home >>vijana wa stonecroft>> mafunzo ya mwongozo
Mafunzo ya Mwongozo
Kazi ya huyu mwongozaji ni kuongoza masomo haya ya kibiblia,na
wakati huo huo washiliki watakuwa na muda wakuleta mabadiliko katika
jamii ya kuwaleta watu kwa Yesu, katika kundi hilo pia wanaweza
kuona ni nani anafaa kuanzisha kundi jingine la kujisomea biblia,
hii ni baada ya kumaliza vitabu vyote vya utatu.
Masomo ya kibiblia ya Stonecroft na mwongozo wake:
• Kuwaombea wote ambao wanakuja katika masomo ya kibiblia.
• Anza masomo haya ya biblia kwa maombi.
• Kiongozi wa masomo haya ya kiungozi, ambaye atampa majukumu
ya kusimamia kikundi husika lakini yeye ataendela kupewa taarifa.
• Huyu kiongozi atahakikisha kuwa anafuata kanuni na sheria
za huduma ya huduma ya Stonecroft kwa kufuata maelekezo yaliyoko
katika video.
• Anandaa kundi lake kwa kupitia kitabu cha mwongozo, atawakumbusha
wana kikundi juu ya umuhimu wa siri katika kundi na kundi kuelekrza
maswali yao katika maandiko.
• Masomo ya kibiblia ya Stonecroft pamoja na mwongozo wake
unatoa fursa kwa wanakikundi kuielewa vizuri huduma ya Stonecroft,
na nafasi za kujiunga nao.
• Atateua watu ambao watajaribu kupata majibu ya maswari yahusuyo
imani, majadiliano yanhimizwa juu ya nini biblia inasema na sio
nini makanisa yetu yanasema au kufundisha.
• Atahakikisha anakwepa majadiliano yote yahusuyo imani na
misimamo ya watu, siasa, kanisa lipi linapinga au kukubali.
SIFA ZA KUWA KIONGOZI
1. Kiongozi lazima awe kaokoka.
2. Awe ni mtu anae itanga nguvu ya mabadiliko kupitia neno.
3. Akubaliane na sheria na kanuni za Stonecroft.
4. Anawasiliana na kufanya kazi na wenzake.
5. Ana shauku ya kuona watu wanakuwa katika maisha yao ya kiroho
na kumjua Mungu.
JINSI YA KUMHOJI MTU AMBAYE UNADHANI ANAWEZA AKAWA KIONGOZI.
KUMCHAGUA KIONGOZI
Wachungaji (kutoka Africa Training Bible School) ambao walifunzwa
kuwa viongozi watawatambua viongozi hao kiurahisi, kwa kuomba, kwa
hekima, na watoke katika makanisa yao, hawa baada kuwateuwa hao
viongozi, watawezesha katika ukuaji na kutanuka kwa masomo ya ka
kibiblia ya Stonecroft.
Ni muhimu sana katika kumtafuta Yule kiongozi atakae kuwa na sifa
zitakazo endana na sifa zilizotajwa katika sehemu hii.
Maelezo yafuatayo ni muhimu sana unapotaka kumteua kiongozi.
Omba kabla hujaonana na mtu husika, omba ili Bwana awapeni nyote
hekima Roho ya kupambanua .
1. Pangeni muda, muwe tayari kukubaliana juu ya masomo ya kibiblia
ya Stonecroft na huduma.(ikihitajika).
2. Kwa yale maeneo tu ambayo yameolodheshwa katika fomu ya maombi
ya Stonecroft.
o Toa maelezo juu ya huduma ya Stonecroft—mwelekezeke akasome:
• Kijitabu cha masomo ya biblia cha Stonecroft.
• Tembelea mtandao www.stonecroft.org kwa maelezo zaidi.
o Mwambie akupatoe ushuhuda wake wa kumwanini Yesu tu katika wokovu
wake na akupe maandiko ya biblia.
o Muulize je anaweza akajibu nini iwapo ataulizwa Yesu ni nani .
o Muulize kwanini anataka kujiunga na masomo ya kibiblia ya Stonecroft
.
o Chunguza juu ya utayari wake wa kufanya kazi na watu, wa imani
tofauti na tamaduni tofauti
o Muulize juu ya mambo mengine anayo yafanya, na pia anafurahishwa
na nini katika kusoma neon na kuwaongoza wengine katika kujisomea
biblia.
o Hakikisha anazielewa sheria na kanuni za Stonecroft na imani.
Mtu yeyote anaetarajia kuwa kiongozi lazima aelewe Kanuni na sheria
za Stonecroft, na mwongoz wake.
Majukumu ya mchungaji ambaye atakuwa Coordinator (Muunganishaji)
Uwe umekwisha pata fomu ya maombi ya mtu anaye taka kuwa kiongozi.
