uct >>stonecroft
>>uongozi
UONGOZI WA STONECROFT:
Viongozi wa Stonecroft wanafanya majukumu yao katika ofisi ya kitaifa
na hata kazi ambazo ziko mbali na hapo.
Lorraine Potter Kalal: Raisi
Lorraine Potter Kalal Huduma yake iliyo jawa na mafanikio, Pamoja
na upendo wake wa Stonecroft na maono na historia, Yeye kama raisi
hujiona kuwa ndie Mtumwa mkubwa, Lorrain anahitaji kuona kuwa huduma
ya Stonecroft ikimtegemea Mungu ili kukamilisha mahitaji yote.
Doris Thompson: Makamu wa Raisi
Doris Thompson anawasaidia wanawake kufikia maono yao na mawazo
yao katika matendo, akiwa kama makamu wa Raisi, Doris anataka kuwafikia
wanawake wengi zaidi katika ulimwengu huu, na anawasaidia wanawake
wengi kupitia Stonecroft, na anawasaidia wale wanao jitolea kuwafikia
wengine katika maeneo mengi zaidi. Anafanya kazi ya kuibadiri Stonecroft
ili iweze kuwafikia watu walio katika maeneo mapya zaidi, Pia kuna
watu wengi zaidi katika uongozi ambao hamuwezi kuwa na mawasiliano
nao.
Huduma ya Stonecroft inatamani kuwaunganisha wanawake kwa Mungu
na kwa wanawake wenzake na katika jamii zao.
Stonecroft inawatia moyo wanawake,kuwa na mawasiliano na wenzao
na hata katika jamii zao, na pia kuwaalika katika masomo ya biblia
katika vijiji vyao na miji yao.
Haya masomo ni rahisi kuyafuata, na pia ni makundi yanayo leta
uzima wa kiroho katika maeneo mkakati wa muda mrefu katika maisha
ya waumini.
Hili toleo la kiafrica litaleta matokeo mawili tofauti, la kwanza
ni mkakati wa Stonecroft wa kuwafikia wasio fikiwa, na la pili ni
mkakati wa Stonecroft wa masomo ya kibiblia. Katika madarasa ya
kujisomea biblia, mwongozo wa vitabu vya Stonecroft utatungwa ili
kuwa na vikundi vya kujisomea biblia na kuwafikia wasio fikiwa,
wasio amini na wanao amini, watatiwa moyo ili wajiunge katika makundi
haya .makundi haya yataundwa na wanawake ambao wamemaliza kujisomea
vitabu vya “Utatu” lakini hawajafikia kiwango cha kuongoza
lakini wanataka kuendelea kujisomea, hili litawezesha ukuwaji na
kutanuka kwa stonecroft katika bara la Africa.
Huduma ya Stonecroft inaelewa na kushukuru huduma ya mwanamke mmoja,ukimfikia
mwanamke nae akakokoka basi umeweza kuifikia jamii, mume wake, watoto,
marafiki, majirani, na anao fanya nao kazi.
Askofu David Akondowi, ambaye ni muwakilishi wa United Caribbean
Trust’s (UCT) Tanzania na muasisi wa mafunzo ya wachungaji
katika chuo kitwacho Training Bible School (ATBS) na mchungaji wa
House of Freedom – Tanzania, ambapo UCT wana mradi wa kuwawezesha
wanawake uitwao "Women's Empowerment Sewing Project"
yeye anazungumzia juu ya mithari ya Kiswahili isemayo, ’Ukimuwezesha
mwanamke umeiwezesha jamii’.
Stonecroft wanawawezesha wanawake ili waweze kufikia jamii zao
ki ukamilifu.
|