuamini kuwa Biblia ni kweli
ni hii, mtu mmoja tu ambaye alithibisha katika kuongea ukweli ndani
ya Luka 24:27 ambaye ni (Yesu.)
9. Neno hili “MUNGU YUPO” lina
umuhimu gani kwako, au lina maana gani kwako tangu umelisoma
katika somo hili ?........(Kubali majibu yote, lakini
sisitiza sana kuwa Mungu mara zote aliishi au alikuwepo na
ataendelea kuwepo.) |
Juma lijalo,somo la 2 ambalo ni utambulisho wa kujisomea wa juma,kila
siku,soma mstari katika Biblia au Kitabu cha Biblia,ambacho ni kiambatanisho
cha mwongozo huu ,mistari ya Biblia inaelezea sana kuhusu Mungu
na hata kujibu maswari mawiri au matatu.
Hakikisha unaandika mambo mapya uliyojifunza kuhusu Mungu katika
mwisho wa ukurasa wa somo hili.
Wiki ijayo katika somo la kwanza utaulizwa unaona nini unapofikiria
kuhusu Mungu? Andika kitu cha kwanza kinapokuja ndani ya ufahamu
wako. Andika kama ni halisia kwa upande wako. Mungu ni nani kwako?
Watu wengine wanafikiria kuwa Mungu ni :
- Mtu mkubwa saana anayeishi mbali sana.
- Asili
- Nguvu iliyopo angani
- Muumbaji aliyetuumba na kutuacha sisi peke yetu.
- Ni mwangaza mzuri na anang’aa na analeta utakatifu mbinguni.
- Mwanaume anayekaa katika kiti chake cha enzi na akiwa amekasirika
kulingana na kile kinachotokea katika ulimwengu huu.
MAOMBI
Mungu mwenyezi, tumeanza kuona jinsi gani ulivyo mkuu. Tusaidia
kulitambua hilo, ingawa uko zaidi ya ufahamu wetu, unataka sisi
tukujue wewe. Endelea kutusaidia na kuelewa jinsi wewe Mungu ulivyo.
Tunaomba katika jina la Yesu kristo ………AMEN
MAELEZO
____________________________________________________________________
____________________________________________________________________
This is a translation of What is God like?
Stonecroft's Guide Book Lesson #1 in Swahili, the English version
of
What is God like? is
available online from Stonecroft's website.
In this fresh, engaging study, you will meet
the Creator of life and the Sustainer of all things. As you study
God's eternal characteristics, you will learn that He is majestic,
all-powerful, holy, faithful, and just.
As you explore together what the Bible tells
us about God, you'll also learn how to decide for yourself who He
is and how He interacts with people. (6 lessons)
The Guide has her own Guidebook
to help her lead and guide the lesson.
Download
Swahili Full Guidebook
Download
Swahili Lesson #1 Guidebook Introduction
Download
Swahili Lesson #1 Guidebook
Download
Swahili Guidebook Bible Verses Lesson#1
|