Kwa umakini wa hali ya juu soma fomu ya maiombi na hakikisha kuwa
ushuhuda wa kiongozi uko sahihi.
Kwa maombi unapaswa kumuuliza huyo mtu maswali machache kuhusiana
na Yesu, kwa mfano.
1. “Ninashauku ya kusikia safari yako na Mungu, hivi Yesu
ana nafasi gani?
2. Iwapo mshiriki wa Stonecroft kakuuliza kuwa anawezaje kuwa na
uhusiano na Yesu utajibu nini?
3. Unaelewa nini kuhusu injili na unawezaje kuihubiri?
Unaweza ukataka kusoma kupitia hili neon je unaweza amini?
Kitabu na mwongozo.
Panga muda wa kumfundisha muhusika kama kiongozi, tumia nyenzo
zifuatazo.
Kitabu cha kibiblia cha Stonecroft cha Africa.
Iwapo hajawahi kukisoma kitabu cha Sonetabu kama “Yesu ni
nani”ili wapate kuelewa ni kitu gani kinahusika katika haya
masomo.
Mchungaji au mkurugenzi atakuwa na fomu za maombi katika faili
lake.
Kumbuka kwamba sio kila mtu yuko tayari kwa ajili ya kuongoza,ukihisi
kuwa huyo mtu hawezi akaepukana na mambo yanayoweza kuleta mkanganyiko
kama vile siasa na mambo mengine ya kijamii ,basi mtie moyo kuwa
yeye asiwe kiongozi bali abaki kama mshiriki tu, wa hicho kikundi.
Baada ya kumaliza haya mafunzo ya uongozi wasiliana na kiongozi
wa Stonecroft wa Africa kwa barua pepe na mawasiliano mengine ya
ziada.
Kiongozi wa Stonecroft wa kijimbo ambaye ni Mchungaji David Akondowe,
atawasiliana na huduma ya Stonecroft ya Marekani, anaweza akafanya
hivi kwa barua pepe: connections@stonecroft.org.
Atuma anuani ya kiongozi iliyo kamili, namba ya simu, na barua
pepe.
Nao Stonecroft wakisha pokea hayo maelezo watamkaribisha huyo kiongozi
mpya kwa barua pepe, ambayo itatafsiriwa katika lugha ya eneo husika,
na kuanzanzia hapo huyu kiongozi ataunganishwa katika mtandao wa
watu wakujitolea na anaweza kunza kupikea barua na majarida katika
barua pepe.na anaweza kutembelea mtandao wa viongozi, na kujipatia
mambo mengi ya kujisomea katia mtandao wa Stonecroft Ministries
website. (www.stonecroft.org)
Hawa viongozi wapya watatambuliwa kama viongozi kwani tunatambua
mchango wa kila mmoja wetu katika kazi hii muhimu ya kuufikia ulimwengu
na injili ya Yesu.
KUWAWEZESHA VIONGOZI WA STONECROFT:
Walimu waliofunzwa vizuri ni muhimu sana katika hii kazi ya kuwafundisha
watu katika imanina hata wale ambao wako katika masomo ya kibiblia
kwa miaka mingi.
Hawa viongozi wengi hutuma majarida mara kwa maana ili kuwa na
mawasiliano na watu,hata mawasiliano ya kuhusu kongamano iwapo wapo
katika Skype, na mawasiliano mengine ya mtandao wa kijamii.
Hawa wakurugeni waandae mikutanio ambayo wanaweza kukutana na viongozi
hawa kwa mwaka mara moja ili watiane moyo na kuweshana ili Stonecroft
ipate kusonga mbele.
Mambo mengi yana shuhudiwa katika mawasiliano, kuwa na maono mamoja,
na kujifunza kwa pamoja,na namna ya kujibu maswali magumu.
Kuwafundisha walimu wapya kunaweza kupangwa katika kipindi maalum
kama vile, muda wa Krismass, na likizo nyingine.
Haya ni mawazo muhimu iwapo unajipanga kuwa na mafunzo ya viongozi:
• Muda maalum kwa ajili ya maombi na ushirika na Mungu.
• Changamoto ya maandiko au maombi.na kuwatia moyo;
• Utangulizi na kushuhudia matokea chanya ya kujisomea biblia.
Muda wa kujifunza: i.e. namna unavyo shuhudia inasadia kuongeza
namna ya kuwafikia wengine, kuanzisha Stonecroft katika makanisa,na
huu uwe muda wa kujifunza kutoka hata wkwa wengine, tuwe na kiongozi
ambae anaelezea namna anavyo waalika wengine, matatizo waliyo kutana
nayo.na eneo lipi walimwona Mungu akiwatetea. Hitimisha kwa maombi
na kuwatia moyo.
MWONGOZO KWA KIONGOZI:
DHUMUNI:
Kuwafikia wasio fikiwa – haya masomo yanawezesha kuhubiri
wokovu kwa kupitia Yesu,
Tunataka kutanua huduma ya Stonecroft kupitia makanisa 280 ambayo
yana wanafunzi wake katika chuo cha ‘Africa Training Bible
School’ (ATBS) katika nchi za Tanzania, Malawi, Zambia na
DR Congo na pia kupitia Hope Community Centre, Kampala, Uganda.
Pia tunamwamini Mungu tunaweza kujumuisha haya kupitia mradi ule
wa kuwezesha wanawake
‘Stonecroft Women’s Empowerment Program’ (SWEP)
ambao mtajifunza mengi hapo baadae. Mradi huu wa kuwawezesha wanawake
utatumia vitabu vya Stonecroft kuanzia vile vijitabu vya utatu,
Mungu yukoje? Yesu ni nani? na Roho Mtakatifu yuko wapi?
Katika kuhakikisha kuwa tunaukuza mradi wa SWEP mafunnzo ya kiafrica,
hawa wanawake watahimizwa kuwa viongozi, watatumia Video ya mafunzo
ya kiafrica, na pia kitabu hiki ambacho kitawawezesha kuanzisha,
Stonecroft katika nyumba zao, makanisa na hata vijiji vyao, kwa
kupata ruhusa maalum kutka kwa mchungaji wao.
Uanafunzi – wakristo wapya na hata wale wa kale wanaweza
kijifunza habari za Yesu na kuweza kuwa na mahusiano ya karibu na
Mungu, masomo haya yanatufundisha namna ya kutumia biblia katika
mazingira yetu ya kila siku, kuna vitabu vingi ambavyo navyo vitatafsiliwa
katika lugha nyingine. ‘Africa Training Bible School’
watatumia masomo haya kama nyenzo moja wapo za kufundishia katika
mitahara yao. Kwa mfano, maisha mapya, kuishi maisha yangu, wafilipi,
Yakobo, Warumi na vingine vingi.
UFAUTI:
Fautisha masomo ya kibiblia ya Stonecroft na masomo mengine ya biblia?
• Masomo haya yameandaliwa mahususi ili yatumike katika agano
jipya ambalo linapatikana sana katika nchi ya Tanzania, lengo kuu
ni kuihubiri injili ya Yesu Kristo, na kuwatia moyo watu ili wapate
kujisomea maandiko kila siku, hatujajumuisha namba ya kila ukulasa
katika biblia maana wengine wanaweza wasiwe na biblia.
• Masomo haya ni rahisi hata kw wale ambao ndio wanaanza kujisomea.
• Kumbuka kuwa kiongozi sio mwalimu wa biblia lakini wote
wanasoma pamoja na washiriki wa kikundi.
.
NYENZO:
Masomo ya kibiblia ya Stonecroft hisi kuyasoma.
Kuna maeneo ambayo yamefungiwa ambayo hupaswi kuyasoma kwa sauti.
Maneno yaliyo chapishwa katika boksi unapaswa kuyasoma kwa sauti
ili washiriki wapate kusikia.
Kwa mfano nucta zikifululiza (.....) inakwambia kuwa kiongozi awaruhusu
washiriki wachangie kwa kuuliza maswali, kusoma biblia au kujadili
somo.
Ukiona wino umekolezwa unao ambatana na nucta Tano, ina maanisha
mstari wa biblia usome kwa sauti kubwa na msomaji.
Ikiwa kama kifungu kilicho nukuliwa kimeandikwwa katika maandishi
ya kawaida ina maana, hakihitaji majibu au ni kirefu sana kusoma
hadhatrani.
KABLA YA MASOMO YA BIBLIA
Vitu muhimu –
Unaweza ukawa kiongozi uliye thibitishwa na Stonecroft wetu kwa
kujaza fomu iliyo tafsiriwa kwa Kiswahili.
Tunataka kujiridhisha kuwa baada ya kusoma kanuni na sheria pamoja
na maelezo yetu ya imani, huna wasiwasi tena nasi.
Vitu vinavyo hitajika katika kujisomea:
1. Vitabu vya utangulizi vya utatu vilivyotafsiriwa kwa lugha ya
Kiswahili vinaweza patikana, katika makao makuu ya ATBS, Mbeya,
Tanzania.
2. Vitabu vya mwongozo vinapatikana makao makuu ya ATBS, Mbeya,
Tanzania.
3. Biblia ya Kiswahili inapatika Tanzania Bible Society.na madukani.
4. Je unaweza kuamini hili? Nacho kimetafsiriwa kwa Kiswahili kinapatikana
katika makao makuu ya ATBS, Mbeya, Tanzania.
5. Kadi ya maelezo nayo imetafsiliwa inapatikana makao makuu ya
ATBS, Mbeya, Tanzania.
6. Fomu ya maombi ya kiongozi nayo inapatika katika makao makuu
ATBS, Mbeya, Tanzania
Tafuta eneo zuli kwa ajili ya kujisomea biblia, labda nyumbani,
kanisani, shuleni, nyumbani katika kivuli chini ya mti.
MAANDALIZI YA KIONGOZI KABLA YA MASOMO:
Hakikisha unajibu maswali yote ya kijitabu cha mwongozo kabla ya
kuanza kusoma vitabu, hii itakuwezesha kuelewa watakao kuwa na wajibu
wanapitia katika wakati gani kabla ya kupata majibu halisi.
• Fanya zoezi la kusoma hayo masomo kwa sauti,ikiwezekana,pigia
msitali maneno muhimu utakayo ongelea katika kundi lako,masomo hayo
yasizidi saa moja na nusu1 – 1 1/2 hasa pale ambapo masomo
haya yanaendeshwa katika kuwezesha wakina mamam yani ‘Stonecroft
Women’s Empowerment Program’ (SWEP) maana wanawake watahitaji
kuondoka na kuanza kujifunza kushona
• Wakati huo huo wanafunzi wa SWEP wanapofurahi masomo yao,watoto
wao watakuwa wakihudhulia “Powerclub” wakijifunza njia
za Mungu kupitia ‘Kids in Ministry International’ (KIMI)
pamoja na watoto wengine kutoka katika mkakati wa ‘Kids Evangelism
Explosion’. (Kids EE)
• Maeneo haya kwa wakatio huu yatakuwa;
Tanzania – Africa Training Bible School (ATBS) – Mbeya
Tanzania
Uganda – Hope Community Centre, Kampala
Malawi – Africa Training Bible School (ATBS) – Uluwa
and Vulwa, Malawi
• Omba juu ya wale watakao kuwa wanakuja.
WAKATI WA MASOMO:
Mara zote anza masomo haya kwa maombi, ikiwa kama kuna mtu ana hoja
basi kundi liandike hiyo hoja yake na mtaiombea katikati mwa juma.
Ikiwa kama hitaji lake ni maombi ya dhalula basi yajumuishwe siku
hiyo hiyo.
Kumbuka kila mara uanzapo somo la “Yesu ni nani” kila
mshiriki ataandika jibu lake katika kijitabu cha kujisomea, na uwakumbushe
kuwa ni vizuri wakawa wanajaza majibu kabla ya kuja darasani.
Soma na kuwapatia washiliki maelezo katika mtindo wa uwazi huku
ukiwangalia usoni, Kiongozi huwa najifunza na kusoma na kundi lote
la washiriki, hutakiwi kuwa umeisimea sana biblia.
KIONGOZI ANAHAKIKISHA NAFASI NA SAUTI HUTUMIKA VIZURI KATIKA
KUJISOMEA:
• Kuanza na kumaliza kwa muda mzuri, kumbuka masomo haya ya
biblia yatakuwa pamoja na shule ya kuwawezesha wanawake.ambao watahitajika
kwenda kushona.
• Tumia kitabu cha kiongozi na biblia ya Kiswahili hakita
hitajika ktabu cha ziada.
• Watie moyo kila mtu ili ashiliki katika kujadili, na hakikisha
hakuna ambaye anaongea kuliko wenginehakikisha unawatia moyo unapowasihi
wajadili.
• Mtazamo wako umuelekee Yesu, na usijadili misimamo ya mafundisho
ya kikanisa, au misimamo ya kisiasa, maswali ya misimamo na mafundisho
ya makanisa yashughurikiwe maeneo mengine.
Tafuta watu ambao watakuwa viongozi wa baadae wa kundi.
Kama kiongozi ni lazima uwe mifano wa kundi, hakikisha watu hawajadili
mambo ambayo yanapaswa kuwa siri, kwa mfano mambo yale ya nyumbani.
Uombe pamoja nao na kuwasihi watafute mwongozo wa Mungu.
Baada ya masomo ya Stonecroft yakina mama kufikia tamati, kila
mtu ambaye anaoneka kuwa ni kiongozi basi apitie mafunzo maalum
ya uongozi, kwa kutumia video na kitabu maalum cha uongozi, ili
waweze kupeleka stonecroft nyumbani kwao. Na katika makanisa yao.
Uwaulize washiriki wafikilie watu ambao wanaweza kuwaarika, uwahimize
waanze kuwaarika watu katika masomo, na pia waanze kuwaombea kwa
kuwataja majina yao.
Mambo muhimu ya kukumbuka.
• Iwapo huwezi kuongoza masomo haya ya biblia kwa sababu yeyote
ile, basi kiongozi aliyethibitiswa aje na kuchukua nafasi hiyo.
• Hutakiwi kumpatia mwenzako kitabu cha mwongozo mtu yeyote
Yule hata kama uko nae katika dara moja.
|